MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI KIGALI, RWANDA KWA AJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA UMOJA WA AFRIKA

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI KIGALI, RWANDA KWA AJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA UMOJA WA AFRIKA

July 17, 2016

KIGA1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Francis Gatare alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rwanda kwa ajili ya  kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo picha na (OMR)
KIGA2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda ,Francis Gatare  mara alipowasili kwenye Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Kigali kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na SerIkali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa rais anamwakilisha Rais Dkt  John Magufuli Katika Mkutano huo ,Picha na (OMR)
KIGA3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda,Francis Gatare kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kigali, Rwanda mara baada ya Kuwasili nchini humo kwa ajili ya Kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt John Magufuli katika Mkutano huo. (Picha na OMR)
MAJALIWA AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA SHULE YA SEKONDARI YA LINDI ILIYOUNGUA

MAJALIWA AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA SHULE YA SEKONDARI YA LINDI ILIYOUNGUA

July 17, 2016

MKU1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakiwashukuru wananchi waliojitokeza kuchangia ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua moto hivi karibuni. Harambee hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya shule hiyo mjini Lindi Julai 17, 2017. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MKU2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakiwashukuru wananchi waliojitokeza kuchangia ujenzi na ukarabati waShule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua moto hivi karibuni. Harambee hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya shule hilyo mjini Lindi Julai 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MKU3

SERIKALI YA KITOZA FAINI KIWANDA CHA SABUNI MABIBO KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA.

July 17, 2016

Hili ni eneo la kiwanda linalotiririsha maji kutoka kiwanda cha kutengeneza sabuni kilichopo  mabibo  jijini Dar es salaam kinachotuhumiwa  kutiririsha maji machafu katika mto kibangu uliopo ubungo kibangu. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Luhaga Mpina akisikiliza kero za wanainchi wa boko zinazosababishwa na kiwanda cha Twiga cement kilichopo wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam 
Naibu Wazirgi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akiwa katika  ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda Royal soap kilichopo mabibo jijini 

EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM
17/7/2016
Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC imekitoza faini ya shilingi milioni kumi, kiwanda cha kutengeneza sabuni cha Royal Soap industry cha Mabibo jijini Dar es Saal kwa kosa la kutiririsha maji machafu na yenye sumu sambamba na vumbi la sabuni lenye kusambaa katika makazi wa watu na mazingira ya mto kibangu.
Uchafuzi huo wa mazingira umekuwa ni wa muda mrefu katika makazi ya mtaa wa mabibo kisimani na kupelekea afya za wakazi wa eneo hilo kuwa hatarini, kutokana na maji machafu yenye kemikali na vumbi la sabuni, na kupelekea wananchi wa mtaa huo wa kibangu kupeleka malalamiko yao katika  Ofisi ya Makamu wa Rais, na ndipo Naibu Waziri wa Ofisi Hiyo anaeshunghuliakia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina, kuinuka ofisini  na kwenda kujionea adha wanayoipata wakazi hao.
Naibu Waziri Mpina alilielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kufuatilia vipimo vya vumbi na maji ya sabuni yanayotiririka katika mazingira na mto kibangu, kama ni rafiki kwa mazingira na viumbe hai na kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku kumi na nne  sanjari na kukitoza faini ya shilingi milioni kumi kiwanda hicho na kukitaka kilipe kwa muda huo wa wiki mbili, kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zaake ya mwaka 2004.
Naibu Waziri Mpina, yupo kwenye ziara ya ukaguzi wa mazingira na kufuatiliaji na uzingatiaji wa sheria ya mazingira na kanuni zake kwa wawekezaji wenye viwanda nchini. Amewashukuru wananchi kwa kuripoti moja kwa moja kwa serikali juu ya waharibifu wa mazingira, na kuonyesha kuwa malalamiko ya wananchi yanafanyiwa kazi, Naibu Waziri Mpina anafanya Ziara nyingi za kushtukiza katika viwanda.

   


   
Wafanyakazi wa TBL Mwanza washerekea tuzo ya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga

Wafanyakazi wa TBL Mwanza washerekea tuzo ya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga

July 17, 2016

jos1 
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye picha ya pamoja katika sherehe ya wafanyakazi kusherekea tuzo kubwa ya Mackay waliyoipata kutokana na kiwanda kufanya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga
jos2 
Meneja wa Kiwanda cha Bia(TBL) mkoani Mwanza, Gabriel Pitso akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati waherehe hiyo
jos3 
Aliyekuwa Meneja wa kiwanda cha Bia TBL mkoani Mwanza, Richmond Raymond akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa sherehe
jos4 
Aliyekuwa Meneja wa kiwanda cha Bia TBL mkoani Mwanza, Richmond Raymond akimkabidhi tuzo Meneja wa Kiwanda hicho, Gabriel Pitso katika sherehe ya wafanyakazi kusherekea tuzo kubwa ya Mackay waliyoipata kutokana na kufanya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga
jos5Mwakilishi wa Wafanyakazi Tuico katika Kiwanda cha Bia TBL mkoani Mwanza, Vedasia Mafuru akizungumza wakati wa hafla hiyo
jos6 
Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia matukio wakati huo wakiburudika
……………………………………………………………………………………………………..
Wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mwanza kilichopo chini ya TBL Group jana walisheherekea mafanikio waliyoyapata mwaka huu ikiwemo  kushinda tuzo kubwa ya Mackay kutokana na kufanya uzalishaji wa kutumia teknolojia ya pumba za mpunga .
Mackay ni tuzo kubwa ya SABMiller ya kumuenzi mmoja wa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Graham Mackay ambaye katika kipindi chake cha kuitumikia kampuni hiyo aliendeleza kwa kiasi kikubwa na alifariki miaka mitatu iliyopita ambapo kampuni imeanzisha tuzo yake kwa viwanda vyake ambavyo vinafanya uzalishaji unaoendana sambamba na malengo ya kampuni .
Moja ya malengo ya SABMiller ambayo baadhi yake yanashahabiana na malengo ya Umoja wa Mataifa yamelenga katika kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira na unaoleta mabadiliko kwa jamii kwa kuziwezesha kujikwamua kiuchumi.
Akiongea katika hafla hiyo,aliyekuwa Meneja wa kiwanda hicho ambaye amehamishiwa kikazi nchini Afrika ya Kusini,Richmond Raymond amewapongeza wafanyakazi wote kwa mafanikio haya kwa kukiwezesha kiwanda  kuendelea kungaa na kujinyakulia tuzo  mbalimbali kama hii ya Mackay.“Ushindani ulikuwa mkubwa na ulihusisha viwanda mbalimbali  lakini hatimaye tumefanikiwa kunyakua tuzo hii na kuweka rekodi ya kuwa kiwanda cha kwanza kuipata barani Afrika”.Alisema
Pia alitoa shukrani kwa wateja wote wanaoendelea kuiunga mkono kampuni kwa kununua bidhaa zake na kuongeza kuwa siku zote kampuni itahakikisha inaongeza  uzalishaji na kuendelea kuingiza bidhaa bora sokoni ikiwemo kusaidia huduma mbalimbali zinazoleta mabadiliko kwenye jamii.
Kwa upande wake Meneja wa TBL Mwanza Gabriel Pitso, alisema kuwa kiwanda hicho ndicho cha kwanza kupata tuzo hii nchini na ushindi huu umetokana na kufanya uzalishaji unaozingatia utunzaji wa mazingira kwa kutumia mashine zinazotumia pumba za mpunga na mashudu ambao kitaalamu hujulikana kama Dry –De- Husking (DDH)  .
Alisema kampuni mama ya SABMiller ilifanya utafiti na baada ya utafiti huo iliamua kabla ya kuanzisha teknolojia  ya uzalishaji usiotumia mafuta  ya dizeli kwenye viwanda vyake vyote ianzie katika kiwanda cha Mwanza ambapo katika miaka ya kwanza ya majaribio mafanikio makubwa yamepatikana kutokana na kutumia teknolojia hii ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji na kupunguza uharibifu wa mazingira.
Mbali na kupunguza athari za uharibifu wa mazingira na gharama za uendeshaji teknolojia hii kwa kiasi kikubwa inasaidia kuongeza vipato kwa wakulima wa pamba na mchele  na wafanyabiashara wanaokusanya pumba kwa ajili ya kukiuzia kiwanda “Zamani pumba za mchele zilikuwa takataka lakini hivi sasa zimegeuka lulu kwa kuwa zina soko tunazitumia katika uzalishaji hivyo kuna wafanyabiashara wanapita maeneo mbalimbali wakizikusanya kwa ajili ya kutuuzia na huu ndio uwekezaji mzuri unaonufaisha jamii inayoishi jirani na maeneo ya kiwanda na  ni moja ya malengo yetu”.Alisema.
ZIARA YA MAJALIWA LINDI NA MTWARA

ZIARA YA MAJALIWA LINDI NA MTWARA

July 17, 2016

LIO1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Ruangwa  ambao walimshukuru kwa jitihada kubwa anazofanya  za kuboresha maisha ya Wanachi wa jimbo lake la uchaguzi.  Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIO2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Ruangwa  ambao walimshukuru kwa jitihada kubwa anazofanya  za kuboresha maisha ya Wanachi wa jimbo lake la uchaguzi.  Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIO3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja uliopo kwenye kata ya  Nachingwea mjini Ruangwa Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIO4 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi  , Renather Mzinga ambaye amepandishwa cheo na kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi. Alikuwa  katika ziara ya mkoa wa Lindi Julai 16,2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIO5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi, viongozi na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIO6 
Baadhi ya Watumishi , Viongozi na wananchi wa mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIO7 
Baadhi ya Watumishi , Viongozi na wananchi wa mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo tano kati ya tisa alizokuwa anakatwa mkulima wa zao la korosho uko pale pale na unatarajiwa kuanza kutumika katika msimu mwaka huu hivyo ameitaka Bodi ya Korosho kusimamia uamuzi huo.
“Watendaji wa Serikali katika ngazi mbalimbali mnatakiwa kuhakikisha kwamba maelekezo haya yanafuatwa. Malengo yetu ni kumpunguzia mkulima mzigo wa tozo nyingi alizokuwa anakatwa,” alisema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Julai 16, 2016) wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa Mtwara pamoja na taarifa ya kuondolewa kwa baadhi ya tozo katika zao la korosho zilizowasilishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego.
Alisema Serikali iliamua kuzifuta tozo hizo baada ya kubainika kuwa zilikuwa zikiwanyonya wakulima hali iliyosababisha wauchukie mfumo wa stakabadhi ghalani.
 “Kuanzia mwaka huu Serikali imeamua mfanyabiashara yeyote wa korosho hana budi kuanza kulipa malipo ya awali kabla ya kuingia kwenye mnada ili tuwe na uhakika wa kununua korosho hizo na kuwalipa wakulima kwa wakati,” alisema.
Akizungumzia kuhusu changamoto ya kushuka kwa uzalishaji wa korosho Waziri Mkuu aliutaka mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao hilo ufanye utafiti wa kubaini sababu ili waweze kutafuta namna ya kuipatia ufumbuzi.
“Nitakuja kukutana na viongozi wa mfuko waniambie wanafanya nini na wamefanya nini miaka mitatu iliyopita na wana mpango gani huko mbele tunakokwenda kama hakuna mpango tutauangalia mara mbili mbili kwani wana fedha nyingi lakini hata mbegu hawapeleki kwa wakulima,” alisema.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha kila msimu wakulima wanapata pembejeo bora na zinawafikia kwa wakati ili waweze kupata mazao ya kutosha.
Serikali yasaidia viwanda vidogo 48,996

Serikali yasaidia viwanda vidogo 48,996

July 17, 2016

DSC_1141 
Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesaidia jumla ya viwanda vidogo 48,996 kwa kuvipa huduma muhimu zinazowawezesha wajasiriamali kusimama wenyewe ili kuondokana na lindi la umasikini.
Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Viwanda Vidogo na vya Kati kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Consolatha Ishebabi alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii kuhusu mikakati ya Serikali juu ya kuendeleza viwanda vidogo pamoja na umuhimu wa viwanda hivyo.
Dkt. Ishebabi amesema kuwa Viwanda Vidogo vikiendelezwa ndio mwanzo wa kuwa na viwanda vya Kati na Vikubwa na hiyo ndio sababu kubwa inayoifanya Serikali kutilia mkazo na kuzidi kuweka mikakati mingi ya kuviinua viwanda hivyo ili vikue na kufikia viwanda vya kati au vikubwa.
“Kwa mujibu wa Sensa ya Viwanda ya mwaka 2013, Tanzania ina jumla ya viwanda vidogo 48,996 ambavyo vimesaidia kutoa jumla ya ajira 156,476 kwa wananchi, hivyo tunaona umuhimu wa viwanda vidogo katika suala la kutoa ajira na kupunguza umasikini kwa kiasi kikubwa”, alisema Dkt. Ishebabi.
Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa viwanda vidogo sio mali ya Serikali bali Serikali iko pamoja na viwanda hivyo katika kuvisaidia ili viendelee na kuhakikisha vinakuwa kufikia viwanda vya kati au vikubwa hivyo, kazi ya Serikali ni kuwahamasisha wananchi na kuwapa misaada ya elimu, mikopo pamoja na kuwawezesha maeneo ya kufanyia shughuli hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na Habari wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Viwanda Vidogo (SIDO), Janeth Minja amesema kuwa Shirika hilo ni kubwa na liko katika Mikoa yote Tanzania, linawasaidia wajasiriamali kwa kuwapa huduma za aina 4 ambazo ni; mafunzo, teknolojia, mikopo pamoja na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.
“Napenda kutoa rai kwa wananchi hasa vijana na wanawake wasio na ajira kuwa wasijibweteke tu majumbani bali watumie fursa zinazotolewa na SIDO ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini, kama mtu ana wazo la biashara anatakiwa awasiliane na ofisi zetu za SIDO zilizopo kwenye Mkoa husika”, alisema Janeth.