BASI LA URIO LAPATA AJALI 31 WAJERUHIWA
picha
ya chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye basi hilo aina
ya Urio lililopata ajali leo jioni katika eneo la Kia wilayani Hai
mkoani Kilimanjaro
wananchi
wawakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea leo jioni katika eneo la kia
ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruliwa
Basi
aina ya Urio yenye namba za usajili T 137 BCX inayofanya safari zake
moshi kuelekea leguruki mkoani Arusha leo limepinduka katika eneo la
kia na kujeruhi watu zaidi ya 31
kwa
mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa
dereva huyo alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka
barabarani
"dereva
huyu alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuama
barabara ndipo ilipo anguka gafla na kubiringita mara tatu apa yenyewe
unavyoiyona tumeigeza ilikuwa kichwa chini matairi juu"alisema mmoja
wapo wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina
mpaka
kamera ya libeneke la kaskazini inaondoka eneo la tukio watu 31
walikuwa wamekwishwa pelekwa katika hospitali ya wilaya ya hai kwa ajili
ya matibabu wakiwemo wanafunzi wa shule ya leguruki ambao walikuwa
wanarejea shuleni mara baada ya kumaliza likizo yao ya sikukuu ya
pasaka
kwa habari zaidi libeneke itaendelea kukujuza nini kinachoendelea.
MZEE MSUYA AJITOA KATIKA SIASA; JK AMPONGEZA
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za CCM wilaya ya Mwanga leo |
Mzee Msuya akitoa pongezi zake kabla ya kuaga rasmi.
Kundi la wazee wa kimila wakiongozwa na Mzee Kasim Msemo wakimkaribisha Mzee Msuya kijijini |
Rais Kikwete akizungumza na wananchi katika hafla ya kumuaga Mzee Msuya katika ulingo wa siasa, uliofanyika leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mwanga.
Mamia ya Wananchi waliokusanyika kushuhudia hafla hiyo
RAIS JAKAYA KIKWETE AFANYA ZIARA MKOANI KILIMANJARO.
Rais
Kikwete akiwasili ikulu mjini Moshi akipokelewa na mwenyeji wake mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na mkuu wa wilaya ya Moshi
Ibrahim Msengi.
Viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakijiandaa kumpokea rais Kikwete alipowasili mjini Moshi.
Mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza mara baada ya rais
kuwasili ikulu mjini Moshi kwa ajili ya ziara wilayani Mwanga .
Baadhi ya wanannchi wakiwemo makada wa chama cha mapinduzi wakiwa Ikulu ya Moshi kungojea rais Jakaya Kikwete.
Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akiteta jambo na Niabu Meya wa manispaa ya Moshi Dk Mmbando ikulu ya mjini Moshi.
Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama na serikali.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Jumuiya ya Kiislamu yaungana na maaskofu kumtetea Warioba
Dar es Salaam. Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania imeungana na maaskofu mbalimbali kuwataka wajumbe wa Bunge la Katiba kuheshimu Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa kwa mujibu wa sheria na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Pia, taasisi hiyo imemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kujiuzulu nafasi
zake zote za uongozi kutokana na kauli waliyodai ya kichochezi,
aliyoitoa katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma kuwa ukipitishwa
muundo wa serikali tatu, jeshi litachukua nchi kwa sababu itashindwa
kuwalipa mishahara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji
wa Jumuiya na Taasisi hizo, Sheikh Rajab Katimba alilaani kauli kuhusu
jeshi na kuwa makanisa yote yatafungwa na nchi itakosa amani kutokana na
kupitisha muundo huo wa serikali.
Sheikh Katimba alisema Rasimu ya Katiba
iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba imetokana na utafiti na uchambuzi wa maoni
ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani ili kuboresha Muungano kutatua
kero zilizodumu kwa miaka 50 sasa.
Msimamo
Jumuiya hiyo iliweka wazi msimamo wake wa kutaka
serikali tatu na kutaka maoni ya makundi mbalimbali ndani ya Bunge la
Katiba kuheshimiwa.
Mjumbe wa Jumuiya hiyo, Sheikh Ramadhan Sanze pia alisema si ustaarabu kwa kundi moja kuhodhi mchakato kwa masilahi binafsi.
Alisema kukosoa maoni ya waasisi wa Taifa si
dhambi kwa sababu wao hawakuwa Mungu kwamba hawakosei, badala yake
alipendekeza watu waachwe wazungumze kwa utashi wa matakwa yao juu ya
kile kilichowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Nchi hii haithamini mchango wa wataalamu, tumeona
Tume ilivyofanya kazi nzuri, leo hii wanatukanwa hadharani, nawashangaa
sana viongozi wa nchi hii,” alisema.
Sheikh Sanze alisema miiko na misingi waliyoiweka
waasisi wa Taifa inavunjwa na viongozi wenyewe ambao leo wanasema
waasisi wanatukanwa kwa kuwa wamependekeza serikali tatu badala ya mbili
walizounda waasisi.
“Kulikuwa na utaratibu wa kubadilishana awamu za
uongozi katika Serikali ya Muungano, awamu hii rais akitoka Tanzania
Bara, ijayo atatoka Zanzibar; hii ndiyo misingi waliyoiweka waasisi,
mbona leo haifuatwi? Huu ni unafiki...” alifafanua Sheikh Sanze.
Jumuiya hiyo imewataka wananchi wote kuendelea na
mshikamano katika kutengeneza Katiba Mpya yenye maridhiano na
itakayoondoa kero zilizodumu kwa zaidi ya miaka 50.
chanzo:Mwananchi
chanzo:Mwananchi
MUZIKI KIMATAIFA : MWANAMUZIKI TOKA UGANDA DKT. JOSE CHAMELONE APAGAWISHA MASHABIKI NDANI YA LONDON, UINGEREZA
Dkt. Jose Chameleone akiwapagawisha wabongo na wazungu wa London, UK |
Jestina George wa Jestina-george.com akiwa bize na simu yake katiak show ya Jose Chameleone |
Jestina George wa kwanza kulia akipata picha na marafiki zake katika show ya Chameleone jijini London |
MWANDISHI ANUSURIKA, MTOTO MCHANGA AOKOLEWA
Mgambo aliyetaka kumtwisha Nyundo mtoto Anna Yohana, akimbeba mtoto akiwa na hofu kuwa amemdhuru vibaya....
Mtoto Anna Yohana aliyenusurika kuuawa kwa nyundo na Mgambo wa Jiji la Mbeya, akiwa amebebwa na msamaria mwema, baada ya mwandishi Gordon Kalulunga, kusogea na kuwapiga picha Mgambo wakashituka na kuanza kumshambulia kisha oparesheni ikaahirishwa.
Mtoto Anna Yohana aliyenusurika kuuawa kwa nyundo na Mgambo wa Jiji la Mbeya, akiwa amebebwa na msamaria mwema, baada ya mwandishi Gordon Kalulunga, kusogea na kuwapiga picha Mgambo wakashituka na kuanza kumshambulia kisha oparesheni ikaahirishwa.
Baada ya kujinasua na kupigana na mgambo zaidi ya saba, nikipiga simu
kwa baadhi ya waandishi wa habari huku Tape recorder ikiwa imeporwa.
*Ni kichanga cha miezi minne kilichofunikwa kwenye salfeti
sokoni.
*Wauza magazeti nao wahaha meza zao kuvunjwa usiku wa
manane.
Na,Christopher Nyenyembe, Mbeya
MWANDISHI wa Habari wa Gazeti hili (Tanzania Daima) mkoa wa Mbeya, Gordon
Kalulunga, ameambulia kipigo kutoka kwa mgambo wa jiji alipokuwa kazini
akipiga picha kwenye ‘operesheni vunja vunja’ sehemu ambayo mtoto mchanga wa
miezi minne alikuwa amelazwa na mama yake mzazi kwenye salfeti sokoni eneo la Kabwe Mwanjelwa.
Tukio hilo lilitokea wakati wa sherehe za pasaka(jumatatu ya
pasaka) baada ya uongozi wa jiji la Mbeya kwa kutumia mgambo wake walipoamua
kuendesha operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara waliopanga bidhaa zao kando
kando ya barabara kuu ya Tanzania- Zambia katika eneo maarufu la Mwanjelwa.
Mwandishi Kalulunga alikutwa na mkasa wa kupigwa na mgambo zaidi ya saba
na kusababisha purukshani kubwa mara alipofanikiwa kupiga picha zilizowahusu
mgambo hao waliokuwa wakivunja vibanda na kuwatimua wafanyabiashara ndogo ndogo
waliopigwa marufuku kupanga bidhaa zao kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa lengo
la kuweka usafi wa jiji hilo.
“Nilikuwa natimiza wajibu wangu wa kazi kama mwandishi wa
habari,alitokea mwanamke mmoja aliyekuwa
amevaa gauni refu la rangi ya njano na kunikaba shati,ndipo mgambo wa jiji
walipokuja na kuanza kunipiga,ilibidi kamera yangu nimkabidhi polisi mmoja
lakini nimepoteza redio yangu ya kurekodia”alisema Kalulunga.
Alisema baada ya tukio hilo kutokea ilibidi akatoe taarifa
kwenye kituo kidogo cha polisi Mwanjelwa na kupewa fomu ya kwenda kutibiwa (PF
3) ambako ilibidi apatiwe matibabu na aliporudi polisi Mwanjelwa alitakiwa na
mkuu wa kituo hicho akatoe maelezo yake kituo kikuu cha polisi mjini kwa OC –CID
au mkuu wa polisi wilaya (OCD).
Kitendo cha Mwandishi huyo kushambuliwa akiwa kazini
kulisababisha habari za haraka zisagae jijini humo na kisha kumfikia Kamanda wa
Polisi mkoa huo,Ahmed Msangi aliyeongea moja kwa moja na Kalulunga ili aweze
kufahamu aina ya uvunjifu wa amani uliojitokeza wakati wa operesheni vunja
vunja iliyokuwa akifanywa na mgambo hao ambao imechangia pia kuvunjwa vibanda
vya kuuzia magazeti tangu zoezi hilo lilipoanza.
“Namshukuru sana mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya,Richard Mchomvu
ametumia busara kubwa sana kunikutanisha na kiongozi wa operesheni hiyo kutoka
idara ya afya aliyejulikana kwa jina la Odas na mkuu wa mgambo pamoja na bosi
wangu kazini,jiji wamekiri kunifanyia kitendo hicho eti walikuwa hawafahamu
kama mimi ni mwandishi” alisema Kalulunga.
Kufuatia tukio hilo lililotulizwa na Mchomvu aliushauri
uongozi wa jiji hilo kushirikiana na vyombo vya habari katika majukumu yake kwa
kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa
zaidi kila jambo linapofanyika na kusisitiza kuwa usafi wa jiji ni muhimu hivyo
kila upande una jukumu lake hivyo hawana sababu yoyote ya kuonyeshana ubabe.
“Nikiwa mkuu wa polisi wa wilaya sipendi kuona haki za
binadamu zikivunjwa kienyeji,uhai wa kila mtu ni muhimu zaidi,tumieni vyombo
vya usalama kuweka mambo yenu vizuri,waandishi nao wana jukumu kubwa la
kuwasaidieni watumieni,angalieni sasa mmepoteza kifaa chake cha kazi,naomba
suala hili mlimalize kwa ustaarabu hata Mkurugenzi anapaswa kujua” alisema
Mchomvu.
Kufuatia tukio hilo na mtoto mchanga aliyenusurika kupigwa
nyundo wakati mgambo hao wakiendelea kubomoa vibanda,operesheni hiyo
ilisitishwa mara moja katika eneo hilo baada ya mama mzazi wa mtoto huyo
alipofanikiwa kutimua mbio na kumuacha mwanae aliyeangukia kwenye mikono ya
wasamaria.
Wakati hali hiyo ikitokea,wauzaji wa magazeti jijini humo
wamelalamikia zoezi hilo ambalo limewasababishia hasara kubwa baada ya meza zao kuvunjwa usiku
wa manane wakati uongozi wa jiji hilo unafahamu fika aina ya meza
zilizoruhusiwa kuwepo kwa ajili ya kuuzia magazeti na haijulikani mahali
zilipotupwa.
Jiji la Mbeya limekubali kulipa kifaa kilichoibwa/kupotea katika tafrani hiyo.
WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 500 KANDA YA KASKAZINI KUKUTANISHWA NA TAASISI ZA FEDHA
Mkurugenzi
wa Tanzania Horticulture Association(TAHA) bi,Jackline Mkindi
akizungumza na vyombo vya habari ambao hawapo pichani juu ya maonesho ya
kilimo ambao yanatarijiwa kufanyika siku ya Aprili 25 na 26 katika
viwanja vya AVRDC vilivyopo eneo la Tengeru wilayani arumeru mkoani
arushakilia kwake ni Mratibu wa Agri-Hub Tanzania bw,Tom ole sikar.
Na Ashura Mohamed-Arusha
WAKULIMA
na wafanyabiashara za kilimo zaidi ya 500 kanda ya kaskazini mwa
Tanzania wanatarajiwa kukutanishwa na taasisi za kifedha 48 ili kuweza
kuongeza ufahamu na uelewa juu ya huduma mbalimbali za nkifedha
zitolewazo na mabenki,taasisi ndogo ndogo za kifedha,mashirika ya
bima,taasisi za elimu na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizungumza
na vyombo vya habari afisa mtendaji mkuu wa TAHA bi.Jackline Mkindi
alisema kuwa wakulima wadogo wadogo wamekukwa wakikabiliwa na changamoto
kubwa ya ya upatikanaji wa huduma za kifedha hususani kwa wadau wa
sekta ya kilimo.
Katika
kutatua changamoto hiyo ya mitaji Agri-Hub Tanzania ikishirikiana na
TAHA mashirika,asasi mbalimbali kwa umoja wao wamethamiria
kuwaunganisha wadau wa kilimobiashara na watoa huduma za kifedha moja
kwa moja ili pande zote mbili ziweze kukuelewana na juu mahitaji yao na
hatimaye watoa huduma za kifedha waweze kubuni huduma bora zaidi za
kuimarisha utoaji huduma zao kwa wadau wa kilimo.
Mkindi
alisem kuwa maonesho hayo yatakwenda sambamba na uwasilishwaji wawa
mada mbalimbali ikiwemo uaandaaji bora wa wa mpango biashara (business
plans),umuhimu wa wa soko la hisa katika kuhakikisha upatikanaji wa
mitaji ya muda mrefu na matumizi bora ya mikopo katika biashara
hususani za kilimo.
Naye
mtaribu kutoka kampuni ya Agri-Hub Tanzania bw,Tom Ole
Sikar,alisisitiza kuwa maonesho hayo yanalenga kuwawezesha wakulima
wajasiriamali pamoja na wamiliki wa biashara za kilimo kama
wachuuzi,wauzaji wa pembejeo na wasindikaji kutambua fursa mbalimbali za
mitaji na usalama wa kifedha(Financial security) zilizopo kwa biashara
za kilimo.
Aidha
sikar alisema kuwa wadau hao wataweza kuunganishwa na taasisi muhimu
za fedha ikiwa ni pamoja na kushiriki katika mawasilisho na majadilino
juu ya fursa za sekta binafsi katika kilimo pamoja na wataalamu wa mambo
ya fedha na watoa huduma za maendeleo ya biashara kupitia semina
zitakazotolewa sambamba na maonesho hayo.
‘’maonesho
hayo yatawawezesha wadau kutambua njia za kuboresha biashara na utoaji
wa huduma kwa walengwa ikiwa ni pamoja na kujifunza kutoka kwa
wafanyabiashra wengine wa kilimo waliofanikiwa kutembelea maonesho
“alisema bw,Sakar
Maonesho
hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Taasisi ya AVRDC(The
World Vegetable Centre) kuanzia tarehe 25 na 26 april kuanzia majira ya
saa tatu aubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.
MCHEZAJI WA ZAMANI WA MAJIMAJI YA SONGEA, MTAWA KAPARATA AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS MKOANI MBEYA
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya
Shindano
la Tanzania Movie Talents Kwa kanda ya Nyanda ya Juu Kusini, Mkoani
Mbeya limefikia Tamati hapo jana kwa washindi watatu kutoka kanda hii ya
nyanda ya juu Kusini Kupatikana na Kutangazwa na Majaji watatu.
