COASTAL UNION YANASA SAINI YA BEKI WA KULIA WA RHINO RANGERS.

June 15, 2014
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
ALIYEKUWA beki wa kulia wa timu ya Rhino Rangers ya Tabora, Amani Juma amesaini mkataba wa kipindi cha miaka miwili kuitumika timu hiyo katika msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambao utaanza hivi karibuni hapa nchini.

Utiliaji saini ulifanywa na Katibu wa timu hiyo Coastal Union,Kassim El Siagi akiwa sambamba na  wajumbe wa kamati ya usajili ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo,Salim Amiri,Razack Yusuph "Kareka" na Salimu Bawaziri.


Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi alisema wana matumaini makubwa ya uwezo alionao mchezaji huyo itakuwa changamoto kubwa ya kuleta maendeleo kwenye kikosi hicho cha wagosi wa kaya ambacho kimedhamiri msimu ujao kufanya mageuzi kwenye ligi kuu.

El Siagi alisema mikakati mikubwa ya timu hiyo ni kuhakikisha wanafanya usajili wa nguvu ambao utawawezesha kufikia malengo yao ya kushiriki mashindano ya kimataifa ikiwemo kuchukua ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania.

Awali akizungumza, Amani alisema atahakikisha anatoa mchango wake mkubwa lengo likiwa kuipa mafanikio timu hiyo kwenye michuano ya ligi kuu msimu ujao ikiwemo kuomba ushirikiano kutoka kwa viongozi na wachezaji wenzake ili kutimiza malengo hayo.

PICHA: MICHEZO YA UMITASHUMTA IKIENDELEA JIJINI TANGA KWA SHULE ZOTE ZA MSINGI MKOANI HAPO.

June 15, 2014









WAZIRI WA UCHUKUZI DK. HARISON MWAKYEMBE AZINDUA LIGI YA BODABODA MBEYA

June 15, 2014

WAZIRI wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe akiongea na waendesha bodaboda jiji la Mbeya  kabla ya kuzindua  ligi ya bodaboda
WAZIRI wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe akipiga mpira teke kuashiria kuzinduliwa kwa ligi ya bodaboda jijini Mbeya
Kabla ya uzinduzi huo wa ligi ya bodaboda kulitangulia maandamano ya waendesha bodaboda yalioanzia Kabwe mpaka kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe
WAZIRI wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe ambae ndiye mgeni rasmi akipokea maandamano ya waendesha bodaboda wa jiji la Mbeya
Baadhi ya ya wazee wa jiji la Mbeya walishiriki katika uzindunzi wa bodaboda cup
WAZIRI wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe akimtunza fedha moja ya waimbaji waliotumbuiza katika uzinduzi wa bodaboda cup
*BALOZI SEIF IDDI ABARIKI TAMASHA LA 17 LA ZIFF 2014 VISIWANI ZANZIBAR.

*BALOZI SEIF IDDI ABARIKI TAMASHA LA 17 LA ZIFF 2014 VISIWANI ZANZIBAR.

June 15, 2014

DSC_0157
Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya wageni alipowasili kwenye ufunguzi wa Tamasha la 17 la ZIFF Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
DSC_0159
Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto ambayo ilifungua tamasha hilo la 17 la ZIFF usiku wa kuamkia leo visiwani Zanzibar.
DSC_0158
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed Jeneby wakati wa tamasha hilo.
DSC_0164
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.
DSC_0174
DSC_0234
Pichani juu na chini ni kikundi cha burudani cha TANURI kutoka Egypt wakitoa burudani kwenye tamasha la 17 la ZIFF.
DSC_0300
DSC_0289
DSC_0386
Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akimkaribisha mgeni Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto kwenye jukwaa.
DSC_0391
Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto akielekea jukwaani wakati wa ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF 2014.
DSC_0391
DSC_0395
Picha juu na chini Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto, akizungumzia changamoto mbalimbali na mafanikio aliyoyapata baada ya kushiriki kwenye filamu hiyo.
DSC_0409
DSC_0414
Mmoja wa wageni waalikwa akimpongeza mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto kwa kazi nzuri aliyofanya kupitia filamu yake.
DSC_0217
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais Balozi Sefu Iddi jukwaani kuzindua rasmi tamasha hilo.
DSC_0213
Mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisoma hotuba wakati akizindua rasmi wa Tamasha la 17 la filamu la nchi za Majahazi (ZIFF) linaloendelea kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.
DSC_0344
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) akimtambulisha mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed (kulia) kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi.
DSC_0348
Mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed akikambidhi zawadi ya kifurushi cha Internet ya mwaka mzima mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi .
DSC_0351
Mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akimshukuru mwakilishi wa Com-net mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo kwa zawadi hiyo.
DSC_0332
Mkurugenzi Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed Jeneby akizungumzia udhamini wao wa miaka 10 kwenye tamasha hilo ambapo kwa sasa lina mwaka wa tatu.
DSC_0490
Meza kuu ikifuatilia filamu ya "Long Walk to Freedom" inayozungumzia maisha ya MANDELA wakati wa ukombozi wa mtu mweusi kutoka kwa makaburu.
DSC_0375
Mwigizaji Terry Pheto akifurahia jambo wakati wa kutazama filamu yake.
DSC_0342
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.
DSC_0370
Picha juu na chini wakazi wa Zanzibar na wageni mbalimbali kutoka nje ya Tanzania wakitazama filamu ya "Long Walk to Freedom kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF.
DSC_0317
DSC_0316
DSC_0431
Mwigizaji Terry Pheto akipozi na mmoja wa ushers waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye tamasha hilo.
DSC_0574
Mdau Lucy (wa pili kushoto) katika pozi na picha yake kwenye viunga vya Ngome Kongwe wakitoa huduma ya vinywaji.
(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIAJI DAMU SALAMA KITAIFA ILIYOFANYIKA KIGOMA.

MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIAJI DAMU SALAMA KITAIFA ILIYOFANYIKA KIGOMA.

June 15, 2014

IMG_0029
IMG_0078Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshuhudia Ndugu Mariam Juma,42, mkazi wa Shirika Mnarani huko Kigoma akitolewa damu wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya waqchangiaji damu iliyofanyika kitaifa huko Kigoma tarehe 14.6.2014. Katikati ni Ndugu Franco Mwikwa, Afisa mtoa damu salama kutoka ofisi ya Kanda ya Magharibi yenye makao yake makuu mjini Tabora. IMG_0082Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshuhudia Ndugu Mariam Juma,42, mkazi wa Shirika Mnarani huko Kigoma akitolewa damu wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya waqchangiaji damu iliyofanyika kitaifa huko Kigoma tarehe 14.6.2014. Katikati ni Ndugu Franco Mwikwa, Afisa mtoa damu salama kutoka ofisi ya Kanda ya Magharibi yenye makao yake makuu mjini Tabora. IMG_0104Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa mji wa Kigoma waliokuwa kwenye maandamano ya kuadhimisha kilele cha siku ya wachangiaji damu salama zilizofanyika kitaifa mjini hapo tarehe 14.6.2014. Wengine katika picha ni (kulia kwenda kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, Mheshimiwa Margareth Sitta, Mbunge na Mwisho ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Ndugu Walid Kabourou. IMG_0129Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa mji wa Kigoma waliokuwa kwenye maandamano ya kuadhimisha kilele cha siku ya wachangiaji damu salama IMG_0131Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakipita kwa furaha mbele ya mgeni wa heshima wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu duniani iliyoadhimishwa kitaifa huko Kigoma ambapo Mama Salma alikuwa Mgeni rasmi. IMG_0152Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakipita kwa furaha mbele ya mgeni wa heshima wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu duniani iliyoadhimishwa kitaifa huko Kigoma ambapo Mama Salma alikuwa Mgeni rasmi. IMG_0196Wacheza ngoma kutoka wilaya ya Makamba nchini Burundi walioalikwa kwenye maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama wakicheza ngoma ya utamaduni  kwa umahiri mkubwa.IMG_0250Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama kitaifa Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwenye uwanja wa Lake Tanganyika taehe 14.6.2014. IMG_0276Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi mfumo wa Kuhifadhi kumbukumbu za wachangiaji damu Tanzania  (Blood Establishment Computer system-BSCF) wakati wa Maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama duniani kwenye sherehe zilizofanyika kitaifa huko Kigoma tarehe 14.6.2014. IMG_0298Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi tuzo Ndugu Emmanuel Essay, Mfanyakazi wa KCMC inayotolewa na Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa mwanaume aliyechangia damu kuliko wote hapa nchini kwa mwaka 2013/14. Ndugu Essay ametoa damu mara 53 katika kipindi hicho. IMG_0303Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa tuzo kwa Ndugu Restituta Mushi  kwa kuwa mwanamke aliyechangia kutoa damu salama kuliko wanawake wote hapa nchini katika mwaka2013/14. Restituta anatoka katika Mkoa wa Mwanza na ameweza kutoa damu mara 28 katika kipindi hicho. IMG_0383Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kucheza pamoja na wananchi waliokuwa wakiwaburudisha wananchi wa Kigoma waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama iliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika tarehe 14.6.2014.
IMG_0388Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kucheza pamoja na wananchi waliokuwa wakiwaburudisha wananchi wa Kigoma waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama iliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika tarehe 14.6.2014.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI