HIVI NDIVYO KATIBU WA BAWACHA MKOA WA TANGA ALIVYOZUNGUMZA NA WANANCHI WA KATA YA MARAMBA WILAYANI MKINGA

May 16, 2015
KATIBU WA BARAZA LA WANAWAKE CHADEMA MKOA WA TANGA(BAWACHA) RACHAEL SADICK AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA MAENEO YA MARAMBA WILAYA MKINGA JUZI WAKATI WA ZIARA YAKE

KATIBU WA BARAZA LA WANAWAKE LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MENDELEO (CHADEMA) WA PILI KUTOKA KULIA AKIWA NA VIONGOZI WENGINE WA MKOA WA TANGA WAKIFUATILIA MKUTANO HUO




MEYA WA ILALA AFUNGUA UZINDUZI WA UJENZI WA ZAHANATI YA MBONDOLE, MSONGOLA

May 16, 2015

Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akizungumza na wananchi wa Kata ya Msongola, Kijiji cha Mbondole katika uzinduzi wa Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji hicho jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Msongola, Angelina Makembeka akimshukuru Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa kwa kutembelea kijiji cha Mbondole jijini Dar es Salaam.
Mwanyekiti wa kijiji cha Mbondole akizungumza jana na wananchi wa kijiji hicho katika uzinduzi wa Ujenzi wa Zahanati ya Mbondole.
Mhasibu Mkuu wa Idara ya Afya wa Manispaa ya Ilala Geoffrey Massi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mbondole katika uzinduzi wa Zahanati ya Mbondole.
Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kifua Kikuu, Ukoma na UKIMWI wa mkoa wa Ilala DK. Mbarouk Seif Khaleif,katikati ni Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Reuben Ngalomba na Mhasibu Mkuu wa Idara ya Afya wa Manispaa ya Ilala Geoffrey Massi wamkisikiliza kwa makini Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa hayupo pichani wakati akizungumza katika uzindizi wa Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Mbondole, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Kijiji cha Mbondole.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mbondole, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
MATUKIO BUNGENI DODOMA

MATUKIO BUNGENI DODOMA

May 16, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Kazi na Ajira , Gaudencia Kabaka kwenye viwanaj vya Bunge mjini Dodoma Mei 15, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) bu2 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi kwenye viwanja vya Bunge Mei 15, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) bu3 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa Viti Maalum, Christawaja Mtinda (kushoto) na Christina Lissu  Mughwai a(katikati) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Mei15, 2015
CHAMA CHA MAPINDUZI CCM CHAAHIRISHA VIKOA VYA HALMAHAURI KUU NA KAMATI KUU

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM CHAAHIRISHA VIKOA VYA HALMAHAURI KUU NA KAMATI KUU

May 16, 2015

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habar katika ofisi za CCM makao  makuu jijini Dar es salaam wakati akizungumzia kusogezwa mbele kwa vikoa vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.(PICHA NA KIKOSIKZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2 
Nape Nnauye akisisitiza jambo katika mkutano huo wakati wa mkutano huo. 3 
Baadhi ya wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………………………………………….
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeahirisha vikao vya Kamati kuu na Halmashauri kuu ya chama hicho vilivyotakiwa kuanza Mei 20 hadi 22 ,mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Katibu wa Nec,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,amesema sababu ya kuahirisha vikao hivyo ni kupisha ratiba ya vikao vya baraza la wawakilishi vitakavyoanza Mei 18 mwaka huu.
”Vikao vya baraza la wawakilishi vitaanza Mei 18 hadi 21,vikao hivi ambavyo vitafanyika mfululizo vitatoa ratiba ya wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais wa Zanzibar,Wabunge na Baraza la Uwakilishi,”amesema Nape
Nape alisema ratiba hiyo itawezesha wagombea kujitangaza na kuchukua fomu kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

