MWILI WA MZEE PIUS MKUNJA WAAGWA JIJINI MWANZA KWA AJILI YA MAZISHI MKOANI MOROGORO.

April 26, 2016
Padri wa Kanisa la Roman Cathoric, Parokia ya Watakatifu Wote Kiloleli Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza, akiongoza ibada ya maombi ya kuuaga mwili wa Marehemu, Mzee Pius Joseph Mkunja, Mzaliwa na Mkazi wa Mpanga Kilombero Mkoani Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika jana kanisani hapo.

Mzee Mkunja alifariki dunia juzi April 25,2016 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza akikokuwa akipata matibabu. Alizaliwa Mwaka 1926 hivyo amefariki akiwa na umri wa miaka 90. Kifo chake kimetokana na tatizo la vidonda vya tumbo. Alikuwa mfanyabiashara maarufu enzi za uhai wake.

Mwili wake unasafirishwa hii leo April 27,2016 kuelekea nyumbani kwake Mpanga, Kilombero Mkoani Morogoro kwa ajili ya Mazishi. 
Tunatoa natoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu, akiwemo mtoto wa Marehemu, Bi.Idda Adam.
Padri wa Kanisa la Roman Cathoric, Parokia ya Watakatifu Wote Kiloleli Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza, akiongoza ibada ya maombi ya kuuaga mwili wa Marehemu, Mzee Pius Joseph Mkunja, Mzaliwa na Mkazi wa Mpanga Kilombero Mkoani Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika jana kanisani hapo.
Padri wa Kanisa la Roman Cathoric, Parokia ya Watakatifu Wote Kiloleli Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza, akiongoza ibada ya maombi ya kuuaga mwili wa Marehemu, Mzee Pius Joseph Mkunja, Mzaliwa na Mkazi wa Mpanga Kilombero Mkoani Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika jana kanisani hapo.
 WAZIRI APIMA MALARIA KWA KUTUMIA MRDT

WAZIRI APIMA MALARIA KWA KUTUMIA MRDT

April 26, 2016

Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Charles Dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewataka watanzania kwa pamoja kuungana kupambana na ugonjwa wa Malaria ili kusaidiana na serikali kutokomeza ugonjwa huo ambao husababisha vifo vya watu wengi nchini.
Waziri Ummy ameyesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya Maralia Duniani ambapo huadhimishwa Aprili, 25 ya kila mwaka na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu ili kutokomeza ugonjwa huo.
“Msisitizo mkubwa wa Wizara yangu ni kwa wananchi na wadau wote kuona umuhimu na kutoa kipaumbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa kuhakikisha matumizi sahihi ya mikakati iliyopo katika kuuthibiti ugonjwa huu,
“Iwapo mikakati hiyo itatekelezwa ipasavyo ni dhahiri kuwa maambukizi yataendelea kupungua kwa kiasi kikubwa na hatimaye kumaliza kabisa tatizo hili,” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy Mwalimu
Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt.Renata Mandike (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na utekelezaji wa udhibiti wa Malaria nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu.
Malaria
Baadhi ya wataalam wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu.
mwalimu
Fundi sanifu maabara, Habiba Malima akimchukua damu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu kwa kipimo cha malaria Rapid Diagnosist Test(mRDT), kipimo hicho ni cha haraka na huchukua dakika ishirini kugundua kama una Malaria, kipimo hiki kilianza kutumika nchini mwaka 2009.
Richard Mwaikenda
Mwandishi wa habari na mmiliki wa globu ya mzee wa matukio, Richard Mwaikenda akichukuliwa kipimo cha malaria na fundi sanifu maabara Habiba Malima ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani katika ukumbi wa viwanja vya Bunge.
Eleuteri Mangi
Afisa habari wa idara ya habari Maelezo, Eleuteri Mangi akipima malaria kwa kipimo cha mRDT.
Kijah Yunus
Mwandishi wa habari kutoka Clouds media, Kijah Yunus akipima Malaria.

