Kampuni ya Bia Serengeti yazindua mradi wa maji wa 81m/- Katesh, Hanang

June 24, 2016

Mradi wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha akizungumza na wananchi wa katesh wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wenye uwezo wa kuhudumia wakazi wapatao 12000 katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang ,mkoa wa Manyara.


Diwani wa Kata ya Gidahababieg,Hassan Hilbagiroy akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata hiyo mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang, mkoa wa Manyara.

Mmoja wa wakazi wa Kata ya Gidahababieg,Katesh akifurahia maji mara baada ya ufunguzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang, mkoa wa Manyara.


Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Thobias Mwilapwa akiwa na picha ya pamoja na wananchi mara ya baada ya ufunguzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang mkoa wa Manyara.



Hanang, Juni 22, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua mradi wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang’ ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.

Mradi huo wenye uwezo wa kuwahudumia watu 12,000 unajumuisha kisima kilichochimbwa pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ukiwa na uwezo wa kuzalisha  lita 45,000 za maji kila baada ya saa sita.

Akizungumza latika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha,  alisema kuwa kisima hicho ni mkakati wa kampuni hiyo ya bia wa kuisaidia jamii chini ya mpango uitwao Maji ya Maisha na kuongeza kuwa SBL imeshatekeleza  miradi kama hiyo katika mikoa ya   Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma  ambayo imenufaisha watu zaidi ya milioni moja kwa kuwapatia maji safi na salama.

Wanyancha alisema kuwa mradi wa Katesh  sio tu kwamba utaboresha afya za wenyeji wa eneo husika bali pia utaongeza uzalishaji  kiuchumi “hususani miongoni mwa wanawake na watoto wa kike  ambao hawatalazimika kutumia saa nyingi   kutafuta maji sehemu nyingine. Hii inatoa fursa kwa watoto wa kike kuhudhuria masomo shuleni.”

“Kampuni ya Bia ya Serengeti ina sera iliyojikita katika kuleta ustawi wa jamii ambapo Maji ya Uhai ni mojawapo ya maeneo manne iliyoyapa kipaumbele. Maeneo mengine utoaji wa Stadi za Maisha, Uendelevu wa Mazingira na Kuhimiza Unywaji wa pombe Kistaarabu.

Mkurugenzi huyo wa mahusiano aliongeza kuwa SBL  ina programu ya kilimo  ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imewasaidia  wakulima zaidi ya 100  hapa nchini kwa kuwapatia misaada ya kitaalamu na kifedha ambapo imewasaidia  kuboresha maisha yao pamoja na maisha ya jamii zao.

Aidha Wanyancha aliongeza: “Kupitia mpango huu wa kusaidia SBL imeweza kuongeza upatikanaji wa shayiri inayotumika kama malighafi katika utengenezaji wa bia kutoka tani sifuri 10,000 jambo ambalo limechochea ukuaji wa kasi wa kampuni yetu.”

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Tobias Mwilapwa  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ameipongeza kampuni ya SBL kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidi miradi ya kijamii nchini jambo ambalo amesema ni chachu katika kuiletea jamii maendeleo.

“Licha ya  kuchangia katika  kukua kwa uchumi wa taifa  kupitia malipo ya kodi kwa wakati, kampuni ya Serengeti  imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa  hususani katika uzinduzi wa huduma za miradi ya maji safi na salama  nchini,” alisema.

photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Website;www.koncept.co.tz
DK. MENGI ACHANGIA MADAWATI 1,000, ATOA SOMO KWA WATU MATAJIRI

DK. MENGI ACHANGIA MADAWATI 1,000, ATOA SOMO KWA WATU MATAJIRI

June 24, 2016
Katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza tatizo hilo katika wilaya hizo.

Akizungumza katika halfa ya kukabidhi pesa hizo kwa wakuu wa wilaya wa kampuni hizo, Dk. Mengi alisema ni muhimu kwa watanzania kuungana kwa pamoja na kusaidia kupatikana kwa madawati kwani kwa kufanya hivyo ni kulisaidia taifa.

Hata hivyo Dk. Mengi alisema kuwa anaamini kama watu matajiri nchini wakiungana kwa pamoja na kujadili jinsi ya kumaliza tatizo la madawati nchini basi jambo hilo litaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka tofauti na sasa ambapo linakwenda kwa mwendo wa kusuasua.

"Ukisaidia mtu mmoja katika elimu ni sawa umesaidia jamii na taifa kwa ujumla kama watu matajiri wakisema wakae kwa pamoja na kuangalia jinsi ya kumaliza tatizo hili linaweza kutatuliwa na shida ya madawati kumalizika.

Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akizungumza katika halfa ya kukabidhi milioni 70 kwa wilaya ya Handeni na Bagamoyo ambazo zitawezesha wilaya hizo kununua madawati 1,000 na kila wilaya kupata madawti 500.

"Matajiri wanatakiwa kutambua kuwa wanatakiwa kurudisha shukrani zao kwa Mungu, taifa na wananchi na hasa kwa walio na hali ya chini kwani hao ndiyo wanaowasaidia kufanya biashara zao kwa amani," alisema Dk. Mengi.

Aidha amewataka wakuu wa wilaya hizo kuondoa hofu ya kufukuzwa kazi kama watakuwa hawajakamilisha na wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuongeza juhudi huku akiwashauri kuandaa mikutano katika wilaya zao na kushirikisha wananchi wao ili waweze kuchangia na hatimaye tatizo hilo kumalizika.

Kwa upande wa mkuu w wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga na mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab wamemshukuru Dk. Mengi kwa msaada ambao amewapatia na kuwataka watanzania wengine kuwa na moyo wa kujitolea kama jinsi amevyofanya Dk. Mengi kwa kuchangia upatikanaji wa elimu bora.

Awali kabla ya msaada ambao umetolewa na Dk. Mengi, wilaya ya Bagamoyo ilikuwa ikikabiliwa na upungufu wa madawati 2,463 na Handeni ikikabiliwa na tatizo la upungufu wa madawati 4,000.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab akizungumza katika halfa hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga akizungumza katika halfa ya kupokea pesa kwa ajili ya madawati 500 yatakayokwenda katika wilaya yake kusaidia kupunguza tatizo la madawati.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akisaini mfano wa hundi kabla ya kuanza kuwakabidhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35, Mkuu wa wilaya ya Haneni, Husna Rajab. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mji wa Handeni, Kenneeth Haule, Mwenyekiti wa Mji wa Handeni, Twaha Mgaya na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Handeni, Ramadhani Diliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 500, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Chalinze, Edes Lukoa, Mkurugenzi wa Bagamoyo, Natujwa Melau, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Issa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu.
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.