JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

August 09, 2016
Timu ya Jamii Media ikitambulishwa mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bukoba.
Mtandao wa JamiiForums.com umezindua rasmi mradi wa unaowashirikisha viongozi wa kuchaguliwa(hususani wabunge na madiwani), Serikali(Halmashauri) na Wananchi katika kurahisisha upatikanaji wa maendeleo.

Mradi huu unaotambulika kama "Tushirikishane" una malengo ya kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi.
Pia Tushirikishane inalenga kuzisaidia Halmashauri kuboresha utoaji huduma za jamii kwa ufanisi zaidi. Mwitikio(maoni, ushauri na kero) wa wananchi katika mnakasha wa Jimbo/Halmashauri utachukuliwa kwa umakini na viongozi hawa ili kuhakikisha mrejesho unatolewa kwa wananchi.
Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Mjini, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanzilishi-Mwenza wa mtandao wa JamiiForums.com, Bwana Maxence Melo aliwapongeza viongozi wa Wilaya, watendaji wa Halmashauri, Madiwani na Mbunge kwa mwitikio mkubwa walioonyesha katika kuupokea mradi wa Tushirikishane.



Maxence aliwafahamisha kwamba Mradi huu utatekelezwa katika majimbo sita (6) kwa kuanzia na Bukoba Mjini limekuwa Jimbo la kwanza katika kuanza utekelezaji wake. Alifafanua kuwa mradi huu utachukua miezi 9 na hivyo Wabunge wanaohusika kwenye mradi huu wanatakiwa kukubaliana na wananchi juu ya ahadi zisizozidi 4 za kuweza kuwa sehemu ya mradi huu zinazoweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa mradi huo.



Bwana Maxence pamoja na timu yake ya wataalam walikuwa Bukoba Mjini kwa siku tano kuendesha warsha iliyowawezesha wadau kuuelewa mradi kwa ufasaha, kutambua majukumu yao na kujua njia zitakazotumika katika kutekeleza mradi kwa faida yao.
Warsha ya Tushirikishane ilifanyika Bukoba Hotel na wadau wanaowakilisha Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Wapiga kura na wananchi wa Bukoba Mjini, Madiwani wa vyama vyote pamoja na Mbunge wa Jimbo walishiriki.
Malengo ya Tushirikishane
Pamoja na lengo kuu tajwa hapo juu, Mradi huu una malengo mahususi yafuatayo:

i. Kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Wananchi na viongozi wa kuchaguliwa na serikali yao (kwa njia ya mtandao, magazeti, redio, televisheni na mikutano ya wazi)
ii. Kurahisisha upatikanaji wa habari na taarifa za umma zikiwa kwenye lugha rahisi
iii. Kuchochea majadiliano ya wazi, yenye tija na staha kati ya wananchi na viongozi wao
iv. Kusaidiana na viongozi wa kuchaguliwa katika kutengeneza nyenzo za muhimu katika kutekeleza ahadi.​

Matarajio ya Mradi

Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:

i. Kujengeka kwa utamaduni wa majadiliano yenye staha kati ya viongozi na wananchi kwenye mitandao ya kijamii
ii. Kuboreshwa kwa mfumo wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika utekelezaji wa sera na ahadi za wakati wa Uchaguzi.
iii. Kuongezeka kwa ufanisi katika utekelezaji wa sera na ahadi za kipindi cha uchaguzi.​

 Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo akimkabidhi kitendea kazi mwakilishi wa JamiiForums (Afisa Mawasiliano) katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bi. Happiness Essau
 Mkufunzi akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.
Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Wilfred Lwakatare akijibu baadhi ya maswali na kutolea ufafanuzi hoja zilizotoka kwa wapiga kura.


 Diwani wa Kata ya Bakoba, Mhe. Mwakyoma akiwasilisha kundi lake juu ya Wajibu wa Mbunge kwa wapiga kura wake.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Mhe. Maxence Melo akibadilishana mawazo na waheshimiwa madiwani Kalumuna(katikati) ambaye ni diwani wa Bilele(CCM) na Kabaju (kulia) ambaye ni diwani wa Kashai(CHADEMA).

Mbunge wa Bukoba Mjini, akishirikiana na wapigakura wa Jimbo lake katika zoezi la kuchambua kazi na wajibu wa mbunge kwa wapiga kura wake.
 Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane katika Jimbo la Bukoba Mjini wakiwa katika picha ya pamoja.
Baraza la Halmashauri ya Bukoba, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Pamoja na Timu ya Jamii Media katika picha ya Pamoja

RC MONGELLA AZUNGUMZIA ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI MWANZA.

August 09, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akitoa taarifa ya ujio wa Rais Magufuli mkoani Mwanza. Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza, CP.Clodwig Mtweve.

Judith Ferdinand, Mwanza
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kufanya ziara fupi ya kikazi mkoani Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, leo amesema, Rais Magufuli atafanya ziara ya siku mbili kuanzia kesho agost 10 na 11, ambapo atapokelewa hiyo kesho wilayani Sengerema akitokea Chato mkoani  Geita alikokuwa na mapumziko mafupi.

"Rais Magufuli atawasili kesho asubuhi katika mkoa wetu akitokea Chato mkoani Geita na ataanza ziara katika wilaya ya sengerema kwa ajili ya kuwasalimia wananchi, kuwapa taarifa za mikakati na maendeleo awamu ya tano pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi". Amesema Mongella.

Pia amesema hiyo kesho Rais Magufuli atasimama maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwasalimu wananchi kabla ya kuwasili wilayani Nyamagana.

Ametanabaisha kwamba Rais Magufuli ataitimisha ziara yake kesho kutwa agost 11, kwa kukagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini Mwanza, pamoja na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi ambapo ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo. 

Mongella amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia majira ya saa nanne mchana katika uwanja wa Furahisha ambapo Rais Magufuli atahutubia wananchi baada ya kukagua miradi hiyo ya ujenzi.
Mwanahabari akiuliza swali
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

Tigo, Kupatana.com kushirikiana kuwezesha biashara kwa mtandao

August 09, 2016
Meneja Miradi ya Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Anthony Njau (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wa biashara kati ya Tigo na Kupatana.com, Wengine kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni inayofanya biashara kwa njia ya mtandao ya Kupatana.com, Philip Ebbersten na Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha.

 Mkurugenzi wa Kampuni inayofanya biashara kwa njia ya mtandao ya Kupatana.com, Philip Ebbersten  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wa biashara kati ya Tigo na Kupatana.com,wengine ni Meneja Miradi ya Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Anthony Njau na mwisho ni Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha 


Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha akifafanua jambo wakati wa mkutano huo mapema leo jijini Dar es salaam.


Wafanyakazi wa tigo wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo na waandishi wa habari mapema leo katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar es salaam,




 Dar es Salaam, Agosti 9, 2016-  Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania na kampuni ya Kupatana.com, moja ya kampuni zinazoongoza Tanzania  katika huduma za masoko katika mtandao  zimeingia katika ubia wa kibiashara ambapo kila kampuni  itauza bidhaa na huduma za  kila mmoja katika majukwaa yao ya kidijitali.
Katika hatua za mwanzo za ushirikiano huu, Kampuni ya Tigo Tanzania itachagua maduka matatu ambayo Kupatana.Com itayatumia kuwawezesha wateja wa Tigo kuuza simu zao zilizotumika kwa kupitia jukwaa la Kupatana.com.
Akizungumza wakati wa  kusaini makubaliano baina ya pande hizo mbili jijini Dar es Salaam,  Meneja miradi ya biashara wa Tigo, Anthony Njau alisema, “tukiwa ni kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali, tumeona kwamba hivi sasa Watanzania wamehamasika mno katika kufanya biashara kupitia njia ya mtandao.”
Njau aliongeza kwamba , “Mtandao na wavuti wa Kupatana.com unatoa jukwaa zuri ambalo linabadilisha  namna ambavyo watu wanaishi kwa kuwezesha kupatikana kwa  huduma na bidhaa katika njia sahihi na rahisi.”
 “Lengo la muda mrefu ni kuwapatia wateja wetu jukwaa  ambalo wanaweza kupakua  vifaa ambavyo vilishatumika ili kuviboresha na kwa upande wa Tigo kuuza  vifaa vipya, kuongeza usambazaji  na kuwa na mafanikio katika  jaribio hili la msingi, Tigo na Kupatana.com zitapanua wigo wa huduma hii na kuhakikisha inapatikana kwa urahisi katika maduka yote 52 ya Tigo  ambayo yamesambaa  kote nchini,” alisema Njau.
 Mkurugenzi wa Kupatana.com, Philip Ebbersten, alisema kwamba kupitia matumizi ya jukwaa hilo, wauzaji (kampuni na watu binafsi) wataweza  kuwafikia maelfu ya  wanunuzi muhimu kila siku bila kujali  maeneo yao ya kijiografia.
Alifafanua kuwa kuorodhesha bidhaa katika jukwaa hilo  ni bure  na kuwashauru wateja umuhimu wa  kufuata kanuni  na miongozo salama kwa bidhaa zote zitakazotangazwa Kupatana.com ili waweze kuzitapa  kwa usalama na uelewa zaidi.
 Mwisho .
photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.tz Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com W: www.koncept.co.tz