RC RUGIMBANA AONGOZA KONGAMANO LA MIAKA 52 YA MUUNGANO UDOM

April 26, 2016
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lugimbana akizungumza na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM -UDOMASA), wakati wa mdahalo wa miaka 52 ya Muungano uliofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga  uliopo UDOM leo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo  hicho,  Professa Idrissa Kikula. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mwenyekiti wa Jmuiya ya Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA),  Mhadhiri Msaidizi, Edson Baradyana akitoa shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lukimbana kwa kukubali kufungua kongamano hilo.
 Baadhi ya wanachuo na wanataaluma wakishiriki kwenye kongamano hilo la miaka 52 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

 Jopo la wawezeshaji wa kongamano hilo





 RC Rugimbana akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM, Kikula kabla ya kuondoka. Kushoto ni Mwenyekiti wa Udomasa, Paradyana.
 Rugimbana akiagana na wahadhiri wa Udom
 Rugimbana akiteta jambo na Profesa Kikula
 Wakiwa katika picha ya kumbukumbu

 Mhadhili wa UDOM, Profesa Davis Mwanfupe akitoa mhadharakuhusu umuhimu wa wanataaluma kuuenzi Muungano


JK AREJEA NCHINI AKITOKEA CHINA

April 26, 2016

 
 Mwenyekiti a CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete akiwa na Katibu wake, Suleiman Mwenda baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, leo akitokea chini China alikokuwa akiwa katika ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
 Mwenyekiti wa CC,M Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na Madabida
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungmza na  baadhi ya viongozi  
 Jk akiingia ukumbini kuzungumza na waandishi
 Jk akiwa tayari kuzungumza na waandishi wa Habari
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari leo baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam, akitoa nchini China alikokuwa katika ziara ya kikazi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam. Ramadhani Madabida. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
RAIS MAGUFULI AFANYA KIKAO NA WATENDAJI WA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, FEDHA NA MIPANGO, TRA, BENKI KUU, TAKUKURU NA TCRA

RAIS MAGUFULI AFANYA KIKAO NA WATENDAJI WA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, FEDHA NA MIPANGO, TRA, BENKI KUU, TAKUKURU NA TCRA

April 26, 2016

ikulu
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, pamoja na ma-Katibu wakuu Wizara ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora, Katibu Mkuu Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Mhe Dottoa James, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola pamoja na uongozzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na watendaji wengine. PICHA NA IKULU
Possi: Serikali kuboresha Makazi ya Watu wenye Ulemavu na wenye mahitaji maalum.

Possi: Serikali kuboresha Makazi ya Watu wenye Ulemavu na wenye mahitaji maalum.

April 26, 2016


pos2
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe Dkt. Abdallah Possi    akiwasilisha hoja za masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa Mkutano wa Bunge wa kujadili Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17 kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde tarehe 25 Aprili, 2016.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pos1
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akiwasilisha hoja zinazohusu masuala ya Kazi na Ajira wakati wa mkutano wa Bunge wa Kujadili Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17 Bungeni Dodoma tarehe 25 Aprili, 2016.
…………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Serikali imeahidi kuboresha Makazi ya watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha yao ya kila siku.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt Abdallah Possi wakati akichangia hoja katika Mkutano wa Bunge wa kujadili Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17 Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Waziri aliwaeleza Wabunge umuhimu wa Serikali kuboresha makazi ya Watu wenye Ulemavu na wenye mahitaji maalum kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya watu wenye Ulemavu namba 9 ya mwaka 2010 inayoeleza haki za watu wenye Ulemavu kuboreshewa maeneo muhimu ikiwemo elimu, ajira, fursa sawa na miundombinu.
“Dhamira ya Serikali ni kuhakikiasha Watu wenye Ulemavu wanashiriki katika shughuli mbalimbali kwa kuwawekea mazingira rafiki yanayowasiaida kutekeleza majukumu yao kulingana na hali zao” Alisema Mhe.Possi.
Aidha, Serikali imefanya jitihada za awali kwa kuyatembelea makazi ya watu wenye ulemavu yakiwemo makazi ya Nunge yaliyopo wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es salaam, Sarame Mkoani Manyara, Kituo cha Wagonjwa wa Ukoma cha Msufini mkoani Tanga pamoja na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kubaini umuhimu wa kuyaangalia maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za uvamizi wa makazi ya watu wenye mahitaji maalum.
“Makazi ya watu wenye ulemavu na wale mahitaji maalum yana changamoto nyingi ikiwemo uchakavu wa majengo, kukosa vifaa, uhaba wa wahudumu, changamoto za kifedha na uvamizi wa mara kwa mara” Alisema Naibu Waziri.
Naibu Waziri Possi alisisitiza kuwa hadi sasa Wizara hiyo imeshakubaliana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuangalia hatua za kuzuia uvamizi katika Makazi ya Watu wenye Ulemavu na wenye Mahitaji maalum ili kuimarisha usalama wao.
Msingi wa hoja iliyojibiwa na Naibu Waziri imetokana na michango iliyotolewa na wabunge kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu kuitaka Serikali kuhakikisha inaboresha mazingira ya watu wenye ulemavu.
Maeneo  yanayoboreshwa na kutekelezwa ni pamoja na kuwaboreshea namna ya wanavyotakiwa kupata elimu bora, kukomesha mauaji ya wenye ualbino, suala la kodi na Makazi ya watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum wakati wa kuchangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17.

