SAFARI YA MWISHO YA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA KIOMONI GEORGE MAYALLA.

September 04, 2013

WAKAZI WA TANGA WAKIUAGA MWILI WA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA KIOMONI JIJINI TANGA,GEORGE MAYALLA NYUMBANI KWAKE JANA.

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA TANGA,OMARI GULEDI (ALIYEVAA SHUTI NYEUSI NA KUKUNJA MIKONI)AKIWA NA WAHESHIMIWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA MSIBANI HAPO JANA.

MKUU WA MKOA WA TANGA ,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA WA KWANZA KULIA KUSHOTO KWAKE ANAYEFUATIA NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO ,MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA WILAYA YA TANGA,KASIMU KISAUJI,ALIYESHIKA TAMA NI MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA TANGA,COMRADE KASSIM MBUGHUNI.

JENEZA LA MAREHEMU MAYALLA LIKICHUKULIWA NA VIJANA WA GREEN GADI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAYARI KWA AJILI YA KUPELEKWA MAKABURINI,

MWILI WA MAREHEMU MAYALLA UKIWA TAYARI KWA AJILI YA KUHIFADHIWA KWENYE MAKAZI YAKE YA MILELE.

UMATI WA WAOMBOLEZAJI WALIOJITOKEZA KWENYE MAZISHI HAYO. HABARI PICHA NA PASCAL MBUNGA ,KIOMONI TANGA.

RC GALLAWA AONGOZA MAZISHI YA DIWANI MAYALLA

September 04, 2013
Na Paskal Mbunga, Kiomoni-Tanga
MAMIA ya wakazi waTanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, leo wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiomoni, jijijini Tanga, George Mayalla aliyefariki juzi katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kutokana na maradhi ya kansa ya ubongo.


Akizungumza katika mazishi hayo, Gallawa aliwataka  viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali Mkpani hapa kujenga  mashirikiano ya dhati kati yao na wananchji ili kuleta maendeleo  ya haraka katika maeneo yao.
 

Gallawa alisema kata ya Kiomoni umesifika na kupata  maendeleo kunatokana na jitahada za marehemu Mayala  ambaye hakuchoka kuwashirikisha wananchi katika masuala ya maendeleo shirikishi.
 

Alisema enzi za uhai wake, marehemu Mayalla alitumia muda wake mwingi kutekeleza dhana ya maendeleo shirikishi ambapo alizishirikisha idara za serikali , taasisi na mashirika ya umma  na binafsi kusukuma  gurudumu la maendeleo.
 

Diwani Mayalla alichaguliwa kushika nafasi ya udiwani kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo tangu kipindi hicho amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanapata maendeleo na hilo alilitimiza kwa vitendo.
 

Marehemu Mayalla alizaliwa   mwaka 1948 mkoani Shinyanga ambapo baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari,alichaguliwa kuingia chuo kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1970 hadi 1973 alipomaliza na kutunukiwa shahada ya kwanza.
 

Mwaka 1974 diwani Mayalla alichaguliwa kwa masomo ya juu  katika chuo kikuu cha Nairobi ambako alihitimu digrii ya maendeleo na mipango miji.
 

Baada ya kufuzu masomo yake huko Nairobi, Kenya  Mayalla aliajiriwa mkoani Dar es Salaam mwaka 1975 kama Ofisa Mipango Miji.
 

Mwaka 1978, Mayalla alihajishiwa Mkoani Tanga ambapo aliajiariwa kuwa Ofisa Mipango Miji wa Manispaa ya Tanga mpaka 1988 alipostaafishwa na kuwa mkulima huko Kiomoni, nje kidogo ya jiji la Tanga.
 

Katika mwaka 1994 hadi 2001, aliteuliwa kuwa mshauri wa kujitegemea wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mazingira katika Manispaa ya Tanga.
 

Kulingana wa wasifu wa marehemu, Mayalla alipata kushika nyadhfa mbalimbali katika Halmashauri na baadaye Jiji la Tanga hadi anakutwa na mauti.
 

Marehemu George Mayalla ameacha mjane mmoja na watoto saba na wajukuu 11.  

Mashishi yake yalihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Tanga wakiwemo viongozi wa Chama na Serikali ambapo Meya wa Jiji la Tanga, Mstahiki Meya Omar Ghuledi alimsifia marehemu wa weledi katika utendaji kazi akisema kwamba amewahi kufanya naye kazi kwa awamu mbili.

Alisema alipata kufanya naye kazi mwaka 1984, yeye (Ghuledi) akiwa Naibu Meya wa Manispaa na marehemu akiwa Ofisa Mipango Miji.


Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga, Kassimu Mbughuni, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kassim Kisauji, Katibu wa CCM wilaya ya Tanga, Lucy Mwiru  na Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa, Shekimweri na viongozi wengine mbalimbali.


Mwenyezi Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu Mayalla. Amin
WANANCHI WAISHIO KARIBU NA HAFADHI ZA TAIFA WATAKIWA KUACHA KUISHI KIMAZOEA

WANANCHI WAISHIO KARIBU NA HAFADHI ZA TAIFA WATAKIWA KUACHA KUISHI KIMAZOEA

September 04, 2013
Raisa  Said,Pangani   
Hifadhi ya Taifa TANAPA imewataka wananchi waishio karibu na hifadhi za wanyama pori nchini kubadilika na kuacha tabia ya kuishi kimazoea badala yake wawe wabunifu kwa kupanda mazao ambayo hayashambuliwi na wanyama waishio  katika maeneo mbalimbali ya mbuga za wanyama.

Meneja Ujirani Mwema Taifa, Ahmed Mbugi alisema endapo wakazi wa maeneo jirani watapanda mazao kama ufuta,pilipili za kuwasha pamoja na miti ya kutanda ili kuzuia njia za wanyama kupita kwenye maeneo yao.

Alikuwa akizungumza katika mahojiano wakati wa mafunzo ya uandishi wa masuala ya Hifadhi ambayo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini na Mazingira Mkoani Tanga (TARUJA) na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wilayani Pangani hivi karibuni.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidi kupunguza uharibifu wa mimea unaofanywa kwa sasa na wanyama hao ikiwemo kuangusha minazi pamoja na kuharibu mazao yao mengine kutokana binadamu kufanya shughuli za kilimo kwenye njia za wanyama.

“njia pekee ya kumaliza tatizo wananchi kulalamikia kuwa uharibifu wa mazao yao na wakati mwingine wanyama hao kuingia ndani ya nyumba ni kuhakikisha mnapata mazao ambayo yatasaidia wanyama kutofika kwenye maeneo ya watu”alisema Mbugi.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Buyuni Kitopeni ambacho kimezungukwa na Hifadhi pande zote na Bahari uapnde mwingine, Diwani Akida alisema kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu zaidi ya minazi 770 imeangushwa na wanyama hao.

Akida alifafanua kuwa kuku 64 wamechukuliwa na tembo huku mbuzi 71 wakiliwa na simba wakiwa kwenye mabanda yao hasa nyakati za usiku na kuleta kero kubwa kwa wanakijiji waoishi maeneo ya jirani.

Alisema  wao kama  kijiji atua  za  awali  walizochukuwa za  kukabiliana  na wanyama  hao  nyakati za  usiku wamekuwa wakiwasha  moto  kwa kufunga  makuti  makavu  ili kuwaogopesha  wanyama kutoingia  kwenye makazi  yao kuwadhuru  wao na  mifugo  yao.

Shabani Omary  mkazi wa  kijiji  cha  Saadani  alisema kero kubwa  ni nyani  na  ngili  kuingia  kwenye  makazi  yao na kuchukua  vyakula  hasa  katika  kipindi cha  ukame .

Mwenyekiti  wa  kijiji  cha  Saadani,Mohamedi  Saidi alieleza  kuwa  vijiji  vilivyoathirika  na  uvamizi  wa wanyama  hao  kuwa  ni  mbwebwe, uvinje  pamoja  na  marumbi .

