BABU SEYA NA PAPII KOCHA WAANZA MAANDALIZI YA UJIO WAO MPYA

BABU SEYA NA PAPII KOCHA WAANZA MAANDALIZI YA UJIO WAO MPYA

January 21, 2018


Muimbaji nguli wa muziki wa dance, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanae, Papii Kocha wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.

Wawili hao walipewa msamaha na Rais Dkt John Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji hao wanaopendwa sana kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Bi. Juliana Shonza aliwakutanisha na uongozi wa Wanene Studios waliokubali kuchukua jukumu la kuwarudisha tena kwenye muziki. Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi mpya katika studio hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Wameanza kwa kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni mno kwao kutokana na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.

“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliyamiss, nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” alisema Papii Kocha wakati wa photoshoot.

Kwa kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali zaidi ya zile za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii.

Kwenye photoshoot hiyo iliyofanywa na mpiga picha mahiri Eric Luga, Babu Seya na Papii Kocha walivalishwa na mbunifu wa mavazi, Mtani Nyamakababi.

Unaweza kufuatilia kila hatua ya safari yao kuelekea kuachia kazi mpya kwa kulike ukurasa wao rasmi wa Instagram @babanamwana, Facebook: baba na mwana. Pia subscribe kwenye channel yao ya Youtube iitwayo Baba na Mwana kuona video mbalimbali za behind the scenes.
​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​
Unaweza kuangalia video ya behind the scenes ya upigaji picha kwa kufuata link hii >> https://youtu.be/h-Kdp87now4

WAZIRI MPINA AKIPIGA FAINI YA SHILINGI MILIONI 100 KIWANDA CHA SUNFLAG CHA ARUSHA KWA KUENDELEA KUFADHILI UVUVI HARAMU.

January 21, 2018
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha, Ajay Shah, akiongoza zoezi la kuchoma  nyavu haramu za dagaa zilizo chini ya sentimita 8 (marobota 584) zenye jumla ya shilingi milioni mia moja zilizokamatwa kwenye Kiwanda chake na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini  kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina kwenye dampo la  takataka nje kidogo ya jiji la Arusha leo.(Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akikagua chumba cha baridi cha kuhifadhia samaki (Cold room) cha kampuni ya Alpha Choice mjini Arusha  leo  akiwa katika operesheni  maalumu ya kudhibiti uvuvi haramu kulia ni mmliki wa kampuni hiyo Yussuf Khatry. (Na John Mapepele)
Marobota 584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100 wakitekea kwenye dampo nje ya jiji la Arusha leo. Marobota hayo alikamatwa na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini  kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina ambapo uteketezaji huo uliongozwa na mmliki  wa kiwanda hicho Ajey Shah(Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akisikiliza taarifa ya ukamataji wa marobota 584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100  kutoka kwa kiongozi wa Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini  West Mbembati aliye kulia, kushoto mwakilishi wa Afisa Tawala wa Mkoa wa Arusha David Lyamongi. (Na John Mapepele)
 
  • Mmiliki wa kiwanda aongoza zoezi la kuteketeza nyavu zilizokamatwa kwenye kiwanda chake.
 
