KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA DAWASA/DAWASCO KWA KAZI NZURI YA KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI

January 20, 2018
 
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, RUVU

KAMATI ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, imeipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASCO), kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji  katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na DAWASA na DAWASCO Dar es Salaami na mkoa wa Pwani leo Januari 20, 2018, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, alisema. Kazi iliyofanyika ni kubwa na Kamati imeona jinsi gani fedha za serikali zimetumika.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema, miradi mingi inatekelezwa kwa fedha za mkopo  kutoka India, lakini Kamati imebaini kuwa kila kitu kinafanywa na makampuni ya kutoka India, jambo ambalo sio sahihi sana.
“Inawezekana kuna mahali ambapo tumezidiwa, au kujichanganya, na kama ni kwenye component ya huo mkopo iliandikwa, kuna jambo la kuangalia na kujadili.” Alisema Mhe. Papian.

Aidha Mhe. Papian alisema Kamati inashauri kuwa watendaji wa ndani (Wakandarasi) wanapomaliza hii miradi basi vijana wa Kitanzania lazima wawe wameshajua na kufundishwa na wajifunze kila kitu ili waweze kuendesha miradi hii kikamilifu.
Ziara ya Kamati hiyo ilianzia makao makuu ya DAWASA, ambapo Kamati ilipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA na DAWASCO, na kasha walipata fursa ya kutembeela baadhi ya miradi hiyo ambayo ni ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji ya Changanyikeni, Salasala, vituo vya kusukuma maji vya Makongo na Salasala.
Kamati pia ilitembelea eneo la utandazaji mabomba ya kusambaza maji huko Mpiji Machimbo na kumalizia ziara yao kwa kutembelea mitambo ya maji ya Ruvu chini na Ruvu Juu.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo alisema, Mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani unaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na katika Miji ya Bagamoyo na Kibaha na tayari umefikia asilimia 72.2 kukamilika.
“Mradi huu unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), ulianza rasmi Machi mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika Februari 28, 2018.” Alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu kazi zinazofanyika kwa sasa, Mhandisi Mwang’ingo alitaja kuwa ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi kati ya lita za ujazo milioni 3.0 hadi milioni 6.0 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vine vya kusukuma maji na ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa za kusukuma maji 16.
Kazi nyingine ni pamoja na ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji mabomba yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilomita zipatazo 477.
“Maeneo yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo, Kitopeni, Ukuni, Buma, Mataya na ukanda maalum wa WPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu.” Alifafanua.
Aidha maeneo mengine yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba Mawili na Msigani na maeneo hayo yote yanapata huduma ya maji kutoka mtambo wa Ruvu Juu uliozindulkiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Juni 21, 2017.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Bw.;aston T. Msongole, alisema ni nia ya DAWASA kuhakikisha maeneo yote ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji hususan baadhi ya maeneo ya wilaya mpya ya Kigamboni, ni kuhakikisha huduma hiyo inawafikia.
“Tayari tumechimba visima virefu vyenye uwezo wa kutoa maji mengi ya kumaliza tatizo la ukosefu wa maji kwenye maeneo hayo lakini tatizo ni uhaba wa fedha za kutengeneza mfumo wa kuyasambaza maji hayo kwa walaji” Alisema Bw.Msongole.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo(kushoto), akifafanua jamnbo mbele ya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kulia) na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, walipotembelea ujemnzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji la Salasala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo Januari 20, 2018.
 