LOWASSA ATIKISA ARUSHA,ACHANGISHA ZAIDI YA SH,MIL 200 ,KUTANGAZA NIA MEI 24 MWAKA HUU

May 16, 2015

SAM_2715
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2723 
Umati mkubwa wa wananchi wa Arusha wakiwa wanampungia mkono Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
SAM_2688 
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh mkuu wa Bakwata mkoani  Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika hafla ya harambe ya ujenzi wa  msikiti wa Patandi iliyofanyika jana katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana
SAM_2682Mkurugenzi wa kituo cha Redio 5 Arusha Francis Robart akiwa anawasilisha jumla ya fedha zilizopatikana katika harembee hiyo kwa Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa
SAM_2709 
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa  msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
?????????????
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anasalimiana na baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee.
SAM_2716 
Taswira ya picha wakati Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anaondoka katika uwanja wa msikiti mkubwa jijini Arusha.
SAM_2727
?????????????
Msafara wa pikipiki
SAM_2695Mgombea anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini kupitia CCM, Mustafa Panju ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bush Buck Safaris  akiwa anasalimiana na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa baada ya kumkabidhi shilingi Milioni sita kwaajili ya ujenzi wa msikiti Patandi
SAM_2693Diwani Mathias Manga  akiwa anawasilisha mchango wa rafiki yake wa karibu Husein Gonga wa shilingi Milion saba
SAM_2679Mkurugenzi wa Redio 5 Arusha Francis Robart  kulia wakiwa wanapiga hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana
SAM_2730Muonekano jiji la Arusha
SAM_2660Kada maarufu wa chama cha CCM,Violet Mfuko katikati akiwa na diwani viti maalum Vick Mollel wakiwa wanamshangilia mgeni rasmi Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo. 
SAM_2669Kushoto ni mtia nia jimbo la Arumeru mashariki Solom Sioi pamoja na mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima wakifatilia jambo katika harambee hiyo
SAM_2673Mbunge wa Kigoma mjini Peter Serukamba akiwasilisha mchango wake.
SAM_2672
SAM_2665
Wananchi wakiwa wanamsikiliza Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa.
……………………………………………………………………….
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa anatarajia kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mnamo Mei 24 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.
Lowasa,alitoa kauli hiyo leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo alifanikisha kuchangisha jumla ya zaidi ya kiasi cha sh,200 milioni ambapo watu mbalimbali walimuunga mkono katika harambee hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo leo kwa mafumbo Lowasa alisema kuwa mnamo Mei 24 mwaka huu anataraji kusema neno ambalo atahitaji wananchi wamuunge mkono siku hiyo.
 
“Niseme neno nisiseme,tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid siku hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono ambalo nitahitaji mniunge mkono “alisema Lowasa
 
Lowasa kwa kujiamini aliwaomba kila mkazi wa Arusha siku hiyo kutoka na kuja uwanja huo na kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini.
 
“Ukiulizwa unaenda wapi sema unakuja kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini”alisisitiza Lowasa 
 
Hatahivyo,Lowasa aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya Askofu wa kanisa katoliki la jimbo kuu mkoani Arusha,Josephat lobullu kusimamia amani ya mkoa huo.
 
Aliipongeza kamati hiyo na kusema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko jambo lolote kwa kuwa Arusha ni mji ambo ni chanzo cha utalii duniani.
 
“Tuendelee kuheshimiana bila kujali misingi ya dini,kabila au rangi lakini niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha kwa kuwa Arusha ni mji wa kitalii bila amani hakuna utalii Arusha”alisema Lowasa na kuibua shangwe

NYALANDU: NASARI MZUSHI

May 16, 2015

Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema kauli zilizotolewa Bungeni na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ni za kutapatapa na zimejaa ukosefu wa busara na uzushi.

Amesema mbunge kusimama bungeni na kutoa kashfa badala ya kueleza masuala ya kisera au kiutendaji ni kupungukiwa busara na jamii haina budi kumpuuza.


Akichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni juzi, Nassari alisema Nyalandu kazi yake kubwa ni kuzunguka katika mapori ya akiba na kupiga picha na askari pamoja na kushangaa mbwa wa kizungu na kupokea ndege, helkopta za msaada. Alisema utendaji huo na mawaziri wengine unaweza ukawa ni ishara ya serikali iliyochoka.



Hata hivyo, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Nyalandu alisema Nassari anapaswa kuwakilisha na kutetea wapigakura wake kwa hoja badala ya kuropoka masuala ambayo hayana tija.


Alisema kauli zinazotolewa na wapinzani bungeni akiwemo Nassari kuishutumu serikali kuwa imechoka na kujaribu kuichonganisha na wananchi, kamwe hakuwezi kuikatisha tamaa kwa kuwa uzushi kwa upinzani ni jambo la kawaida.


Alikumbusha kuwa mapema mwaka huu alifanya ziara wilayani Arumeru ikiwemo jimbo la Nassari kutatua mgogoro baina ya wananchi na hifadhi, ambapo mbunge huyo alimtia moyo na kumtaka kupuuza kauli za kukatisha tamaa zinazotolewa dhidi yake.



“Hizi kauli za Nassari ni za kitoto na haziwezi kuleta tija kwa wapigakura wake…asimame kuzungumzia utendaji na masuala ya kisera sio kashfa ambazo hazipo…Namshauri awatumikie wapiga kura wake.



Nilifanya ziara jimboni kwake kutatua mgogoro na alinitia moyo kutokata tamaa na kauli za watu wanaonibeza na kunipongeza kwa utendaji kazi wangu,” alisema Nyalandu katika taarifa yake.



Taarifa hiyo pia ilikariri kauli ya Nassari aliyoitoa katika mkutano wa viongozi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, ambapo mbunge huyo na Aggrey Mwanry (Siha) walihudhuria akisema: “Naomba kukutia moyo kwani anayefanya kazi ya Mungu atapata nguvu, nikisikia mtu bungeni anasema wewe ni waziri mzigo, mimi nitaruka juu na kumwangukia vibaya.”



Imeeleza kuwa mafanikio makubwa ambayo wizara hiyo imepata kwa kumaliza migogoro ya ardhi mingi kwa muda mfupi wakati alipotembelea mapori ya akiba na hifadhi za taifa zenye migogoro ya ardhi na wananchi na kuipatia ufumbuzi.



Akiwa huko amekuwa na utaratibu wa kuzungumza na askari wa wanyamapori pamoja na wananchi kusikiliza kero zinazowakabili.



Miongoni mwa maeneo ambayo Nyalandu ametembelea ni wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, ambako kulikuwa na mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa vijiji 21 na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, uliodumu kwa miaka zaidi ya mitano bila kupatiwa ufumbuzi.



Nyalandu alimaliza mgogoro huo kwa kuruhusu wananchi wa vijiji hivyo kuendelea na maisha kama kawaida na kuagiza kufanyika kwa ukaguzi wa mipaka ya eneo hilo upya.



Awali, wananchi wa Mbarali waliishitaki serikali kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ambaye aliitaka serikali kumaliza mgogoro huo kwa maslahi ya wananchi.



Maeneo mengine yenye mgogoro ambayo Nyalandu alifanya ziara kwa lengo la kutoa ufumbuzi ni Pori la Burigi wilayani Biharamulo, Iringa, Masasi, Lamadi ambako alikutana na wafugaji kutoka mikoa yote nchini pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Saadani wilayani Bagamoyo ambako pia kulikuwa na mgogoro wa ardhi.



“Ninapofanya ziara natekeleza majukumu yangu kama waziri, siwezi kukaa ofisini wakati kuna mgogoro baina ya wananchi na hifadhi za taifa na mapori ya akiba…nina dhamana ya kushughulikia mambo haya hivyo, kauli za kitoto kamwe haziwezi kunikatisha tamaa,” aliongeza Nyalandu.



Aidha, aliongeza kuwa katika kuhakikisha serikali inashinda vita dhidi ya ujangili, amekuwa mstari wa mbele kushirikiana na wadau wa uhifadhi na kwa jitihada zake amefanikisha kupatikana kwa ndege, helkopta na vifaa vingine ili kukabiliana na majangili.



Alisema vifaa hivyo ikiwemo ndege, magari, helkopta, silaha na vitendea kazi vingine hukabidhiwa kwake na baadaye huvikabidhi kwa watendaji wake kwa ajili ya kukagiwiwa kwenye hifadhi za taifa na mapori ya akiba.



“Tumeanzisha vita dhidi ya majangili hivyo ni lazima tuwe na vitedea kazi vya kutosha, nimefanya jitihada za kupata helkopta, ndege, silaha za kisasa, magari na juzi Marekani imetupa mbwa maalumu ambao tutawatumia pia kwenye viwanja vya ndege na bandarini kwa usalama zaidi.



“Sasa Nassari anaumia kuona hizi jitihada zetu kama serikali katika kulinda rasilimali zetu au alitaka akabidhiwe yeye,” alihoji Nyalandu.



Akizungumza kupiga picha na askari wa wanyamapori, Nyalandu aliwapuuza watu wenye mawazo tofauti akisema si jambo baya kufurahi na wapiganaji wake, ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi wa maisha yao msituni.



Alisema amekuwa na utaratibu wa kufurahi pamoja, kula na kunywa na askari wa wanyamapori pindi anapofanya ziara zake katika hifadhi na mapori ya akiba.



“Watu wenye nia mbaya siku zote ndio wamekuwa na imani potofu, ninapofanya ziara kwanza nawafikiria wapiganaji wetu wanaoishi msituni kukabiliana na majangili hatari…siwezi kwenda huko na kukunja sura kama tuna ugomvi bali baada ya kupeana maagizo ya kazi tunakuwa kitu kimoja, tunafurahi na kutiana moyo ili kuongeza ari ya kulinda rasilimali za taifa. Kauli zingine zinasikitisha mno,” alisema.

HABRI KATIKA PICHA

 WAZIRI Nyalandu akikagua gwaride la askari wa wanyamapori wakati akiwa kwenye moja ya ziara zake.

 Waziri Nyalandu akikagua nyara a serikali zilizokamatwa kutoka kwa majangili alipokagua moja ya mbuga za wanyama kwenye moja ya ziara zake hivu karibuni
 NYALANDU akiwa kwenye picha ya pamoja na askari wa wanyamapori, maofisa na wafanyakazi wa Pori la Selous, muda mfupi baada ya kuzungumza nao na kupeana mikakati ya kiutendaji.

 Waziri Nyalandu akikagua meno ya tembo yaliyokamatwa kutoka kwa majangili kufuatia operesheni zinazofanywa na askari wa wanyamapori.
  WAZIRI Nyalandu (katikati) akiwa amezungukwa na wananchi wilayani Chemba alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa kijiji na hifadhi ya misitu.
 WAZIRI Nyalandu akiwa na wanafunzi wa Sekondari ya Selous wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za uhifadhi na vita dhidi ya ujangili, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi shuleni hapo.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akila chakula cha mchana na wanafunzi wa sekondari ya Selous, iliyopo Kijiji cha Lukuyu Sekamaganga wilayani Namtumbo, Ruvuma.

 WAZIRI Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na vijana wanaounda vikundi vya ulinzi kwa lengo la kukabiliana na ujangili kwenye maeneo ya Pori la Akiba la Selous wilayani Namtumbo.

Jinsi Rais Kikwete alivyongoza Sherehe za Kilele Cha wiki ya Elimu jana Mkoani Dodoma.

May 16, 2015

 Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015. 
 Balozi wa Chini nchini Tanzania,Lu Youging akizungumza jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015,kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Anne Kilango Mallecela. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwanafunzi Agatha Julius Ninga kutoka Shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora akiwa ni miongoni mwa wanafunzi sita waliofaulu vizuri katika mitihani ya sayansi ya kidato cha nne mwaka jana 2014.Agatha alifanya vizuri katika somo la Biolojia.Rais Kikwete alitoa zawadi kwa wanafunzi, shule,halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa kumaliza Elimu ya msingi na elimu ya sekondari.Tuzo na zawadi hizo zilitolewa leo katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu nchini.
Waziri wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa akitoa tuzo maalum kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Elimu kitaifa iliyofanyika mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wanafunzi Maria Sagasii na Neema Harry kutoka Shule ya msingi ya Ignatius ya mjini Dodoma wakionyesha viungo vya ndani vya mwili wa binadamu somo la Biolojia katia banda la maonyesho katika Uwanja wa michezi wa Jamhuri wa mjini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu leo.
 Baadhi ya Wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mjini Dodoma waliohudhuria sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15,2015 .PICHA ZA FREDDY MARO, IKULU.