DK.SHEIN AHUDHURIA MAZISHI YA MAREHEMU ABDALLA MOHAMD MSHINDO (MWENYEKITI CCM)

April 26, 2016


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia)akijumuika na Viongizi na Waislamu katika kumswalia aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo katika msikiti wa Khinani,Wilaya ya Magharibi 'A'Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo.
Maelfu ya wananchi na waislamu waliobeba jeneza la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo katika mazishi yake yaliyofanyika leo kijiji cha Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A'Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto)akitia udongo katika kaburi la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba katika mazishi yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A',Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi (Gavu) akitia udongo katika kaburi la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba katika mazishi yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A' Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Haji Juma Haji akitia udongo katika kaburi la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba katika mazishi yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A' Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Sif Ali Iddi(katikati)pamoja na wananchi na wanaCCM wakiitkiia dua iliyoombwa baada ya mazishi ya Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa wenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A' Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiwapa pole familia ya Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba kabla ya mazishi yake yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi'A' Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Picha na Ikulu.

UVCCM ARUMERU WALAANI KITENDO CHA MWENYEKITI WA MKOA KUMSIMAMISHA KAMANDA WAO

April 26, 2016


Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya 
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo

Na Woinde Shizza,Arusha

BARAZA la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya
Arumeru umelaani kitendo cha UVCCM mkoani hapa kumsimamisha kamanda wa umoja wa Vijana wa UVCCM wilaya ya Arumeru Mathias Manga kutokana na kuisaliti CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Aidda baraza hilo limelaani tamko lililotolewa wiki iliyopita na
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Sabaya na kumtaka ajitathmini na kujipima kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa,kama ataona hawezi ajing'oe mwenyewe.

Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya,alisema kuwa wanamtambua Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC),kama Kamanda wao wa vijana.

"Tunalaani tamko lililotolewa na Mkoa na hatumtambui kamanda
mwingine,Kamanda wetu hajatendewa haki,wajumbe wa baraza tumetathmini tamko la Lengai tunaona ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni,amepoka madaraka yasiyo yake,kitendo ambacho ni kurudisha chama nyuma badala ya kukijenga.

Mungaya alisema kuwa "Sabaya ajitathmini,ajipime kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa kwani tunaona akiendelea hivi kukiuka kanuni atakiua chama,ni bora ajing'oe mwenyewe kama anaona hawezi,tunampa siku saba akanushe madai aliyoyatoa dhidi ya kamanda wetu".

Alisema kuwa tamko hilo ni batili na hawalitambui na kumtaka Manga
asivunjike moyo aendelee na haratkati za kukijenga chama hivyo asirudishwe nyuma na changamoto anazokabiliana nazo.Akizungumzia yeye kuwepo kwenye baraza hilo alidai kuwa siku ya kikao alikuwepo ila alikataa kupiga kura ya kumkataa Kamanda wake na kuamua
kutoka nje.

Naye Anjelina Lukumay ambaye ni mjumbe wa baraza hilo kutoka Kata ya
Oldonyosambu,alimuomba Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa,Lekule Laizer
kuliangalia suala hilo na kulitafutia ufumbuzi kwani Sabaya amekiuka kanuni za chama.

"Mwenyekiti wa wilaya ametumia kanuni ipi kumkataa kamanda wetu bila
kutushirikisha?hatutakubali kuvurugwa wilaya ya Arumeru,tumepokea kwa
mfadhaiko kauli hiyo kwani Sabaya kachaguliwa hata miezi miwili hana ila
inakuwaje anataka kumtoa Manga tena bila kutushirikisha?alihoji Anjelina
Wiki iliyopita uamuzi wa kumsimamisha Manga ulifikiwa katika kikao cha
baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kilichozinduliwa na kaimu katibu mkuu Shaka Hamdu Shaka,ambapo kikao hicho kilikuwa na wajumbe 34 huku 33 kati yao wakipiga kura za ndiyo.

