RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SOKO LA CRDB KIZIMKAZI DIMBANI,KUSINI UNGUJA ZANZIBAR

August 29, 2023

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (watatu kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (kushoto) wakifanya tukio la uzinduzi wa ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (watatu kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (kushoto) wakifanya tukio la uzinduzi wa ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (katikati) akipata maeleo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa kuhusu ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
 
======   ======   =======

 Kizimkazi, Zanzibar, 29 Agosti 2023: Katika juhudi za kuendelea kuwezesha jamii inayoizunguka kupitia sera yake ya uwekezaji kwa jamii, Benki ya CRDB kupitia Tasisi yake ya CRDB Bank Foundation inatarajia kujenga soko la kisasa katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja visiwani Zanzibar. Hafla ya kuweka jiwe la msingi la soko hilo imefanyika katika eneo la Kizimkazi Dimbani kama sehemu ya shamra shamra za tamasha la Kizimkazi na kuhududhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko hilo, Rais Dkt. Samia ameishukuru Benki ya CRDB kwa kukubali ombi la Mkoa wa Kusini kujenga soko hilo la kisasa ambalo litachochea maendeleo ya watu wa Kizimkazi na Mkoa wa Kusini Unguja kwa ujumla.
“Mwaka jana kama mnakumbuka mlinipa kilio hiki cha soko la jamii ya Kizimkazi. Sasa mimi nikalitupa Mkoa ambapo na wao wakalipeleka CRDB na leo wako hapa kwenye field tayari kuweka jiwe la msingi na ujenzi unaendelea. Kwa hiyo tuwashukuru sana CRDB kwa kutushika mkono katika hilo na haya ndo maendeleo ya Kusini tuliyoyasema na ndo madhumuni ya tamasha letu hili la Kizimkazi” alisema Rais Dkt. Samia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kwa kutambua uchumi wa watu wa kusini unatemegea sana uvuvi, Benki chini ya Taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeamua kuwekeza katika ujenzi wa soko la kisasa ambalo litakwenda kuongeza thamani katika biashara kwa wakazi wa eneo la Kizimkazi. Katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa soko, Benki imetenga takribani Shilingi Milioni 157.8 na tayari ujenzi wa sehemu ya kwanza tayari umeanza.

“Kwa muda mrefu Benki ya CRDB imekua mdau mkubwa wa maendeleo ya Kizimkazi kupitia tamasha la Kizimkazi ambapo hadi kufikia tamasha la mwaka huu, Benki ya CRDB imeshafanya uwekezaji wa takribani Shilingi Bilioni 1 na soko hili la kisasa la Samaki litaghrarimu zaidi ya Bilioni 2 hadi kukamilika kwake ambapo sehemu ya kwanza ya ujenzi itakamilika mnamo mwezi Oktoba 2023” amesema Nsekela.
Mbali na utoaji wa huduma za fedha kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano, Benk ya CRDB pia imekua ikitekeleza sera yake ya uwekezaji katika jamii katika pande zote mbili. Sera hiyo ya uwekezaji katika jamii inaelekeza 1% ya faida kurejeshwa katika jamii katika maeneo ya elimu, afya, mazingira na uwezeshaji kwa wanawake na vijana.

“Mbali na ujenzi wa soko hili la kisasa, Benki kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeendelea na dhamira yake ya kuleta mageuzi katika mchezo wa Resi za Ngalawa ambapo katika tamasha la Kizimkazi la mwaka 2023, Benki imewekeza zaidi ya Milioni 119.5 katika mashindano ya Resi za Ngalawa ambazo ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi” aliongeza Nsekela.
Mwaka 2021, Benki ya CRDB ilikua mdhamini kuu wa Tamasha la Kizimkazi kwa kugharamia tamasha lote asilimia kuanzia mafunzo kwa wajasiriamali, michezo, maonyesho ya wafanyabiashara hadi kilele cha tamasha. Mbali na hilo Benki ilifadhili ujenzi wa nyumba za madaktari na Ofisi ya Sheha.

Mwaka 2022, Benki ya CRDB ilijenga maabara ya Shule ya Sekondari ya Kizimkazi pamoja na kununua vifaa vyake vya maabara. Sambamba na hilo Benki ilifadhili michezo yote na zaidi kuleta mapinduzi katika mchezo wa Resi za Ngalawa ambapo uliweza kuvutia watu wengi zaidi na kutoa zawadi kubwa zilizoweza kubadili maisha ya wana Kizimkazi ikiwemo zawadi kubwa ya boti ya kisasa yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 kwa mshindi.





