LE BIG SHOW LEO LIVE AT THE UZINDUZI WA KTMA MUSIC AWARDS 2015 AT THE MILLENIUM TOWERS KIJITONYAMA LIVE!!

March 23, 2015
The Uzinduzi wa Msimu wa KTMA live leo at Millenium Towers Kijitonyama live!!







Le Big Show with Star TV Super Star Joy

Nchi 19 zashiriki Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni nchini

Nchi 19 zashiriki Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni nchini

March 23, 2015

1
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwahutubia washiriki wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana Jijini Dar es Salaam na kuhusisha washiriki kutoka nchi 19 wakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya lugha ya kiswahili.
2
Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz akizungumza na washiriki wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
3
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz wakati wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
4
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kushoto akifurahia maonyesho mbalimbali yaliyokua yakionyeshwa na vijana wakati wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz na wapili kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.
5
Washiriki kutoka nchi 19 wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokua yakiendelea katika Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar es Salaam.
7
Wanafunzi kutoka shule za Feza wakiburudisha wakati wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar es Salaam na kuhusisha washiriki kutoka nchi 19 wakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya lugha ya kiswahili.
…………………………….
Na Lorietha Laurence na May-Zuhura Simba -Maelezo
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara ameeleza kuwa lugha ina mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii ikiwa itakuzwa sambamba na maendelao ya teknolojia. Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni na kufafanua kuwa tamasha hilo limeonyesha kukua kwa lugha ya Kiswahili ambao ni utambulisho wa nchi yetu tangu kupatikana kwa uhuru. “Mkusanyiko wa leo umeanzisha safari ndefu ya kukuza lugha yetu ya Taifa toka ngazi za chini hadi za kimataifa, hivyo Tanzania imefarijika kuwa mwenyeji wa shughuli hii muhimu “alisema Mhe. Dkt. Mukangara. Aliongeza kuwa kwa upande wa serikali ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali ya kukiendeleza Kiswahili kwa kukifanya kuwa lugha ya kufundishia kuanzi shule ya Msingi hadi Elimu ya Juu. Dkt. Mukangara ametoa wito kwa vijana kujifunza Kiswahili na kuitumia lugha hiyo kuweza kujipatia ajira kwa kutangaza utumiaji wa bidhaa za lugha na utamaduni ambazo zina thamani kubwa kiuchumi. “Lugha ni sawa na kiwanda ikitumiwa vizuri italeta ajira kwa jamii husika na kutumika kama lugha ya kufundisha wageni mbalimbali wanaokuja nchini na hata nchi za nje kwa kuipa hadhi ya kuzungumzwa sehemu mbalimbali” alisema Mhe. Dkt. Mukangara Kwa Upande wa muandaaji wa tamasha hilo ambaye ni Rais wa Asasi za Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw. Ali Akkiz amesema kuwa kupitia tamasha hilo wameweza kutangaza vivutio mbalimbali vya kiutamaduni vya jijini Dar es salaam na Zanzibar. “Kwa kweli watoto wamefurahi kushiriki katika tamasha hili kwa kuweza kutembelea sehemu zenye vivutio vya utamaduni pamoja na historia najua wataondoka na taswira nzuri ya kutokuisahau nchi ya Tanzania” alisema Bw. Akkiz Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni ni la kumi 13 kufanyika ambalo limeshirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 18 kutoka katika nchi 19 na nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tukio hili kwa mara ya kwanza.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA ENEO LA BUGURUNI KWA MNYAMANI LILILOATHIRIKA NA MAFURIKO

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA ENEO LA BUGURUNI KWA MNYAMANI LILILOATHIRIKA NA MAFURIKO

March 23, 2015

2
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mkandalasi wa ujenzi wa mtaro wa kupitishia maji machafu wakati alipotembelea eneo la Buguruni kwa Mnyamani leo Machi 23, 2015 kwa ajili ya kukagua maeneo yaliyoathirika kutokana na mafuriko ya mvua zinazoendele kunyesha jijini Dar es Salaam.
Picha na OMR
3 4
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo juu ya hatua zilizokwishachukuliwa na Serikali, kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, wakati Makamu alipotembelea eneo la Buguruni Kwa Mnyamani lililoathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
6 8
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo hilo baada ya kujionea athari zilizotokana na mafuriko hayo kwa wakati wa Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam, leo machi 23,
9 10

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOA WA DODOMA

March 23, 2015

 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akikata utepe kama ishara ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akifungua bomba la maji kama moja ya zoezi lililofanyika wakati wa kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akinawa mikono yake kwa maji safi na salama wakati wa kiongozi huyo akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akimtwisha ndoo ya maji bi. Asha Omary wa kijiji cha Mseta Wilayani Kongwa mara baada ya kiongozi huyo kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji ulioanza kuhudumia wananchi kijijini hapo mapema jana (Machi 22,2015) wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akiwasilisha hotuba yake ya kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya maji Mkoani Dodoma yaliyofanyika Kijiji cha Mseta Wilayani Kongwa MACHI 22, 2015.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mseta Wilayani Kongwa wakiserebuka ngoma za asili wakati wa sherehe za kilele cha wiki ya maji Mkoa wa Dodoma zilizofanyika kijijini hapo Machi 22,2015.