Washindi
waliotangazwa na Jaji Mkuu wa Shindano hilo, Roy Sarungi kwa
kushirikiana na Majaji wawili Single Mtambalike na Yvonne Chery ni
Steven Mapunda, Issalito Issaya na Mtawa Kaparata "BABU"
Mmoja
kati ya washindi watatu waliopatikana Jana na Kutangazwa na Jaji Mkuu wa
Shindano hilo Roy Sarungi ni mchezaji wa zamani wa timu ya mpira wa
Miguu ya Majimaji ya Songea, Bw Mtawa Kaparata.
Mtawa
Kaparata aliibuka mshindi kwa kuweza kuonyesha kipaji chake cha kuigiza
achilia mbali uwezo wa mpira aliokuwa nao kipindi hiko.
Kwa
upande wake mmoja wa washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents
ambae pia alikuwa mchezaji wa zamani wa Majimaji ya Songea , Bwa Mtawa
Kaparata alithibitisha kuwa 'Tanzania
Movie Talents imepokelewa vizuri na watanzania wa Mkoa wa Mbeya kwani
ameona usaili ulivyokuwa mgumu kutokana na vipaji vilivyoonyeshwa na
vijana wengi waliojitokeza na kuona ongezeko la washiriki waliojitokeza
kwaajili ya usaili wa kushiriki katika Shindano hili kubwa na la kwanza
Afrika Mashariki na Kati.
Hii
nikutokana na ukweli kwamba washiriki wote wanaofika kwaajili ya Usaili
hawatozwi kiasi chochote cha pesa kutoka timu ya Tanzania Movie Talents
na pia kufurahishwa na uamuzi wa Majaji wa Timu ya Tanzania Movie
Talents, niwazi kabisa kuwa kutotozwa kwa kiasi chochote cha pesa kwa
washiriki kumekuwa ni kivutio kikubwa kabisa hivyo kuongeza idadi ya
washiriki katika kila Kanda tunayoenda"alisema Mtawa Kaparata Mkazi wa
Mkoa wa Mbeya, Eneo la Soko Matola.
Shindano
hili kwa kanda ya nyanda Ya juu kusini limehitimishwa rasmi jana kwa
washindi watatu kupatikana na hatimaye shindano hili litahamia Kanda ya
Kusini na Usaili utafanyika Mkoani Mtwara
Shindano hili limelenga kuinua na kukuza vipaji vya kuigiza Tanzania na hatimaye kuendeleza vipaji hivi vya kuigiza Tanzania.
Usaili wa Shindano hili ni bure kabisa na fomu hupatikana eneo la usaili.
*MALINZI AWAPONGEZA SUKER, LEKJAA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amewapongeza marais Davor Suker na Fouzi Lekjaa kwa kuchaguliwa tena
hivi karibuni kuongoza mashirikisho ya mpira wa miguu katika nchi zao.
Suker
amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Croatia
(CFF) wakati Lekjaa amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu la Morocco (FRFM).
Katika
salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amesema ushindi waliopata ni
uthibitisho kuwa familia ya mpira wa miguu katika nchi zao ina imani
kubwa kwao katika kuendeleza mchezo huo ndani na nje ya nchi hizo.
Rais
Malinzi amesema Lekjaa na Suker wana uwezo wa kuendeleza kazi nzuri
ambayo tayari imefanyika, lakini vilevile kuja na mawazo mapya ambayo
yatakuwa changamoto kwa ustawi wa mchezo huo nchini Morocco na Croatia
kwa ujumla.
BURUNDI YAWASILI KUIKABILI TAIFA STARS JUMAMOSI
Timu
ya Taifa ya Burundi (Intamba M Rugamba) inatarajiwa kuwasili nchini
kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways
tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi (Aprili 26
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Intamba
Mu Rugamba itakuwa na msafara wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la
ufundi na viongozi, na itafikia hoteli ya Accomondia. Mechi hiyo
itachezwa kuanzia saa 10 jioni.
Nayo
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini
kwenye hoteli ya Kunduchi Beach ikijiandaa kwa mechi hiyo
itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa,
bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C
ni sh. 10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya
muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Subscribe to:
Posts (Atom)