Na John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina  amekitoza  faini ya Shilingi milioni mia moja Kiwanda cha Sunflag  Tanzania Limited cha jijini Arusha  baada ya kukutwa na makosa  mawili ambayo ni kuzalisha na kuuza nyavu bila kuwa na leseni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuzalisha na kuuza nyavu ambazo ziko kinyume na matakwa ya Sheria ya Uvuvi  namba 22 ya mwaka 2009.
Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ajay Shah, kiwanda kimekuwa kikitengeneza  vyavu hizo haramu kwa miaka mitatu mfululizo sasa ambapo inakadiliwa kuwa tayari kimeshatengeneza tani  1296 nyavu hizo  zenye thamani ya shilingi bilioni nne.
Akitoa taarifa kwa Waziri Mpina, Kiongozi wa kikosi kazi cha kutokomeza  uvuvi haramu katika kanda ya Ziwa Victoria, West Mbembati amesema kuwa tarehe 17/1/2018 walifika kwenye kiwanda hicho na kukamata marobota 584 yenye thamani ya milioni mia kufuatia  maelekezo ya Waziri Mpina yaliyotolewa Mjini mwanza hivi karibuni baada ya mfanyabiashara Dastan Venanti kukamatwa na nyavu hizo zenye thamani ya milioni sitini na tano ambazo nyaraka zilionyesha alinunua katika kiwanda hicho.
Akipokea taarifa hiyo Waziri Mpina alisema mkakati uliopo kwa sasa ni kuwabaini watengenezaji na wasambazaji wote wa zana haribifu za uvuvi ikiwa ni pamoja na vyavu zisizoruhusiwa kisheria ambapo amesema hatua za kali za kisheria dhidi yao zitatumika ili kudhibiti uvuvi haramu kwenye  maji(mito,maziwa na bahari) ya nchi yetu.
“Operesheni ya kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanya biashara wakuu wanaofadhili na kuendeleza  biashara ya uvuvi haramu ni ya kudumu ambapo mkakati uliopo  sasa ni kuwanyang’anya na kuwafutia lesseni zao za biashara” alisisitiza Mpina
Aliwaonya wafanyabiashara wanaosafirisha  samaki na mazao yake katika nchi za jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kongo wanaotishia kugoma ambapo amesisitiza kwamba hatua waliyoichukuwa ni ndogo badala yake waachane kabisa na biashara hiyo kwa kuwa wamekuwa wakikwepa kodi na kuikosesha  Serikali mapato yake kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ajay Shah alikiri kutenda makosa hayo na kueleza kuwa  kiwanda kimekuwa kikiendelea kutengeneza vyavu hizo bila kujua kuwa kilikuwa hakizingatii sheria  za Uvuvi ambapo alisema kimekuwa kinauza nje ya nchi hususan kwenye soko la Nairobi nchini Kenya  na Mwanza
Aliwataja baadhi ya wateja wake wakuu  wa mkoani Mwanza kuwa ni pamoja na Dastan Venant, Morice Otieno na Majani Masagati  ambao wote walikamatwa hivi karibuni na nyavu zisizoruhusiwa kisheria  na kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi haramu kilichoundwa na Waziri Mpina na kutozwa faini ya jumla ya shilingi milioni 120 huku vyavu hizo zikitaifishwa na kuteketezwa mara moja.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliongoza zoezi la kuteketeza  nyavu hizo haramu kwa kushirikiana na Waziri na Watendaji  mbalimbali wa Serikali katika dampo la kuwekea takataka nje kidogo ya jiji la Arusha huku akikiri kuwa  atazingatia taratibu zote za Serikali katika kutengeneza nyavu zinazoruhusiwa kisheria ambapo alisema tayari wameshapeleka barua Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupata kibali cha kutengeneza nyavu.
Aidha Waziri Mpina ametoa siku tatu kwa Watendaji wa Wizara yake  kumempatia kibali cha kutengeneza nyavu hizo kwa mujibu wa sheria za nchi. Kulingana na Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 kibali hicho kinatolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi.

