Chama cha soka mkoa wa Dar es
salaam DRFA,kimetangaza timu 18 zilizofanikiwa kutingia katika hatua ya
18 bora (raundi ya pili) ya michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam.
Timu hizo ni kutoka katika kundi
(A) ambazo ni Red Coast,Yanga U20,Changanyikeni na Ukonga UTD,kundi (B)
Simba U20,Stakishari,Zakhem na Beira Hotspurs,kundi (C) FFU,Sifa
UTD,Pan Africa na Sinza Stars,huku kundi (D) likitoa timu za
Shababi,New Kunduchi,Ugimbi na Azania Ngano.
Timu mbili zilizopata nafasi ya
kuongezwa kwenye hatua hiyo ya pili,ni Sifa Politan FC pamoja na Tuamoyo
FC,zinazokamilisha idadi ya timu 18.
Makatibu wakuu wa timu zote
18,wanatakiwa kufika katika ofisi za DRFA zilizopo kwenye jengo la
Machinga Complex Ilala (Ghorofa ya 3),siku ya jumatano 04/02/2015,saa 8
mchana,kukutana na kamati ya mshindano kwaajili ya kupata utaratibu.
Baada ya kikao hicho DRFA itapanga makundi na kutoa ratiba ya kuanza kwa patashika hiyo.