MKUTANO MZIMA: MAALIM SEIF ALIVYOZUNGUMZA NA WAZANZIBARI BOSTON

August 09, 2016
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, alipokuwa akizungumza na Wazanzibari waishio nchini Marekani kwenye mkutano uliofanyika Siku ya Jumamosi Julai 30, 2016 katika jiji la Boston.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JULAI, 2016 UMEPUNGUA KWA KWA ASILIMIA 5.1

August 09, 2016
 Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwekisigabo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa za mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Julai, 2016. Kushoto ni Kaimu Meneja, Idara ya Takwimu ya Ajira na Bei, Ruth Minja
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wapiga picha wakiwa kazini.

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2016 umepungua hadi asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 ilivyokuwa mwezi Juni, 2016.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwekisigabo  wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Julai, 2016.

"Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2016" alisema Kwesigwabo.

Kwesigabo alisema kuwa Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.50 Mwezi Julai, 2016 kutoka 98.48 mwezi Julai 2015 na kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Julai 2016 umepungua hadi asilimia 7.6 kutoka asilimia 8.1 ilivyokuwa mwezi Juni, 2016.

Kwesigabo aliongeza kuwa kupungua kwa mfumuko huo wa bei wa mwezi Julai 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Julai, 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Julai 2015.

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za samaki kwa asilimia 6.6, mafuta ya kupikia kwa asilimia 4.9 na maharage kwa asilimia 1.9.

Aliongeza kuwa kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa ziliso za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za  gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa kwa asilimia 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3

Alisema pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 kuna baadhi ya bidhaa zilionesha kuongezeka katika kipindi hicho zikiwa ni pamoja na bei za mchele kwa asilimia 4.7, mahindi kwa asilimia 31.6, unga wa mahindi kwa asilimia 24.1, vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 15.6 na mkaa kwa asilimia 16.0.

TIGO, KUPATANA.COM KUSHIRIKIANA KUWEZESHA BIASHARA KWA MTANDAO

August 09, 2016
 Meneja Miradi wa Tigo, Anthony Njau (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Dar es Salaam leo aasubuhi kuhusu kampuni hiyo na Kampuni ya ya Kupatana.com, kushirikiana kuwezesha biashara kwa mtandao. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kupatana.com, Philip Ebbersten na kushoto ni Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Makusaro Tesha. 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Kupatana.com, Philip Ebbersten (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Makusaro Tesha (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania na kampuni ya Kupatana.com, moja ya kampuni zinazoongoza Tanzania  katika huduma za masoko katika mtandao  zimeingia katika ubia wa kibiashara ambapo kila kampuni  itauza bidhaa na huduma za  kila mmoja katika majukwaa yao ya kidijitali.

Katika hatua za mwanzo za ushirikiano huu, Kampuni ya Tigo Tanzania itachagua maduka matatu ambayo Kupatana.Com itayatumia kuwawezesha wateja wa Tigo kuuza simu zao zilizotumika kwa kupitia jukwaa la Kupatana.com.

Akizungumza wakati wa  kusaini makubaliano baina ya pande hizo mbili jijini Dar es Salaam,  Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Tigo, Anthony Njau  alisema, “tukiwa ni kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali, tumeona kwamba hivi sasa Watanzania wamehamasika mno katika kufanya biashara kupitia njia ya mtandao.”Njau aliongeza kwamba , “Mtandao na wavuti wa Kupatana.com unatoa jukwaa zuri ambalo linabadilisha  namna ambavyo watu wanaishi kwa kuwezesha kupatikana kwa  huduma na bidhaa katika njia sahihi na rahisi.”

