MAKAMU WA RAIS AHIMIZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KUTENDA ILIYOAHIDI

November 17, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Nsola ambapo alikagua miradi mbali mbali ya ufugaji samaki ikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua shamba la kilimo cha kisasa Greenhouse (Bandakitalu) la Ngongoseke lililopo kijiji cha Nsola  wilayani Magu mkoa wa Mwanza
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini mwanafunzi Evodia Anatori wa shule ya sekondari ya kata ya Idetemya akionyesha kwa vitendo namna ya kuchanganya kemikali kwenye maabara ya shule hiyo iliyopo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi wa Idetemya mara baada ya kufungua bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsalimia kwenye maeneo ya  Nyakato mkoani Mwanza.
                                                      ………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi mkoa wa Mwanza kuimarisha maradufu doria katika Ziwa Victoria kama hatua ya kukabiliana na tatizo la uvuvi haramu ambao umepunguza kwa kiasi kikubwa samaki kwenye ziwa hilo
Rais ametoa maagiza hayo katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika wilaya za Kwimba, Misungwi na Magu mkoani  Mwanza katika ziara yake ya kikazi ambayo imeigia siku ya PILI mkoani humo.
Makamu wa Rais amewataka viongozi hao kuwachukulia hatua kali za kisheria watu watakaokamatwa wakivua kwa zana haramu ua kwa sumu ili kukomesha tatizo hilo katika Ziwa Victoria.
Ameonya kuwa wavuvi haramu wakiachwa waendelee kufanya uvuvi huo wataharibu ziwa lote hasa mazalia ya samaki hali ambayo itasababisha viwanda wa kusindika samaki mkoani humo kufungwa na mamia ya watu kukosa ajira kutokana na shughuli za
uvuvi.

Akizindua na kuweka mawe ya msingi kweye mabweni  ya wanafunzi wasichana katika shule za sekondari ya Idetemya wilayani Misungwi na shule ya Sekondari ya Archbishop Anthony Mayala wilayani Kwimba, Makamu wa Rais amepongeza juhudi za viongozi wa mkoa wa Mwanza na wadau wa maendeleo kwa kujenga mabweni hayo ambayo yatasaidia wasichana kuondokana na mazingira hatarishi ikiwemo kupata
mimba.

Makamu wa Rais amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuweka mikakati madhubuti ya kujenga mabweni ya wasichana kama hatua ya kukabiliana na tatizo la wanafunzi kupata mimba na kuacha shule.
Akisalimia mamia ya wananchi wa maeneo ya Igoma na Nyakato jijini Mwanza waliojitokeza barabarani ili kumsalimia, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi hao kuwa ahadi zote zilizotolewa na viongozi hao wakati wa kampeni zitatekelezwa ikiwemo tatizo la ajira kwa vijana.

Amewahimiza wananchi waunge mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kubaini walarushwa na watendaji wanaohujumu miradi ya maendeleo ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano inataka kuona rasilimali zilizopo nchini zinatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote na sio kwa idadi ya watu wachache.

Akiwa mkoani Mwanza Makamu wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara na kuwaeleza mipango ya mikakati ya serikali ya awamu ya Tano ya kuwaletea wananchi hao maendeleo.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amechangia mabati 100 na mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya wasichana ya Archbishop Anthony Mayala wilayani Kwimba mkoani Mwanza.

ANNE MAKINDA AZITAKA HOSPITALI ZA SERIKALI ZIBORESHE HUDUMA ILI ZIPATE WATEJA WENGI WA BIMA YA AFYA.

November 17, 2016



Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda katikati kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mtahew John Mtigumwe na kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo, wa kwanza kulia ni meneja Mfuko wa Bima ya Tifa Mkoa wa Singida Bwana Adamu Salumu.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda akikagua hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida, mwenye tai nyekundu ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda akikagua hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida,kulia kwake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dokta Ramadhani Kabala na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe.


Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda amezishauri hospitali, vituo vya afya na zahanati za serikali kuboresha huduma za afya ili wananchi waliojiunga katika mifuko ya afya ya jamii (CHF) na mfuko wa bima ya afya washawishike kutumia huduma katika hospitali zao.

Makinda ametoa rai hiyo alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kujionea huduma za Bima ya afya zinavyotolewa na changamoto zilizopo ili kwa ushirikiano wa mfuko wa bima ya afya na wadau wake waweze kuzitatua.