TAMASHA LA BUSARA KUENZI SANAA NA UTAMADUNI WA MWAFRIKA

January 21, 2018
Na Mwandishi Wetu. Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni waliona kwa ajili ya kizazi kijacho ili kukijendea uzalendo wa kupenda nchi yao. Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud wakati akielezea ujio wa Tamasha la 15 linalotarajiwa kufanyika Ngome Kongwe, Unguja - Zanzibar kwa kushirikisha wanamuziki na vikundi mbali mbali vya sanaa kutoka pande zote za bara la Afrika na Ulaya. “Katika Tamasha hili, ni sehemu ambapo watu wenye weledi wa sanaa mbalimbali hukutana, kuanzia kwa wakurugenzi wa matamasha mpaka kwa wazalishaji wa muziki, mameneja wa wanamuziki, wasambazaji wa muziki, wote hawa huja hapa Zanzibar mwezi Februari kuja kushuhudia utamu wa midundo ya muziki wa Ukanda wa Afrika Mashariki,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud. Anaongeza kuwa, “Hili siyo tu tukio ambalo watumbuizaji wa Tamasha pekee huhudhuria, bali hata baadhi ya wanamuziki ambao hawapo katika orodha ya kutumbuiza huja kwa minajili ya kujifunza kutoka kwa wale wanaofanya maonesho mbalimbali, na pia hupata fursa ya kufahamiana na wadau muhimu wa tasnia yao na kutengeneza mahusiano ya kikazi kwa miezi ijayo, hata zaidi ya hapo baada ya tamasha kuisha.” Likisifika kuwa miongoni mwa matamasha yanayoheshimika, Sauti za Busara likiwa na kauli mbiu ya “Kuunganishwa na Muziki” kwa mwaka huu, linawakutanisha pamoja zaidi ya wanamuziki 460 katika visiwa vya Zanzibar. Likiwa ni tamasha ambalo limeshuhudia ukuaji mkubwa katika uadhimishwaji wake na mwaka huu ukiwa wa 15, Tamasha hili linavutia wataalamu wa habari na muziki kutoka katika kila pembe ya Afrika, Ulaya na mahali pengine, ambapo hutoa jukwaa la kipekee kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuutanganza muziki wao duniani. “Kila mwaka, kila mwanamuziki anayepata fursa ya kutumbuiza katika jukwaa la Sauti za Busara, hualikwa kuzunguka katika miji mbalimbali duniani na kufanya maonesho kwenye matamasha yanayofanyika katika nchi hizo. Wanamuziki ambao hupata fursa ya kualikwa aghalabu, ni wale ambao wamethibitika katika maonesho yao kuwa wabunifu, wenye kuzungumza ujumbe fulani, na wanaocheza muziki wenye utambulisho fulani,” anasema Yusuf, akiwataja Msafiri Zawose, Jagwa Music, Leo Mkanyia, Tausi Women’s Taarab na Maulidi ya Homu ya Mtendeni kama mifano ya vikundi vya Kitanzania ambavyo tayari vimekwishaitwa katika safari za kimataifa baada ya kuonekana katika Tamasha la Sauti za Busara. Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud, Tamasha la Sauti za Busara ni fursa adhimu ambayo wanamuziki kutoka Tanzania hawatakiwi kukosa, kwa kuwa fursa kama hizi ni chache na ngumu kuzipata ndani ya Afrika. “Watu wa rangi tofauti huungana kwa pamoja kusheherekea muziki wa Kiafrika. Matarajio na msisimko ni mkubwa, hoteli zinazopatikana Stone Town huwa zinajaa katika wiki ya tamasha zikiwahudumia watu wanaotoka katika kila kona ya Tanzania, Afrika na Ulaya,” anasema Yusuf. Kwa makadirio ya haraka, tamasha linachangia kiasi cha Dola za Marekani 7 milioni katika uchumi kila mwaka, kikiwa ni kipindi cha mavuno kwa biashara nyingi zinazofanyika kwenye kila pembe ya Zanzibar na sehemu zingine, na kulifanya Tamasha la Sauti za Busara kuwa zaidi ya ‘Tamasha la Muziki’. Hata hivyo, licha ya kuwa na mafanikio hayo yote, lakini changamoto kubwa inayolikumba tamasha hili ni ufadhili, na ndiyo sababu hata tamasha la mwaka 2016 lilifutwa na kusababisha hasara kubwa sana kwa biashara nyingi visiwani Zanzibar. “Tunaendelea kutegemea fedha za wafadhili kutoka katika balozi mbalimbali, ambapo balozi za Norway na Uswisi zikiwa miongoni mwa wafadhili wakubwa, zikisaidia mafunzo na jitihada za ujengaji uwezo,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud. Tamasha la Sauti za Busara 2018 linafadhiliwa na Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na Zambia, Africalia, Mozeti, Zanlink, Memories of Zanzibar, Zenj FM, Chuchu FM, Tifu TV, Music In Africa, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Emerson Zanzibar, Coastal Aviation, 2Tech Security, Ubalozi wa Ujerumani, Golden Tulip Dar City Centre. -- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''
RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN AWASILI UMOJA WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU KUANZA ZIARA YAKE

RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN AWASILI UMOJA WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU KUANZA ZIARA YAKE

January 21, 2018
????????????????????????????????????
RAIS wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na  Kiongozi wa Ngazi za Juu wa  nchi za Umoja wa  nchi za Falme za  Kiarabu( UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi,  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai, kuaza ziara yake ya wiki moja kulia ni Balozi wa Tanzania Katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk 
????????????????????????????????????
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Ngazi za Juu wa  nchi za Umoja wa  nchi za Falme za  Kiarabu( UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai kuaza ziara yake ya Wiki moja.(Picha na Ikulu)
????????????????????????????????????
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Mke wa Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai.(Picha na Ikulu)
????????????????????????????????????
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kiongozi wa ngazi za Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi,alipowasili katika Uwanja waNdege wa  Kimataifa wa Al Majlis Dubai kuaza ziara yake ya Kiserikali ya Wiki moja. kushoto Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) Mbarouk Nassor Mbarouk(Picha na Ikulu)
????????????????????????????????????
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi,  alipowaili katka Uwanja waNdege wa Kimataifa wa Al Maljis Dubai kuaza ziara yake ya Wiki moja, kushoto Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohammed.(Picha na Ikulu)
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai.(Picha na Ikulu)
????????????????????????????????????

WAZIRI MKUU AMUAGIZA RAS MARA KUKAGUA HALMASHAURI YA BUTIAMA

January 21, 2018
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Amesema Halmashauri hiyo imekuwa na tabia ya kutumia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo zinazotolewa na Serikali katika shughuli nyingine jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Januari 20, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Bitiama katika ukumbi wa chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere cha Mara.

Pia Waziri Mkuu aliagiza kuchunguzwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama Bw Solomon Ngiliule pamoja na Mweka Hazina wa Halmashauri Bw. Masanja Sabuni na Ofisa Manunuzi wa Halmashauri hiyo Bw. Robert Makendo.

Alisema viongozi hao wanatakiwa wachunguzwe kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu alisema fedha zingine ni pamoja na sh. milioni 70 za elimu maalumu, sh. milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote hazijulikani zimetumikaje. “Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi fanyeni uchunguzi na naomba taarifa yake mara mtakapokamilisha.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliiagiza Taasisi ya Kuzuzia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mara imkamate na kumuhoji Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoani Mara, Mhandisi Peter Salim baada ya kushindwa kutekeleza ujenzi wa mradi wa ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Butiama.
Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilitoa sh milioni 600 Aprili, 2017 kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo lakini hadi sasa wakala huo haujafanya kazi yoyote.

Katika maelezo yake Mhandisi Salim alisema ujenzi wa ofisi hiyo hadi kukamilika utagharimu sh. bilioni tatu, kati ya sh. milioni 600 zilizotolewa na Serikali sh milioni 400 zimetumika kujengea msingi, kauli ambayo ilipingwa na Mkuu wa wilaya hiyo Bibi Anna-Rose Nyamubi.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu siyo kweli kwamba kuna kazi inayoendelea bali kilichopo pale ni mashimo ambayo hayajulikani ni ya nini. Pia kuna jengo moja lilijengwa kwa mabati kama stoo na hakuna mafundi wanaoendelea na kazi"

Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali iko katika mchakato wa kuboresha mazingira ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ofisi za watumishi na kwamba haitamvumilia mtu yeyote atayekwamisha juhudi hizo.

