MABARAZA YA WAFANYAKAZI TAASISI ZA ELIMU YA JUU YATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

April 18, 2015

Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa ameambatana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Prof. Isaya Jairo kabla ya kuzindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) lililojumuisha wawakilishi kutoka matawi 6 ya taasisi hiyo katika mikoa ya Kigoma, Singida, Mwanza , Mtwara, Dar es salaam na Mbeya.
Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akizindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) jana mjini Bagamoyo.
Wajumbe wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya kuanza kwa mkutano wao jana mjini Bagamoyo.

Wajumbe na viongozi wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza hilo leo mjini Bagamoyo. Picha na Aron Msigwa/MAELEZO.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

SERIKALI imeyata Mabaraza ya wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu kote nchini kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi, kanuni na sheria zinazosimamia  mabaraza hayo ili yawe chachu katika kuleta maendeleo ya Elimu  na mabadiliko ya kiuchumi ya taasisi hizo.

Kauli hiyo imetolewa  na Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akizindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) lililojumuisha wawakilishi kutoka matawi 6 ya taasisi hiyo  katika mikoa ya Kigoma, Singida, Mwanza , Mtwara, Dar es salaam na Mbeya.

Mhe. Mwigulu amesema kuwa iwapo mabaraza hayo yatazingatia weledi katika kusimamia masuala mbalimbali ya taasisi hizo nchini  yataleta mabadiliko ya kiutendaji katika usimamizi wa mapato na matumizi  na kutoa  ushauri utakaoisaidia Serikali kutekeleza mipango mbalimbali ya  maendeleo.

Mhe. Mwigulu ameeleza  kuwa endapo mabaraza hayo yataacha kufanya kazi kwa mazoea na kujikita katika kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa, taasisi hizo zitaongeza uzalishaji, zitakuza mapato na kutatua kero mbalimbali za wafanyakazi mahali pa kazi.

“ Napenda niweke wazi kuwa mabaraza haya  ni muhimu sana kwa wafanyakazi, hayana tofauti na bunge ,kazi yake  kubwa ni kusimamia mapato na matumizi, kushauri taasisi na Serikali juu ya utekelezaji wa  mipango mbalimbali ikiwemo ajira kwa watumishi wapya” Amesisitiza.

Akizungumzia changamato ya uhaba wa walimu na watumishi wa kada mbalimbali  katika taasisi hiyo na taasisi nyingine za Umma za Elimu ya juu amesema Serikali inaendelea  kutenga fedha katika bajeti ya kila mwaka ili kuondoa tatizo hilo.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kulishughulikia suala la usimamizi wa ziada ya mapato yanayozalishwa na taasisi za umma ili yaweze kupelekwa  katika maeneo mengine yenye uhitaji.

“Serikali tunaendelea kuangalia utaratibu wa kutumia ziada ya mapato inayozalishwa na taasisi mbalimbali za umma ili iweze kupelekwa katika maeneo mengine yenye uhitaji maana fedha hizi ni za umma,taasisi moja ya Serikali haiwezi kung’ania ziada ya mapato iliyozalisha, hizo ni fedha za umma lazima zikafanye kazi maeneo mengine yenye uhitaji hasa kwenye kugharamia mahitaji ya wodi za akina mama kote nchini”

Pia amesisitiza mkakati wa Serikali wa kuzifanya taasisi hizo za elimu ya juu kuwa na mamlaka yake katika kuajili watumishi wake na kjitegemea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ndiye Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda  akizungumza na wajumbe wa baraza hilo amesema kuwa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka 5 imepata mafanikio makubwa ya kuongeza  ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi Bilioni 6 za mwaka 2010 hadi kufikia shilingi Bilioni 18 mwaka 2014/2015.

Amesema Taasisi hiyo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uhaba wa miundombinu, ufinyu wa bajeti , uhaba wa walimu wenye shahada za uzamivu (PhD)  na watumishi kimeendelea kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaodahiliwa kutoka  7635 waliodahiliwa mwaka 2011/2012 hadi kufikia 14974 mwaka 2014/2015.

“Licha ya kuendelea kufanya vizuri taasisi yetu inakabiliwa na tatizo la waalimu katika matawi yetu yaliyo mikoani ,jambo hili hutufanya tutumie gharama kubwa kuwasafirisha kutoka makao makuu kwenda kufundisha wanafunzi wetu wanaochukua michepuo ya Biashara, Uhasibu, Rasilimali Watu, Ununuzi na Ugavi,Uhasibu katika Sekta ya Umma na Masoko na Mahusiano kwenye matawi yetu” Amesisitiza.  


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya wizara ya Fedha wa Taasisi hiyo Prof. Isaya Jairo akizungumza na wajumbe waliohudhuria mkutano huo amesema kuwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)katika kukuza na kuongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi kutoka serikalini itaendelea kufanya shughuli kibiashara ,kufanya utafiti, kutoa ushauri katika Nyanja za uhasibu, ununuzi na ugavi kote nchini.

MAMBO 10 ALIYOSEMA WEMA KATIKA MAISHA BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND

April 18, 2015
Ijumaa hii Wema Sepetu alikuwa mgeni kwenye kipindi cha Ubaoni cha EFM. Miongoni mwa mambo aliyoulizwa ni pamoja maisha baada ya kuachana na Diamond Platnumz.
Coastal Union yajiandaa na mechi ya Ligi kuu dhidi ya Polisi Morogoro itakayochezwa Jumatano wiki ijayo

Coastal Union yajiandaa na mechi ya Ligi kuu dhidi ya Polisi Morogoro itakayochezwa Jumatano wiki ijayo

April 18, 2015

unnamed
Kocha Mkuu wa Coastal Union,Jamhuri Kihwelu “Julio”  (kulia) akisisitiza jambo kwa wachezaji wa timu hiyo mara baada ya
kumalizika mazoezi yao juzi kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya Ligi kuu dhidi ya Polisi Morogoro itakayochezwa Jumatano wiki ijayo kwenye uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
Picha kwa Hisani ya Coastal Union.
MKUU WA WILAYA YA TEMEKE SOPHIA MJEMA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA SIKU 5 YA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI WILAYANI TEMEKE.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE SOPHIA MJEMA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA SIKU 5 YA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI WILAYANI TEMEKE.

April 18, 2015

1
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akilakiwa na Dkt. Martha Kisanga, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Shirika la Engender Health mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Shule ya Sekondari Kibasila kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya siku 5 yaliyohusu mradi wa kuzuia mimba za utotoni katika Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke tarehe 17.4.2015. Waliosimama katikati ni Ndugu Donald Siliva, Afisa-Elimu Sekondari, Wilaya ya Temeke na Dkt. Sarah Maongezi, Mkurugenzi wa Afya  kutoka Taasisi ya WAMA.
2 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akisalimiana na baadhi ya wanafunzi kutoka baadhi ya Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke walioshiriki katika mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni. Mafunzo hayo yalifanywa na Taasisi ya WAMA ikishirikiana na Shirika la Engender Health kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani, USAID. 3
Baadhi ya wanafunzi na walimu kutoka Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakiimba wimbo wa kumkaribisha mgeni rasmi alipokuwa akiingia ukumbini.
  6
Meneja wa Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wana wake na Maendeleo, Ndugu Philomena Marijani akitoa maelezo ya awali kuhusiana semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke iliyofanyika huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
8
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kutoka Wilaya ya Temeke wakimsikiliza salamu kutoka Taasisi ya WAMA zilizotolewa na Meneja wa Uragibishi na Mawasiliano wa Taasisi ya hiyo Ndugu Philomena Marijani wakati wa sherehe ya kufunga rasmi mafunzo hayo huko Kibasila Sekondari tarehe 17.5.2015.
12
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akitoa hotuba ya kufunga rasmi mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari za Wilaya ya Temeke yaliyofanyika Kibasila Sekondari.
14
Washiriki wa semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati akifunga rasmi mafunzo hayo huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
10
Meneja wa Kanda ya Pwani kutoka Shirika la Engender Health, Dkt. Martha Kisanga akimkabidhi Mkuu wa Wilayaya Temeke Ndugu Sophia Mjema maelezo ya mradi wa kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari za Temeke unaosimamiwa kwa pamoja baina ya Shirika lake na Taasisi ya WAMA wakati wa sherehe ya kufunga mafuzo hayo. 
  9
Washiriki wa mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini sherehe za kufunga mafonzo yao huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
     15
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
16
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akiwaaga washiriki wa mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI
NHIF yatoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha

NHIF yatoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha

April 18, 2015

New Picture (1)
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ezekiel Oluwochi akiwasilisha mada ya kwa wanafunzi hao na kuwasisitizia umuhimu wa kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii inayowazunguka.
  New Picture
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, ambapo aliwahakiikishia wanafunzi hao kuwa Mfuko umejipanga kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama.
Aidha amewashauri wanafunzi hao wajiunge na Mfuko huo mara baada ya kuhitimu mafunzo yao ili kujihakikishia kupata huduma bora za matibabu wao na familia zao.
New Picture (2)
Umati wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha wakifuatilia mada katika semina hiyo.