MOJA YA NDEGE MPYA ZA ATCL YAWASILI JIJINI DAR LEO

MOJA YA NDEGE MPYA ZA ATCL YAWASILI JIJINI DAR LEO

September 20, 2016
nd1
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
nd2
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016
nd3 nd4
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016
nd5 nd6
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na Rubani aliyerusha Ndege mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
nd7
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016
nd8 nd9 nd10 nd11
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu mara baada ya  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016, Wengine ni marubani wa ndege hiyo
PICHA NA IKULU


     Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye

DC MUHEZA APIGA MARUFUKU BODABODA KUENDESHWA ZAIDI YA SAA SITA

September 20, 2016


Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ambapo alipiga marufuku kuendeshwa usiku zaidi ya saa sita.

Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ambapo alipiga marufuku kuendeshwa usiku zaidi ya saa sita.


Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (Das) akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya hiyo,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kushoto na anayefuata ni Mwenyekiti wa Waendesha Boda Boda wilayani Muheza
 
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa Biashara wa wilaya hiyo,Ally Mokiwa akielezea namna walivyojipanga kuhakikisha waendesha bodaboda hao wanakata leseni za kuendesha shughuli zao katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo
wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani Muheza(DTO) Herbert Kazonde wakati wa mkutano huo na waendesha bodaboda uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.

Katibu wa Chama cha Waendesha Boda Boda wilayani Muheza,Francis Gerald akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto ambazo zinawakabili


Baadhi ya waendesha bodaboda wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo alipokuwa akizungumza nao kusisitiza umuhimu wa wao kutii sheria za usalama barabarani ikiwemo kuacha kufanya vitendo vya uhalifu


 Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimepaki kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza huku madereva wakiwa kwenye kikao chao na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo