TPST yawanoa wajasiriamali Mkinga.

TPST yawanoa wajasiriamali Mkinga.

April 20, 2013
Na Mwandishi wetu,Mkinga.
TAASISI ya Sekta Binafasi Tanzania (TPST)leo imeendesha semina ya mafunzo ya elimu ya wajasiliamali kwa vikundi vya Tawsei kwa wanachama wake wapato 50 kutoka maeneo mbalimbali katika kata ya Maramba wilayani Mkinga.


Akizungumza ufunguzi wa mafunzo hayo,Mshauri Mwelekezi wa mafunzo ya Biashara(BD Provider)Jane Gonsalves amesema mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha wajasiliama mali hao pamoja na kujengea uwezo katika uendelezaji wa shughuli zao za ila siku.

Gonsalves amesema suala la ujasiria mali ni ajira kwa vijana kutokana na ajira kuwa ngumu hivyo kutokana na kuwepo kwa hali hiyo katika jamii yetu taasisi hiyo imeona bora kuanzisha ajira wa vijana kwa kuwapatia elimu ya ujasiria mali ili kuwewezesha kufanya shughuli zao na kuweza kupata mafanikio.

Amesema umuhimu wa sekta binafasi inajumuisha wafanyabiashara wa aina mbalimbali wakubwa,wakati na wadogo katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutoa ajira zaidi ya asilimia 80 kwa watanzania wote katika kujipatia riziki za kila siku.

Aidha ameongeza kuwa sekta binafasi ni mwajiri wa hiari hususani kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wengi wao wakiwa wameingia katika sektta binafsi bila maandalizi ya kutosha ya elimu ya ujasiriamali na kushindwa kabisa kuendesha biashara bila kujua kwamba mafanikio katika biashara yanataka maandalizi ya muda mrefu na ambayo ni makini.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo,Afisa Tarafa wa kata ya Maramba wilayani Mkinga,Nisa Mwakibete amesifu jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo kuwajengea uwezo wajasiriamali na kuwataka washiriki kuyatumia vema mafunzo hayo katika kuendesha shughuli zao kila siku pamoja na kuhakisha wanapata mafanikio kwa kujiwekea malengo endelevu.

Kwa upande wake,Mratibu wa Asasi ya kiraia isiyokuwa ya kiserikali ya Tanzania Woman For Self Imlietive,Benadeta Choma amesema asasi yao imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuwaendeleza wajasiria mali ili waweza kujikomboa kutoka katika hali duni na kwenda katika hali nzuri kimaisha

Choma amesema asasi hiyo pia imeona bora ijikinge pembezoni ili kuweza kuwatumikia wananchi katika maeneo yao pamoja na kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye jamii.

Semina hiyo imeanza leo na itakuwa ni ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wajasiria mali waliopo kwenye kata hiyo.
Mwisho.

Umependeza sana mdau,wikiendi njema.

April 20, 2013
Jamani leo ni Jumamosi wadada wazuri kama hawa wanakuwa na nafasi nzuri sana ya kubadilishana mawazo na wafanyakazi wenzao hasa kwenye kipindi hiki cha mapumziko,nawatakieni mapumziko mema hii picha ni ya mdau wa blog hii na dada yetu Sussan Uhinga mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Tanga akiwa amepozi akisubiri wageni wake.

Picha za Bangi iliyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga.

April 20, 2013
Bangi yenye kg 178 iliyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Tanga katika matukio mawili toafuti.

HII SIO NZURI KWA MATUMIZI YA BINADAMU.

April 20, 2013
KAMANDA wa Polisi mkoa wa Tanga,Constatine Massawe akiwaonyesha waandishi wa habari vifuruhsi vya Bangi iliyokamatwa na Jeshi hilo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa ambapo jumla ya kg 178 zilikamatwa picha na Mwandishi Wetu
Kg 178 za Bangi zakamatwa Tanga.

Kg 178 za Bangi zakamatwa Tanga.

April 20, 2013
Na Oscar Assenga, Sussan Uhinga, Tanga.
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kukamata kg 178 za madawa ya kulevya aina ya bangi zenye thamani ya sh.milioni 2,670,000 katika matukio mawili tofauti mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Constatine Massawe alisema katika tukio la kwanza lilitokea Aprili 19 majira ya 2.45 usiku kufuatia taarifa toka kwa wasamaria wema na askari walifika eneo la Mwanzang’ombe Chumbageni jijini Tanga, kwenye nyumba ya Hemed Salum Hugo ambaye alifanikiwa kutoroka kabla ya polisi kufika eneo hilo.

Alisema baada ya polisi kufika katika eneo hilo walianza kupekua nyumba hiyo na kukuta madawa ya kulevya aina ya bangi kg 100 ambayo ilikuwa imepakiwa kwenye vifurushi na nyengine ilikuwa imehifadhiwa katika maeneo mengine ndani ya nyumba hiyo.

Aidha kamanda Massawe alisema Jeshi hilo linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo ili kuweza kujibu tuhuma zinazomkabili pamoja na kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo kamanda Massawe alitoa wito kwa wananchi wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji wa bangi kuwaonea huruma wenzao na kuacha mara moja kwani ina madhara makubwa kwa watumiaji.

Alisema madawa mengine ya kulevya aina ya bangi kg 78 yalikamatwa katika eneo la barabara iendeyo horohoro wakati polisi wakiwa katika doria na walikutana na mwendesha baiskeli ambaye alikuwa amebeba gunia lenye madawa ya kulevya aina ya bangi ambapo alipowaona polisi alilitupa gunia hilo na kukimbia

Wakati huo huo,Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga linamshikilia kondakta wa basi lenye namba za usajili T.398 CEK Juma Salehe (32) kwa kosa la kukutwa na kg 52 za madawa ya kulevya aina ya mirungi katika basi hilo.

Kamanda Massawe alisema tukio hilo lilitokea Aprili 18 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni eneo la Zingibari kufuatia polisi wa usalama barabarani kulisimamisha basi hilo na kuanza kulipekua na kukuta madawa hayo.

Alisema baada ya askari hao kuanza kulipekua basi hilo ilikutwa mirungi yenye kg 55 ambayo alikutwa nayo Juma Salehe ambaye ni msafirishaji na kueleza kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

Mwisho.