SALAM ZA SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO LA TANGA

December 25, 2017

WAHAMIAJI HARAMU 224 WAKAMATWA MKOANI TANGA

December 25, 2017
ZAIDI ya  wahamiaji haramu 200 wamekamatwa mkoani Tanga kufuatia operesheni zilizokuwa zikifanyika na Jeshi la Polisi kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu kutokana na kuingia nchini kinyume cha sheria.
Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna  Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi  hilo, Edward Bukombe (Pichani kushoto) wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema wahamiaji hao walimatawa maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Aliwataja wahamiaji ambao walimatwa kuwa ni 55 raia kutoka nchini Somalia,Waethiopia walikuwa 149 na Wakenya walikuwa 20 ambapo alitoa wito kwa watanzania wanaoshirikiana nao kuwaingiza hapa nchini kuacha mara moja vitendo hivyo kabla hawajakumbana na mkono wa kisheria.

“Wahamiaji hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali kufuatia operesheni ambazo zilikuwa zikifanyika lakini niwatake watu wanaoshiriki kuwaingiza wahamiaji haramu hao kuacha biashara hivyo mara moja na watafute nyengine kwani hawatakuwa salama watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria “Alisema RPC.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha 14 kwa kipindi cha mwaka  mzima wakati wa operesheni ikiwa ni mkakati wa kudhibiti matukio ya ujambazi na unyang’anyi wa kutumia silaha mkoani hapa.

“Katika operesheni hizo tulikamata  Pistol 2,Shortgun 3,Gobore 9
ambazo bila shaka hizi kwa namna moja ama nyengine zingeweza kutumika katika masuala mbalimbali ya uhalifu “Alisema.

Hata hivyo alisema Jeshi la Polisi limejipanga imara kuweza
kuhakikisha linazibiti vitendo viovu vinavyoweza kusababisha kutoweka kwa amani kwenye maeneo yao kwa kuwachukulia hatua watu ambao watabainika kuhusikaa navyo.

“Sisi kama Jeshi la Polisi hatujalala tupo macho kila wakati
kuhakikisha wananchi wanakuwa na amani kwenye maeneo yao na wale ambao watakuwa chanzo cha kusababisha amani kutoweka tutakula nao sahani moja kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya dola “Alisema.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA SIKUKUU YA KRISIMASI

December 25, 2017
Na Jumia Travel Tanzania


Ule msimu wa watu kufurahi na kujumuika umewadia tena!


Haina ubishi kwamba sikukuu na mapumziko ya mwisho wa mwaka ambayo huambatana na sikukuu za Krismasi (Desemba 25) na mwaka mpya ndiyo huwa na shamrashamra nyingi zaidi duniani.

Ni kipindi hiko ndicho familia, ndugu, jamaa na marafiki hukutana kwa pamoja na kufurahia kuumaliza mwaka na kuukaribisha mwaka mpya unaofuatia. Mbali na hilo, kutokana na shughuli za mwaka mzima katika kutafuta kipato na kujenga maisha, hiki ni kipindi ambacho watu hupumzisha mwili na akili kwa kufurahia matunda waliyoyachuma kwenye kipindi cha mwaka mzima lakini hata kutafakari namna watakavyoukabili mwaka mpya ambao huja na majukumu na matarajio mapya.


Katika kipindi hiki cha sikukuu mambo mengi hutokea ambayo kwa namna moja ama nyingine endapo hautokuwa makini yatakuacha kwenye hali mbaya. Jumia Travel ingependa kukumbusha wakati ukiwa kwenye ari ya shamrashamra za msimu huu wa sikukuu kuepuka kuyafanya mambo yafuatayo.


Tumia muda wa kutosha na familia. Itapendeza endapo sikukuu ya Krisimasi na mapumziko ya mwisho wa mwaka ukazitumia kufurahia na familia yako. Ni kipindi ambacho miongoni mwenu mpo likizo, watoto wamefunga shule na ndugu hupata fursa ya kutembeleana. Ni jambo la kawaida kuona watanzania mbalimbali kilo kona ya nchi wakifurika kurudi makwao au wengine wakialikana ili kufurahia kipindi hiki. Kamwe usiipoteze fursa hii ya kujumuika na wale uwapendao kwani hutokea mara moja tu kwa mwaka na ni vema ukaitumia ipasavyo.