Amesema hospitali na vituo binafsi au vya mashirika mbalimbali wamekuwa wanufaikaji wakubwa wa kupata wateja wengi wa bima ya afya na mifuko ya afya ya jamii kutokana na kusifiwa kuwa wanatoa huduma bora tofauti na hospitali za serikali ambazo hupata wateja wachache na hivyo kupata faida kidogo.

Makinda amesema hamasa anayoitoa ya kuboresha huduma kwa vituo vya serikali haimaanishi mfuko wa taifa wa bima ya afya hauthamini vituo na hospitali binafsi bali inataka hospitali za serikali kuboresha huduma na kuingia katika ushindani.

Ameongeza kuwa changamoto ya ukosefu wa dawa na vifaa tiba inawakatisha tamaa watumiaji wa bima ya afya pamoja na watu wengine kujiunga hata hivyo mfuko wa bima ya afya na hospitali za serikali zimejipanga kuziondoa changamoto hizo.

Aidha Makinda ameupongeza Mkoa wa Singida kwa kufanya vizuri katika mfuko wa afya jamii na bima ya afya huku akisisitiza kuendelea kuboresha ili Mkoa wa Singida uwe mfano kwa mikoa mingine ya Tanzania.

Akitembelea majengo mapya ya hospitali rufaa iliyopo eneo la Mandewa Makinda amevutiwa sana na majengo hayo huku akiutaka uongozi wa Mkoa kwa kushirikia na wadau wengine hasa mfuko wa bima ya afya kutafuta pesa za ukamilishaji wa majengo muhimu ili huduma zianze kutolewa katika hospitali hiyo kwakuwa itakuwa msaada hata kwa kanda nzima ya kati.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew J Mtigumwe  amemshukuru Anne Makinda kwa kuutembelea mkoa wa Singida ili kujionea  huduma za Bima ya afya zinavyotolewa.

Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amemuahidi Makinda kuwa Mkoa utaendeleza ushirikiano mzuri na Mfuko huo na kuomba waendelee kutoa ushirikiano wa vifaa tiba na ukarabati wa miundombinu ya hospitali na vituo vya afya vya serikali ili kuboresha huduma za afya Mkoani Singida.

Ameongeza kuwa Mkoa utaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii na bima ya afya ili wapate huduma bora hata wakati wakiwa na upungufu wa fedha kwani bima huokoa maisha. MAELEZO YA PICHA

WAZIRI MAHIGA AKUTANA NA MABALOZI

November 17, 2016


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Yemen nchini Mhe.Fikri Taleb Abubaker Al Sakaf mara baada ya kuwasili Wizarani kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho 
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga akionesha Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Yemeni nchi Tanzania Mhe.Fikri Taleb Abubaker Al Sakaf mara baada ya kukabidhiwa 
aziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Mohammed Bin Mansoor Al Malyk alipowasili Wizarani Jijini Dar es Salaam kukabidhi Hati za Utambulisho 
Balozi Mteule wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Mohammed Bin Mansoor Al Malyk akikabidhi Hati za Utambulisho kwa Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga Wizarani Jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Hawa Ndolowe alipomtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam .

ASASI ZA KIDINI PAMOJA NA ASASI ZA KIRAIA ZATAKIWA KUWEKEZA KATIKA HUDUMA ZA KIJAMII.

November 17, 2016
   Na,Abel Daud,Globu ya Jamii- Kgoma.

Katika kuepuka vifo vya mama wajawazito na watoto,wazazi wameshauriwa kutotumia dawa za asili sambamba na kuwahi kufika katika vituo vya afya ili kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto.

Rai hiyo imetolewa na Daktari mfawidhi wa kituo cha afya Nguruka Dkt.Stanford Chamgeni ,wakati akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi,Mwanamvua Mlindoko katika kukabidhiwa jengo la maternity ward lililopo katika kijiji cha Mganza kata ya Mganza Wilayani Uvinza lenye dhamani ya tsh.30 million,lililotolewa na Kanisa la POOL OF SLOAM.

Naye Kuhani ISRAEL EXTRA POWER,ambaye alimwakilisha kiongozi mkuu wa kanisa hilo hapa nchini,alisema kuwa kupitia hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kukamilisha huduma za kijamii.

Akinukuu maneno ya kitabu cha Isaya 58 aya ya 7 na Yakobo 2-14,Kuhani ISRAEL POWER alieleza kuwa,sehemu ya kusaidia maisha ya wenye uhitaji lazima kuwepo na umoja kwa viongozi na jamii kwa ujumla,sambamba na kuongeza kuwa,kwa kuwa MUNGU hana upendeleo,kama kanisa ni lazima kuendelea kuona uchungu wa kuhudumia jamii.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Mganza Bw,BONIFACE BAHINGAI,ametoa shukurani kwa kanisa hilo ambapo alisema kuwa kuwepo sasa kwa ward hiyo,itasaidia kutatua changamoto zilizokuwepo kijijni humo,sambamba na kutoa wito kwa taasisi zingine za kidini kuona umuhimu kusaidia huduma za kijamii.

Nao baadhi ya wananchi kijijini humo akiwemo DAFROZA GWIMO,alitanabaisha kuwa uwepo sasa wa ward hiyo itawarahisishia kuondoa changamoto iliyokuwepo ya kwenda kujifungulia mbali,na kupelekea kuhatarisha maisha ya mama mjamzito na mtoto.
Waumini wa kanisa hilo pamoja na wanakijiji wakiwa wamelizunguka jengo hilo
 Kuhani Israel Extra Power akiongea na wana kijiji pamoja na waumini waliohudhuria sherehe hiyo
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya pamoja na Kuhani Israel Power wakielekea kwenye jengo tyr kwa uzinduzi
 Kuhani Israel Power akimkabidhi ufunguo wa jengo hilo Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya Dr.Chamgeni
Kuhani Israel  pomoja na Dr.Chamgeni wakifunua kitambaa kilichofunika jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa jengo hilo
HII NI KWA AJILI YA VIJANA WOTE JAPO WAZAZI NA WALEZI WANARUHUSIWA KUSOMA.

HII NI KWA AJILI YA VIJANA WOTE JAPO WAZAZI NA WALEZI WANARUHUSIWA KUSOMA.

November 17, 2016

Ujana ni ngazi ambayo inahitaji umakini mkubwa katika ngazi zote za maisha mwanadamu (maoni binafsi).

Ni kipindi ambacho asilimia kubwa ya vijana hufanya mambo ili waonekane na jamii inayowazunguka.

Ni wakati ambao wengi hupoteza muda na mwelekeo wa maisha yao kwa sababu, asilimia kubwa hufanya mambo kwa kufuata mkumbo. 

Wengi hupotea maana ni muda ambao huanza kuwa na maamuzi binafsi. Hapa wazazi na walezi wakijitenga kando, kijana huangamia maana wengi huchagua maovu kuliko mema. 

Kama hujaanza mahusiano, utaanza kwa sababu yule ameanza. Hata kama huna kazi nzuri, utaanza kubagua kazi kwa sababu fulani ana kazi nzuri. Ulevi na uzinzi huanzia katika ngazi ya ujana. Inasikitisha.

Hayo ni machache miongoni mwa mambo mengi ambayo hukatisha mafanikio ya vijama (Me & Ke).

Mimi nasema utumie ujana wako vizuri leo ili kesho usijutie. Najua peke yako huwezi hivyo kaa chini, tafakari, kisha chagua dini ya kweli inayokufaa, kisha anza maisha yako ya ujana ukiwa na mahusiano mema na Mungu.

HALMASHAURI ZA ILEMELA NA JIJI LA MWANZA ZAKUMBUSHWA KUHUSU USAFI.

November 17, 2016

Na George Binagi-GB Pazzo
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogondogo kwenye Masoko na Minada katika Halmashauri za Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza, wamelalamikia uchafu kukithiri katika maeneo yao ya kufanyia biashara hali ambayo inawasababishia kero bubwa.

Wakizungumza na Lake Fm, wafanyabiashara hao wamesema hali hiyo inawapa kero kubwa ikiwemo harumbu mabya, licha ya kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kipindupindu.

Katika masoko na minada mbalimbali ikiwemo Kitangiri, mrundikano wa uchafu katika maeneo ya kukusanyia uchafu imeelezwa kuwa kero kubwa hadi kwa makazi jirani huku changamoto ya ukosefu wa vyoo ikiibua malalamiko zaidi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara ndogondogo kwenye Masoko na Minada mkoani Mwanza, Justine Sagara, alisema changamoto hiyo imesababishwa na halmashauri za Ilemela na Jiji la Mwanza kushindwa kuondoa uchafu kwa wakati hatua ambayo imepelekea baadhi ya machinga kugoma kulipa ushuru kwa ajili ya usafi.

"Tuliomba watujengee vyoo lakini ombi letu bado halijafanyiwa kazi ambapo hadi sasa ni Soko la Kiloleli tu ndo lenye choo, lakini masoko na minada mingine hakuna vyoo". Anabainisha Sagara.

Awamu pili shindano la SBL kutafuta DJ mbobezi kuchanganya muziki yaanza

November 17, 2016

Mkuu wa Masoko na  Vinywaji vikali wa SBL , Stanley Samtu (katikati)  akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) katika mkutano wa waandishi wa habari ambapo alitangaza kuanza kwa msimu wa pili wa  shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.Kulia kwake ni Meneja chapa wa vinwaji vikali Shomari Shija na kushoto ni DJ PQ ambaye ndiye Jaji Mkuu katika shindano hilo.
Meneja chapa wa vinwaji vikali Shomari Shija akifafanua jambo wkwa waaandishii wa habari katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za SBl Temeke jijini Dar es salaam,katikati ni jaji mkuu wa shindano hilo Dj PQ na kushoto mwishoni ni Mkuu wa Masoko na  Vinywaji vikali wa SBL , Stanley Samtu .

Meneja Biashara wa SBL Esther Raphael akimkabidhi mmoja wa washindi waliofanikiwa kuingia msimu wa pili wa shindano la msimu wa pili wa  shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.

MaDJ waliofanikiwa kuingia msimu wa pili wa shindano la SBL la  kutafuta DJ mbobezi kuchanganya muziki wakiwa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.


                                            ·        Kuibua vipaji vya ndani

Dar es Salaam,  Novemba 17, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza  kuanza kwa awamu ya pili ya miezi mitatu ya shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.
Akizungumza wakati wa kutambulisha awamu ya pili  ya shindano hilo jijini Dar es Salaam  Mkuu wa Masoko na  Vinywaji vikali wa SBL , Stanley Samtu alisema kuwa shindano hilo  linadhaminiwa na kinywaji cha Smirnof Black Ice linamaanisha pia kuwapa wapenzi wa muziki kote nchini fursa ya kufurahia vibao vipya vya muziki vitakavyochezeshwa na ma+DJ  walio na vipaji katika sekta hiyo.
 “Leo tunatangaza ma+DJ 18 kati ya 40 kutoka mikoa mine  ambao wamefanikiwa  kuingia katika awamu ya  pili ambapo Dar es Salaam  wapo 10, Dodoma wawili, Arusha wawili, Morogoro wawili na Mwanza wawili,” alisema.
Kwa mujibu wa Samtu ni kwamba Smirnof Black Ice  ni chapa ya kinywaji inayoongoza  katika kipengele cha  kinywaji maarufu  miongoni mwa watumiaji wa tabaka la kati, katika maeneo yaote ya mijini na vijijini.
Tunaamini  kwamba kupitia shindano kupitia shindano hili SBL itatoa vipindi vya kufurahisha miongoni mwa wapenzi wa muziki watakaotembelea  yatakakofanyika mashindano na wakati huo huo kuwapatia fursa ya kipekee  ya kuibua, kukuza na kuangalia vipaji vilivyopo katika ulimwengu wa muziki na ma-DJ.”
 Alisema kwamba kundi  la  vipaji vinavyosakwa katika mashindano hayo ni la vijana walio na umri kati ya  miaka 18 hadi 30, ambao kwa mujibu wa Samtu  ni kwamba shindano hilo linawafaa wanafunzi  walio katika ngazi ya eilimu ya juu  pamoja na wanataaluma ambao ni vijana. vijina.
“Zitatolewa zawadi nzuri kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema na kudokeza  kuwa zawadi hizo ni pamoja na seti ya  vifaa vya kuchanganya muziki, kompyuta mpakato, na mashine ya kuchanganya muziki kwa washindi watatu watakafika fainali.
  
“Tunatoa wito kwa  kwa ma-DJ wote , wasimamizi wa mabaa na wapenzi wa muziki katika miji hii  kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia ili waweze kuifurahia sekta ya muziki ya Tanzania,” alisema Samtu.

SERIKALI YAOMBWA BAJETI KUSAIDIA PASADA NA WENGINE

November 17, 2016
SERIKALI imeombwa kutengeneza bajeti ya kusaidia taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na kusaidia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ikiwa ndio njia ya kuhakikisha huduma kwa waathirika hao zinaendelea kuimarika.

Imeelezwa kuwa ingawa serikali ndiyo inayotoa dawa za kufubaza makali ya UKIMWI ARVs, haitengenezi bajeti kwa ajili ya wafanyakazi wanaohudumia waathirika kisaikolojia na kitiba.

Hoja hiyo imetolewa na Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA) Jovin Riziki wakati akijibu maswali katika mkutano na ujumbe wa nchi za jumuiya ya NORDIC waliotembelea makao makuu ya PASADA yaliyopo Chang’ombe, Temeke Dare s salaam kuangalia miradi mbalimbali ya kijamii inayofadhiliwa na UNICEF.

Nchi za Jumuiya ya Nordic ni wafadhili wakubwa wa miradi inayoendeshwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA) Jovin Riziki (kushoto) akitoa maelezo kwa sehemu ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) katika chumba cha kuhifadhia kumbukumbu za wagonjwa ulipotembelea kwenye kituo hicho cha PASADA jijini Dar es Salaam. Kulia ni kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist.(Habari picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Akijibu swali nini ambacho atataka kumweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikutana naye, Riziki alisema kwamba angelipenda kuona serikali inawajibika kusaidia huduma katika taasisi mbalimbali zinazoigusa jamii zinaendelea kutolewa.

Alisema asasi zinazosaidia waathirika wa UKIMWI kama hiyo ya PASADA hutegemea asilimia 100 misaada ya nchi na wafadhili wa kigeni ambapo miradi ikimalizika mara nyingi waliokuwa wanahudumiwa hukosa mahali pa kupata misaada iliyokuwa inawawezesha kuendelea kuishi kiutu kwa kuwa na siha njema na kufanya shughuli za kiuchumi.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki (kushoto) na ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa mtoa huduma katika kitengo cha dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI ARV's ulipotembelea kwenye kituo hicho cha PASADA jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna changamoto kubwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya elfu 21 wengine wakiwa kufani majumbani bila kuwa na mtaji wa kutosha hasa malipo kwa watoa huduma ambao ni wataalamu.

“Ipo haja ya serikali kuchangia kazi hii ya kibinadamu hasa fedha kwa ajili ya kulipa wataalamu na kuendeleza miradi ambayo inasaidia jamii moja kwa moja” alisema huku akiongeza kwamba kwa sasa mathalani wanaendelea kufanya mazungumzo na watu mbalimbali kuendeleza mradi uliokuwa ukisaidiwa na USAID.

Alisema Septemba mwaka huu USAID wamemaliza mchango wao wa mradi muhimu ambao ndani yake ulikuwa unawasaidia waathirika katika elimu, tiba na pia kiuchumi.
Ujumbe huo ukiwa kwenye mazungumzo na vijana wanaoishi na VVU ambao wamepata mafunzo ya ujasiriamali yaliyowawezesha kujiajiri kwa kufanya biashara ndogo ndogo zinazowapatia kipato cha kusaidia familia zao na mahitaji yao madogo madogo.

Alisema mara nyingi kunapoendeshwa mradi ambao ndani yake watu wanawezeshwa kiuchumi hujitokeza kwa wingi na hivyo kama serikali ikitenga bajeti maana yake watu hao watafika kupata elimu na pia kufufua matumaini ya maisha kwa kuwezeshwa kiuchumi.

PASADA iliyoanza Agosti 1992 wakati kundi dogo la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kujikusanya ili kupata msaada wa pamoja sasa hivi ina wateja 36,000, ikitoa huduma za upimaji kwa watu 10,000 kila mwezi.

Aidha PASADA ambayo imekuwa ikikua ikitegemea fedha za wahisani imekuwa ikiwafikia watu walio majumbani ambao hawawezi na waliokufani kuwapatia huduma za kibinadamu.
Ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakipata maelezo nje ya eneo la vipimo katika kituo cha PASADA.