Pia kikao hicho kilitoa onyo kali kwa kamanda wa UVCCM wilaya ya Arusha
Mjini,Longido na Monduli na kuwataka wajipime na kujitathimini kama
wanatosha kuwa makamanda wa UVCCM na wakiona hawatoshi tunaomba wakae pembeni kabla baraza halijawachukulia hatua.Uamuzi wa kumsimamisha Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC)wilaya ya Arumeru ulifikiwa katika Manga

Akisoma tamko lilitolewa na Kikao hicho cha baraza kikao hicho cha
baraza Katibu wa Hamasa wa (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Lucas Nsomi alisema Manga kuanzia wakati huo si kamanda wa Vijana Wilaya ya Arumeru tena kwani amepoteza sifa baada ya kudhibitika kukisaliti chama kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,kwani wakati wa uchaguzi huo alionekana akifanya vikao vyakufanikisha ushindi kwa UKAWA.

“Kikubwa alichofanikiwa Manga ni kuwagawa vijana wa Arumeru hali
inayopelekea kushindwa kuijenga jumuiya hiyo na kuanzia sasa sio kamanda wa vijana tena wa wialaya hiyo na sipo tayari kufanya naye kazi yoyote ile ndani ya CCM”.

Sabaya alidai kuwa vijana waliompitisha kuwa kamanda lilikuwa ni genge
la wahuni ambao walikuwa wakiendesha vikao vya vijana wenye njaa na kuwa hayupo tayari kuwa Mwenyekiti wa magenge ya vijana wenye njaa na wasaliti ndani ya CCM.
Serikali inaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wanahabari nchini.

Serikali inaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wanahabari nchini.

April 26, 2016

E1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa Serikali inaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wanahabari nchini
E3
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (aliyesimama) akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma  na kusisitiza Wizara yake inavyochangia masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii nchini.
E4
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Possy Abdallah akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma na kusisitiza juu ya Serikali inavyosimamia suala la watu wenye ulemavu nchini. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Walemavu Jenista Muhagama na kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Anthony Mavunde.
E5
Wabunge wakifuatilia mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali inaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wanahabari nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa mbalimbali zinazofanywa na Serikali yao katika nyanja za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ili kuhakikisha Watanzania wanafikia maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipokuwa akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma.
“Waandishi wa habari wapo huru kuuliza maswali kwa Wabunge na kuandika habari kupitia vyombo vyao na kuwapatia wananchi taarifa mbalimbali zinazoendelea bungeni” alisema Waziri Nape.
Kuhusu idadi ya vyombo vya habari nchini, Waziri Nape amesema kuwa Tanzania ni nchi yenye vyombo vingi vya habari yakiwemo magazeti, redio na televisheni ambavyo ni ishara wazi kuwa vyombo hivyo vipo huru kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya tasnia ya habari pamoja na katiba, Sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Waziri huyo alisema kuwa Tanzania sio nchi ya kwanza kutokurusha matangazo ya bunge moja kwa moja (live), utaratibu huo unafuatwa na Mabunge yote ya jumuiya ya Madola.
Waziri Nape amesema kuwa bado Serikali inakusudia kuboresha mazingira ya waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa hali ya uhuru hasa wanapotimiza majukumu yao ya kiundishi wa habari.
Aidha, amewashukuru wabunge kwa uzalendo wao wa kubaki ndani ya bunge na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi yao kwa manufaa ya wananchi wanaowawakilisha.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gorge Masaju amewashukuru wabunge kutimiza haki yao ya Kikatiba kuingia Bungeni na kushiriki mijadala mbalimbali kulingana na ratiba iliyopo
Kwa mujibu wa ibara ya 63 (2), Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kuhusu matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Masaju alisema kuwa Watanzania wanaendelea kupata taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara 18. (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.
Akitoa ufafanuzi wa ibara hiyo Masaju alisema kuwa haki ya kupewa taarifa, siyo haki ya kuonekana na vile vile maamuzi ya Bunge hayafanywi kwa muonekano, bali hufanywa kwa majadiliano ya Wabunge wakiwa Bungeni.
Bunge litaendelea na vikao vyake Jumatano Aprili 27, baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 52 ya Muungano wa Tanzania na ambapo mwaka huu Watanzania wametakiwa kuiadhimisha wakiwa majumbani au wakiwa katika shughuli zao binafsi.
Mapema mwezi huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alielekeza fedha zilizopangwa kutumika katika maadhimisho hayo ambazo ni sawa na Shilingi bilioni 2 za Tanzania zitumike kupanua barabara ya Mwanza Airport katika eneo linaloanzia Ghana Quarters hadi uwanja wa ndege wa Mwanza ili kupunguza adha ya msongamono wa magari katika barabara hiyo Jijini humo.