Zingatia kiwango na aina ya vyakula unavyokula. Kwa sababu katika kipindi hiki kunakuwa na vyakula vya kila aina, ndiyo ukawa unakula tu bila ya kuwa makini. Ulaji wa vyakula tofauti bila ya mpangilio na kiwango maalumu unaweza kukusababishia madhara kwenye mwili wako na kukusesha raha ya kufurahia sikukuu. Hivyo basi, kama inawezekana basi jaribu kuendana na utaratibu wako uliojiwekea wa kula. Usizidishe kwa sababu siku hii vyakula ni vingi.


Kuwa makini na kiasi cha pombe. Ndiyo ni sikukuu, hauna wajibu siku inayofuatia au mtondogoo. Lakini hii isiwe sababu ya kutokuwa makini na kiwango cha pombe unachokunywa. Unywaji wa pombe kuzidi kiwango unaweza kukusababishia mbali tu na uchovu kwenye mwili wako na kushindwa kufurahia matukio ya muhimu na familia yako bali pia hata madhara kwako na watu wanaokuzunguka. Jaribu kuwa mvumilivu kwa kipindi hiki kifupi, furahia kwa kunywa kiasi na familia pamoja na wapendwa wako. Kwa kuongezea, unywaji wa pombe kupitiliza unaweza kukusababishia ukaingia matatani na vyombo vya sheria, kwa sababu ni kipindi cha mapumziko haimaanishi kwamba sheria na taratibu za nchi zimelala.


Tumia pesa kwa makini. Kipindi hiki pia watu wengi hushuhudia wakitumia kiwango cha pesa bila ya kutarajia. Ni vema ukawa umetenga kiwango fulani cha fedha kwa ajili kutumika kwenye msimu huu wa sikukuu. Kama haukufanikiwa kutenga mapema bajeti ya kutumika kipindi hiki basi hakikisha fedha utakayoitumia haitaathiri matumizi yako ya baadaye. Unaweza kufanya hivyo kwa kubana matumizi kwani sio lazima kuwa na shamrashamra kubwa. Kwa sababu ni kipindi cha mwisho wa mwaka na tunafahamu namna maisha yetu watanzania yalivyo, mwaka mpya huja na majukumu kama vile kodi za nyumba, karo za shule, pango za sehemu za biashara, leseni au vibali vya vyombo vya moto nakadhalika.

Usijibane sana, furahia! Inawezekana mipango haijakaa sawa kwenye msimu huu wa sikukuu hivyo kukunyima fursa ya kufurahia vilivyo. Kumbuka, kipindi hiki hutokea mara moja tu kwa mwaka na hautakiwi kujuta sana kwamba kwa nini haukufanikiwa. Ni mafanikio kuwa mzima mpaka kufanikiwa kuuona msimu huu wa sikukuu kwani wengine hawajafanikiwa. Jumia Travel inaamini kwamba kwa kuumaliza mwaka ukiwa na matumaini kutakupa fursa ya kujipanga vema zaidi na mwaka ujao.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHE. LUHAGA MPINA ASHEHEREKEA SIKUKUU YA KRISMAS KWA KUFANYA SHUGHULI ZA KILIMO SHAMBANI KWAKE

December 25, 2017
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.  Luhaga Mpina akishiriki kusafisha shamba lake la mpunga lililoko Kijiji cha Dalla mkoani Morogoro alipokuwa kwenye wa mapumziko ya sikukuu ya  Krismas leo.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akishirikiana na wafanyakazi wake kusafisha shamba lake liliko Kijiji cha Dalla mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kupanda mpunga leo wakati wa mapumziko ya sikukuu ya Krismas.
Moja ya matrekta yaliyoko katika shamba la Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akiliendesha kwa  shughuli za kulima kwa ajili ya maandalizi ya kupanda mpunga wakati Waziri huyo alipokwenda kushiriki shughuli za shamba wakati wa mapumziko ya sikukuu ya Krismas leo.
WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA KUENDELEZA PAMBA

WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA KUENDELEZA PAMBA

December 25, 2017
PMO_4308
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa Onyo kwa watumishi wa umma na Madiwani  wa Manispaa ya Songea kwa kuweka mbele maslahi yao binafsi na akawataka wajirekebishe mara moja.Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa manispaa na madiwani kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Songea, mjini Songea Mkoani Ruvuma
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
………………
*Aaagiza wahusika wachunguzwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Pamba (CDTF) na amegiza wahusika wote wachunguzwe ili kubaini fedha walizokusanya zimetumikaje.

Alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki (Ijumaa, Desemba 22, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao alichokiitisha mkoani Shinyanga kufanya ufuatiliaji wa maagizo ambayo alikwishakuyatoa. Waziri Mkuu alishafanya vikao vitatu na wadau mbalimbali wa zao hilo.

Alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watendaji wa mfuko huo hawajatekeleza majukumu ya kuundwa kwa mfuko huo lakini pia majukumu yao yanaingiliana na yale ya Bodi ya Pamba Tanzania (TCB).

“Kuna CDTF katika zao la pamba lakini hakuna inachofanya ambacho kinawalenga wakulima moja kwa moja. Tunaiondoa CDTF na kazi zake kuanzia sasa zifanywe na Bodi,” alisema.

“Waziri wa Kilimo peleka timu ya ukaguzi kuona wamefanya nini hadi sasa. Tunataka Bodi ifanye kazi na iulizwe maswali kuhusu zao hili. Endapo kuna jambo halijafanyika, Bodi iwe na uwezo wa kutoa majibu si kusubiri tena mtu wa chombo kingine aje kutoa majibu,” alisema Waziri Mkuu.

“Kwa muundo huu, Mkurugenzi wa Bodi anakaa tu, wakati akisubiri kazi yake ifanywe na CDTF,” aliongeza.

Mfuko wa CDTF unaundwa na wajumbe sita ambao ni wawakilishi wa wakulima wawili, wawakilishi wa wenye viwanda vya kuchambua pamba wawili, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba na Mkurugenzi wa Mazao kutoka Wizara ya Kilimo.

Mfuko huu uliundwa mwaka 1999 na Bodi ya Pamba (TCB) ili uwashirikishe wadau wa zao hilo kuondoa matatizo yaliyojitokeza kwenye sekta hiyo baada ya Serikali kujitoa kwenye uendeshaji wa moja kwa moja wa mazao nchini ikiwemo uzalishaji na biashara kutokana na mfumo wa soko huria.

Desemba mwaka jana, Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba alifikia uamuzi kama huo na kuamua kusimamisha shughuli zilizokuwa zinafanywa na Mfuko wa Kuendesha Zao la Korosho Nchini (CIDTF) ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za mfuko huo.

Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam, Waziri Tizeba alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mfuko huo kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu pamoja na kuwapo kwa malalamiko ya muda mrefu kuhusu utendaji wa mfuko huo.

 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAPILI, DESEMBA 24, 2017

MAPOKEZI YA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR LEO UKUMBI WA CCM MKOA WA MJINI AMAAN UNGUJA

December 25, 2017
 MAKAMU Mwenyekiti  wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib, alipowasili katika viwanja vya Afiisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakati wa mapokezi yake
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akifungwa kiskafu na Vijana wa Chipukizi wa Mkoa wakati wa mapokezi yake alipowasili katika Viwanja vya Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amaan
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akifungwa kiskafu na Vijana wa Chipukizi wa Mkoa wakati wa mapokezi yake alipowasili katika Viwanja vya Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amaan
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiangalia ngoma ya kibati wakati wa mapokezi yake yalioandaliwa katika viwanja Afisi Kuu ya CCM Mkoa wa Mjini Amani, baada ya kuwasili Zanzibar wiki iliopita akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu wa CCM na kuchaguliwa tena kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura nyingi.
 WANACHAMA wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wakimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakati wa mapokezi yake.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa CCM meza kuu wakisimama baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa CCM meza kuu wakisimama baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.
 BAADHI ya Wanachama wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa hafla ya mapokezi yake Zanzibar.
 BAADHI ya Wanachama wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa hafla ya mapokezi yake Zanzibar.
 KATIBU wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja Mohammed Omar Nyawenga akitowa Salamu kwa Niaba ya Makatibu wa CCM wa Zanzibar wakati wa hafla ya mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Afisi ya  Mkoa wa Mjini Amaan Unguja
 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdalla Kichupa akitowa salamu kwa niaba ya Wenyeviti wa CCM Mikoa ya Zanzibar wakati wa hafla ya mapokezi ya Makamu Mwenyekiti yaliofanyika katika ukumbi wa CCM Amaan Zanzibar.
 KATIBU wa Chama cha TADEA Mhe Juma Ali Khatib akiwasalimia Wanachama wa CCM wakati wa mkutano huo wa hafla ya mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika ukumbi wa mkutano Afisi ya CCM Amaan Zanzibar.
 Wanachama wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa hafla ya mapokezi yake Zanzibar.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa CCM katika hafla ya mapokezi yake yaliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM MKoa wa Mjini Amaan Zanzibar. baada ya kuwasili akitokea Dodoma wiki iliopita baada ya kuchaguliwa kwa mara ya Pili kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura nyingi katika mkutano Mkuu wa Tisa wa CCM uliofanyika Dodoma.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa CCM katika hafla ya mapokezi yake yaliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM MKoa wa Mjini Amaan Zanzibar. baada ya kuwasili akitokea Dodoma wiki iliopita baada ya kuchaguliwa kwa mara ya Pili kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura nyingi katika mkutano Mkuu wa Tisa wa CCM uliofanyika Dodoma.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa CCM katika hafla ya mapokezi yake yaliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM MKoa wa Mjini Amaan Zanzibar. baada ya kuwasili akitokea Dodoma wiki iliopita baada ya kuchaguliwa kwa mara ya Pili kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura nyingi katika mkutano Mkuu wa Tisa wa CCM uliofanyika Dodoma.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wanachama wa CCM baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya mapokezi yake katika viwanja vya Afisi CCM Mkoa wa Mjini Unguja Amaan. Picha na IKULU

WAFUGAJI BUKOMBE MKOANI GEITA WAWALALAMIKIA ASKARI WANYAMA PORI LA AKIBA KIGOSI

December 25, 2017
Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, wamewalalamikia askari wa pori la Akiba la Kigosi Myobosi kwa madai ya  kuwanyanyasa pindi wanapokamata ng'ombe zao katika pori hilo.

Wakiongea mwishon mwa wiki ,mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega,wafugaji hao wamesema kuwa Mifugo yao inauzwa bila kufuata utaratibu pindi inapokamatwa kwenye pori hilo na matokeo yake wafugaji wanabaki Maskini.

"Magufuli anafanya kazi nzuri sana na hatuamini kabisa kuwa hapendi Mifugo,lakini kuna baadhi ya watendaji wake sio waadilifu kabisa,askari wa Pori la akiba Kigosi Myobosi wakikamata ng'ombe hawatupi fursa ya kulipa faini,badala yake wanataifisha Mifugo yetu na kuipiga mnada bila kufuata utaratibu wa serikali uliowekwa na sisi tunabaki Maskini"alisema mfugaji mmoja.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Mkoa wa Geita Bw.Hamisi Mashaka Biteko ameiomba serikali kutafuta masoko ya uhakika ya mifugo Ili  wafugaji wewe na uhakika wa soko la Mifugo yao.

