RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MABADIRIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI, AMTEUA DKT. CHARLES TIZEBA KUWA WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI, MH. NCHEMBA APELEKWA MAMBO YA NDANI

June 11, 2016



 Dkt. Charles Tizeba

ZAIDI YA BILIONI 23 ZAOKOLEWA KWA KUONDOA WATUMISHI HEWA.

June 11, 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairukiakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambayo hufanyika Juni 16 -23 kila mwaka.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 23 kwa kuondoa watumishi hewa katika mfumo malipo ya mishahara ya serikali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki  jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa kiasi hicho kimepatikana  mara baada ya kuanza kwa kutafuta watumishi hewa wa serikali.

Amesema kuwa watumishi ambao wameshaondolewa tangu Machi, 1 hadi Mai 30 ni watumishi 12,246 ameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ya Serikali kwa sababu mbalimbali ikimo kutimiza umri wa Kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kuhitimishwa kwa mikataba.

Aidha amesema kuwa wasingeondolewa kwenye mfumo wa mishara kwa wafanyakazi wa serikali zaidi ya shilini Bilioni 25 zingepotea.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUTARISHA WANANCHI DAR ES SALAAM

June 11, 2016

 Mke wa Waziri Mkuu,  Mary  Majaliwa  akiwa na baadhi ya  waalikwa  katika  futari ilyoandaliwa na  Waziri Mkuu, kwenye makazi yake  jijini Dar es salaam  Juni 10, 2016.  Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya waalikwa waliohudhuria futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jiji Dar es salaam 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya waalikwa waliohudhuria futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jiji Dar es salaam 
 Waziri Mkuu Kassim Majliwa akisalimiana na  Bw. Seif Ali Seif   katika futari  aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimian na  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymound Mushi  katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. 
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya waalikwa walioshiriki katika futari  iliyoandaliwa na  Waziri Mkuu kwenye Makazi  yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya waalikwa waliohudhuria futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jiji Dar es salaam 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiongea na  waalikwa waliohudhuria futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jiji Dar es salaam
 Waziri Mkuum Kassim  Majaliwa akisalimiana  na Katibu Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya mkoa wa Dar es salaam, Padri John Solomon wa Kanisa la Anglikani (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam , Alhad Mussa Salum katika Futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni10, 2016.
 Swala kabla ya kufuturu
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanawake walioshiriki katika futari aliyoiandaa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. Kulia  kwake  ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema. 
 Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akisalimiana na Mke wa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Azalina Madabida katika futari aliyoiandaa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Makazi yake jijini Dar es salaam
  Baadhi ya  waalikwa  wakishiriki katika futari  iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi yake  jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HALMASHAURI YA MBEYA YAKAMILISHA UTENGENEZAJI MADAWATI WAMKABIDHI MKUU WA MKOA WA MBEYA AYAGAWE KWA SHULE 51

June 11, 2016

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akikagua madawati hayo kabla ya kuyagawa.
 Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla akigawa madawati hayo.
Halmashauri ya Mbeya imekamilisha utengenezaji wa madawati 5,371 ikiwa ni agizo la Rais kuhakikisha wanafunzi wote wanakaa katika madawati.

Akisema taarifa kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, mkurugenzi wa halmashauri hiyo Upendo Sanga amesema wamekamilisha maoema utengenezaji madawati mapema kabla ya juni 30 kwenda sambamba na agizo la Mkuu wa mkoa halmashauri zote zikamilishe madawati tarehe 20 juni siku kumi kabla ya tarehe ya mwisho ya mheshimiwa Rais.

Mkuu wa Mkoa amekabidhi madawati 3,746 kwa shule 51 na yaliyobaki ameagiza yaendelee kukabidhiwa kwa Shule zingine.

Amesisitiza halmashauri zote kukamilisha utengenezaji wa madawati ifikapo tarehe 20 Juni.

MASAUNI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, ATEMBELEA KITUO CHA POLISI KILICHOLALAMIKIWA BUNGENI

June 11, 2016



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita ambao ni majirani wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo. Wananchi hao wamelalamika kuwepo na vitendo vya ukatili dhidi yao vinavyofanywa na baadhi wa askari wa kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.

Mkazi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita, Biosi Makongoro akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyekaa) dhidi ya Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo ambayo ipo jirani na kijiji hicho, kuwa askari wa kampuni hiyo wanadaiwa kuwanyanyasa wananchi hao wanapopita katika eneo la Kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)  akiwasili Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.

Mkuu wa Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Jackson Kirahuka akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa koti) sehemu mbalimbali za kituo hicho ambacho Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dotto Biteko (katikati) aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri. Aliyevaa Kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Amani Mwenegoha.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali, Mstaafu Ezekiel Kyunga (meza kuu), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (watatu kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)  akitoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukendo, Amani Mwenegoha (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo iliyopo mkoani Geita. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi mkoani Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI PROF. MBARAWA AKEMEA HUJUMA KWENYE MIUNDOMBINU YA BARABARA MKOANI SINGIDA

June 11, 2016

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bw. Gishuli Charles (wa nne kushoto), wakati alipoanza ziara yake ya ukaguzi wa miundombinu katika Mkoa wa Singida. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu, na wa tatu kushoto ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo.
 Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo akimuonesha Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa uharibifu wa barabara unaotokana na ajali za barabarani katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilometa 89.3 mkoani Singida.
 Wananchi wa Itigi wakimsilikiza Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, (hayupo pichani) alipotangaza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Mkiwa-Itigi-Makongorosi kwa kiwango cha lami itakayoanza kujengwa kwa kilomita 35 mkoani Singida.
 Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo (wa tano kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto) kuhusu mradi wa ujenzi wa mzani katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya ambao ujenzi utakamilika hivi karibuni.
 Muonekano wa ujenzi wa kituo cha Mzani Itigi, kinachojengwa katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, mkoani Singida.
 Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akionesha moja ya picha ya uharibifu wa alama za barabarani uliofanywa na wananchi katika ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3.
 Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akihutubia wananchi wa Itigi mara baada ya kukagua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 mkoani Singida, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 98.
 Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisalimiana na wananchi wa Itigi mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara. Katikati ni Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Omary Yahya Massare.

Muonekano wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 inayojengwa na Mkandarasi SynoHydro Corporation Limited kutoka China inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 109 mkoani Singida.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

KONGAMANO KUBWA NA LA KIHISTORIA LILILOTARAJIWA KUFANYIKA LEO JIJINI MWANZA LAAHIRISHWA

June 11, 2016
Lile Kongamano Kubwa la Wajasiriamali lililotarajiwa kufanyika hii leo June 11,2016 katika Uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza, limeahirishwa hadi Julai 16,2016.