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Daniel; Nsanzugwanko, (katikati) akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo, (kushoto) na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, walipotembelea mtambo wa maji wa Ruvu Juu, Mlandizi mkoani Pwani.
 Kaimu Mwewnyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kushoto) na mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Daniel Nsanzugwanko, (katikati), wakimsikilzia Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye eneo la ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji wa Salasala.
 Taswira ya maendeleo ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhi na kusambaza maji la Salasala ukiwa umefikia hatua ya ufunikaji kabla ya kumwaga zege.
 Mafundi wakisuka non do tayari kwa kumwaga zege kwenye tenki la Salasala.
 Modester Mushi (kushoto), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa ufundi DAWASA akiwa na Afisa Habari na UHusiano wa Jamii Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Bi.Mecky Mdaku wakati wa ziara hiyo ya Kamati ya Bunge huko Salasala.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, (kushoto), akizungumza jambo na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya.
 Kamati ikipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA/DAWASCO mwanzoni mwa ziara hiyo.
Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya, akigawa taarifa ya DAWASA kwa wajumbe wa Kamati.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati, wakisikiliza taarifa hiyo.
 Mjumbe wa Kamati, Mhe,Kuntyi Yusuph Majala, akizunhgumza wakati wa Kamati ikipkea taarifa.
 Mhandisi Mwangi’ngo, akitoa taarifa ya utendaji ya DAWASA.
 Picha ya pamoja ya Kamati na watendaji wa DAWASA/DAWASCO na wajenzi.
 Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
  Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.


-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com

MAOMBI YA VIONGOZI WA DINI YALISAIDIA NCHI KUPATA RAIS MWENYE HOFU YA MUNGU

January 20, 2018



Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila ambaye ndiye Mratibu wa maombi hayo akizungumza kwenye ibada ya maombi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila, akimkaribisha Waziri wa HabariUtamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwenye ibada hiyo mara baada ya kuwasili.

 Waziri wa HabariUtamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati), akishiriki katika maombi ya shukurani na kuikabidhi Nchi kwa Mungu yaliyofanyika leo Nyumba ya Huduma Abundant Blessing Centre  (ABC) Tabata  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa ABC,  na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama.
 Kwaya ya Haleluya Selebration wakitoa burudani ya nyimbo za kusifu katika ibada hiyo.
 Maombi yakifanyika.
 Mtumishi wa mungu, John Kanafunzi kutoka Kanisa la KLPT Mbezi Mwisho akiongoza kuimba nyimbo za kusifu.
 Watumishi wa Mungu  wakiwa kwenye maombi hayo. Kutoka kushoto ni Nabii Elijah Krasian Mollel kutoka Kanisa la Jehova Shammah na Askofu Mhina.
 Wachungaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Wanamaombi kutoka Kibaha mkoani Pwani wakiwa kwenye maombi hayo.
 Maombi yakiendelea.

Mmoja wa waombaji  Baba Askofu, David Mwasota akiongoza maombi ya shukurani.
 Taswira ndani wakati wa maombi hayo.
 Nabii Elijah Krasian Mollel kutoka Kanisa la Jehova Shammah, akifanya maombi.



Askofu Emanuel Mhina akiongoza maombi hayo.
Mtumishi wa Mungu akiomba katika ibada hiyo.
 Viongozi wa dini na waumini wakiwa kwenye maombi hayo.
 Utulivu wa viongozi wakati wimbo wa taifa ulipokuwa ukiimbwa.
Waziri Mwakyembe akizungumza na waumini wakati wa maombi hayo

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Habari Utamaduni, Sanaa  na Michezo,  Dk.Harrison Mwakyembe amesema maombi yaliyofanywa na viongozi wa dini wakati wa uchaguzi mkuu kuomba nchi ipate rais mwenye hofu ya Mungu ndiyo yaliyo mleta Rais Dk, John Magufuli.

Mwakyembe ameyasema hayo wakati wa maombi maalumu ya shukurani na kuikabidhi nchi kwa Mungu yaliyofanywa na maaskofu na viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali katika Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre Tabata jijini Dar es Salaam leo.

"Maombi yenu ya kumuomba Mungu atupe rais mwenye hofu ya Mungu ndiyo yalisababisha kumpata Rais John Magufuli wakati wa uchaguzi mkuu ambaye anapigania maslahi ya wanyonge hasa maskini kwa kupambana na watu waliokuwa wakijineemesha wenyewe kwa kutumia fedha za umma vibaya" alisema Mwakyembe.

Alisema katika hatua nyingine Rais Magufuli ni rais pekee ambaye amekuwa akiwaomba viongozi wa dini wamuombee kwa kuwa anafahamu bila ya maombi hawezi kufanya chochote na maamuzi yake yote yanatokana na maombi ambayo anafanyiwa na viongozi wa dini.