Ofisa  wanyamapori  wa  wilaya  Burhan  Ngulungu  alisema ujangili  umekithiri  kwa  kiasi  kikubwa  kutokana  na kutokuwepo  kwa  poli la  akiba .

Hata  hivyo  alibainisha  kuwa  kwa  sasa  wamepanga mpango  mkakati  wa  kuhakikisha  wanalinda  ili  kupunguza madhara  ya  wanyama hao.
 

TANAPA KUANZISHA VIVUTIO VYA ASILI KWENYE VIJIJI.

September 04, 2013
NA RAISA SAID,PANGANI
HIFADHI za Taifa ya Saadani (Sanapa)  inatarajia kuanzisha miradi ya vivutio vya asili vilivyoko kwenye vijiji vya maeneo yanayozunguka  hifadhi hizo ili  kuleta  maendeleo  ya  haraka  na  kuongeza  uchumi kwa  jamii inayozunguka hifadhi hizo .
Kwa mujibu  wa Muhifadhi  mkuu  wa  Hifadhi ya Saadani Hassan  Nguluma  alisema  miradi  hiyo  ni sehemu  ya  mipango  waliyokuwanayo  ya kuhakikisha  vijiji vinavyopakana  na  hifadhi  vinanufaika .
Hayo  yalisemwa  wakati wa  mafunzo  ya  uandishi  wa  masuala  ya hifadhi  yalioandaliwa  na  Chama  Cha  Waandishi  wa  Habari za  Vijijini  na  Mazingira (Taruja) na Shirika  la Hifadhi  za  Taifa  (Tanapa) yilayani  pangani  hivi  karibuni.
 “Nia yetu ni kuona wanachi wananufaika na raslimali walizonazo  kwa kuweka utaratibu wa kila maeneo kutangaza vivutio walivyonavyo zaidi ya wanyama walioko kwenye hifadhi basi wajionee mila na tamaduni zilizoko sehemu husika “.Alisema Muhifadhi  huyo.
Awali  Mwenyekiti  wa  Taruja  George Sembony alisema  kuwa lengo  la kuanzisha  chama  hicho  ni  kukuza  tasnia  ya  habari  kwa  kuongeza  ujuzi na  ufanisi  kwa  watendaji  wake  pamoja  na  kuwapa  uelewa  waandishi  juu ya  kuandika  habari  za  vijijini.
Alisema  kuwa   chama  hiki  hakikuanzishwa  ili kukinzana  na  vyama  vingine  vya  waandishi  bali  hiki  kinasaidia  katika  kuyashughulikia  masuala  moja  moja  kwa  undani  badala  ya  kuyashughulikia  kwa  ujumla .
Hata  hivyo  alisema pamoja  na  changamoto  ya  mbuga  ya  Saadani  ambayo  ndiyo  iliyowasukuma  kuomba  mafunzo  hayo  ya  siku nne yataweza  kuwapa  uelewa  zaidi  juu ya  changamoto hizo  nakuongeza  kuwa  japokuwa  mbuga  hiyo  ni mpya  napengine  wananchi  wa  eneo  hili  bado  hawajaweza  kuona  faida  ya  kuwepo  kwa  mbuga  hiyo.   
Alisema  kuwa  anaamini  kuwa  sio wote  waandishi  wanaelewa  faida  ya  kuwepo  kwa  mbuga  hiyo  kwa  maendeleo  na  ndio  maana  mambo  ambayo  yanarushwa  hewani  ni malalamiko  ya  wananchi  dhidi  ya  watendaji   wa  mbuga  hizi  ambao wanatimiza  wajibu  wao  kwa  mujibu  wa  sheria  au dhidi ya  wanyama  ambao wanaonekana  kuwa  hawana  faida  bali wanaharibu  mazao.
 Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Hussein Mselo alisema kuwa bado wananchi wa maeneo hayo hawana muako wa kutangaza vivituo vilivyoko kutoka na kukosa uwelewa wa taratibu za uendeshaji wa vivutio hivyo.
Alisema kwa sasa waandaa utaratibu wa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi  wa maeneo ya jirani yenye vivutio hivyo ili kujua umuhimu wake pamoja na fursa zilizopo ili waweze kuiongezea kipato kitakacho saidia kijiji na wananchi wake.
   