ICF na TIC Kuongeza Uwekezaji Nchini

March 23, 2015

Rais mtaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awamu ya tatu) na Mwenyekiti Mwenza wa ICF,Mh. Benjamin Mkapa akikaribishwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji,Mh. Ing. Christopher Chiza wakati alipowasili kwenye Ofisi za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) leo Machi 23.Picha zote na Othman Michuzi.
Rais mtaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awamu ya tatu) na Mwenyekiti Mwenza wa ICF,Mh. Benjamin Mkapa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Prof. Lucian Msambichaka wakati alipowasili kwenye Ofisi za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) leo Machi 23.Kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji,Mh. Ing. Christopher Chiza.
Rais mtaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awamu ya tatu) na Mwenyekiti Mwenza wa ICF,Mh. Benjamin Mkapa akiwasalimia baadhi ya Wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) waliojitokeza kumpokea wakati alipowasili.
Rais mtaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awamu ya tatu) na Mwenyekiti Mwenza wa ICF,Mh. Benjamin Mkapa (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji,Mh. Ing. Christopher Chiza pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Prof. Lucian Msambichaka.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Juliet Kairuki.

Waziri Membe awaasa waimbaji wa nyimbo za injili nchini kuwa chachu ya amani na uadilifu nchini

March 23, 2015

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb.) amezindua albamu mbili za nyimbo za injili zinazokwenda kwa majina ya "Pisha Mbele" na "Ni Ujumbe wa Bwana" za mwimbaji Mercy Nyagwaswa katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza uliopo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Machi, 2015. 
Askofu Mstaafu na Baba mzazi wa Mercy Askofu Nyagwaswa (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Mchungaji David Mangoti (wa pili kulia) na  Balozi Mstaafu Costa Mahalu wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia wakati wa uzinduzi huo.  
Sehemu ya Wachungaji walioudhuria  uzinduzi wa albamu hiyo.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Bi. Mercy Nyagwaswa kulia akiwa na Mwimbaji mwenzake Bi. Upendo Nkone kwa pamoja wakimsikiliza Mhe. Membe ambaye  hayupo pichani alipozindua albamu zake za "Pisha Mbele" na Ni "Ujumbe wa Bwana". Wakati wa uzinduzi huo Waziri Membe alitoa rai kwa waimbaji wa nyimbo za injili nchini kuwa chachu ya amani na uadilifu ili nchi iendelee kuwa na utulivu na upendo. 

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) MKOA WA TANGA WAHAMASISHA MPANGO WA MIKOPO YA VIFAA TIBA KWA WATOA HUDUMA LEO

March 23, 2015
MKUU WA MKOA WA TANGA,SAID MAGALULA AKIFUNGUA KIKAO HICHO CHA UHAMASISHAJI WA MPANGO WA MIKOPO YA VIFAA TIBA KWA WATOA HUDUMA ANAYEFUATA NI KAIMU MGANGA MKUU WA MKOA WA TANGA,DR.CLEMENCE MARCELLY NA MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOA WA TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU

MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOA WA TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU AKIZUNGUMZA WAKATI WA KIKAO HICHO LEO

KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA,MONICA KINALA AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO  LEO

KAIMU MGANGA MKUU WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,DR.JESTINA MSUMARI AKIULIZA SWALI KATIKA KIKAO HICHO

DR.SANA KUTOKA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOA WA TANGA(NHIF) AKIFUATILIA HOTUBA YA RC MAGALULA LEO

MGANGA MFAWIZI WA HOSPITALI YA MKOA WA TANGA BOMBO,DR KARIA AKIFUATILIA KIKAO HICHO LEO



WASHIRIKI WAKIFUATILIA KIKAO HICHO


Dkt. Bilal afunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa mjini Musoma.

Dkt. Bilal afunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa mjini Musoma.

March 23, 2015

1
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma
2
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiambatana na wenyeji wake baada ya kuwasili mjini Musoma.
3
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Mara Adam Ngalawa baada ya kuwasili mjini Musoma.
4
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisikiliza wimbo wa Tanzania uliokuwa unaimbwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisangula.
5
 Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala, akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati), ramani ya Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma. Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.
6
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akimkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal kuzungumza na wananchi kwenye eneo la mradi.
7
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akizungumza na wananchi.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu Aseri Msangi na kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Maghembe.
8
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati) akikata utepe wa Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto kwake ni Balozi wa Ufaransa nchini, Melika Berak na viongozi wengine wa chama.
9
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak.
10
 Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Nadhifa Kemikimba akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal teknolojia ya kusafisha maji kwa kutumia mifupa.
11
 Baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Maji Kitaifa
13
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akimpa kikombe Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji wa Chuo cha Maji, Eng. Pantaleo Tumbo ikiwa ni moja ya zawadi zilizotolewa kwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Maji.
……………………………………………………………………..
Hussein Makame-MAELEZO, Musoma
MAKAMU wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohgamed Ghalib Bilal amesema kuwa kila ahadi ya Serikali iliyotolewa itatimizwa ili kuhakikisha kuwa inaacha kazi nyepesi kwa viongozi watakaokuja katika kuendeleza maendeleo ya Tanzania.
Dkt. Bilal aliyasema hayo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mara yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Mandeleo Endelevu.
Katika kilele cha Maadhimisho hayo, Dkt. Bilal aliweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma ambao utagharimu Shilingi Bilioni 44 hadi kukamilika kwake.
“Tumewaahidi kupata maji na hilo tutatekeleza.Kila ahadi ya Serikali itatimizwa swali ni muda na wakati lakini kwa kweli hatukusudii kuwaacha njiani, mambo tuliyosema tutayafanya ili tuwaachie watakaokuja kazi nyepesi ya kuendeleza maendeleo ya nchi yetu” alisema Dkt. Bilal.
Mradi huo mkubwa wa maji unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2015 ambapo Dkt. Bilal alisema mradi huo utakapokamilika itaipatia Manispaa ya Musoma maji ya uhakika kwa asilimia 100.
Aliongeza kuwa mafanikio ya mradi huo pia ni kuongezeka kwa uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 10,000 za sasa kwa siku, hadi mita za ujazo 36,000 kwa siku.
Dkt. Bilal alitoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Musoma na mkoa wa Mara kutunza mradi huo na miradi yote inayoendelea kutekelezwa ili iendelee kuwasaidia wananchi na vizazi vijavyo.
“Na juu ya haya yote, ni msisitizo katika utunzaji endelevu wa mazingira yetu ili yaendelee kutuhifadhi. Aidha, teknolojia za uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa ni maeneo ambayo yatatuhakikishia kwamba tunakuwa na huduma endelevu ya rasilimali ya maji” alisema.
Alisema Tanzania haina budi kuwa na mikakati ya makusudi kukabiliana na changamoto hizo, jambo ambalo Serikali imeanza kulifanyia kazi.
Alifafanua kuwa uhaba wa maji na kutopatikana kwake kwa uhakika kunaleta athari mbaya katika shughuli zote za kiuchumi.
“Majanga yanayohusiana na maji kama vile, mafuriko na ukame kwa kiwango kikubwa ni maafa yanayojitokeza mara nyingi katika sehemu mbalimbali duniani hivi sasa” alisema Dkt. Bilal na kupngeza kuwa:
“Vifo, uharibifu wa mali, makazi na miundombinu vina athari kubwa kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kikundi, jamii na hata Taifa”
Hivyo, alitoa wito kwa wadau wote kuunganisha nguvu pamoja katika kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kwani, mabadiliko hayo yana athari kuanzia kwenye kupungua kwa misitu na vyanzo vya maji.
Alitaja athari nyingine kuwa ni kupungua kwa rasilimali za maji juu na chini ya ardhi; kuathirika kwa ubora wa maji ya kunywa; hadi kukua kwa utoaji wa gesi ya ukaa.
Hata hivyo alisema, Serikali ya Tanzania itaendeleza juhudi za kuhakikisha inawafikishia wananchi maji safi na salama katika maeneo ya nchi ambayo yamekosa huduma hiyo.
Aliwakumbusha wananchi kuwa wana jukumu kubwa la kutunza vyanzo vya maji popote pale vinapopatikana na kwamba wana kubwa kwenu wananchi ni kutoa mchango unaostahili katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji.
Akimkaribisha Dkt. Bilal, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema wizara yake itajitahidi na kufanya kila linalowezekana ili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu maji yatoke mjini Musoma na wananchi wafurahie huduma hiyo.
Alisema katika kipindi cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji, viongozi mbalimbali walishiriki katika kukagua miradi ya maji na kutembelea wilaya zote za Mara na kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maji ambayo imekamilika. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala alisema mradi huo unajengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD). Alisema mradi huo unajumuisha ujenzi wa chanzo kipya cha maji, chujio, mtambo wa kisasa wa kutibu maji na ujenzi wa matenki mapya mawili yenye mita za ujazo 5,500. Aliongeza pia kuwa, ujenzi huo utajumuisha ujenzi wa mfumo mpya wa mabomba ya usambazaji maji na ujezni wa miundombinu mingine. “Mheshimiwa mgeni Rasmi Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la AFD kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Jumuiya ya Ulaya (EAD) wamekubali kufadhili mradi wa kuondoa majitaka katika manispaa ya Musoma” alisema Mhandisi Gantala. Naye Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak alisema kuwa amefurahishwa na ushirikiano anaoupata kutoka Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha wanapunguza tatizo la maji nchini. Katika kilele cha maadhimisho hayo ya 27 ya Wiki ya Maji Duniani, washiriki wa maonesho katika maadhimisho hayo walipewa vyeti vya kushiriki na zawadi za vikombe kutokana na makundi washiriki.