RAIS KIKWETE APIGA KURA KIJIJINI KWAKE MSOGA

RAIS KIKWETE APIGA KURA KIJIJINI KWAKE MSOGA

October 25, 2015

1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika foleni akisuburi zamu yake ya kupiga kura leo katika kituo cha hospitali ya kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo  Oktoba 25, 2015.
2
Ofisa katika kituo cha kupigia kura katika kituo cha hospitali ya kijiji cha Msoga akihakiki kadi ya kupiga kura ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
3 4
Ofisa katika kitu cha kupiga kura akimkabidhi Rais Kikwete karatasi za kupiga kura.
5
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiandika kura yake ya siri.
7 8
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura ya Rais Mbunge na Diwani katika kituo cha kupiga kura cha hospitali ya kijiji cha Msoga,Kata ya Msoga wilayani Bagamoyo Oktoba 25, 2015.
9
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwekwa wino na msimamizi wa kituo unaotambulisha kuwa amepiga kura.
(Picha na Freddy Maro) 

MKE WA RAIS MAMA SALMA APIGA KURA KATIKA KITUO CHA MTANDA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

October 25, 2015

Mama Salma Kikwete akisubiri kadi inayokaguliwa na msimamizi wa Kituo alichojiandikisha na hatimaye kupiga kura  katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Mtanda Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mjini.
Mama Salma akisubiri moja ya fomu za kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani
Msimamizi wa kituo akiangalia picha ya Mama Salma katika dafutari la wapigakura
Mama Salma akiweka tiki kumchagua kiongozi BORA.
Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Diwani.
Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Mbunge.
Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Rais.
Mama Salma akiwekwa vino na msimamizi wa kituo unaotambulisha kuwa amepiga kura.
Mama Salma akiwatakia kila la heri wananchi wanaotarajia kupiga kura kituoni hapo
Wananchi wakiwa katika mstari tayari kuelekea kupiga kura.
Wananchi wakiwa katika mstari tayari kuelekea kupiga kura.
Mama Salma akiagana na baadhi ya wananchi Uwanja wa Ndege wa Kikwetu Lindi.
Mama Salma akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Jordan Rugimbana.
Mama Salma akipanda Ndege  na kuwapungia mkono Maofisa waliopo Uwanja wa Ndege Kikwetu Lindi  tayari kuelekea Dar es Salaam baada ya kupiga kura.
DK.SHEIN APIGA KURA KITUO CHA BUNGI.

DK.SHEIN APIGA KURA KITUO CHA BUNGI.

October 25, 2015

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija (kushoto) wakati alipowasili katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi msingi wilaya ya Kati Unguja.Oktoba 25, 2015.
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika foleni ya wapiga kura katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo,(wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija.
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akipokea karatasi ya kupigia kura kutoka kwa Afisa Sibira Ramadhan Iddi katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika.
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
6
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akifanya mahojiano na waandishi wa habari baada ya kipiga kura leo katika kituo cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja,
8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija(kushoto)baada ya kupiga kura katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo,(kulia)Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdalla Ali,
[Picha na Ikulu.]

MTONI KIJICHI, MBAGALA WENGI WAJITOKEZA KUPIGA KURA KWA UTULIVU NA AMANI JIJINI DAR ES SALAAM

October 25, 2015

 Rukia Omari (kushoto), akimsaidia kupiga kura jamaa yake Mwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho wakati wa kupiga kura katika kituo cha Mbagala Misheni Dar es Salaam leo asubuhi.
  Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shimbwe Mbagala Kuu.
 Hapa wakihakiki majina yao.
 Mkazi wa Njia ya Ng'ombe Mbagala Kuu, Sarah Simba akipiga kura katika kituo cha Shimbwe Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kuwachagua viongozi wake, Rais, Mbiunge na Diwani.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mbagala Kuu.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Bwawani Mtoni Kijichi leo asubuhi.
 Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.

 Wasimamizi wa uchaguzi katika kituo cha Mbagala Misheni wakiwa kazini.
Msimamizi wa uchaguzi Mkuu katika kituo cha Mbagala Misheni, Yona Komba (kulia), akimpaka winoMwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho baada ya kumaliza kupiga kura katika kituo hicho Dar es Salaam  leo asubuhi. Kushoto ni binti aliyemuomba amsaidie kupiga kura  Rukia Said.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)