Mbunge
wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Kibunguchana,kata ya mkamba ikiwa ni sehemu ya utaratibu ambao
ameuweka wa kwenda kushukuru,na kuhimiza utekelezaji wa miradi ya
maendeleo leo katiaka kijiji cha kibunguchana mkoani Pwani.
Mwenyekiti
wa Serikali ya kijiji cha Kibunguchana, Ahamad Mbonde akizungumza
maneno yaufunguzi kabla ya kumkaribisha mbunge wa jimbo hilo Abdallah
Ulega kuzungumza na wananchi hao leo mkoani Pwani.
Mbunge ulega wajimbo la Mkuranga akihesabu fedha.
Mbunge
wa Mkuranga Abdallah Ulega akikabidhi fedha taslimu shilingi laki tatu
kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Kibunguchana, Ahamad Mbonde kwa
ajili ya kuazisha msingi wa ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo
ambapo pia alifanya harambee ndogo iliyowashirikisha baadhi ya viongozi
wa halmashauri hiyo akiwa Mwenyekiti wa halmashauri, Juma abed ambaye
alichangia mifuko kumi yacementi na diwani wa kata hiyo Hassan Dunda
alichangia pia mifuko kumi ya cementi leo mkoani Pwani.
Wananchi
wa kijiji cha Lupondo,kata ya mkamba wakimsikiliza kwa makini mbunge
wao Abdallah ulega katika mkutano wake wakuwashuruku wananchi hao kwa
kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo huku akihaidi kutoawaangusha
nakwamba atakuwa karibu na watu wake. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya
Jamii.
Na Mwandishi wetu.
MBUNGE
wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amewataka vijana wa Wilaya hiyo
kujiunga katika vikundi vya vikoba vinavyoazishwa kwenye maeneo yao na
kwamba wastarajie kuwa ahadi ya rais ya kutoa sh. Milioni50 kila
kijijihaitaenda kwa mtu mmoja mmoja bali kwa kukaa katika makundi.
Amesema
kuwa kama wananchi wanataka fedha hizo ziwafikie lazima wakae kwenye
vikundi na si vinginevyo ,huku akisisitiza akina baba nao kuacha kutumia
muda wao mwingi kucheza bao badala yake wajiunge katika vikundi.
Ulega
ametoa wito huo jimbo humo wakati akizungumza na wanachama wa kikundi
cha Vikoba cha Tuamke kilichopo katika kijiji cha Lupondo kata ya
mkamba.
Alisema
kuwa hakuna namna kwani maendeleo yanakuja Kwa kukaa katika vikundi
mbalimbali na hata fedha za rais zitaelekezwa katika vikundi hivyo,hivyo
kazima watanzania wachangamkie fursa hiyo.
"Binafsi
Leo nawachangia sh.laki tatu kwani mmeonesha dhamira ya dhati kupitia
risala yenu ambayo mmesoma mbele yangu nami nahaidi nitakuwa pamoja nami
kamwe si tawaacha."alisema Ulega.
Aidha
alisema kuwa yeye kama mbunge kuna mipango mingi ambayo anayo Kwa ajili
ya watu wake ikiwa pamoja na kuleta watu wenye makampuni ya Pikipiki ili
kuja katika wilaya hiyo na kukopesha vijana Pikipiki hizo na baadae
kulipa kidogokidogo Kwa muda wa miezi 11.
Alisema
kuwa lazima vijana,akina baba na akina mama Kwa pamoja wakubali
kutengeneza vikundi vya vikoba kwani fursa nyingi zinapitia katika
vikoba na si Kwa mtu mmoja mmoja.
Aidha
Ulega akiwa katika ziara ya kijiji cha Lupondo alipata fursa ya kufungua
jengo la Tuamke Vikoba ambapo pia alitembelea Zahanati ya Kijiji hicho
nakuhaidi kutatua tatizo la miundombinu ya Maji.
Alisema
kuwa anatambua kuwa Zahanati hiyo inachangamoto kubwa ya Maji hivyo
atahakaikisha anasimamia ujenzi wa kisima pamoja na kuona Zahanati hiyo
inapata umeme wa Tanesco Kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma.
"Nitajitahidi
kadri ya uwezo wangu wote kuleta umeme hapa na kama ule wa tanesco
utachelewa basi nitahakikisha naleta solar hapa."alisema Ulega.
Pia
mbunge huyo alisema kuwa wananchi watambue kuwa yupo Kwa ajili yao na
kwamba watakuwa pamoja katika kipindi chonde cha uongozi wake ikiwa
pamoja na kuhakikisha anasukuma huduma jwa wananchi wake.
Naye
Diwani wa Kata Dundani ,Hassan Dunda aliwaeleza wananchi hao kuwa
uchaguzi umekwisha kilichobaki ni Kazi huku akisisitiza kuwa watu kukaa
katika makundi Kwa ajili kupata mikopo.
Ulega
mbali na kufanya ziara katika kijiji cha Kupondo pia alitembelea vijiji
vingine mbalimbali ndani ya Kata ya Mkamba ,ambapo pia anaendelea na
ziara hizo za kutoa shukrani na kukagua miradi ya maendeleo.