January 04, 2014

Mwili wa Dkt. William Mgimwa Wawasili Kutoka Nchini Afrika Kusini.

January 4, 2014

Ndege iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ilipowasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo Kutokea Nchini Afrika Kusini alipokutwa na Mauti siku chache zilizopita.

Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini

Naibu Waziri Wizara ya Fedha Saada Mkuya(kulia) akimsindikiza Mke wa Marehemu Mama Jane Mgimwa(katikati)katika chumba cha mapumziko mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo.Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa heshima kwa kugusa Jeneza Lililobeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu  Dkt. Willium Mgimwa Katikati ni Waziri wa Ujenzi Mh. John Magufuli na wa Mwisho ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Fenella Mukangara.

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ukiingizwa kwenye gari Maalum Tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa taratibu nyingine za mazishi.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (wa kwanza Kushoto)akisalimiana na baadhi wa Watu walifika kuupokea Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Leo Jijini Dar es Salaam.
   Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
January 04, 2014

CHADEMA YATOA MAELEZO KUHUSU PINGAMIZI ALILOWEKA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI-CHADEMA ZITTO KABWE MAHAKAMA KUU

 
 Mmoja wa wanachama watatu wa CHADEMA waliovuliwa nafasi zao za uongozi ndani ya chama, Zitto Kabwe kupitia kwa Wakili wake, Alberto Msando,jana ameanza kufanya ‘FORUM SHOPPING’ kwa kupeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, akiomba Kamati Kuu isijadili na kuamua jambo lolote kuhusu uanachama wake, kwenye kikao maalum kinachofanyika leo.

Awali muombaji kwa namna ambayo inaweza kuitwa kuwa ni kuvizia, alitaka Mahakama Kuu hiyo itoe amri kutokana na ombi lake hilo, bila upande wa chama kuwepo mahakamani, lakini kwa bahati nzuri mawakili wa chama, Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala; wakafanikiwa kuwepo kortini, hivyo wakawa-served maombi hayo kisha mahakama ikalazimika kusikiliza Preliminary Objections (PO) kutoka kwa mawakili wa CHADEMA dhidi ya waleta maombi.

Maombi hayo ya wakili Msando kwa niaba ya Zitto yamefunguliwa mahakamani dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama.

ASHANTI UNITED YATOKA SARE NA SPICE STARS HUKU MBEYA CITY IKICHEZEA KICHAPO TOKA KWA CLOVE STARS

January 04, 2014

Saturday, January 4, 2014 Na Mahmoud Zubeiry,Zanzibar.
 
ASHANTI United na Mbeya City zimejiweka pagumu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya jioni hii kupata matokeo yasiyofurahisha katika viwanja viwili tofauti visiwani Zanzibar.
Wakati Ashanti United inayofundishwa na kocha mkongwe Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ imetoa sare ya 1-1 na Spice Stars Uwanja wa Amaan, Unguja, Mbeya City ya Juma Mwambusi imefungwa mabao 2-1 na Clove Stars Uwanja wa Gombani, Pemba.   
Beki wa Spice Stars,Said Ahmed kushoto akiupitia mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Ashanti United, Kassim Kilungo jioni hii Uwanja wa Amaan

Huu ni mchezo wa kwanza Mbeya City inafungwa tangu ipande Ligi Kuu.
Uwanja wa Amaan, Ashanti ilitangulia kupata bao kupitia kwa Mnigeria, Ekee Brayton Oina dakika ya 21 katika mchezo wa Kundi C, kabla ya Abdillah Seif Bausi kuisawazishia Spice dakika ya 70.
Uwanja wa Gombani, Paul Nonga alitangulia kuifungia Mbeya City dakika ya tisa katika mchezo wa Kundi A, lakini Mwinyi Mngwali akaisawazishia Chuoni dakika ya 41 kabla ya George Thomas Mkoba kufunga la ushindi dakika ya 64.