"Tunaomba serikali ijenge viwanda vya kutosha vya kuchakata nyama Ili wafugaji wenye Mifugo mingi waweze kuuza Mifugo yao,inayobaki wafuge kwa tija"

Kwa Upande wake naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega amesema kuwa Sheria ya Maliasili na utalii inaruhusu kupigwa mnada Mifugo yote inayoingia kwenye mapori ya akiba. lakini wamepeleka mswada Bungeni ili kuzipitia upya sheria hizo .

"Katika Bunge la mwezi wa pili 2018,sheria hizo zitapitiwa upya,nawaombeni sana ikifika wakati huo mjipange vizuri nanyi mtoe maoni yenu"

Awali katibu tawala wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bw.Paul Cheyo, akitoa taarifa fupi ya Wilaya hiyo alimwambia Mhe.Ulega kuwa wao wametekeleza zoezi la kitaifa la upigaji chapa mifugo kwa Asilimia 73.

"Halmashauri inaendelea na zoezi la upigaji chapa mifugo.Wilaya yetu ina jumla ya ng'ombe 130,750, hadi sasa ng'ombe waliopigwa chapa ni 95,743 sawa na asilimia 73".alisema Cheyo.
 Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali baada ya kupokea  taarifa fupi ya  Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali na wafungaji  Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
 .Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji  Mkoa wa Geita Bw.Hamisi Mashaka Biteko  (kushoto)akizungumza katika mkutano huu.
 Mmoja wa wa wafungaji wa akitoa kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
 Sehemu ya viongonzi mbalimbali na wafungaji waliofika katika mkutano huo.

 Sehemu ya viongonzi mbalimbali na wafungaji waliofika katika mkutano huo.

WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU WILAYANI YA GAIRO WAONDOLEWA

December 25, 2017
 Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (kushoto) akiwa pamoja na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bw. David Mahiba pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakati wakitoa elimu kwa wananchi walioshiriki zoezi hilo kwa asilimia 100 kwa amani na upendo.
Wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Vibanda vya wavamizi wa Hifadhi ya Misitu Gairo vikiteketezwa kwa moto.
Miti ya asili yenye zaidi ya miaka 35 ikiteketezwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa. Sehemu kubwa ya miti hii ni miti ya mbao ngumu aina ya mitondoro.



Wadau wa mazingira nchini Tanzania wameombwa kujitokeza kuinusuru wilaya ya Gairo ambayo inahekari zaidi ya 3,000 zilizokuwa zimevamiwa waharibifu wa mazingira.

Kauli hiyo imekuja hivi karibuni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa lakuwaondoa wavamizi wa Misitu ya Hifadhi kabla ya Disemba 31, 2017.

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo alipokuwa akiahitisha Bunge la mjini Dodoma Novemba 18, 2017. Kati ya maeneo ambayo yalikuwa na uvamizi na uharibifu mkubwa wa mazingira ni Misitu ya Hifadhi Wilaya ya Gairo.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya walifanya vikao na wananchi huku wakipitia muhtasari ya vikao vya nyuma vya ushirikishwaji kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa vya kuwaondoa wavamizi hao. 

Aidha kupitia taarifa ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji hicho ambayo ilisomwa na mwenyekiti wa Kijiji ikibainisha utengwaji wa maeneo mbalimbali zikiwemo ekari 1,000 za hifadhi walizogawiwa wananchi kwa ajili ya kilimo.

Vikao vilifanyika kuanzia mwaka 2012 wakati huo Mkuu wa Mkoa akiwa Mhe. Kanali Machibya. Baadae Mkuu wa Mkoa alikuwa marehemu Joel Bendera ambapo nyumba kadhaa ziliteketezwa.Licha ya juhudi zote hizo bado wavamizi hao waligoma kutoka. 

Hivyo basi, kwa kauli ya Waziri Mkuu zoezi limefanikiwa wavamizi wote wameondoka katika Misitu Hifadhi ya No. 30 Kijiji cha Kumbulu Kata ya Chanjale na nyumba zote ziliteketezwa kwa moto.Eneo hilo la misitu lina ukubwa wa ekari 3,000 limepakana na Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa na kutokana na uharibifu huo mkubwa umesababisha hali kubwa ya ujangwa kwa Gairo na maeneo ya Dodoma. 

Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Gairo inategemeana sana na Mkoa wa Dodoma kwenye hali ya hewa kwani uwanda wa juu wa Gairo kupitia milima iliyopo Tarafa ya Nongwe ni kichocheo kikubwa cha hali ya hewa nzuri makao makuu ya nchi Dodoma. Ipo misitu mingine kama misitu ya Hifadhi ya Ukaguru ambayo ni namba tano kwa ukubwa nchini Tanzania. Ipo misitu mingine mikubwa mitatu.

Zoezi hilo liliweza kukamilika kwa asilimia 100 lkinachofuata ni operesheni kubwa ya kupanda miti inayofanywa Wilayani kwa usimamizi makini wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Meneja wake, Bw. David Mahiba.

WASHINDI WA DROO YA PILI MLIMANI CITY WAPATIKANA.

December 25, 2017
Na Mwandishi Wetu.
WASHINDI 20 wa promosheni ya Mlimani City Shoping Fest wamepatika mara baada ya kucheza droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City jijini Dar es Salaam ambao ni Grace Mushi,Samson K. Samson,Grace Hoka, Mnyamani, Mushi Kimaro, Judith Shayo, Erick Msumati, Gwamaka Hezron, Ally Nyaga, Amani Sepetu, Masood Wanani, Jonathan Nkya, Hellen Mngutu, Omary Khary, Linda Bahati, Agrum Maringo, Saidi Kheri, Paul Charles, Beatrice Kaswaga na Suzan Said.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Kampeni hiyo, Neema Utouh alisema mpaka sasa jumla ya washindi 40 wamepatikana tangu Kampeni hiyo izinduliwe rasmi na tayari zawadi zao za vocha ya kufanya manunuzi yenye thamani ya Shilingi 100,000 kila mmoja wameshapatiwa.
Alisema Neema, ni nafasi yakow ewe ambaye hujaja kufanya manunuzi mlimani City karibia fanya manunuzi ya shilingi laki moja au zaidi utapewa kuponi ambayo itakuwezesha kuingia moja kwa moja kwenye droo ya ushindani.
Hii ni wiki ya pili taku promosheni hii izinduliwe na bado wiki tatu ambapo mwisho kabisa kutakuwa na droo kubwa ambayo mshindi mmoja atajishindia vocha yenye thamani ya shilingi 10,000 000 ambayo itamuwezesha kufanya manunuzi duka lolote ndani ya Mlimani City pamoja na washindi watano watakaojishindia vocha yenye thamani ya shilingi milioni moja kila mmoja.
Mwisho Neema alitoa wito kwa wateja wa mlimani City na watu wote kujitokeza kwa wingi kuja kufanya manunuzi Mlimani City katika kipindi hiki cha siku kuu ya Chrismass na Mwaka mpya ili kupata fursa ya kushiriki katika shindano la promosheni ya “Mlimani City Shopping Fest”.

AKatika kusherehekea Sikukuu za X-Mas na Mwaka Mpya, uongozi wa Mlimani City kwa kushirikiana na wafanyabiashara wenye maduka ndani yake umetangaza ofa maalumu kwa wateja  wake watakaofanya manunuzi katika msimu huu wa sikukuu.
Ofa hiyo inatoa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ambazo zimegawanywa kwa makundi matano ambapo kila wiki washindi 20 watajishindia vocha yenye thamani ya kufanya shoping kwa vitu vya thamani ya Shilingi 100,000 lakini pia watakuwa mwameingia moja kwa moja kwenye droo kubwa ya mwisho ambayo mshindi wa kwanza atajishindia vocha ya manunuzi ya bidhaa za nyumbani yenye thamani ya Shilingi Milioni 10, na mshindi 5 watajinyakulia vocha yenye thamani ya shilingi milioni 1, kila mmoja.  

