COASTAL UNION KUTUMIA PIPA KESHO KUELEKEA PEMBA.

August 18, 2014


TIMU ya Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kundoka mkoani hapa Jumanne kuelekea Kisiwani Pemba kwa ajili ya kuweka kambi ya Mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Akizungumza na Tanga Raha Blog leo katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa kambi hiyo itawekwa visiwani humo mahali pamoja na kufanyia mazoezi kwa timu hiyo kwenye uwanja wa Migombani kila siku.

El Siagi alisema kuwa kikosi cha wachezaji wapatao 25 ikiwemo Benchi la Ufundi litakuwa na watu watano ambao wataelekea visiwani humo wakiwa na lengo la kukisuka kikosi hicho kwa ajili ya kuleta ushindani msimu ujao.

Alisema katika benchi la ufundi litakuwa na Kocha mkuu Yusuph Chipoo,Kocha Msaidizi Benard Mwalala na Kocha wa makipa Razack Siwa,Daktari wa timu pamaoja na Kiti meneja.

Aidha alisema msafara wa timu hiyo utaondoka mapema mkoani hapa siku hiyo kwa ajili ya kwenda kuanza kambi mpya ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara.
KAAT WAJITAMBULISHA KWA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

KAAT WAJITAMBULISHA KWA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

August 18, 2014

????????
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akiwakaribisha viongozi wa KAAT walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba na Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
????????
Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar. Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
????????
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akifurahia jambo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
????????
Bw. Bukheti Juma (Kulia) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar) akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba akiwasikiliza.
????????
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akitilia mkazo umuhimu wa jamii kusaidia wazee wasiojiweza, wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
????????
Baadhi ya wanachama wa KAAT wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Katikati).
………………………………………………………………………….
Na Saidi Mkabakuli
*Yadhamiria kuwasaidia wazee wasiojiweza
Uongozi mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT) wamekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Zanzibar na kutoa ombi rasmi la kuharakishwa kwa kufunguliwa kwa Ofisi za Kibalozi nchini Korea Kusini.
Wakizungumza mara baada ya kukaribishwa na Mhe. Balozi Iddi, Rais wa KAAT, Bw. Stephen Katemba alitoa wito kwa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kufikiria kufungua ubalozi nchi Korea Kusini kwa kuzingatia umuhimu wa nchi hiyo katika uchumi wa Tanzania.
Bw. Katemba alisema kuwa kufunguliwa kwa ubalozi huo kutaongeza chachu ya mahusiano ya kibiashara na kindugu baina ya nchi hizi mbili zenye urafiki wa hali ya juu.
“Tunakosa fursa nyingi za kufanya biashara na Korea Kusini kwani wengi wa wafanyabiashara wa Korea Kusini tuliokutana nao nchini humo wanaona usumbufu kufuata huduma za kibalozi nje ya nchi yao,” alisema Bw. Katemba.
Kwa mujibu wa Bw. Katemba, Korea Kusini ina soko kubwa kwa bidhaa za Tanzania ikiwemo bidhaa za vyakula na matunda, pia Tanzania ina fursa kubwa ya kupata ujuzi hasa kwenye eneo la kiteknolojia na ujenzi.
Kwa upande wake Balozi Iddi, alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu na fursa zilizopo nchini Korea, na kuahidi kulifanyia kazi ombi hilo.
Wakati huo huo, katika kutimiza wajibu wa kusaidia wazee na watu wasiojiweza, uongozi mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT) upo mbioni kufanyia matengenezo nyumba za kukaa wazee za Sebuleni, mjini Zanzibar.
Akizungumzia mpango huo, Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar), Bw. Bukheti Juma amesema “KAAT inatambua mchango mkubwa wa wazee nchini Tanzania, hivyo katika kuhakikisha wanaishi katika mazingira safi na salama, KAAT tutafanyia matengenezo baadhi ya majengo yaliyo kwenye hali mbaya kituoni hapo,” alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Juma zoezi hilo linatarajiwa kufanywa katikati ya mwezi ujao.
Warembo wa Miss Tanzania kuvaa nguo za S &D Collection

Warembo wa Miss Tanzania kuvaa nguo za S &D Collection

August 18, 2014

DSC_0307
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga akimtambulisha Mkurugenzi wa Kampuni ya S&D Collection iliyotangaza udhamini wa shindano la Miss Tanzania Bi. Devotha Kajogoo Mtambo kulia wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hotli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam.
DSC_0341
Mkurugenzi wa Kampuni ya S&D Collection Bi. Devotha Kajogoo Mtambo akisisitiza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hotli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na kulia ni Bi.Esther Maro Mkurugemzi wa S&D Collection 
…………………………………………………………….
Na Majuto Omary
Kampuni ya S &D collection kwa upande wa Boutique imetangaza udhamini wa nguo kwa warembo wote 30 watakao wania taji la Miss Tanzania 2014  watakaopambana mwezi  Oktoba jijini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jumatatu, mkurugenzi wa S&D Collection, Devota Kijogoo Mtambo alisema kuwa hatua ya kudhamini mashindano hayo ni kujihusisha katika shughuli za kijamii mbali ya kujitangaza kupitia jukwaa hilo.
Devota alisema kuwa warembo wote 30 watazawadiwa nguo kuanzia shoo ya ufunguzi, vazi la  ubunifu, ufukweni na warembo watano watakaoingia katika hatua ya fainali. Alisema kuwa pia watadhamini nguo za mshindi wa taji la Miss Tanzania ambaye ataiwakilisha nchi katika mashindano ya mwakani ya kumsaka mrembo wa dunia.
“Lengo letu ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Kampuni ya Lino International Agency ya kuendeleza mashindano ya urembo hapa nchini, ni mashindano makubwa na ndiyo maana sisi tumeingia kutokana na ubora wake na ubora wa bidhaa zetu,” alisema Devota.
Alisema kuwa kampuni yao itatumia si chini Dola za Kimarekani 27,000 (zaidi ya Sh Milioni 44) kwa ajili ya nguo za warembo hao.
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga aliipongeza kampuni hiyo kwa kudhamini mashindano hayo na wameikubali kutokana na uwekezaji wake katika shughuli hiyo.
“Mashindano yetu ni makubwa, kampuni ya S&D Collection ni kubwa na imewekeza vilivyo katika mashindano yetu, hii itasaidia kuongeza ubora huku warembo wakipata hafueni kwani hawataingia katika gharama za mavazi,” alisema Lundenga.
Alisema kuwa kwa sasa wanaendelea na mashindano ya Kanda kabla ya kuanza maandalizi ya kambi ya Taifa mara baada ya kukamilika kupatikana kwa warembo wote 30.