DR.SLAA AWAASA WATANZANIA KUHUSU KATIBA .

August 17, 2013
Elizabeth Kilindi,Tanga
KATIBU  Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Dr Willbroad slaa amewaasa watanzania watambue kuwa katiba ni uhai wa Taifa hivyo wawe huru kutoa maoni ili baadae iweze kuwatetea na kuwalinda.

Dr. Slaa alisema  hayo katika mkutano wenye lengo la kukusanya maoni ya katiba mpya iliyofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini hapa  ikiwa  maelfu ya wananchi walikusanyika kutoa maoni ambapo amesema chama hicho kitakusanya maoni si chini ya milioni tano ili kuyapeleka kwa  Jaji Warioba.

Aidha alisema chama chake kimeamua kukusanya maoni kwani katiba si mali ya chama bali ni ya watanzania wenyewe hivyo wameona ni vyema kuwakusanya kwa pamoja kutoa maoni yao ambayo ni haki ya kila mtanzania.

Katibu huyo alisema kuwa wenye mawazo ya kufanana wanauwezo wa kutengeneza katiba hivyo tunaitaji katiba  ambayo itawalinda watanzania na wala sio itakayolinda chama chochote cha siasa.

Katika atua nyengine Dr Slaa alisema katika katiba ya sasa imetumiwa vibaya na viongozi wa sasa walioko madarakani na pamoja na kutowachukulia hatua  wanaovunja maadili kwa kuiba rasilimali za umma.

Sambamba na hayo aliweza kuongelea umuhimu wa serikali tatu ambapo alisema kuwa itapunguzia ghalama za uendeshaji wa serikali kwa kuokoa fedha nyingi kwani asilimia ya wabunge na mawaziri itapungua kwa kiasi kikubwa.

Pia aliwata watanzania  kuacha woga katika kudai haki kwani kufanya hivyo ni kutojitendea haki na hata mungu anakataza.

Naye mjumbe wa kamati kuu wa chama cha demokrasia na maendeleo{chadema} Mabere Marando alisema kuwa watahakikisha kwa kila njia kuwafikiwa watanzania na kuwaelewesha rasimu ya katiba mpya na msimamo wa chama hicho.

Hata hivyo alisema kuwa chama hicho kitawafikia wananchi katika maeneo yao kuwaelewesha na kupata maoni na vyema kusema nini wanataka kiwepo katika  katiba hiyo mpya.

UVCCM WAPINGA SERIKALI TATU.

August 17, 2013
Na Oscar Assenga,Korogwe.
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (UVCCM)imepinga mfumo wa kuwepo kwa serikali tatu na kueleza endapo mchakato wa uundwaji wake ufanyika utarudisha nyuma maendeleo ya watanzania pamoja na kuuvunja muungano uliopo baina ya Tanzania bara na visiwani.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga(UVCCM)Abdi Makange wakati akizungumza katika kikao cha baraza hilo ambacho kilifanyika wilayani hapa na kuhudhuriwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Gustav Mubba.

Makange alisema yenye anashangazwa na viongozi wa vyama vya upinzani vyenye sera ya kuridhia uwepo wa serikali tatu bila kuangalia athari ambazo zinaweza kutokea kwa wanannchi na jamii ambazo zinawazunguka.

   "Binafasi nashangazwa sana na sera zinazotolewa na vyama vya upinzani hapa nchini kwa kuzungumzia uanzishwaji wa serikali tatu bila kuangalia kuna athari gani kwa wananchi wanaowaongoza "Alisema Makange.

Alisema maoni ambayo waliyatoa kuhusu uanzihwaji wa serikali tatu hawaamini kama yanatoka kwa wananchi na kueleza kuwa ni ya watu wachache wenye dhamira ya kuudhofisha muungano wetu ambao tulioachiwa na waasisi wa Taifa hili.

Mwenyekiti huyo aliwataka vijana waliopo ndani ya umoja huo kusimama kwenye mapendekezo ya chama cha mapinduzi kuwa serikali tatu haiwezekani kwa sababu itaongeza gharama za uendeshaji na kuwafanya wananchi kuendelea kuwa maskini.

Aidha aliwataka wananchi kuepukana na viongozi wasioitakia mema serikali yao kwa kuwa mstari wa mbele kuzungumzia suala hilo na kuwataka wajumbe hao watakaopata nafasi ya kwenda kwenye mabaraza ya katiba wakayazungumze hayo kwamba serikali tatu haiwezekani.

PICHA ZA MATUKIO YA BARAZA LA UVCCM MKOA WA TANGA JANA KOROGWE.

August 17, 2013



KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA TANGA,GUSTAV MUBBA AKITOA NENO KATIKA BARAZA HILO .



MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA BARAZA HILO AMBACHO KILIFANYIKA WILAYANI KOROGWE JANA.

KATIBU WA CHAMA CHA MAPOINDUZI MKOA WA TANGA KUSHOTO GUSTAV MUBBA AKITETA JAMBO NA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA ,ABDI MAKANGE JANA

MAKAMANDA WA UVCCM WILAYA YA TANGA WAKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAO,SALIM PEREMBE KUSHOTO WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MWENYEKITI WA MKOA UVCCM JANA KWENYE BARAZA HILO.