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja mkuu wa Mlimani City Ndugu Pastory Mrosso alisema kuwa washindi wa kila wiki watafanya manunuzi katika duka lolote ndani ya Mlimani City kwa kutumia vocha zao.
Promosheni hii maalumu imeanza Desemba 15 na inatarajia kufikia mwisho Januari 14, 2018, ambapo droo kubwa ya kupata mshindi wa kwanza wa Vocha yenye thamani ya Shilingi milioni 10.
Meneja huyo aliwaomba watanzania kuendelea kufanya manunuzi yao katika maduka ya Mlimani City, kutokana na kuwajali wateja wake na kutoa huduma zinazokwenda na wakati na hasa katika kipindi hiki cha X-Mas na Mwaka Mpya.
 Coordinator/Mratibu wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping fest), Neema Utouh akichanganya kuponi ili kupata washindi 20 wa droo ya pili wa vocha ya thamani ya Shilingi 100,000 kila mmoja ya kufanya manunuzi tena katika duka lolote ndani ya Mlimani City iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City Dar es Salaam.Wengine ni mabalozi wa Promosheni hiyo.
 Coordinator/Mratibu wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping fest), Neema Utouh akifungua kuponi ya msindi wa kwanza wa droo ya pili wa vocha ya thamani ya Shilingi 100,000 ya kufanya manunuzi tena katika duka lolote ndani ya Mlimani City iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City Dar es Salaam.Wengine ni mabalozi wa Promosheni hiyo.
Coordinator/Mratibu wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping fest), Neema Utouh(kushoto) akimkabidhi vocha ya thamani ya Shilingi 100,000, Grace Mushi mara baada ya kuibuka mshindi katika droo ya pili ya promosheni ya fanya manunuzi Mlimani City na ushinde(Mlimani City Grand Shopping Fest) iliyofanyika Mlimani City mwishoni mwa wiki.

BALOZI WA KUWAIT NCHINI AKABIDHI VIFAA VYA MILIONI 18 KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU MKOANI TABORA

December 25, 2017
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Dkt. Amon Mkoga, Bwana Amon Mkoga na kulia kwake ni Mhe.Stella Ikupa Naibu waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu akifuatiwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe.Jasem Al Najem, Ubalozi wa Kuwaiti umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.

Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa leo

MHE MWANJELWA AWATAKA WAKUFUNZI WA VYUO VYA KILIMO NCHINI KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

December 25, 2017
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Kitalu Nyumba (Green House) katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji ch a Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo, Juzi 22 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kukagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.

Na Mathias Canal, Mtwara

Wakufunzi wa Vyuo vya Kilimo kote nchini wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kufanya kazi kwa Weledi, Ubunifu na Maarifa ili kuongeza tija katika majukumu yao ya kufundisha wanafunzi ambapo baadae wanazalisha wataalamu mbalimbali katika sekta ya Kilimo.

Kauli hiyo imetolewa juzi 22 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini.

Alisema kuwa watendaji hao wanapaswa kuwa wabunifu katika nyanja mbalimbali zitakazowawezesha kuwa na kipato cha ziada kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni.

Alisema kuwa kufanya hivyo kutawanufaisha kuwa na kipato kitakachowawezesha kuendesha chuo pasina kutegemea serikali kwa kina jambo ambalo litapunguza malalamiko dhidi ya serikali kufanya kila kitu.

Aidha, alisisitiza viongozi wa vyuo vyote vya Kilimo nchini kutumia vyombo mbalimbali vya Habari sambamba na mitandao ya kijamii ili kutangaza maudhui ya vyuo na kozi zinazofundishwa ili kurahisisha wanafunzi kupata wepesi katika uchaguzi wa vyuo vya kusoma.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alitembelea na kujionea miundombinu ya Taasisi na kazi za mafunzo ikiwa ni pamoja na kuangalia shughuli za uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo alimpongeza Naibu Waziri huyo wa Wizara ya Kilimo kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na hatimaye kuteuliwa kumsaidia katika majukumu yake ambapo pia ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa.