Jeshi la
polisi nchini limefanikiwa kuwakamata watu 96 wengi wao wakiwa ni raia
wa nchi jirani ya burundi, wanaotuhumiwa kujihusisha na ujangili kwenye
hifadhi ya taifa ya Katavi.
Jeshi la
polisi nchini limefanikiwa kuwakamata watu 96 wengi wao wakiwa ni raia
wa nchi jirani ya burundi, wanaotuhumiwa kujihusisha na ujangili kwenye
hifadhi ya taifa ya Katavi ikiwa ni pamoja na mapori mbalimbali ya akiba
(Game Reserve) mkoani Katavi, na kukutwa na silaha nne pamoja na risasi
118 na Radio Call kwa ajili ya mawasiliano.
Kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi SSP FOCUS MALENGO, akiongea mjini
Mpanda amesema mafanikio hayo yanatokana na operesheni maalumu
iliyofanywa na askari wa jeshi hilo la polisi kutoka mikoa ya Dar es
salaam na Tanga, kwa ushirikiano na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama.
Amesema
oparesheni hiyo ina lengo la kupambana na vitendo vya ujangili
vinavyoendelea mkoani humo vinavyohatarisha uwepo wa baadhi ya wanyama
na rasilimali nyingine ambazo ni vivutio vya utalii.
Hata hivyo
kaimu kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoani Katavi hakuwa tayari
kufafanua juu ya baadhi ya watuhumiwa hao ambao wamehamishwa kutoka
mkoani Katavi, mahali walikohamishiwa na idadi yao, ingawa inaaminika
kuwa ni raia wa nchi ya jirani ya burundi, ambao wamekuwa wakijihusisha
na vitendo vya ujangili, na kuishi katikati ya mapori yaliyoko mkoani
Katavi.