“Lengo la muda mrefu ni kuwapatia wateja wetu jukwaa  ambalo wanaweza kupakua  vifaa ambavyo vilishatumika ili kuviboresha na kwa upande wa Tigo kuuza  vifaa vipya, kuongeza usambazaji  na kuwa na mafanikio katika  jaribio hili la msingi, Tigo na Kupatana.com zitapanua wigo wa huduma hii na kuhakikisha inapatikana kwa urahisi katika maduka yote 52 ya Tigo  ambayo yamesambaa  kote nchini,” alisema Njau.

 Mkurugenzi wa Kupatana.com, Philip Ebbersten, alisema kwamba kupitia matumizi ya jukwaa hilo, wauzaji (kampuni na watu binafsi) wataweza  kuwafikia maelfu ya  wanunuzi muhimu kila siku bila kujali  maeneo yao ya kijiografia.

Alifafanua kuwa kuorodhesha bidhaa katika jukwaa hilo  ni bure  na kuwashauru wateja umuhimu wa  kufuata kanuni  na miongozo salama kwa bidhaa zote zitakazotangazwa Kupatana.com ili waweze kuzitapa  kwa usalama na uelewa zaidi.


Hassan Abbas ateuliwa kuwa mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)

Hassan Abbas ateuliwa kuwa mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)

August 09, 2016
mkur1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimtangaza Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas (kushoto) anayechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Assah Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
mkur2
Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas akieleza mikakati yake ikiwemo kuongeza mbinu za Mawasiliano kati ya serikali na wananchi ili kuchochea maendeleo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
PICHA NA ABUSHEHE NONDO-MAELEZO

NAIBU WAZIRI MPINA AMUWAKILISHA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA SIKU YA KIZIMKAZI

August 09, 2016
                                                  EVELYN MKOKOI
                                   OFISI YA MAKAMU WA RAIS
                                             ZANZIBAR

Wakazi wa kijiji cha Kizimkazi kilichopo katika  jimbo la Makunduchi Mkoa wa kusini unguja, kimekuwa na utaratibu wa kuadhimisha siku ya kizimkazi, maarufu kama kizimkazi day ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa nane.
 
Siku hiyo maarufu katika kijiji hicho ambayo imeanzishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo la Makunduchi mhe.Samia Suluhu Hassan ambae sasa ni Makamu wa Rais wa JAmuhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikiadhimishwa kijijini hapo kwa namna ya kipekee ya burudani, mashairi na michezo mbali mbali ambapo pia wana kizimkazi wamekuwa wakipata nafasi ya kuainisha changamoto mbali mbali zinazo wakabili kagtika kijiji hicho.

Akimuwalisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa RAis Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amehaidi kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Makunduchi mhe. Haruna Suleiman ambae pia ni Waziri wa Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia mifuko 100 ya simenti na mabati 100, na matofali 2000 ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vimeanishwa kuwa moja ya changamoto kijijini hapo.

Aidha, amehaidi wana kizimkazi kuwa kwa kushirikiana na mbunge na uongozi wa serikali uwanja wa mpira ambao umekuwa ukihitaji matengezo nao utaanza kusawazishwa kwa ajili ya michezo kijijini hapo.

Wana Kizimkazi wamebainisha kukabiliana na changamoto itokanayo na mapato na matumizi ya rasilimali ya bahari, pamoja na kupungua kwa nishati ya umeme kutokana na ongezeko la mahitaji litokanalo na mji huo kupanuka.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Mpina Pia alimuwailisha Makamo wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kampuni inayotengeneza nishati ya mkaa rafiki wa mazingira inayotumia malighafi itoknayo na taka za maganda ya miwa na  makarati na kuwapongeza kwa jitihada kubwa za utunzaji wa mazingira kwa kutokukata miti ovyo na ubunifu wa nishati hiyo.

Ziara ya naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar ni Sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Pamoja na kumuwakilisha Mhe, Makamu wa Rais katika siku maalum ya Kizimkazi. Kizimkazi Day.



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina aliyevaa suti akishika na kuangalia nishati ya mkaa unaotengenezwa  na malighafi itokanayo na taka za miwa na karatasi mjini Unguja, alipomuwakilisha Makamu wa Raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kampuni ya Blue Spot, inayotengeneza nishati hiyo bila kuharibu Mazingira.
 




