WAPENDANAO WA TATU MZUKA WAZIDI KUJIZOELEA MAMILIONI

February 12, 2018
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la Aslay akimhoji mmoja wa wapendanao Mwanaidi Msangi ambaye alikuwa ni mmoja kati ya Washindi na Mpenzi wake Kelvini Gibson pichani kulia.Wakazi hao wa Buguruni malapa walijinyakuliwa milioni kumi na kugawana kila mmoja milioni tano,kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Nandy
Kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Nandy akimhoji mmoja wa wapenda nao Kelvini Gibson,wakazi wa Buguruni malapa waliojinyakuliwa milioni tano tano kwa kila mmoja mwishoni mwa wiki,katika kushiriki kampeni ya Wapendanao ilionzishwa na mchezo huo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka,uliobeba kauli mbiu iliyojulikana kwa jina la 'Ukishinda na umpendae anashinda' ,kushoto ni  Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina Aslay
Pichani kati ni Wawili wapenda nao Mwanaidi Msangi pamoja na Kelvin Gibson wakiwa sambamba katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshika mfano wa hundi ya shilingi milioni Kumi waliojishindia kwenye muendelezo wa kampeni ya Wapendanao ilioanzishwa na Tatu Mzuka, Kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Nandy pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la Aslay,ambao kwa pamoja wanatarajiwa kutumbuiza jumamosi hii katika ufukwe wa kiota cha maraha cha Escape One,Mikocheni jijini Dar.

-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

Wakazi Mwananyamala wavutiwa na huduma za 'One Stop Centre' za CRC

February 12, 2018
Mwanasheria wa Kituo cha Usuluhishi–CRC, Suzan Charles (kulia) akitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jana jijini Dar es Salaam.

Afisa wa Polisi na Mratibu wa Kituo cha One Stop Center (OSC) Amana, Bi. Christina Onyango (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja waliofika kupata huduma leo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wahudumu wa afya kwenye kituo hicho akitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika kupata huduma.


Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.

Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.


Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya wananchi wanaoishi Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam wamevutiwa na huzahuduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ namsaada wa ushauri kisheria zilizotolewa jana na Kituo cha Usuluhishi – CRC.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi waliopata huduma hizo kwenye Ofisi yaMtendaji Kata ya Mwananyamala 'A' walisema wamefurahishwa na kitendo cha CRC kusogezahuduma hizo eneo lao jambo ambalo limewavutia wakazi wengi.

"...Binafsi nimevutiwa na kitendo cha huduma kama hii kutolewa eneo letu, mimi nilikuwa nakesi kuna mtu anataka kunidhulumu kiwanja kesi yangu inaendelea lakini baada ya kuona
kuna huduma hizi nimekuja kupata msaada wa kisheria na nimeshauriwa cha kufanya...,"alisema Bi. Nzela Khamis akizungumza mara baada ya kuhudumiwa.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Usuluhishi – CRC, Bi. Violeth Chonya akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio alisema Mwananyamala kumekuwa namuitikio mkubwa kwa wananchi kujitokeza kupata huduma za pamoja kwa waathirika kwavitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

Alisema jumla ya kesi 31 wamezisikiliza na kufikia hatua mbalimbali huku kesi mbili zamatuzo kwa watoto zikitatuliwa baada ya kukutanishwa pande zote mbili na wazazi kufikiamuafaka juu ya mvutano wao.

Bi. Chonya alisema kwa muitikio wa wananchi wa leo umeonesha kuna uhitaji mkubwa wa

huduma hizo hivyo kuwashauri wananchi wa Mwananyamala kujitokeza tena kesho ambapohuduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ naushauri wa kisheria utatolewa.

"...Kimsingi bado uhitaji ni mkubwa hivyo tunawashauri kesho wananchi wanaohitaji hudumahizi wajitokeze tena kesho tunaendelea kutoa huduma zetu, na baadhi ambao watashindwa
uja kesho wanaweza kuja ofisi za TAMWA Sinza Mori kwenye ofisi zetu (CRC) watahudumiwapia," alisema Bi. Chonya.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI, PIA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU PAMOJA NA MWENYEKITI WA BODI YA SHIRIKA LA MAWASILIANO LA TANZANIA TTCL CORPORATION IKULU DAR ES SALAAM

February 12, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke  aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya mazungumzo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu  mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Waziri Kindamba aliyefika Ikulu pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Waziri Kindamba Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari kuhusiana na Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Waziri Kindamba




Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu akizungumza kuhusu Shirika hilo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha  na  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Waziri Kindamba Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU