LAPF yasajili wanachama wapya 27, 362

LAPF yasajili wanachama wapya 27, 362

June 20, 2016


jame1 
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na mfuko huo katika huduma zake mbalimbali nchini kwa jamii Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
jame2 
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.
……………………………………………………………………………………………………………….
HASSAN SILAYO
Mfuko wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama wapya 27, 362 katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 tofauti na mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo walisajili wanachama 23,228.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Elimu na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe wakati na mkutano wa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Mlowe alisema kuwa mafanikio hayo yanatokana na huduma na mafao bora yenye wigo mpana na kugusa moja kwa moja maisha ya mtanzania ambapo wamepanga kufikia wanachama 180,000 kufikia mwezi June 2016.
Mlowe aliongeza kuwa miongoni mwa sekta zilizoingiza wanachama wapya kwa mwaka 2014/2015  ni Walimu ambapo imetoa wanachama 39,537, Zimamoto na uokoaji wanachama 851, Polisi na Uhamiaji wanachama 415 na Magereza wanachama 205.
Aidha Bw. Mlowe aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 mfuko huo ulikusanya kiasi cha shilingi bilioni 210.069 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.9, ambapo wamepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 286 billioni kufikia mwezi Juni 2016.
Pia Mfuko huo umesajili waajiri wapya 88 katika kipindi cha mwaka 2014/2015 na unategemea kuendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na mfuko huo kuendelea kuboresha huduma zake.

Mamia wajitokeza Usaili wa Maisha Plus Dar es salaam

June 20, 2016

677A0614
Akitaja vigezo vya kushiriki Maisha Plus, Kaka Bonda, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa Maisha Plus alisema, “Tunachukua washiriki wenye umri wa miaka 18 hadi 26, walio na elimu na ambao hawajasoma kabisa, wawe raia kutoka nchi za Afrika Mashariki”
677A0389
677A0646
677A0422
Maisha Plus kwa mwaka huu wa 2016 inatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi tano ambazo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ambapo mshindi atafadhiliwa wazo la biashara lenye thamani ya fedha ya kitanzania Milioni 30. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni ‘Vijana Ndio Ngazi’.
677A0857
677A0262
677A0763
Usaili unaendelea katika mikoa mingine na nchi nyingine nje ya Tanzania. Vijana wametakiwa kusikiliza matangazo ya ratiba kupitia redio mbalimbali katika nchi shiriki, runinga ya Azam Two, mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na tovuti maalum ya mashindano hayo ya www.maishaplus.tv
677A0946

BENKI YA CRDB YAKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA KAMPENI YA “Shinda na TemboCard”

June 20, 2016

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafala ya kukabidhi zawadi kwa kwa washindi wa Kampeni ya “Shinda na TemboCard” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake wakati wa hafala ya kukabidhi zawadi kwa kwa washindi wa Kampeni ya “Shinda na TemboCard” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Kampeni ya “Shinda na TemboCard” akiwa katikapicha ya pamoja na mshindi aliyejishindia simu aina ya iphone 6, Barbara Hassan (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia).
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto), akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege ya kwenda Dubai mshindi wa kwanza wa Kampeni ya “Shinda na TemboCard” kwa upande wa wateja, Ismail Jimroger wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB  wakiwa katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wakurugenzi na Mameneja wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

June 20, 2016

ua1 
Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.
ua2 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero.
ua3 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero  na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.
……………………………………………………………………………………………………………
Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino
Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
“Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino,” alisema Ero.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.
“Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino,” alisema Nyanduga..
Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.
KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI HOLILI

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI HOLILI

June 20, 2016

ban1 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akikagua mzigo wa John Evarist ambaye ni  mfanyabiashara aliyekua akipita kutoka nchini Kenya  kupitia mpaka uliopo katika  kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban2Mfanyabiashara John Evarist aliyekua akipita kutoka nchini Kenya  kupitia mpaka uliopo katika  kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro, akijibu maswali aliyoulizwa na Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea(wa kwanza kushoto).Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyepo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban3 
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea ( aliyenyoosha mkono), akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), mwisho wa mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kukagua njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.Wa pili kushoto ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, RPC Wilbrod Mutafungwa. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban4 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipanda Mlima   kwenda kukagua jiwe linalotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya katika Mpaka uliopo eneo la Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo  mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban5 
Ujumbe ulioongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(), ukishuka kutoka mlimani   baada ya ukaguzi wa mpaka uliopo Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo  mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA AKABIDHI MADAWATI KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI.

June 20, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga, akizungumza wakati wa kukabidhi madawati katika Manispaa hiyo.
Na BMG
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imekabidhi madawati 2,600 kwa shule zote 74 za Msingi za umma zilizopo kwenye manispaa hiyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli la kutaka kila wilaya kumaliza tatizo la madawati ifikapo Juni 30 mwaka huu.

Madawati hayo ambayo yametengenezwa kwenye karakana ya shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru, ni sehemu ya mpango wa kutengeneza madawati 9,080 na hivyo kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika manispaa hiyo.

Akikabidhi madawati hayo hii leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga, amesema madawati hayo yametengenezwa kutokana na fedha zitokanazo na makusanyo ya ndani pamoja na michango ya wadau wengine ambapo katika mgawo wa awali, kata zote 19 za manispaa hiyo zimepewa madawati 139 kila moja.

Wanga amesema kila dawati moja lenye uwezo wa kukaliwa na wanafunzi watatu, limegharimu shilingi 98,000 ambapo manispaa ilinunua vifaa ikiwemo mbao, misumari na vyuma na kulipa gharama za ufundi zinazofikia shilingi 15,000 kwa kila dawati na kwamba madawati mengine yaliyobakia kukidhi mahitaji yanaendelea kutengenezwa kwenye karakana hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambya, amepiga marufuku matumizi ya madawati hayo kwenye shughuli nyingine ikiwemo mikutano ya kisiasa huku akiwataka wazazi,walezi na jamii nzima kwa ujumla kutambua umuhimu wa kuchangia juhudi za kuboresha elimu.

Renatus Mulunga ambae ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela amesema halmashauri hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba inatatua tatizo la upungufu wa madawati kwa shule za msingi katika manispaa hiyo, hatua ambayo itasaidia kuboresha ari ya wanafunzi kujisomea.
Utengenezaji wa Madawati ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ukiendelea katika karakana ya Shule ya Sekondari ya wavulana Bwiru.
Picha Zaidi Bonyeza Hapa