OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YAENDELEA NA UHAKIKI WA VYAMA NCHINI

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YAENDELEA NA UHAKIKI WA VYAMA NCHINI

July 02, 2016


C1
Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw.Willium Brown Nyamtiga akisisitiza jambo kwa viongozi wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Jana wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Jijini  Buguruni Dar es salaam .
Zoezi la uhakiki wa  utekelezaji wa masharti ya usajili wa Vyama va Siasa  kwa upande wa Tanzania Bara  linaendelea .Tayari  vyama 18 vimekwishakuhakikiwa. Vyama vinne vinatarajiwa  kuhakikiwa  Julai 4. Zoezi hili ni zoezi la kawaida na endelevu  ambalo hufanyika  kila mwaka ili kupima endapo vyama vya siasa   vinakidhi matakwa ya  Sheria ya usajili wa vyama vya Siasa.
Uhakiki wa Vyama vya siasa ni zoezi muhimu sana kwa sababu ni zoezi ambalo hugusa uhai wa  kila  chama cha siasa.  Kwa upande wa Tanzania Visiwani , uhakiki unatarajiwa kuanza  mara baada ya kumalizika Bara  kwa tarehe ambazo zitatangazwa baadaye.
C2
Bw.Eugene Kabendera, Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) akitoa taarifa  wa watumishi  kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Jijini Makumbusho Dar es salaam Juzi
C3
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Jahazi Asilia, Bw. Mbwana S. Kibanda akifafanua jambo wakati wa zoezi la uhakiki  liliofanyika  Leo katika ofisi za chama hicho zilizopo ilala Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho na kushoto ni watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. (P.T)
C4
Bi. Esther B.Mwanri, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akikagua katiba ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo  Buguruni Malapa Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Bw. Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchumi na Mipango.
C5
Msajili Msaidizi wa Vyama Siasa  “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi. Piencia Kiurea akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha United Democratic Party (UDP) Bw. Godluck Ole-Medeye wakati akitoa taarifa muhimu za chama chake katika zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Kisiasa unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
C6
Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila (kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.
C7
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Usajili wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kushoto) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha NRA ( National Reconstruction Alliance) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jana Jijini Dar es Salaam.
C8
Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila (kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.
(Picha zote na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa)

MKURUGENZI MKUU NSSF AJIONEA MIRADI YA SHIRIKA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA 2016

July 02, 2016


Muonekano wa Banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika Maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.

Ofisa Masuala ya Bima wa NSSF, Peter Isack akitoa ufafanuzi kwa kuhusu majukumu ya kitengo chake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto), wakati mkurugenzi huyo alipotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba.
Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Moringe Nyerere akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushto), juu ya viwanja vinavyouzwa na NSSF vilivyopo eneo la Kiluvya.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia), akiangalia michoro ya nyumba ambayo ni sehemu ya miradi ya shirika hilo. Wa pili kulia ni Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Moringe Nyerere.

Msimamizi wa Mradi wa Mtoni Kijichi, Mohames Kimbe akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Msimamizi wa Mradi wa Mtoni Kijichi, Mohames Kimbe akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), kuhusu mradi wa nyumba za Kijichi. Kulia ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Salim Kimaro na Juma Kintu kutoka Idara ya Uhusiano.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), akiangalia mradi wa Mtoni Kijichi.
Ofisa Mauzo wa NSSF, Abbas Ramadhan akitoa maelezo kuhusu mradi wa nyumba wa Kijichi.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi, Salim Kimaro (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Aman Marcel wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara kifaa maalum kinachotumiwa na wanachama kutoa maoni yao kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo. 
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la NSSF.
Ofisa wa Masuala ya Bima wa NSSF, Peter Isaack akitoa maelezo mmoja wa watu waliofika katika banda la NSSF katika viwanja vya Sabasaba.
 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF akizungumza na maofisa waandamizi wa NSSF.
 Ofisa Uhusiano wa NSSF, Rehema Urembo akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja wa mfuko huo.

MADC WAPYA MKOANI TANGA WATAKIWA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA UMAKINI MKUBWA

July 02, 2016
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akizungumza kwenye halfa ya kuapishwa wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Othumani Shijja.

Mkuu wa wilaya mpya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella leo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanaisha Rajabu akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martne Shigella 

Add caption

Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah Issa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga leo.

Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella


Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Robert Gabriel akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella anayeshuhudia kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Said.




Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarfu Professa Maji Marefu kulia akimtambulisha Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM)Stanslaus Mabula wakati wa Halfa ya kuapishwa wakuu wa wilaya wapya leo







Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe kulia akitete jambo na Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga,William Mngazija mara baada ya kuapishwa


Mkuu wa Mkoa wa Tanga katikati akiwa picha ya pamoja na wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Tanga leo mara baada ya kuwaapisha