January 25, 2014

*BREAKING NEEEWZZZZ!!!!! NDEGE YA ZAN AIR YAANGUKA PEMBA

Ndege ya shirika la Zan Air imeanguka Pemba jioni hii ikiwa imebeba jumla ya abiria 19, miongoni mwa abiria hao pia alikuwamo Waziri wa Habari na Katiba wa Zanzibar mhe. Abubakar Kahamis, abiria wote wametoka salama.
 
Source:Sufianimafoto.com

COASTAL UNION ,OLJORO JKT ZASHINDWA KUTAMBIANA ZATOKA SARE YA BAO 1-1.

January 25, 2014

                      Kikosi cha leo kilichomenyana na JKT Oljoro uwanja wa Mkwakwani leo.

                   Viongozi wa Coastal Union wakifuatilia mechi ya leo uwanja wa Mkwakwani.

 Meneja wa Coastal Union akitaniana na Kocha wa JKT Oljoro Hemed Morocco kabla ya mchezo leo.

                     Atupele Green akimtoka mchezaji wa JKT Oljoro uwanja wa Mkwakwani leo.

 Kenneth Masumbuko, akitafuta mbinu za kumtoka Nurdin Mohammed wa JKT Oljoro katika uwanja wa Mkwakwani leo.

                                                             Yayo Kato Lutimba

COASTAL UNION,OLJORO JKT HAKUNA MBABE,ZATOKA SARE YA BAO 1-1

January 25, 2014


Na Oscar Assenga,Tanga.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga leo imeshindwa kuutimia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare na Oljoro JKT ya Arusha kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa                  pili.
Mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la soka Mkwakwani ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko Coastal Union walikuwa wakiongoza bao 1-0.

Bao ambalo lilifungwa na Yayo Lutimba aliyeunganisha pasi nzuri iliyopigwa na Hamadi Hamisi bao ambalo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Coastal Union na Oljoro JKT waliingia kwenye ngwe hiyo kwa kila timu kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake.

Wakicheza kwa kujituma na umakini mkubwa Coastal Union waliweza kutawala mchezo huo mpaka dakika ya 75 ya kipindi cha pili ambapo nao wapinzani wao walipocharuka.

Baada ya kucharuka Oljoro JKT waliweza kucheza pasi fupi fupi na ndefu wakitumia udhaifu wa wapinzani wao na ndipo walipofanikiwa kuandika bao la kusawadhisha kwenye dakika ya 87 kupitia Hamis Salehe.

Hata hivyo mechi ya leo ilikuwa haina mashabiki wengi kwa kile kilichoelezwa kuwa mfumo wa kielectroniki ulichangia kuwepo kwa hali hiyo.

Kikosi cha Coastal Union leo gk Said Lubawa,Hamadi Hamisi,Othumani Tamimu,Juma Nyoso,Jerry Santo,Mbwana Hamisi,Atupele Green,Razack Khalifani,Yayo Lutimba,Daniel Lyanga na Keneth Masumbuko.

Kwa upande wa JKT Oljoro gk Mohamed Ally,Paul Malipesa,Ally Omari,Nurdin Mohamed,Sabri Makame,Babu Ally,Jacob Massawe,Azizi Shaweji,Amiri Omari,Shija Mkina na Majaliwa Shabani.
 
Michezo mengine iliyochezwa kwenye ligi hiyo ni Ashanti United walicheza na Yanga ambapo mpaka dakika 90 Yanga 2-1 Ashanti United.

Mabao ya Yanga yakifungwa na Didier Kavumbangu na David Luhende dakika ya 51 na 82 na la Ashanti United limefungwa Bright Obinna dakika ya 61

Kwenye dimba la Chamazi,Azam Fc waliibika na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar bao likifungwa na Kipre Tchetche.
Hali kadhalika Mbeya City nao waliibuka na ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye dimba la soka Katiba Bukoba  bao hilo likifungwa na Swita Julius

UHARIBIFU WA MAZINGIRA UNACHANGIA KUPUNGUA KWA MAKUNDI YA NYUKI MKOANI TANGA.

January 25, 2014
Na Oscar Assenga, Tanga.
IMEELEZWA kuwa uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti ovyo,uchomaji wa moto misitu ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji husababisha kupungua kwa makundi ya nyuki mkoani Tanga.

Kauli hiyo alitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku
  Gallawa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake hivi karibuni ofisini kwake ambapo alisema changamoto nyingine ni uhaba wa maafisa ugani katika mamlaka za serikali za mitaa.

TFF,UONGOZI WA UWANJA WA MKWAKWANI WAJIPANGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KIELECTRONIKI LEO.

January 25, 2014
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga,Gustav Mubba(kushoto)akizungunza na waandishi wa habari jana na kulia ni Meneja wa uwanja huo,Mbwana Msumari.
Oscar Assenga,Tanga.
Shirikisho la Soka nchini TFF kwa kushirikiana na uongozi wa uwanja wa Mkwakwani limejipanga kubaliana na changamoto zitakazojitokeza katika mchezo wa leo kuhusiana na tiketi za Kielektroniki.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana uwanjani
  hapo,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF,Khalid Abdallah  na katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga,Gustav Muba walisema wamejipanga kukabiliana na changamoto hizo.

Khalid ambaye pia ni msimamizi wa ligi kuu Vodacom,kituo cha Tanga
  alisema baada ya kukamilika kwa matengenezo ya uwanja wa Mkwakwani kuna changamoto ambazo zitajitokeza kutokana na ukweli kwamba milango iliyoandaliwa ni miwili tu.

“Tatizo ni kwamba wawekaji wa mashine za kielektroniki wameweka mageti
  mawili tu ambayo kwa uzoefu ukataji wa tiketi hautatosheleza idadi ya mashabiki watakaoingia”alisema Khalid.

MKWAKWANI UPO TAYARI KWA LIGI KUU LEO.

January 25, 2014
Kutoka kushoto ni Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani,Mbwana Msumari akitoa ufafanuzi kwa katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM)Gustav Muba kuhusu maandalizi ya uwanja huo kabla ya kuanza ligi leo.