Katika mchezo uliotangulia Saa 8:00 mchana wa Kundi A Gombani, URA ya Uganda iliitandika mabao 3-1 Clove Stars ya Pemba. 
Mabao ya URA yamefungwa na Owen Kasuule na Thery Ali mawili, wakati bao la Clove lilifungwa na Ahmed Ali Omar.
Kwa matokeo hayo, Ashanti inakuwa na pointi moja baada ya kucheza mechi mbili, hivyo inalazimika kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Azam FC keshokutwa ili kuweka matumaini ya kwenda Robo Fainali. 

Kwa Mbeya City nayo ina pointi moja baada ya kucheza mbili na sasa inalazimika kushinda mechi ya mwisho dhidi ya URA ili kuweka hai matumaini ya kwenda Robo Fainali.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT. WILLIAM MGIMWA

January 04, 2014
Saturday, January 04, 2014  
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni. 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Pia wageni wengine walipata fursa ya kusaini kitabu cha maombolezo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Dkt. Mgimwa, Jane Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
Baadhi ya Mawaziri na wabunge waliofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, leo.
Kwa hisani ya Sufianmafotoblog

PATO LA MKOA WA TANGA LAONGEZEKA TOKA TRILIONI 1.78 HADI TRILIONI 2.009

January 04, 2014
Na Oscar Assenga
Pato la Mkoa wa Tanga limeongezeka kutoka trilioni 1.78 hadi kufikia trilioni 2.099 kwa mwaka 2012 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 17.8.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mkoani hapa desemba 30 mwaka huu kuhusiana na mafanikio ya Mkoa wa Tanga ya mwaka 2012 hadi 2013.

MATUKIO KATIKA PICHA YA FAINALI YA MASHINDANO YA KOMBE LA MWIDAU CUP

January 04, 2014
Mbunge Amina Mwidau, akimkabidhi kikombe cha ushindi Nahodha wa timu ya APL Mwera Shabani Athuman, baada ya timu hiyo kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi ya Mwidau CUP, mjini Pangani jana

            Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akihutubia kabla ya kuchezwa kwa fainali kati ya timu ya APL Mwera na Torino (kulia) ni Katibu wa Chama cha Soka Wilaya ya Pangani, Salehe Swazi.

 
        Mgeni rasmi katika Mashindano ya Mwidau CUP, Amina Mwidau akijadiliana na viongozi wenzake wakati wa mchezo wa fainali ya Mwidau CUP kati ya APL Mwera dhidi ya Torino leo mjini hapa.

APL Mwera yaibuka kidedea Mwidau CUP

APL Mwera yaibuka kidedea Mwidau CUP

January 04, 2014
Na Mwandishi Wetu, Pangani

TIMU ya Soka la APL kutoka Kata ya Mwera, imetoka kifua mbele huku wakitangazwa mabingwa wapya wa kombe la Mwidau CUP.

Timu hiyo iliibuka na ushindi dhidi ya timu ya Torino ya mjini Pangani, ambayo ilishindwa kufua dafu kwa kufungwa kupitia penati.

Hadi dakika tisini za mchezo huo wa fainali hiyo ya Mwidau CUP zinamalizika timu zote zilishindwa kutambiana na kulazimika kutoka suluhu ya bao 1-1.
January 04, 2014

MADIWANI BUMBULI WAPEWA SOMO.

       (Katibu wa January Makamba(Hoza Mandia ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Milingano)
 
Na Raisa Said, Bumbuli
Imewekwa Januari 4.
MADIWANI  wa Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto wametakiwa kusimamia ipasavyo maazimio na mikakati wanayopitisha katika vikao vyao  ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo hilo.

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Bumbuli, January Makamba akizungumza katika mahojiano na waandishi wa Habari hivi karibuni kufuatia kikao maalumu cha wajumbe wa Kamati ya Madiwani wa CCM kilichoitishwa kwa niaba yake na Katibu wake Hoza Mandia.