Aliyesimama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na baadhi yaViongozi mbali mbali wa jimbo la Makunduchi mkoa wa kusini Unguja, akizungumza na wanachi (hawapo pichani) wa jimbo hilo katika kijiji cha kizimkazi .katika siku ya kizimkazi maarufu kama kizimkazi day, alipomuwakilisha mhe. Mkamu wa Rais Mama Samia Suhulu Hassan aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo.



Aliyesimama katikati Mkurugenzi wa Kampuni ya Blue Spot Bw Buhet Juma ya Mjini Unguja inayotengeneza nishati ya mkaa ambayo ni rafiki kwa mazingira  akimuonyesha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira aliyesimama kushoto, ambavyo nishati hiyo inavoengenezwa

Naibu Waziri  Mpina aliyesimama kati kati akishika chembe za malighafi inayotengeneza nishati ya mkaa rafiki kwa mazingira, alipotembelea kiwanda kidogo cha Ble Spot Mjini Unguja kumwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  Aliyekaa katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Ris Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika Picha ya Pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Raisi, Pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya kutengeza nishati ya Mkaa rafiki wa mazingira, katika kiwanda cha Blue Spot. (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)
MAVUNDE AFUNGA MAONESHO YA 9 YA NANENANE KANDA YA KATI DODOMA

MAVUNDE AFUNGA MAONESHO YA 9 YA NANENANE KANDA YA KATI DODOMA

August 09, 2016
ant1
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimia na Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Maonesho ya wakulima Nane nane kwa ajili ya kufunga maonesho hayo
ant2
Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini maelekezo ya namna ya kuchakata mihogo kutoka kwa mkulima wa zao hilo tangu mwaka 1980 kutoka Kijiji cha Nzuguni Josiah Malogo Ndoya
ant3
Mhe Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini namna ya kulima mahindi kwa mbinu bora na za kisasa ili kuwa na mavuno yenye tija
ant4
Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza maelekezo katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuhusu umuhimu wa matumizi ya dawa katika kilimo cha kisasa
ant5
Mhe Mavunde alipotembelea banda la ushonaji la Jeshi la kujenga Taifa JKT katika Maonesho ya Nane nane kabla ya kuyafunga rasmi
ant6
Mhe Mavunde alipotembelea banda la maonesho ya wanyama aina ya mbuzi, Ng’ombe na Kondoo la kampuni ya Ranchi za taifa (NARCO LTD)
ant7
007 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akipokea zawadi ya mboga za majani kutoka kwa vijana wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) mara baada ya kutembelea banda hilo
ant8
008 Mhe Mavunde alipotembelea banda la Maonesho ya kilimo cha Vitunguu
ant9
009 Mhe Mavunde akisalimiana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma marabaada ya kutembelea banda la maonesho la Wilaya hiyo
ant10
Mhe Mavunde akitazama ubora wa matrekta yaliyofikishwa katika Maonesho ya wakulima ya Nanen nane
ant11
0011 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki katika maonesho ya Nane nane katika uwanja wa Nzuguni Kanda ya kati Dodoma
……………………………………………………………………………………………….
Na Mathias Canal, Dodoma
Maonesho na Mashindano ya mifugo Kitaifa sanjari na Maonesho ya Kilimo yametoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde wakati akifunga maonesho ya wakulima Nane nane Kanda ya Kati Dodoma yaliyokuwa yanafanyika katika uwanja wa Nzuguni kwa kauli mbiu ya “Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya Maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Amesema kwa kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli inatekeleza azma ya kuhamishia makao makuu mjini Dodoma ameishauri Wizara ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi na ile ya Biashara na masoko kuangalia uwezekano wa kuanzisha rasmi maonesho ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi ya Kimataifa (International Agriculture Trade Fair) katika uwanja wa Nzuguni ambao ndio uwanja wenye eneo kubwa kwa maonesho ya Kilimo hapa nchini.
Aidha ametoa wito kwa Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo kuendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.
“Naomba niwaambie wakulima na wafugaji wetu kuwa maonesho ninayoyafunga hii leo ni muafaka na fursa nzuri kwao hususani vijana kwenda kuanza mara moja kutumia mlichojifunza na kuleta mapinduzi yenye maendeleo chanya yanayotarajiwa kiuchumi, hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuzikumbusha Halmashauri za serikali za mitaa zote kuwahamasisha wakulima, Wafugaji na wadau wengine kutumia teknolojia zilizooneshwa hapa kuongeza ufanisi wao katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi” Alisema Mavunde
Naibu waziri huyo pia ametoa zawadi kwa washindi katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma na Singida, Wizara za serikali, Taasisi za uzalishaji wa serikali, Makampuni ya pembejeo za Kilimo na Mifugo, Makampuni ya zana za Kilimo na Mifugo, Taasisi za serikali na Mashirika ya Umma, Taasisi za fedha na Mabenki, Taaisisi za mafunzo na utafiti, Taaisisi zisizo za kiserikali (NGOs na CBOs), Taasisi za mawasiliano ya kibiashara, Mamlaka za udhibiti, Vyombo vya habari, na Kampuni za nishati mbadala kwa kufanya vizuri katika maonesho hayo.
Pia zawadi hizo zimetolewa pia kwa watu wenye mashamba makubwa ya ufugaji ng’ombe wa maziwa, Wafugaji wadogo wa ng’ombe wa nyama, Wafugaji bora, na Wakulima bora.
Sambamba na hao pia Jeshi la Kujenga Taifa JKT limeibuka kidedea kwa ushindi wa jumla likifuatiwa na Jeshi la Magereza ambapo nafasi ya tatu imechukuliwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvu.
Akitoa maelezo ya awali kuhusu maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa Malengo ya maonesho hayo ni utoaji elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi.
Mtaturu alisema kuwa mpaka tarehe 7 hapo jana jumla ya watu waliokuwa wametembelea inakadiriwa kuwa 40,000 huku matarajio ya siku ya ufungaji ikitarajiwa kuongezeka watu 12,000 na kufikia idadi ya watu 52,000.
Dc Mtaturu amesema kuwa Teknolojia/Bidhaa zilizooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa (JKT Kondoa) Taasisi za kitafiti ambazo zimeonyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa ya kanda ya kati na udhibiti wa magonjwa.
Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, Taasisis za elimu zimeonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waandaaji wa Maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amemshukuru mgeni rasmi Antony P. Mavunde kwa kuitikia wito wa kufunga maonesho hayo ambapo pia ameishukuru Benki kuu ya Tanzania (BOT), Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, LAPF, Mkuu wa Mkoa wa Singida na Chuo kikuu cha Dodoma kwa uwakilishi na uchangiaji kwa ajili ya maonesho hayo.
Maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane Kanda ya kati Dodoma yaliyohusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yalifunguliwa tarehe 03 Agosti 2016 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe.

