MWANAHABARI MTOTO GETRUDE CLEMENT ASEMA HAKUTENDEWA HAKI BAADA YA KUTOKA MAREKANI.

May 21, 2016
Getrude Clement (Kushoto) ni Mwanahabari Mtoto kutoka Jijini Mwanza ambae pia ni mwanamazingira anaewakilisha kundi la Watoto na Vijana katika Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UN kutoka Tanzania.

MWANACHUO BENADETHA MSIGWA ANAOMBA MSAADA ILI AKATIBIWE MACHO

May 21, 2016
Jaman wapendwa kuna mwanafunzi mwenzetu amepata upofu akiwa chuo na sisi kama wanafunzi tumeamua kumchangia pesa kama inawezekana akatibiwe ila inahitaji kama milion 30 kwa hiyo kwa yeyote atakaeguswa anaweza tuma chochote kupitia namba hizo hapo kwenye hicho kipeperushi.
Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA

WACHAGA WAKUMBUSHWA KUISAPOTI TIMU YAO YA KILIMANJARO INAYOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA WA MIKOA.

May 21, 2016
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akizungumza wakati wa kuwaaga mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro, timu ya Kitayosce wanaojiandaa kuelekea mkoani Singida kushiriki ligi ya Mabingwa wa mikoa katika kituo hicho.
Baadhi ya wachezaji timu ya Kitayosce wakiwa katika uwanja wa Meimoria ambako waliagwa na uongozi wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)
Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Mohamed Musa akizungumza wakati wa kuiga timu ya Kitaysce.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Kitayosce.
Mjumbe wa kamati ya kuisadia timu ya Kitayosce,Dalabu Maulid Dalabu akizungumza katika hafla hiyo fupi.
Mwenyekiti wa Chama cha soka Manispaa ya Moshi (MMFA) Japhet Mpande akitoa nasaha zake kwa wacheaji wa timu ya Kitayosce wakati wa kuiaga timu hiyo.
Kocha wa timu ya Kitayosce,Hamad Haule akielezea matarajio yao katika ligi ya mabingwa ambapo timu yake imepangwa kituo cha Singida.
Nahodha wa timu ya soka ya Kitaysce ,Chimko Vidic akieleza namna walivyojiandaa na ligi hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Godluck Mosha akimkabidhi Mweka hazina wa timu ya Kitaysce ,Festus nauli kwa ajili ya safari ya kuelekea Singida ,KRFA imetoa nauli ya kwenda Sindida na kurudi.
Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akikabidhi mpira kwa ajili ya timu ya Kitayosce.
Mwenyekiti Mosha akikabidhi kiasi cha Sh Laki moja kwa nahodha wa timu ya Kitayosce kwa ajili ya kunua viatu kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.
Wachezaji wa Kitayosce wakiagana na Viongozi wa KRFA katika uwanja wa Meimoria. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro,Timu ya Kitayosce inataraji kuondoka jumapili hii kuelekea Singida huku ikikabiliwa na ukata .

Kamati ya kuisadia timu hiyo imeendelea kuhamasisha wadau mbalimbali wa soka hasa wale ambao ni wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kuisadia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kuuwakilisha vyema mkoa wa Kilimanjaro.

Hata hivyo kamati inatoa pongezi kwa Kampuni inayosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA(KADCO) kwa msaada wa awali iliyotoa huku ikiwakumbusha wadau wengine waliofikishiwa barua za ombi la msaada kwa timu hiyo kuzifanyia kazi.

Kwa sasa kamati ya kuisadia timu hiyo inakusanya michango kupitia namba za simu 0715331274 na 0746331274.

MANDHARI ZA KUVUTIA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

May 21, 2016
Miti ya Mibuyu iliyochimbwa na Tembo ni moja vivutio katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Uoto wa asili katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ni kivuto kingine.
Mkundi ya Tembo ni sehemu pia ya vivutio vinavyo ibeba Hifadhi ya Taifa ya Tarangire,
Ndege wa aina mbalimbali pia wanaweka mvuto katika Hifadhi hiyo
Mnyama Ngiri ni miongoni mwa wanayama wanaoonekana kwa urahisi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Muonekano wa Mibuyu iliyochimbwa na Tembo.
Tumbili pia wamo.
Sehemu ya Chanzo cha Mto Tarangire.
Mnyama Kuro pia ni kivutio kimoja wapo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Kundi la Tembo likivuka mmoja wa mito iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Maandhari ya uoto wa asili unavyoonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

RC PAUL MAKONDA AFUNGUA MACHINJIO YA VINGUNGUTI JIJINI DAR ES SALAAM

May 21, 2016
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakati alipowasili kuzungumza na wafanyabiashara wa nyama katika Machinjio ya Vingunguti kabla ya kuifungua rasmi jana. Katikati ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto (wa pili kulia), akielekeza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Isaya Mngurumi.



 RC Makonda akiongoza ukaguzi huo.
 Taswira ya choo cha kisasa kilichojengwa kwenye machinjio hiyo.
 Wafanyabiashara katika machinjio hiyo wakimsikiliza Makonda (hayupo pichani)
 Mwonekano wa machinjio hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati.
 Wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo wa ufunguzi wa machinji hiyo.
 Makonda akisalimiana na wafanyabiashara baada ya kufungua machinjio hiyo.
Wafanyabiashara wakimkabidhi zawadi ya mbuzi RC Makonda, DC Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi katika hafla hiyo ya ufunguzi wa machinjio hiyo.