Ingawa PASADA ipo chini ya kanisa katoliki huduma zake hupatikana kwa kila mwananchi bila ubaguzi na huendesha pia huduma za elimu kuhusu afya ya uzazi, ujana na maradhi ya UKIMWI.

Sehemu kubwa ya elimu ni kuondoa unyanyapaa na kuhimiza wananchi kupima afya zao. Aidha elimu imelenga watu kubadilika tabia.

Ikiwa na watu wazima 3000 wanaotumia dawa na watoto 600, PASADA imesema kwamba bado inakabiliwa na changamoto kubwa hasa pale ambapo wahisani wanapojitoa kusaidia miradi iliyopo ya elimu na kiuchumi.

Aidha PASADA imekuwa ikipambana kwa kusaidiana na wadau wengine kuhakikisha kwamba haki za msingi za wenye virusi vya UKIMWI hazikiukwi.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki akiongoza ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) kutembelea vitengo mbalimbali vinavyotoa huduma kituo cha PASADA jijini Dar es Salaam.

Ikiwa imefanikiwa kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa asilimia 97, huku ikiwa imefikia asilimia 4 ya waathirika nchini na kwa mikoa ya Dar es salaam na Pwani asilimia 30, PASADA ikiwa na wafanyakazi 140 inahitaji sana uhakika wa bajeti na serikali ndiyo inayoweza kutoa kwa kuwa kazi inayofanywa na serikali kupitia vituo vya umma ndiyo inafanywa na PASADA.

Ujumbe huo wa NORDIC ambao ulikujwa na wenyeji wao Mashirika ya Umoja wa Mataifa ulielezea kuridhishwa kwake na kazi inayofanywa na PASADA na kusema ipo haja kwa wadau kushirikiana kurejesha heshima ya binadamu na kufanya serikali kuwajibika kwa watu wake.

Naye Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye ndiye mwenyeji wa ujumbe huo unaopita katika miradi mbalimbali serikalini na hata katika taasisi binafsi, Alvaro Rodriguez, alisema kuna changamoto nyingi katika kusaidia wananchi katika maradhi yanawasibu kwa sababu ni kazi ya kibinadamu zaidi na wala si ya kimaendeleo.
Ziara ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiendelea kutembelea vitengo mbalimbali vinavyotoa huduma za afya kwa watu wanaoishi na VVU kituo cha PASADA jijini Dar es Salaam.

Alisema hata hivyo ili kuwa na haki sawa mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakisaidia kupatikana kwa haki za maisha kwa kusaidia mambo kadhaa ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na wagonjwa lakini yakiwa na mchango mkubwa katika afya na shughuli za uzalishaji mali.

Alisema amefurahishwa na ziara ya ujumbe huo wa Nordic ambao ni wafadhili wakubwa wa miradi mbalimbali yenye lengo la kuwezesha uwajibikaji na utawala bora nchini ikiwemo misaada ya kibinadamu.

Alisema ni kazi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kushawishi mabadiliko ya kitamaduni ili kujiweka sawa katika shughuli za maendeleo.
Ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ukiwa katika eneo maalum lililotengwa na kituo cha PASADA kwa ajili ya watoto kufanya michezo mbalimbali walipofanya ziara kituoni hapo. 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akibadilishana mawazo na kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist wakati wa ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali katika kituo kinachohudumia watu wanaoishi na VVU, PASADA jijini Dar es Salaam.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki akitoa historia fupi ya kituo hicho pamoja na changamoto zinazowakabili katika kuhudumia watu wanaoishi na VVU nchini kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea kituo hicho.
Sehemu ya ujumbe huo ukimsikiliza Bwana Jovin Riziki.
Kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist akifafanua jambo wakati wa kutoa mrejesho baada ya ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali katika kituo cha PASADA jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa PASADA baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho na kujionea changamoto zinazowakabili.

KAMPUNI YA HANSPAUL GROUP OF COMPANIES ARUSHA YAIDI KUSHIRIKIANA BEGA KWA BEGA KUSAIDIA MAENDELEO ZAIDI

November 17, 2016
 mmiliki wa kampuni ya hanspaul group of companies Arusha  ndugu Hans Paul  akiwa anasoma maelezo mafupi ya mradi walioujenga kwa ajili ya wananchi wa kata ya Engutoto pamoja na kata ya Moshono

 ndugu Hans Paul katikati akimuonyesha mkuu wa mkoa daraja la zamani ambalo wananchi hao walikuwa wanalitumia
 pia viongozi wa vyama mbalimbali walijitokeza katika uzinduzi huo
 sehemu ya wafanyakazi wa hanspaul waliouthuria uzinduzi huo
 baadhi ya mameneja wa hans paul wakiwa wanafatilia uizinduzi
 Mkuu wa Mkoa na mkurugenzi wa hanspaul group of companies Arusha  wakikata utepe kwa ajili ya uhashirikia kuwa daraja limezinduliwa
 mkuu wa mkoa wa Arusha akipita juu ya daraja mara baada ya kulizindua rasmi
 huu ndio muonekano wa daraja lililo jengwa na kampuni ya Dharam Singh Hanspaul Group 
 mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) ambaye aliaidi kutoa mabati ya ujenzi wa zahanati 1000 pamoja na  na Bw. Jagjit Aggarwal ambaye aliahidi kutoa mifuko 500 ya cimenti kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kisasa ya kata ya Engutoto iliopo ndani ya jiji la Arusha

habari picha na  Woinde Shizza ,Arusha

  Jumla ya zaidi ya shilingi milioni 67.7 zimetolewa na kampuni ya Dharam Singh Hanspaul   inaojishulisha na utengenezaji wa bodi za magari ya utalii jijini hapa  kwa ajili ya ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Ongutoto  pamoja na kata ya Moshono iliopo ndani ya jiji  la Arusha .

Akiongea wakati wa kukabidhi daraja hilo mara baada ya kukamilika kwa ujenzi  mmiliki wa kampuni hiyo Hans Paul alisema kuwa kampuni yake ipo tayari kushirikiana na kuunga mkono serikali ya awamu ya tano pamoja na serikali ya mkoa wa Arusha katika swala zima la kuleta maendeleo na kusaidia wananchi  wa hali ya chini hivyo ndio maana wameamua kuunga mkono serikali kwa kusaidia shughuli mbalimbali za kijiamii ikiwa ni pamoja na kujenga daraja

" sisi kama kampuni ya Dharam singh Hanspaul tunahaidi kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kila jambo ili kuweza kuwasaidia wananchi wanyonge pamoja na wale wa hali ya chini na tupo tayari kushirikiana na viongozi wa serikali hii bega kwa bega"alisema Hans Paul

Alisema kuwa daraja hilo  la Mto kijenge lilianza  kujengwa mwezi Juni na kukamilika Agost 2016 lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani tatu(3), urefu kwenda juu ni mita 2.2, uimara wa pekee na linaweza kudumu kwa miaka 50; Ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 67 .

Aliongeza kuwa daraja hilo ni ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikua wakipata adha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika na kivuko kilichokuwepo awali kiliashiria hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee, waendesha pikipiki, waenda kwa miguu wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo wa kupita hapo. 


Paul aliongeza kuwa mbali na kujenga daraja hilo pia kampuni yake imejenga madarasa matatu yaliko katika kata ya Engutoto yaliyogarimu kiasi cha shilingi milioni 50 ikiwa ni njia moja wapo ya  kusaidia watoto wa kata hiyo kukaa darasani na kusoma kwa  raha na amaani zaidi .

“pia mbali na hivyo kampuni hii imeajiri wananchi vijana ambao ni wazawa zaidi ya 500 ambao vijana hawa wanafanya kazi katika kampuni hizi zangu tatu tofauti  hii ikiwa ni njia moja wapo ya kuweza kusaidia serikali kutatua tatizo la ajira ambalo linaikamili nchini yetu kwa kipindi hichi na sitaishia apa kwani pia ninampango wa kuendelea kutoa ajira kwa vijana wengine “alisema mmiliki wa kampuni hii ya Dharam Singh Hanspaul   

Adha kutokana na kuwa natatizo la kutokuwepo na zahanati katika kata hiyo pia kampuni hiyo iliweza kuhaidi ofisi ya mkuu wa mkoa kuwa itatoa bati 1000 kwa ajili ya zahanati ambayo itajengwa katika kijiji hicho ili wakina mama na watoto waweze kutibiwa kwa uharaka na uhakika zaidi .