TANGA WALAANI COASTAL KUFANYIWA VURUGU.

September 04, 2013
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
WAPENZI na Mashabiki wa soka mkoa Tanga wamelaani vikali kitendo cha Mashabiki na Wanachama wa Yanga kufanya vurugu katika mechi ya Ligi kuu Tanzania bara kati ya Coastal Union na Yanga iliyochezwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuzitaka mamlaka husika kutolifumbia macho suala hilo.

Mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1,ambapo wakati mwamuzi akipuliza kipenga cha mwisho kulizuka vurugu ambacho ziliwashangaza mashabiki wa soka waliofika kuuangalia mchezo huo kwa kitendo cha wachezaji wa Yanga kuwafanyia vurugu wachezaji wa Coastal Union.

Licha ya mashabiki hao kuwashambulia wachezaji lakini pia walilivamia basi la Coastal Union na kufanya uharibifu mkubwa ikiwemo kulivunja vioo jambo hilo halipaswi kuachwa lipite hivi hivi bali lazima likemewe na klabu ya Yanga iwajibike kutokana na kuwa mashabiki wao ndio waliofanya vurugu hizo

Akizungumzia suala hilo,Katibu Mkuu wa Zamani wa Coastal Union,Salim Bawazir alilaani sana kitendo hicho ambacho kilifanywa na mashabiki hao pamoja na kushangazwa na ukimya wa shirikisho la soka hapa nchini TFF kwa sababu jambo hilo haliitaji Coastal Union
kuwaandikia barua wala kulalamika bali ni kitu ambacho wanakijua hivyo tulitegemea wangechukua uamuzi wa haraka kwani mashindani hayo yana ugenini na nyumbani.

Bawazir alisema shirikisho la soka nchini TFF lisitoe nafasi kwa wapenzi wa timu hizo kushambuliana kwa sababu hatimayake yanaweza kutokea maafa makubwa sana alitolea mfano kwa timu ya Yanga ilifaniywa vurugu kubwa kabuku,Coastal Union na kabuku wapi na wapi
alisisitiza bawaziri.

Aidha alitolea mfano wa timu ya Yanga kufanyiwa vurugu mlandizi,Je watasema timu ya Simba ndio iliwashambulia?Katibu huyo alisisitiza kwa kuzitaka klabu hizo kuweka mahusiano mazuri ili kuepusha vurugu na ni vyema Yanga katika hili wakawa waungwana na kulikemea na TFF kwa sababu walikuwa uwanjani wachukue hatua kwani itawasaidia

Katibu huyo alisema watu wa Tanga mjini ni wastaarabu sana na wataendelea kuichunga heshima ya mkoa huu kwa kutokuwafanyia vurugu Yanga na timu yoyote itakayokuja kucheza kwenye uwanja wa Mkwakwani pamoja na kuwasihi sana viongozi wa Yanga wasitetee kwa njia yoyote ile vurugu hizo bali walaani hii itasaidia TFF kwani itakuwa imetoa msaada mkubwa kwenye maamuzi yake.

Wakati huo huo,Bawazir alisema anashangazwa na suala la Kocha mkuu wa timu ya Taifa(Taifa Stars) Kim Poulsen kutowajumuisha kwenye kikiso hicho wachezaji kama Shabani Kado,Hassani Banda na Hamadi Juma katika timu ya Taifa kutokana na uwezo walionao wangeweza kuisaidia timu hiyo hasa kwenye mechi zake hali hiyo inaonekana kama wachezaji wana uwezo mkubwa lakini hawachezi Simba wala Yanga hawawezi kuchaguliwa timu ya Taifa.