Waziri Mkuu baada ya kuwasili wilayani Butiama akiambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa walizuru kaburi la Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo na kufanya mazungumzo na mjane wa Baba wa Taia, Mama Maria Nyerere.

Baada ya kuwasili katika eneo alilozikwa Mwalimu Nyerere, Waziri Mkuu na Mkewe waliweka shada la maua juu ya kaburi na kisha walishirikiana na wananchi kufanya maombi yaliyoongozwa na Chifu wa Wazanaki, Japheth Wanzagi.

Pia Waziri Mkuu alihutubia wakazi wa wilaya ya Butiama kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwenge, ambapo alitumia fursa hiyo kueleza juhudi mbalimbali za kuwaletea maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, JANUARI 21, 2018.
WALIMU WAWILI HUKO KIBAHA WASHUSHWA VYEO KWA KUKAIDI AGIZO LA ELIMU BURE

WALIMU WAWILI HUKO KIBAHA WASHUSHWA VYEO KWA KUKAIDI AGIZO LA ELIMU BURE

January 21, 2018

20160729_110251
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ,Assumpter Mshama ,aliyesimama akizungumza jambo kuhusiana na masuala ya Elimu bure .
Picha na Mwamvua Mwinyi
……………….
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MKUU wa wilaya ya Kibaha,Mkoani Pwani, Assumpter Mshama ameamuru walimu wawili wa shule za msingi washushwe vyeo kutoka nafasi ya mwalimu mkuu na kuwa walimu wa kawaida ,kutokana na kosa la kuchangisha michango wazazi.
Hatua hiyo ,ameichukua siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,kukemea tabia inayofanywa na baadhi ya walimu wakuu na bodi za shule kuchangisha wazazi na walezi michango ambayo serikali imeizuia.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha ,alisema walimu hao wamekiuka agizo la serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk .John Magufuli .
Mshama aliwataja walimu hao kuwa ni mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Miembesaba, Rashinde Kilakala ambaye alikuwa akipokea sh.1,000 kwa kila mwanafunzi kwa ajili ya mitihani jambo ambalo  ni kinyume cha agizo la serikali.
Mwalimu mwingine  ni wa shule ya msingi Jitegemee, Sapiensia Kilongozi ambae aliweka kikao na kuita wazazi na kuwataka wazazi wenye watoto watoe shilingi 2,000 kwa wiki kwa ajili ya masomo ya ziada na mitihani.
Mshama alisema,huo ni mwanzo kwani ataendelea kusimamia maagizo yanayotolewa na serikali ili iwe fundisho kwa walimu wanaokaidi mipango ya serikali hiyo.
Alieleza atakaeendelea kufanya hivyo akibainika atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi .
“Nilipata malalamiko kutoka kwa wazazi kwamba kuna walimu wakuu wa shule hizo wanachangisha wazazi fedha kwa ajili ya michango mbalimbali ambayo imekatazwa na siku chache zilizopita” alisema Mshama.
“Mwalimu huyu wa shule ya Miembesaba hana kibali wala hajapeleka barua na hakuwa na sababu wala kibali cha kufanya hivyo ambapo mtihani wa mwisho wa mwaka kila mtoto hutoa 1,000 na alikuwa hatoi risiti,” 
“Lazima tumheshimu Rais kwani juzi tu kaongelea suala la elimu bure,hata kama umechangisha risiti ulitoa hivyo mpumzike nafasi hizo mbaki walimu wakawaida,” alisema Mshama.
Aidha anashangaa walimu hao walipata wapi nguvu ya kuwashawishi wazazi na kupokea fedha hizo wakati Rais alishazuia mambo hayo.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jeniffer Omollo alisema suala la kuchangisha michango mashuleni lilipigwa marufuku na walimu waliaambiwa kuwa hawaruhusiwi kuwachangisha wazazi .
Alisema kuanzia sasa watawachukulia hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria.
Kwa upande wake mwalimu Kilakala alisema anashindwa kueleza kwani walikubaliana na wazazi lakini wakamgeuka kuwa walikuwa wakichanga kinyume cha taratibu hata hivyo hawezi kusema zaidi.
Mwalimu wa shule ya msingi Jitegemee Sapiensia Kilongozi yeye alijieleza”:niliitisha kikao cha wazazi na kujadili masuala ya taaluma na wazazi wenyewe waliingiza kipengele wanahitaji watoto wao wasaidiwe kwenye masomo ya ziada na mitihani,” alisema Kilongozi.
Alisema walikubaliana baada ya hapo wakaandika muhutasari lakini baadhi ya wazazi walikuja huku kueleza lakini nia na madhumuni ilikuwa ni kufuata taratibu kwani asingeweza kutoa maamuzi ya kupitisha jambo hilo ,maamuzi lazima yapelekwe kwa ofisa elimu kata na baadaye kwa mkurugenzi.
Kutokana na hali hiyo ,Mshama alisema ni lazima wapate fundisho kwa kushushwa nafasi zao za kazi ili wabaki walimu wa kawaida.

ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA

January 21, 2018

Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa  zana haramu za uvuvi  kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita .

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akielezea mikakati ya wilaya ya kuhakikisha wanapamba zaidi na vitendo ambavyo vimeendelea kufanywa na wavuvi ambao awana mapenzi mema na samaki waliomo kwenye ziwa viktoria wakati wa zoezi la uteketezaji wa zana haramu.

Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo.

Kiongozi wa kikosi maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi  kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu .
Na,Joel Maduka,Geita.
Serikali Mkoani Geita Imeteketeza  zana haramu zenye thamani ya shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila  zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142 makokoro ya dagaa 7 na dududu 11.
 
Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi  huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.
 
Zoezi hili la uteketezaji zana hizo limefanyika  kwenye Kata ya Nkome ,ambapo kiongozi wa oparesheni hiyo Gabriel  Mageni ,amemweleza mkuu wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa  hifadhi ya Rubondo  wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi  na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha wafanyakazi hao maarufu kwa jina la  “KIFUNDA”
 
Kufuatianmalalamiko hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na  taratibu za sheria  askari wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba taratibu za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha na vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na hawawezi kuwakingia kifua.
Aidha Mageni aliongeza kuwa  katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na  baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha serikali kukosa
mapato.
Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi,amewataadhalisha  watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.
 
Nyawalwa Wange  ni moja kati ya watu ambao wanajishughulisha na kazi ya uvuvi alisema  agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono kutokana na kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki
ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.
 
Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni  zaidi ya milion, 111 fedha
zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.
MAJALIWA AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NA KUTOA HESHIMA KWENYE KABURI LA BABA WA TAIFA

MAJALIWA AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NA KUTOA HESHIMA KWENYE KABURI LA BABA WA TAIFA

January 21, 2018
PMO_0425
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na Mama Maria Nyerere wakati walipomtembelea nyumbani kwake Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018
PMO_0645
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozana na Mama Maria Nyerere kuingia kwenye  uwanja wa Mwenge  katika  mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu katika kijiji cha Butiama Januari 20, 2018.
PMO_0457
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea  nyumbani kwake Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018. Kulia ni mkewe Mary .
PMO_0363
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere  eneo la Mwitongo, Butiama, Januari 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni mkewe Naima .
PMO_0326
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere  eneo la Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018.
PMO_0538
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Mkewe Mary na Mama Maria Nyerere wakiwapungia wananchi  katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uwanja wa Mwenge kijijini Butiama Januari 20, 2018
PMO_0600
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mwenge  katika kijiji cha Butiama Januari 20, 2017
PMO_0621
Wananchi wa Butiama wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa  Mwenge katika kijijini hapo Januari 2018
PMO_0560
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Butiama katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mwengekijijini hapo  Januari 20, 2018.
PMO_0579
Mama Maria Nyerere akiwasalimia wananchi wa Butiama katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mwenge  kijijini hapo  Januari 20, 2018.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu