Mashindano ya Kigwangalla Cup 2017 yazinduliwa jimbo la Nzega vijijini

July 28, 2017
Mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za Kata zilizo ndani ya Jimbo la Nzega Vijijini maalufu kama ‘Kigwangalla Cup’ yamezinduliwa rasmi jioni ya Julai 27, 2017 huku miamba 20 ikitarajiwa kuumana kumpata bingwa wa Jimbo hilo kwa mwaka huu.
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliwataka wachezaji wote wanaoshiriki michuano hiyo kuwa na nidhamu iliwaitumie michuano hiyo kama kipimo cha wao cha kuonesha vipaji vyao ili waonekane ngazi za juu.
“Mpambane kweli kweli. Kila mmoja wenu aoneshe uwezo wake wa kusakata kabumbu. Pia muzingatie nidhamu ya hali ya juu kwani michezo inaleta umoja na amani, inaimalisha afya ya miili yetu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati akuzungumza na wachezaji katika ufunguzi wa michuano hiyo.
Dk. Kigwangalla pia alipata wasaha wa kukagua timu zilizofungua rasmi michuano hiyo kati ya Mizibaziba dhidi ya Nkiniziwa ambazo hata hivyo mpaka kipyenga cha mwisho zilitoka droo ya bao 1-1.
Dk. Kigwangalla alieleza kuwa, jumla ya Kata 19 za jimbo lake hilo zimeweza kutoa timu ilikushiriki michuano hiyo huku timu maalum ikiingizwa ambayo itajumuisha Madiwani wote kutoka Kata hizo ili kufanya jumla ya timu 20.
Dk. Kigwangalla alizitaja baadhi ya Kata zinazochuana kwenye michuano hiyo ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata, Sanzu,Lusu, Milambo Itobo, Magengati,Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi.
Kata zingine ni Kata za Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.
Awali kabla ya kuanza rasmi kwa mchezo wa ufunguzi, Madiwani wa Kata zote waliweza kukabidhiwa baadhi ya vifaa kwa timu zao sambamba na hilo wananchi waliweza kufurahia michezo mbalimbali ikiwemo ile ya jadi hasa mchezo wa asili wa bao la Kinyamwezi, kucheza drafti, kukimbiza kuku, michezo ya mbio kwa Wazee huku mchezo wa mbio kwa watu wenye vitambi ukitia fola kwenye ufunguzi huo, uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Nkiniziwa iliyopo kwenye Kata hiyo ya Nkiniziwa.
 
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na timu ya Kata ya Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
 
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wachezaji wa Kata ya Nkiniziwa wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wachezaji wa timu za Kata za Nkiniziwa na Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
Mtanange baina ya Mzimaziba dhidi ya Nkiniziwa ukiendelea katika mchezo wa ufunguzi wa Kigwangalla Cup 2017
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu za Nkiniziwa na Mzibaziba (Msibasiba) wakati wa ufunguzi huo.

Tusichanganye mifugo na wanyamapori ni hatari kiafya - Waziri Prof Magembe

July 28, 2017
Mkuu wa Masoko na Utalii, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Ibrahim Mussa akiwasilisha mada leo kwa wahariri na wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanyika jijini Tanga.

Mratibu Miradi wa Taifa, kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda akiwasilisha mada leo kwa wahariri na wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanyika jijini Tanga.

Mratibu Miradi wa Taifa, kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda akiwasilisha mada leo kwa wahariri na wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanyika jijini Tanga.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Magembe alipokuwa akizungumza na Wahariri na Wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika semina ya mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA kwa wanatasinia hiyo ya habari.

Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, ambayo ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, The African na Bingwa, Absalom Kibanda (kushoto) akiuliza swali kwenye semina hiyo. Wengine ni baadhi ya washiriki wa semina hiyo kwa wahariri na wanahabari waandamizi.

Na Joachim Mushi, Tanga
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Magembe amewaonya wananchi walio jirani na hifadhi za taifa kuacha mara moja kitendo cha kuchanganya mifungo na wanyamapori kwani kitendo hicho ni hatari kubwa kwa afya za wananchi na mifugo yao. Alisema wanyamapori wana magonjwa mbalimbali na hatari kwa afya zetu hivyo kitendo cha kuchanganya mifugo na wanyamapori huamisha magonjwa kutoka huko na kuingia kwa wananchi wanapokula nyama.
Waziri huyo mwenye dhamana na Maliasili na Utalii alitoa onyo hilo jana jijini Mbea alipokuwa akifungua Mkutano na Semina ya mwaka kwa wahariri na wanahabari waandamizi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA). Alisema kitendo cha wafugaji kuchanganya wanyamapori na mifugo ni changamoto nyingine kubwa, hivyo kuwaomba waandishi wa habari kupitia vyombo vyao kutoa elimu kwa wafugaji. Alisema wanyamapori huwa na magonjwa mengine ambao kwao hayana madhara makubwa lakini yanapoingia kwa mwanadamu huhatarisha maisha yake kiafya.
"...Wananchi kuingiza mifugo yao mbugani hili ni tatizo kubwa, tunaomba mtusaidie...kwanza sheria zetu haziruhusu kabisa suala hili. Tusichanganye mifugo na wanyamapori hii ni hatari tunaweza kubeba magonjwa kule na yakawa na madhara makubwa kwetu...kuna magonjwa kama kimeta, TB na homa za vipindi ambazo zipo kwa wanyamapori zikija kwetu hizi ni hatari," alisisitiza Profesa Magembe.
Hata hivyo, Waziri Magembe alipongeza juhudi zinazofanywa na wanahabari kupitia vyombo vyao kwani wamekuwa msaada mkubwa kutoa elimu ndani na nje ya nchi. Aliongeza kuwa matokeo ya wanahabari kutumia kalamu zao kutangaza utalii yanajionesha wazi kwa ongezeko la idadi ya watalii kutoka nchi mbalimbali kutembelea hifadhi zetu.
Aidha ameitaka TANAPA kuendelea kushirikiana na wanahabari kwa kufanya semina hizo kila mwaka ili kupata mrejesho juu ya kazi wanayoifanya, kwani vyombo vya habari ni fursa nzuri ya kutoa elimu kwa umma na kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo. Mkutano huo wa siku tatu ulioanza leo Julai 26 unatarajia kumalizika Julai 29, ambapo wanahabari watajifunza na kujadiliana masuala mbalimbali ya utalii na uhifadhi.
Idadi kubwa ya watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani bado wanamiminika kuja nchini Tanzania kutembelea vivutio anuai vya utalii. Alisema hali hiyo imebainika baada ya ziara aliyoifanya kutembelea hoteli mbalimbali za kitalii na kujionea namna zinavyopokea watalii mfululizo, huku baadhi zikiwa zimejaa na wateja kulazimika kuweka oda mapema kabla ya kuanza safari ya utalii.
"...Mimi nimetembelea kabla ya kuja hapa baadhi ya hoteli kwenye maeneo ya utalii kujionea, kweli hoteli baadhi zinawatalii wa kutosha kiasi kwamba zingine zimejaa...mteja ukienda bila ya kufanya 'booking' ya chumba huwezi kupata, hawana nafasi pia. Na watalii wanaokuja wanatoka kila upande, kimsingi ujio huo wa watalii kwa wingi ni mafanikio yenu wanahabari," alisema Waziri Prof. Magembe.
Alisema watu wa kupongezwa ni waandishi wa habari ambao kiasi kikubwa; ningekuwa na kofia hapa ningewavulia kwa heshima na kutambua mchango wenu kwa kazi hii," alisema.
Hata hivyo alisema bado suala la ujangili dhidi ya wanyamapori ni changamoto japokuwa kwa sehemu kubwa kuna tunaweza kujivunia mapambano na jitihada tulizozifanya kudhibiti hali hiyo. mabadiliko makndiyo wanaotumia kalamu zao kuutangazia utalii wetu.

sehemu ya washiriki wa Semina ya Wahariri na Wanahabari waandamizi kwa mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA.

sehemu ya washiriki wa Semina ya Wahariri na Wanahabari waandamizi kwa mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA. Imeandaliwa;- www.thehabari.com
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, UMMY MWALIMU ATOA TAMKO LA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA HOMA YA INI DUNIANI

July 28, 2017
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akitoa tamko katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya  Homa ya Ini Duniani wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Bakari Kambi.

WASICHANA WAISHUKURU TGGA KUFANIKISHA ZIARA YA MAFUNZO NJE YA NCHI

July 28, 2017
 Wasichana wanachama wa Tanzania Girl Guides wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakitokea kwenye ziara ya programu ya miezi sita ya mafunzo ya kubadilisha uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili. Kutoka kushoto ni Ummy Mwabondo alikwenda Zambia, Edna Chembele (Zimbabwe), Elizabeth Betha (Madagascar) na Farida Mjoge aliyekuwa Uganda. PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

WASICHANA wanne wanachama wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) wamerejea nchini kutoka kwenye programu ya mafunzo ya miezi sita katika nchi mbalimbali za Afrika.

Wasichana hao waliokuwa kwenye mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika mambo ya utamaduni, uongozi na maadili katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagascar na Uganda wameipongeza TGGA kwa kufanikisha ziara hiyo yenye mafanikio makubwa katika maisha yao.

Walipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana kwa ndege ya Kenya Airways, walilakiwa na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba, ndugu jamaa na marafiki huku wengine wakivishwa mashada na kupatiwa zawadi mbalimbali. Wasichana waliokwenda kwenye mafunzo hayo ni; Ummy Mwabondo, Elizabeth Betha, Edna Chembele na Farida Mjoge ambao kila mmoja anaeleza jinsi alivyonufaika na ziara hiyo.

Elizabeth Betha ambaye programu yake aliifanyia Madagascar, anaeleza kuwa Wananchi wa Kisiwa hicho utamaduni wao ni tofauti kabisa na wa Tanzania na  maeneo mengine ya Afrika, ambapo mara nyingi hutumia lugha yao ya asili na  kifaransa kama Lugha yao ya Taifa, ni wakarimu sana na wana upendo.

Anasema kuwa licha ya kuwafundisha mambo mengi ya Tanzania ikiwemo utamaduni, mapishi ya vyakula mbalimbali, lugha ya kiswahili na vivutio mbalimbali vya kitalii pia wakiwa huko walipanda  miti, kufundishana kwa uwazi masuala ya hedhi salama, kuzuia ukatili wa kijinsia pamoja na kuwapa stamina ya kujiamini na kujithamini.

Edna Chembele, ambaye alikwenda  Zimbabwe, anasema akiwa huko alijifunza kuhusu uendeshaji wa Guides, kuishi maisha ya kawaida mashuleni na mitaani, mambo ya kimila na kiutamaduni, msichana kujiamini na kujithamini.  Pia walitembelea maeneo mbalimbali maarufu nchini humo. kuwaeleza wasichana kwamba nao wana  uwezo kufanya kazi zinazofanywa na wanaume.

Farida Njope yeye alipelekwa Uganda ambako anaelezea kuwa alijifunza mambo mengi kuhusu  Utamaduni, mavazi, mapishi ya aina mbalimbali za vyakula kama vile matoke chakula kinachotokana na ndizi zilizopondwa pondwa.

Naye aliwafundisha Girl Guides wa huko, kujiamini na kujielewa kwa kuthamini usichana wao katika jamii, pia aliona tofauti ya matumizi ya Lugha ambapo Tanzania lugha ya Taifa ni Kiswahili na Uganda Lugha yao ya Taifa ni Kiingereza ambayo alidai inawasaidia sana kujieleza kirahisi katika mambo mbalimbali yakiwemo ya kimataifa.

Alishauri Serikali ya Tanzania kubadilisha mitaala Kiingereza kitiliwe mkazo kwa kuwa somo la lazima kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu akidai lugha hiyo ni muhimu sana kwa mawasiliano kimataifa.

"Naishukuru sana TGGA kunipepeleka Uganda nimejifunza mengi. imenijenga kiakili na kuishi na watu wa aina mbalimbali nikiwa  mbali na wazazi wangu jambo ambalo sitolisahau kati maisha yangu."Alisema kwa msisitizo.

Naye Ummy Mwabondo ambaye programu ya kubadilisha uzoefu alifanyia Zambia, anasema alijifunza mambo mengi ikiwemo  
Jinsi ya kushirikiana na watu na kuongea nao hivyo kuimarisha uwezo wake wa kuzungumza jambo ambalo awali hakuwa nalo, alishiriki pia kupanda miti katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo.

Anasema alipata wasaa wa kuwafundisha wasichana kuwa wakakamavu na kujiamini kutenda mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo kupinga ukandamizaji, unyanyasaji dhidi ya watoto wa kike pamoja na kutoa elimu ya hedhi salama kwa wasichana kwa kuwafanya wasiogope kuwa kwenye hali hiyo kwani jambo hilo ni la maumbile ya kibailojia.

 Girl Guides wakiwasili na mizigo yao
 Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba  (kushoto) akiwalaki Girl Guides Uwanja wa Ndege Dar es Salaam
DC Babati awataka wakulima kuunga mkono jitihada za watafiti wa mbegu

DC Babati awataka wakulima kuunga mkono jitihada za watafiti wa mbegu

July 28, 2017
[ Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi akizungumza na wakulima na watafiti wa Mradi wa utafiti mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA), katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati. Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kulia) juu ya shamba la majaribio ya mbegu chotara za mahindi zinazostahimili magonjwa na ukame (WEMA), katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea. Mtafiti wa Mradi wa WEMA, Ismail Ngolinda (kulia) akimtembeza mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kushoto) ndani ya shamba la majaribio katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea. Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi akitembelea shamba la majaribio ya mbegu chotara za mahindi zinazostahimili magonjwa na ukame (WEMA), katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea.  Mtafiti wa Mradi wa WEMA, Ismail Ngolinda (kwa kwanza kulia) akijibu maswali ya baadhi ya wakulima ndani ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea. Mahindi ndani ya shamba la utafiti shirikishi na wakulima la Mradi wa WEMA lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati. Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano na uratibu Mradi wa WEMA, Bw. Temu akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo akijibu maswali ya wakulima (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea shamba la utafiti shirikishi wa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA). Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati, Cade Mshamu (wa pili kulia) akizungumza na wakulima na watafiti wa Mradi wa utafiti mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA), katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati. Baadhi ya wakulima na wageni anuai wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati. Mkulima akiuliza swali kwa watafiti katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati. Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Maendeleo ya Utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Jackson Nkuba (kulia) kwenye hafla hiyo. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabaan Husein (kulia) akizungumza kwenye hafla hiyo.