MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA'

September 23, 2017
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizindua kampeni ya upandaji miti ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo Septemba 23,2017-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
*****
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack amezindua kampeni ya upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ili kuboresha mazingira  Shinyanga na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa. 
Kampeni hiyo inayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, imezinduliwa leo Jumamosi Septemba 23,2017 katika manispaa ya Shinyanga ,kwa lengo la kuboresha mazingira ya mji wa Shinyanga,maeneo ya taasisi,maeneo ya wazi,maeneo yanayozunguka kaya,kandokando ya barabara na sehemu zingine ambazo hazina miti. 
Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni hiyo,Telack alisema kutokana na mvua haba katika mkoa wa Shinyanga, kumekuwepo na mabadiliko ya tabia nchi hali inayosababisha kuwepo na hali ya jangwa. 
Telack aliwataka wananchi na wadau wote kuhakikisha wanatunza miti hiyo na kuzuia mifugo kuzurura ovyo mitaani. 
“Tutakuwa wakali,kuanzia sasa ni marufuku kwa mifugo kuzurura mitaani,ikikamatwa kwa kila mfugo faini ni kati ya shilingi 50,000/= na 100,000/=,iwe ng’ombe,mbuzi,kondoo au punda, tukikuta mti umekauka faini ni shilingi 50,000/=”,alieleza mkuu huyo wa mkoa. 
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro alisema uzinduzi wa kampeni hiyo umeanza na barabara 25 za mji wa Shinyanga ambapo jumla ya miti 3000 imepandwa na ofisi zote kata 17 za manispaa ya Shinyanga zitaendelea kutekeleza zoezi hilo. 
“Kampeni hii ni kwa wilaya ya Shinyanga,leo tumeanza katika manispaa ya Shinyanga,tunataka wilaya yetu iwe na mandhari nzuri ya kuvutia,ardhi iboreke,tuzuie upepo mkali katika majengo,tuhifadhi vyanzo vya maji,kuongeza vivuli katika maeneo ya kupumzikia,kujinasua na athari za mabadiliko ya tabia nchi lakini pia jamii itanufaika na miti ya matunda itakayopandwa”,alifafanua Matiro. Alibainisha kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,sasa wilaya hiyo imekuja na teknolojia rahisi ya kumwagilia miti kwa njia ya matone,teknolojia ambayo inatumia maji kidogo lakini inaweza kumwagilia miti mingi na kwa muda wote.
“Tumekuwa tukipanda miti kila mwaka lakini miti hii ilikumbwa na changamoto nyingi wakati wa usimamizi na kusababisha miti mingi kufa,kwa sasa tumekuja na mpango huu mpya wa kupanda miti itayosimamiwa na wananchi na wadau wote”,alieleza Matiro. 
Alisema kauli mbiu hiyo ya Upandaji miti ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ina maana ya kuwaasa watu wote wa Shinyanga kuachana na tabia ya kuharibu miti na hivyo wahifadhi miti. 
“Tutatekeleza kampeni hii katika halmashauri zote,kila halmashauri itaanzisha kitalu na kuzalisha miche isiyopungua 25,000,kila kata ipande miti isiyopungua 1000 na iwe na kitalu cha kudumu,ofisi za mitaa na vijiji miti 100,vitongoji miti 50,kila mwananchi miti isiyopungua mitatu na taasisi zote zipande miti”,alifafanua Matiro.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha kampeni hiyo,taasisi mbalimbali zitachangia mbegu,miche na kupanda miti ili kufikia lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1,500,000 kwa mwaka.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya upandaji miti ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro wakati wa uzinduzi huo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya upandaji miti ambapo alisema miongoni mwa malengo yake ni kuhifadhi ardhi na kuiongezea thamani,kuzuia mmomonyoko wa adhi na kuboresha mazingira
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.Alieleza kuwa kila kiongozi akialikwa kwenye tukio lolote,kabla ya shughuli ni vyema kwanza apande mti.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akisisitiza kuwa kampeni hiyo inalenga kujinasua na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Wananchi wakiwa wameshikilia vijiti vinavyotumika katika zoezi la upandaji miti.
Uzinduzi unaendelea
Mdau wa Mazingira Ezra Manjerenga akieleza namna ya kupanda miti hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akipanda mti nje ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakishuhudia mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akipanda mti.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akichomeka vijiti kwenye mti aliopanda.
Meneja wa Benki ya CRDB,Said Pamui akipanda mti nje ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 'Shinyanga mpya,mti kwanza'.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB na wananchi wakishuhudia Meneja wa Benki ya CRDB,Said Pamui akipanda mti.
 MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI

MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI

September 23, 2017
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga ametangaza kikosi kipya kitakachocheza na Malawi ‘The Flame’ katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Oktoba 2 hadi Jumatano ya Oktoba 11, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Malawi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Oktoba 7, 2017 katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.

Katika kikosi hicho cha wachezaji 22, Kocha Mayanga ambaye aliteuliwa Januari 4, mwaka huu ameita nyota watano wanacheza soka nje ya mipaka ya Tanzania akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.

Kikosi hicho kinachotarajiwa kuingia kambini Ijumaa Oktoba mosi, mwaka huu kwenye Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Young Africans) na Peter Manyika (Singida United).

Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).

Viungo wa kati ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC) na Raphael Daud (Young Africans).

Viungo wa pembeni ni Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya), Ibrahim Ajib (Young Africans) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Mbaraka Yussuph (Azam FC). 

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 apatikana jijini Mwanza

September 23, 2017
Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 toka Mwanza, Fatuma Msafiri akiimba wakati wa kumtafuta mkali wa kipaji cha kuimba jijini Mwanza
 Msanii Chipukizi Lusinde Michael a.k.a Real Da Best akionesha umahiri wake wa kufoka foka kwenye mchuano wa kusaka kipaji cha Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 jijini Mwanza
Top 2 wakisubiri kutajwa kwa mshindi kati yao.
Majaji wakijadiliana jambo.
Wasanii walioingia Top 4 wakisubiri mchujo wa kuingia top 2.

WAZIRI MWIJAGE AFUNGUA KIWANDA CHA MABATI CHA ALAF MKOANI DODOMA

WAZIRI MWIJAGE AFUNGUA KIWANDA CHA MABATI CHA ALAF MKOANI DODOMA

September 23, 2017
Mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Kiwanda cha kutengeneza mabati cha Kampuni ya ALAF Kanda ya Dodoma, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (mwenye tai), Waheshimiwa Wabunge ambao ni Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Viwanda pamoja na Viongozi wajuu wa Kampuni ya ALAF Tanzania wakishirikiana kukata utepe pamoja na kuashilia ufunguzi wa kiwanda cha mabati cha ALAF kanda ya kati mjini Dodoma.
Kampuni ya ALAF (Tanzania) imefungua tawi lake jipya Mkoani Dodoma ikiwa ni kutekeleza maagizo ya Sera ya Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma kwa wananchi baada ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha. Tawi hili limezinduliwa tarehe Septemba 9, 2017 Kizota, Dodoma.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akifungua jiwe la msingi la kiwanda cha mabati cha ALAF Dodoma kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa mikoa ya kanda ya kati (Dodoma, Singida na Tabora), Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema "Napenda kuwahakikishia kwamba Serikali yetu inafanya kila linalowezekana kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa sehemu muhimu ya kuwekeza kwa kulinda mitaji yao kupitia kuondoa ushindani usiokuwa wa haki hasa unaotokana na baadhi ya wafanya biashara kudanganya thamani ya bidhaa za bati zinazoingizwa toka nje ya nchi na kulipa kodi pungufu, kudhibiti uingizaji wa bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora na zaidi kulinda amani na maelewano yaliyopo baina ya Serikali na wadau mbalimbali ili kujenga ustawi wa nchi yetu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) akimueleza jambo Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty.
Waziri Mwijage aliendelea kwa kusema “Napenda kuwashukuru Kampuni ya ALAF (Tanzania) Ltd kwa kutekeleza vizuri maelekezo ya Sera ya Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma zao kwa wananchi wa Dodoma baada ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.”
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty alisema "uwekezaji huu wa Dodoma ni wa thamani ya shilingi bilioni tatu ukiajiri watu 15 moja kwa moja na wengine zaidi ya 100 ajira zisizo za moja kwa moja kama kupakia na kushusha bati, kusafilisha bati, huduma za maji, stationary n.k."
Wageni waalikwa toka mikoa ya kanda ya kati Dodoma, Singida na Tabora.
Pia aliongeza kwa kusema "ALAF inakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo uagizaji wa bidhaa sizizokidhi viwango unaofanywa na makampuni mbalimbali na pia ukwepaji wa kodi, kupelekea serikali kukosa mapato stahiki na walaji kutumia bidhaa zilizo chini ya viwango na hii hupelekea kukatisha tama wawekezaji wa ndani ambao wanajitaidi kuzalisha bidhaa zenye ubora na kulipa kodi zote stahiki.
Meneja wa ALAF kanda ya kati, Grayson Francis Mwakasege akizungumza jambo katika hadhira iliyofika kwa ajiri ya uzinduzi wa kiwanda cha mabati cha ALAF tawi la Dodoma kwa ajiri ya kuhudumia mikoa ya kanda ya kati. [/caption]
ALAF imekuwa ikishiliki kwenye kama vile elimu, makazi, afya na mazingira.Mpaka sasa ALAF imetumia takriban shilingi milioni 200 kwenye mradi wa kuwaelimisha wafanyakazi na jamii kuhusu ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa kushilikia na shirika la fedha duniani.
Alikadhalika kwa upande wake Meneja wa ALAF kanda ya kati, Grayson Francis Mwakasege nae aliongeza kwa kusema ufunguaji wa kiwanda hiki Dodoma umeleta ahuenei kwa wakazi wa kanda ya kati Dodoma, Singida na Tabora ambao hapo mwanzo walikuwa wakiagiza bati kutoka Dar es salaam kwa ghalama ya kati ya sh 3000 - 5000 kwa bati la rangi lenye urefu wa kuanzia mita 3 na kuendelea. Pia aliongelea uwezo wa machine zilizofungwa Dodoma kuwa zinaweza kuzalisha tani 50 sawa na nyumba 50 kwa siku.
Picha ya pamoja kati ya mgeni rasmi na wafanyakazi wa ALAF ,wakurugenzi wa wialya za Dodoma pamoja na wabunge wa mkoa wa Dodoma na Singida
Uzinduzi huo pia ulihudhuliwa na kamati ya bunge ya uwekezaji na viwanda pia wabunge kutoka Dodoma na Singida pamoja na mkuu wa wilaya ya Chamwino pia wakurugenzi wa wilaya za Dodoma.
Baadhi ya bidhaa zinazotolewa na ALAF ni Lifestile, Romantile, Versatile, Tekdek (It5), Resincot na Simba Dumu.Wasilana nasi kwa namba hizi Dar es Salaam- O768 555 560, Arusha - 0763 707 071, Mbeya - 0765 555 560, Dodoma - 0764 131442 na Mwanza 0682 808 080. Tunapatikana pia kuitia mitandao ya kijamii Facebook -Alaf Limited na Instagram - Alaf Limited