"Serikali ina utambua mchango mkubwa mnaoufanya wa kumuombea Rais na nchi kwa ujumla hivyo mnapokuwa na malalamiko yenu msiyazungumzie chini chini tuelezeni tutayafanyia kazi kwa kushirikiana na viongozi wengine" alisema Mwakyembe.

Akizungumza katika ibada hiyo ya maombi ya kuliombea taifa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alisema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayemsema rais vibaya wakati sasa anafanya mambo makubwa ya kuijenga nchi.

"Kuna baadhi ya watu wanamnenea vibaya rais wetu kutokana na kazi nzuri anayoifanya nasema hatutakubali kuona rais akifanyiwa hivyo mtu yeyote atakayebainika tutamkamata bila ya kumuonea huruma" alisema Mshama.

Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila ambaye ndiye mratibu wa maombi hayo alisema maombi hayo ya shukurani na kuikabidhi nchi kwa Mungu yameshirikisha viongozi wa makanisa mbalimbali na huduma za Kikristo na kuandaliwa na I GO Africa for Jesus Prayer Movement na kuwa maombi ya namna hiyo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara.

Alisema maombi yaliyofanyika ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya Uhuru wa Taifa letu ulipatikana pasipo kumwaga damu pamoja na ulinzi na neema na rehema katika nchi yetu.

Alitaja eneo lingine la maombi ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya nchi yetu kuwa na utajiri na rasilimali nyingi kama dhahabu, almasi, uranium, mafuta ya petroli, ardhi nzuri, mbuga za wanyama, gesi, mito na milima.

Alisema maombi mengine yaliyofanyika ni kumshukuru Mungu kwa viongozi ambao wameliwezesha taifa kupiga hatua mbalimbali za maendeleo licha ya kuwepo changamoto kama za umaskini, maradhi na ujinga.

Askofu Ndabila alisema maombi mengine yalikuwa ni kuliombea Taifa, Kanisa na Afrika kwa ujumla.

Alisema anashangaa kuwasikia watu wakilalamika kuwa eti vyuma vimekaza wakati nchi ina kila rasilimali.

Maombi hayo yalihudhuriwa na maaskofu takriban tisa kutoka makanisa mbalimbali.



SEKTA BINAFSI YARIDHISHWA NA UHUSIANO WAKE NA SERIKALI

SEKTA BINAFSI YARIDHISHWA NA UHUSIANO WAKE NA SERIKALI

January 20, 2018
IMG_9340
Baadhi ya Wawekezaji na wageni kutoka Taasisi za Kimataifa walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
IMG_9354
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Salum Shamte, akizungumza wakati wa mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliojadili namna ya kuboresha masuala ya biashara na uwekezaji nchini, mjini Dodoma.
IMG_9365
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji  walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
IMG_9366
Baadhi ya Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu na Maafisa wengine kutoka Wizara mbalimbali wakifuatilia mkutano kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma, Mjini Dodoma.
IMG_9384
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji  walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
IMG_9393
Sehemu ya wadau mbalimbali wakiwemo wabunge, wawekezaji na viongozi wa Serikali walioshiriki mkutano kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma, Mjini Dodoma.
IMG_9431
Baadhi ya wabunge wakifuatilia kwa makini mkutano wa tatu wa wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma
IMG_9460
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifungua mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Serikali uliofanyika mjini Dodoma.
IMG_9506
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole-Gabriel, akionesha kabrasha lenye maelezo ya utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyotekelezwa na yanayoendelea kutekelezwa baada ya mikutano miwili ya awali kufanyika Mjini Dodoma na Jijini Dar es Salaam.
IMG_9517
Baadhi ya Maafisa wa Serikali wakishiriki Mkutano wa tatu wa wadau kutoka Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliojadili namna ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, mjini Dodoma
…………………………………………………………………………..
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Sekta Binafsi nchini imekiri kuwa uhusiano kati yake na Serikali umezidi kuimarika kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji na ufanyajibiashara hapa nchini kuliko ilivyokuwa hapo awali na kwamba hatua hiyo itachochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Salum Shamte, wakati wa mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliojadili namna ya kukuza ushiriki wa Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa viwanda nchini.
“Sekta binafsi imenituma kuleta pongezi kwa Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo utambuzi wa kwamba Sekta Binafsi ni mbia muhimu wa maendeleo ya Taifa letu” alisema Bw. Shamte.
Aliyataja baadhi ya mafanikio yanayo onekana bayana kuwa ni pamoja na kuinusuru Bandari ya Dar es Salaam kwa mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2017 hasa kuondoa VAT kwenye biashara ya mizigo ya kimataifa na kuondokana na umoja wa forodha ambao ulipunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Bw. Shamte alisema kuwa majadiliano hayo kati ya Serikali na Sekta Binafsi kumeikoa sekta ya utalii hasa kwa kuondokana na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye leseni mbalimbali hatua ambayo imerejesha msisimko wa sekta hiyo.
“Serikali imepunguza pia  mlolongo wa kodi kwa wakulima, japokuwa – kazi haijakamilika lakini mwanzo ni mzuri” aliongeza Bw. Shamte
Alieleza kuwa jitihada mpya na nzuri za kutatua changamoto za kodi kwa kampuni zinazojihusisha na biashara kati ya Tanzania Bara na Visiwani, na kuanza kufanya malipo kwa wakandarasi na watoa huduma wa ndani hatua ambayo wanaamini itakuza matumizi ya ndani na mzunguko wa fedha.
Makamu mwenyekiti huyo wa TPSF alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni sikivu na kwamba kwa mara ya kwanza, wanatarajia kushuhudia Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2018/2019 ikiwa bora zaidi kwa kubeba mapendekezo yao mengi yatakayosaidia kukuza sekta hiyo na pia kuboresha masuala ya kodi na mapato ya Serikali.
Wakizungumza kwenye mkutano huo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage, wamesema kuwa Serikali inathamini mchango wa Sekta Binafsi katika maendeleo ya uchumi wa viwanda na kwamba itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta hiyo ikiwemo masuala ya kodi.
“Sekta Binafsi ndiyo mhimili wa uchumi kwa hiyo ni muhimu tuhakikishe upande wa Serikali tunafanya wajibu wetu kuiweesha Sekta hiyo iwe imara zaidi na iweze kukua kwa sababu tutapata ajira, bidhaa bora na huduma mbalimbali hatimaye kukuza uchumi wetu wa viwanda” alisisitiza Dkt. Mpango
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji naye aliongeza kuwa Sekta Binafsi ndiyo itakayojenga viwanda wakati Serikali itakuwa mwezeshaji ndio maana wameamua kukaa  pamoja kujadili changamoto zinazozikabili pande zote mbili na kwamba baadae watajielekeza kujadili na kila Sekta ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.
Wametoa wito kwa Sekta binafsi nchini kujenga uaminifu na kufuata sheria na kanuni za ufanyajibiashara na uwekezaji nchini ikiwemo kulipa kodi stahiki.
Akizungumza katika mkutano huo wa tatu uliojumuisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) hapa nchini, Bw. Andy Karas, ameimwagia sifa Tanzania kwa kukuza uchumi wake kwa wastani wa asilimia 7 na kushauri kuwa uchumi huo sasa uelekezwe kutatua changamoto za wananchi hususan kukuza sekta ya kilimo inayoa ajiri idadi kubwa ya watanzania.
MKUU WA MAJESHI YA ULINZI JENERALI MABEYO AKAGUA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA RELI KILOSA MKOANI MOROGORO

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI JENERALI MABEYO AKAGUA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA RELI KILOSA MKOANI MOROGORO

January 20, 2018

01
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe akimuongoza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kushoto na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa  Mh. Adam Mgoyi katikati wakati  walipokagua athari za uharibifu wa madaraja, Mashamba na nyumba za wananchi   kufuatia  mafuriko yaliyosababishwa na  mvua kubwa zinazonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro
3
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe akitoa maelezo kwa  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo katikati  na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa  Mh. Adam Mgoyi kushoto  wakati walipokagua athari za uharibifu wa madaraja, Mashamba na nyumba za wananchi   kufuatia  mafuriko yaliyosababishwa na  mvua kubwa zinazonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro
DSCN8690
Maji yakiwa yametapakaa kandokando ya Reli ya kati na kusababisha uharibifu mkubwa wa reli, Mashamba  pamoja na nyumba za wananchi.
DSCN8693
Madaraja yakiwa katika hatari ya kusombwa  kutokana na mvua hizo
DSCN8702
…………………………………………………………………………………………………….
Na. Andrew Chimesela – Morogoro
Hali  mbaya ya mafuriko yanayoendela kuathiri wananchi wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro yamemfanya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Generali Venance Mabeyo kufika Kilosa na kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika ili kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa kuokoa maisha ya wananchi wa maeneo hayo na mali zao.
Generali Mabeyo aliwasili Kilosa Jan.19, 2018 majira ya jioni na kuungana na mwenyeji wake Dkt. Kebwe Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyepiga kambi Wilayani humo kwa ajili ya mafuriko hayo kisha bila kujali mvua iliyokuwa inaendelea kunyesha muda wote wakatembelea baadhi ya  maeneo yaliyoakuwa yamethiriwa ili kuona hali halisi ya mafuriko hayo.
Kwenye kikao cha majumuisho Mkuu huyo wa Majeshi nchini alishauri kuwa ili kutatua changamoto hiyo inatakiwa nguvu ya ziada na ya pamoja kwa taasisi zote kuungana, Ikiwa ni pamoja na taasisi mbali ili kuweza kuokoa maisha ya watu, mali zao pamoja na miundombinu iliyoathiriwa.
Hata hivyo alisema changamoto hiyo inatakiwa kuwe na mpango wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Amesema suluhisho la mpango wa mda mfupi ni kuwa na kazi ya dharura, na kazi hiyo ya dharura inahitajika kuwepo na mpango wa dharura ambao ni kuokoa maisha ya watu waliozingirwa na maji ili wasiendelee kukosa huduma za kijamii na pia kuathiri afya zao kwa kunywa maji ambayo si salama.
Pamoja na kuwepo kwa wazo la kurekebisha tuta la mto Mkondoa ikiwa ni mpango wa muda wa kati ili maji hayo yafuate mkondo wake lakini pia Generali Mabeyo ameshauri kuangalia namna ya kupunguza kasi ya maji hayo kuanzia yanakotoka kwa kujenga mabwawa ikiwa ni mpango wa muda mrefu.
“Maji haya yanakuja huku ni kama sisi ni waathirika zaidi lakini yanakoanzia hatujui hali iko namna gani, pengine katika mpango wa muda mrefu ingetazamwa namna ya kuyapunguza haya maji kasi yake.Sasa katika kuyapunguza, taasisi mablimbali zina wataalamu ambao wanaweza kusaidia kuweza kujenga mabwawa makubwa huko yanakoanzia ili haya maji  kupunguza kasi yake kabla hayajafika huku” alisema Generali Mabeyo.
Akitoa maelezo ya awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema tuta hilo la mto Mkondoa lilijengwa enzi za Mkoloni kama kinga kwa  mji wa Kilosa na kwa mara ya kwanza lilipasuka mwaka 2010. Ujenzi  wake kuanzia hapo haukukamilika vizuri kutokan na hali ya kifedha na sasa limepasuka baada ya Mvua nyingi kunyesha kuamkia Jan,11 mwaka huu.
Hata hivyo Dkt. Kebwe ametoa Ombi kwa Mkuu huyo wa Majeshi, kupata nguvu kazi ya wanajeshi, vifaa na utaalamu wao ili baada ya mvua hizi kupungua waendelee na kutafuta mbinu ya kuuongozo mto Mkondoa uweze kupita katika sehemu yake ya awali na hivyo kutoathiri wananchi, mali zao na miundombinu iliyopo eneo hilo .