HALMASHAURI YA WILAYA YA LUSHOTO YATISHIA KUWAONDOA WAPANGAJI KWENYE MAJENGO YAO WASIOLIPA KODI KWA WAKATI

August 09, 2016
Kushoto  ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto,Kazimbaya Makwega Kazimbaya akizungumza na waandishi wa habari
HALMASHAURI  ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga imetishia kuwaondoa watu waliopangisha katika nyumba za Serikali na vibanda vya biashara watakaoshindwa kulipa kodi za pango kwa wakati uliopangwa na kuwagaiwa wengine wenye uwezo wa kufanya hivyo ili kuongeza kasi ya ukusanyaji
wa mapato.

Hatua hiyo inatokana na baadhi yao kutokulipa kodi zao kwa muda
ulioweka na hivyo halmashauri hiyo kutoa hadi kufikia Agosti 13 mwaka huu wawe wamekwisha lipa la sivyo watashughulikiwa ikiwemo kuondolewa kwenye nyumba hizo.

Haya yalisemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya
hiyo,Kazimbaya Makwega Kazimbaya ambapo  alisema kuwa Serikali haitakuwa tayari kuona inapoteza mapato yake kwa kuwaachia watu wakikaa kwenye majengo hayo ya serikali kwa kutegemea vyeo au nafasi zao za kifedha bila ya kulipia kodi jambo ambalo katika serikali ya awamu ya tano watu wa namna hiyo hawatakuwa na nafasi.

Alisema kuwa zipo mali za serikali ikiwemo nyumba,vibanda vya biashara na vizimba katika soko kuu ambavyo vinafanyiwa kazi na wafanyabiashara bila ya kulipiwa kodi kwa muda mrefu na kupoteza pato la Halmashauri idara ya biashara itakuwa na wajibu wa upotevu wa pesa hizo.

Makwega alisema kuwa lazima Halmashauri kwa kushirikiana na idara ya biashara itumuie vizuri rasilimali zake na kuzisimamia ili kuhakikisha swala la ukusanyaji wa kodi katika vyanzo hivyo unafanyika kwa wakati na bila ya ubabaishaji.

Alisema katika suala hilo hawataangalia cheo cha mtu awe Mbunge,Diwani ama mfanyakazi yeyote serikalini na halmashauri badala yake wasiokuwa tayari wataondolewa ili kupisha watu watakao kuwa na uwezo wa kulipia kodi ya mapango kwa wakati ili kuchangia ongezeko la mapato.

Aidha alisema zipo tabia zilizojengeka kwa muda mrefu kwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri kufanya kazi kwa kulindana na baadhi ya wateja wao kutokana na nafasi zao hali hiyo ndiyo iliyopelekea kupoteza kiasi kikubwa cha pato la Halmashauri.

Mkurugenzi huyo alisema huu si muda wa kulindana tena kila mmoja anapaswa awajibike katika nafasi yake ya kazi kiukamilifu na kuhakikisha Halmashauri inakusanya kodi ya kutosha itakayaokidhi uwezo wa kuboresha shughuli mbalimbali za maendeleo Wilayani humo.

Akitolea mfano mkurugenzi huyo alisema wanahitajika kukusanya kiasi cha shilingi 200 ushuru wa wafanya biashara sokoni na shilingi 800 gharama ya kulipia kizimba jambo kwa siku jambo ambalo halikufanyika kwa miaka mingi na kupoteza pesa nyingi na sasa wafanya biashara wanaowajibu wa kulipia kiashi hicho kama nilivyoelekeza.

Hata hivyo alisema Wilaya imekuwa na rasilimali nyingi ambazo
hazikutumiwa vizuri kwa ajili ya kuwaleta maendeleo wananchi wa maeneo husika huku wananchi wakilalama kutokuwepo kwa baadhi ya huduma na kupelekea kuichukia Serikali yao jambo ambalo  linahitaji kusimamiwa kwa nguvu zote ili rasilimali hizo ziwe na manufaa kwa wananchi wote.

Makwega alisema hatomvumila mtumishi yeyote atakae kwenda kinyume na taratibu za kazi na kutoa onyo kwa watumishi wote sharia kali zitachuliwa kwa yoyote atake bainika ni miongoni mwa wanaokwamisha jitihada za kupambana na jitihada za  kuwapunguzia kero wananchi.

Matukio mbalimbali ya Maonesho ya nanenane yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi

August 09, 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akipokea maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi, jana katika banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwenye maonesho ya Nanenane Kitaifa mkoani Lindi, kabla ya kufungwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwaeleza jambo washiriki wa maonesho ya Nanenane wa banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), alipotembelea jana kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Maonesho hayo yalifungwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mhe. Geofrey Zambi (wa kwanza kulia) akipokea maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi (wa pili kushoto), wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Nanenane mkoani Lindi, ambapo yalifikia kilele jana na kufungwa na Mhe. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan .
Bi. Fatma Matimba (kulia) akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lindi, juu ya ufanyaji wa kazi wa kifaa cha ukaguzi wa abiria kabla ya kuingia eneo la kwenda kupanda ndege, walipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Nanenane kitaifa Lindi.
Bi. Nuru Nyoni (kulia) akitoa maelezo ya kifaa cha ukaguzi kwa mkazi wa Lindi, alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Bi. Bahati Mollel (kushoto) akiwafafanulia jambo wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ngongo juu ya viwanja vya ndege vilivyo chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), walipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho ya Nanenane kitaifa mkoani Lindi.
Bi. Janet Mugini (kushoto) akitoa maelezo mbalimbali kwa mkazi wa Kilwa, aliyetembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Lindi.
Bw. Edward Kimaro (kulia) akimwelekeza mkazi wa Lindi namna ndege inavyopaa baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, katika maonesho ya Nanenane kitaifa mkoani Lindi, yaliyofungwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wakipata maelezo mbalimbali kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mkoani Lindi.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Lindi, Bw. Boniface Njanda akitoa maelezo mbalimbali kwa Mwananchi aliyetembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Lindi.