MKUU WA MKOA WA TANGA APOKEA VIFAA TIBA KUTOKA KWA UZALENDO KWANZA

September 23, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, akitokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - TANGA. Vifaa vilivyotolewa na wasanii na wachezaji hao katika uwanja wa Tangamano ikiwa ni Kampeni ya Uzalendo kwanza ni pamoja na Ultra Sound, mashine ya X- Ray, Wheel Chair, Magongo ya walemavu na craches. Shigella amepokea vifaa hivyo ikiwa ni moja ya Kampeni ya UZALENDO KWANZA ambayo inaongozwa na wasanii na wacheza mpira ikiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuchangia maendeleo ya nchi. Ambapo vifaa hivyo vinagawiwa katika hospitali za Ngamiani, Makorola, Pongwe na Mikanjuni.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, akitokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Vijana wazalendo wa UZALENDO KWANZA wakibeba vifaa Tiba ambavyo walitoa kwa ajili ya hospitali za mkoa wa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella aliwataka wasanii na wacheza mpira hao kuhakikisha wanatumia umaarufu walionao ili kuweza kuwavutia wawekazaji kutoka nje ya nchi ili kukuza uchumi wa nchi.
"Wasanii mnadhamana kubwa ya kuhakikisha mnatumia vema vipaji vyenu ili kuweza kusaidia juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda kwa wao kuvutia wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza katika nyanja mbalimbali." alisema "Ninatambua asilimia kubwa mlizunguka kwenye kampeni mkiwaomba watanzania wamchague Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na dhamira yake nzuri ya kuletea maendeleo lakini pia hivi sasa mnashirikiana naye kwenye sekta ya afya kwa kumuunga mkono kwa kutoa mchango wenu niwaambie huu ni uzalendo ambao ni msingi wa maendeleo ya Taifa" "Kwa mfano Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na wazee wengine walipigania Taifa hii kwa sababu ya uzalendo na ndio maana mnaona Rais wetu namna anavyopambana kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa na kutunzwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na baadae kwa lengo la kila mtanzania kuweza kunufaika nazo "
Wananchi wakifuatilia wakati halfa ya ugawaji wa vifaa tiba. Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, akiwashukuru UZALENDO KWANZA kwa jinsi walivyoweza kujitoa kwa hali na mali vifaa tiba kwa hospitali za mkoa wa Tanga.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa akitoa msisitizo kwa wasanii wa Tanga kuwa na moyo kama wa UZANDO KWANZA wa kuweza kujitoa kwa moyo mmoja wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. 
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere akieleza machache wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Kampeni ya UZALENDO KWANZA, Steven Mengele 'Nyerere' alisema uzalendo kwanza imemaua kuchangia vifaa tiba kwa hospitali ya Tanga na kwamba kampeni hizo zitaelekea mikoa mingine mbali mbali ikiwemo Lindi na Mtwara, Dodoma, Arusha, na Mwanza.
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere akiwatambulisha baadhi ya wazanii ambao wanaunda UZALENDO KWANZA.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella akimtunza msanii wa UZALENDO KWANZA ambaye alikuwa akitoa burudani.
Meza kuu ikifuatilia tukio wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Mhe. Thobias Mwilapwa na mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akiteta jambo na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. Kutoka kulia ni mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa na mwishoni kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi.
Wasanii wa UZALENDO KWANZA akitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akisalimiana na Msanii Ruby ambaye ni mmoja ya wana UZALENDO KWANZA wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akiteta jambo na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere.
UZALENDO KWANZA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi vifaa tiba.. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa (wa kwanza kushoto), Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi (mwenye tisheti ya mistari) pamoja na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere  wakati akipokea vifaa tiba kutoka kwa UZALENDO KWANZA ambao wametoa vifaa tiba.