MBUNGE MAIMUNA PATHANI UTAJIRI WA LINDI UPO KWENYE MADINI

August 29, 2023

 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan akiongea wakati wa kongamano la madini lililofanyika katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi huku akielezea fursa mbalimbali zinazotokana na upatikanaji wa madini katika mkoa huo.


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan amesema Lindi utakuwa mkoa tajili Tanzania kutokana na uwepo wa madini ya Kila aina katika ardhi ya mkoa huo.


Akizungumza wakati wa kongamano la madini lililofanyika katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi,Mbunge Maimuna Pathan alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Lindi wanatakiwa kuzitumia vilivyo fursa za uwepo wa madini katika ardhi ya mkoa huo ambao utakuza uchumi wa taifa zima.


Pathan alisema kuwa baada ya miaka mitano kila mtu anatakuwa anazungumzia utajiri wa madini uliopo katika katika mkoa wa Lindi tofauti na ilivyokuwa awali.


Aliwataka wananchi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa zote zilizopo kwenye sekta ya madini ili kukuza uchumi wao na kupata maendeleo kutokana uwepo wa madini mbalimbali.


Pathan alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na utunzaji wa mazingira kwenye maeneo ambayo madini yanachimbwa 

PROF. MBARAWA: WAKANDARASI ONGEZENI WATAALAM NA MITAMBO KAZI ZIENDE HARAKA

August 29, 2023



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akipata ufafanuzi toka kwa mhandisi mkazi anayesimamia ujenzi wa barabara ya Tungumaa-Mkwaja-Mkange KM 95.4 alipokagua ujenzi wa barabara hiyo inayounganisha wilaya za Handeni, Bagamoyo na Pangani mkoani Tanga.

Muonekano wa moja ya daraja katika barabara ya Tungumaa-Mkwaja-Mkange KM 95.4 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa mkandarasi M/s Shandong Luqiao Group Ltd anayejenga daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 na barabara za maingilio takriban KM 25 mjini Pangani

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Pangani ambaye pia ni waziri wa maji mhe. Jumaa Aweso alipokagua ujenzi wa daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525.


Muonekano wa baranbara ya Tanga–Pangani KM 50 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewataka wakandarasi wanaojenga barabara za Tanga-Pangani KM 50, Tungumaa-Mkwaja-Mkange KM 95.4 na daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 mkoani Tanga kuongeza wataalam na mitambo ili kuharakisha kazi za ujenzi huo.


Prof. Mbarawa amesema Serikali haitasita kuchukua hatua za kimkataba kwa mkandarasi yeyote anayeshindwa kuajiri wataalam sahihi na wakutosha na hivyo kusababisha miradi kuchelewa kumalizika na kuwanyima wananchi fursa ya kunufaika na miradi hiyo mapema.

“Tunaleta fedha na tutaendelea kuleta kwa awamu hivyo hakikisheni wataalam stahiki wapo site na mitambo ifike kwa wakati ili kulinda dhana ya value for money”, amesema Prof. Mbarawa.

Amewataka wakandarasi M/s China Henan International Cooperation Group Co. Ltd anayejenga barabara ya Tanga-Pangani, KM 50, China Railway 15 Bureau Group Corporation anayejenga barabara ya Tungumaa-Mkwaja-Mkange KM 95.4 na M/s Shandong Luqiao Group Ltd anayejenga daraja la Pangani mita 525 na barabara za maingilio takriban KM 25 mjini Pangani kufanya kazi kwa bidii na viwango vya juu ili kukidhi matarajio ya watanzania.

Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua ushoroba wa mwambao wa bahari ya hindi na kukuza uchumi wa wakazi wa mikoa ya Tanga,Pwani na Dar es salaam.

Kwa upande wake Mbunge wa Pangani ambae pia ni Waziri wa maji Mhe. Jumaa Aweso ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa inaoufanya mkoani Tanga na kuwataka wananchi wa maeneo inapopita miradi ya ujenzi kuchangamkia fursa za ajira, ujuzi na biashara.

Naye meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Eng. Eliazary Rweikiza amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa wataalam wamejipanga vizuri kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa ubora na kuleta tija kwa taifa.

Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya siku mbili mkoani Tanga kukagua miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja ikiwa ni mkakati wa kuwakumbusha wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wakati huu ili kuepuka visingizio vya kuchelewesha miradi pindi mvua za vuli zitakapoanza kunyesha baadae mwezi Oktoba.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI