KAMPENI MAALUM YA KUINUA MAADILI KITAIFA JAN - DEC, 2017

January 19, 2017
Kiongozi wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa Bi Mayrose Kavura Majinge, siku ya Jumamosi Jan 14, ameweza kushirikiana na wadau mbali mbali jijini hapa Washington kwa lengo la kuinua Maendeleo Maalum ya Maadili Kitaifa, yaliyoanza rasmi kufanyika mwezi huu Januari hadi Disemba 2017, kwa lengo la kuinua na kudumisha maadili ya Watanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha mfumo wa muundo wa jamii yetu ya Kitanzania.

SERIKALI YAONYA WAWEKEZAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO

January 19, 2017



Na Woinde Shizza,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali haitasita
kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya
Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo.


Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali.

Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa macho

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu
wachache


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi  ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha  Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo utasaidia kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za kimaendeleo badala ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo



Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea katika vijiji mbalimbali ikiwa ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori tengefu katika wilaya hiyo.

WAKUU WA MASHIRIKA YA UMEME KUTOKA NCHI KUMI ZA EASTERN AFRICA WAKUTANA ARUSHA KUJADILI NAMNA YA KUUNDA MIFUMO YA USAFIRISHAJI UMEME KWA NCHI HIZO

January 19, 2017


Na Woinde Shizza,Arusha

Wakuu wa  mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha
umeme(Eastern Africa Power pool(EAPP)          zimekutana  jijini arusha kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na
namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa uraisi tofauti na sasa.

 
Hayo yalisemwa na naibu katibu mkuu wizara ya nishati na madini Dkt.Juliana Palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa mashirika ya umeme katika nchi hizo za eastern Africa power
pool(eapp)mapema leo.

 
Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani  kuna uwezekano  mkubwa wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo.

 
Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza umeme kwa gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama nafuu.

 
"Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi hiyo itaweza kuuza umeme  kwa bei ndogo"aliongeza palangyo.

 

Hataivyo kwa upande  kaimu meneja uhusiano wa shirika la tanesco  Leila Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo itatoka nchi ya tanzania kwends kenya,zambia,pamoja na nchi nyingine.
 
Muhaji alisema kuwa tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo jamiii itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo zimeeendelea duniani.

 
"Hataivyo mara baada ya huu mkutano wa wakuu wa nchi zinazolisha umeme tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni mawaziri kutoka nchi zote ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia
mlengwa"aliongeza Muhaji

Alimalizia kwa kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni  Tanzania ,Kenya,Uganda ,Rwanda ,Burundi ,Sudan , Dr congo, Ethiopia ,Djbout, Libya pamoja na Egypt.