SUDANI YA KUSINI YAJIUNGA NA EAC

SUDANI YA KUSINI YAJIUNGA NA EAC

April 15, 2016

sam1
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa  wakimsubiri  Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016.
sam2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016.
sam3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016, Kushoto ni Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
sam5
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit akikagua gwaride la heshima  wakati Rais Kiir   alipowasili Ikulu leo.
sam6
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir akiwapungia mikono viongozi mbalimbali huku akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakati alipowasili Ikulu
sam7
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki CEAC) na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir wakibadilishana hati za makubaliano ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kusaini 
sam8
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir. Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo ya utiaji saini.

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NI SEHEMU SAHIHI KWA SUDANI YA KUSINI-KIIR

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NI SEHEMU SAHIHI KWA SUDANI YA KUSINI-KIIR

April 15, 2016

MA1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Magufuli akisaini makubaliano ya kuikaribisha Sudan kusini katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
MA2
Rais wa Jamhuri ya Sudan kusini Mhe. Salva Kiir  akisaini hati za makubaliano ya kuikaribisha rasmi Sudan kusini kuwa Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
MA3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Magufuli akizungumza wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Sudan kusini Mhe. Salva Kiir Salaam katika ziara yake ya kikazi lenye dhumuni la kujiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
MA4
Rais wa Jamhuri ya Sudan kusini Mhe. Salva kiir akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania jaji O5thman Chabde mara baada ya kumaliza kutia saini ya makubaliano ya nchi yake kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki.
MA5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Magufuli akiaga viongozi mbalimbali wa ikiatifa na kimataifa mara baada ya kumaliza kutia saini ya makubaliano ya nchi ya Sudan Kusini kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki.
………………………………………………………………………………………………..
Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Sudani ya Kusini Salva Kiiri  ametia saini makubaliano ya mkataba wa kujiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kutia saini mkataba huo, Rais Salva Kiiri amesema uamuzi wa nchi yake kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki si tu kuwa  kunaimarisha ujirani ulipo kati ya nchi hizo, lakini pia kunaimarisha ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki pamoja na watu wake ikiwa ni pamoja na kuendelea kukuza utamaduni wa Afrika.
“Naishukuru Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kukubali Sudani ya Kusini kuwa mwanachama wa Jumuiya, na sasa Sudani ya Kusini imepata sehemu sahihi kwa kujiunga na Jumuiya hii ambayo inalenga kuleta maendeleo kwa wananchi wake” amesema Rais Kiir.
Rais Kiir amesema “tunajua malengo makubwa ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake, na tunashuhudia kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mfani bora Afrika na duniani kwa ujumla”.
Ameongeza kuwa Sudani ya Kusini imeona fursa zilizopo katika Jumuiya hii ikiwa ni pamoja na soko la pamoja (Common markert). Tayari tumetengeneza mifumo itakayosaidia ushiriki wetu katika Jumuiya ikiwemo kuanzishwa kwa Wizara itakayoshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria mbalimbali zitakazowezesha kupatikana kwa Amani ya kudumu nchini humo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambaye pia ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amepongeza juhudi zilizofanywa na Sudani ya Kusini na hatimaye   kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ikiwa ni muda mfupi tu tangu nchi hiyo ipate uhuru wake mnamo  Julai 20, 2012.
Rais Magufuli amesema kuwa siku zote Sudani ya Kusini imekuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa uchumi wake, utamaduni wake, lugha pamoja na historia yake na inaunganishwa na nchi za Jumiya hii kwa barabara pamoja na mto Nile.
Aidha, Rais Magufuli “amesema malengo ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji, kutoa bure huduma na uhuru wa wananchi kwenda popote ndani ya Jumuiya. Hata hivyo, Jumuiya hii inakumbwa na machafuko ya mara kwa mara na kuwa kikwazo kwa maendeleo ya uchumi wake”.
Amesema Sudani ya Kusini imekubaliwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kuwa imetimiza makubalino yaliyowekwa na Jumuiya ikiwemo kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi, Dkt. Augustine Mahiga, amesema kuwa Sudani ya Kusini inakuwa mwanachama wa sita wa Jumuiya hiyo, na kuwa ushirikiano wa kiuchumi uliopo katika nchi hizi utakuwa mfano wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea.
Sudani ya Kusini iliomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki mnamo Novemba 10, 2012, ikiwa ni chini ya miezi minne tangu nchi hiyo ipate uhuru wake.
LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI

LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI

April 15, 2016
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.

Jumamosi, Young Africans watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Ndanda FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Nang’wanda Sijaona mjini Mtwara.

Coastal Union watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani jinini Tanga, huku Jumapili, Simba SC wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

SIMBA KUSHIRIKI KOMBE LA NILE BASIN

SIMBA KUSHIRIKI KOMBE LA NILE BASIN

April 15, 2016
Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayoanza kutumia vumbi Mei 22, 2016 nchini Sudan.
Mashindano ya vilabu Kombe la Nile Basin huandailiwa na CECAFA kwa kushirikisha vilabu vilivyoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi kwa nchi wanachama wa CECAFA.

Bingwa michuano ya kombe hilo atajinyakulia zawadi ya dola za kimarekani U$30,000, mshindi wa pili dola U$20,000, huku mshindi wa tatu akipata kitita cha dola za kimarekani U$10,000.

Nile Basin inashirikisha vilabu kutoka katika nchi wanachama wa CECAFA ambazo ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na Zanzibar.

Vitoria University kutoka Uganda ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika mwaka 2014.

 MALINZI AMPONGEZA RAVIA

MALINZI AMPONGEZA RAVIA

April 15, 2016
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Ravia Idarous Faina wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi ulifanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Gombani, Pemba.

Katika salamu zake, Malinzi amesema anampongeza Ravia kwa kuchaguliwa kwake, na hiyo imeonyesha imani kubwa kwa waliomchagua kuongoza ZFA katika kipindi kingine.

Malinzi amewapongeza vingozi wote wapya waliochaguliwa katika uchaguzi huo, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika shughuli zote za maendeleo ya mpira wa miguu.

Uchaguzi wa kupata viongozi wa ZFA ulifanyika jana Gombani kisiwani Pemba, ambapo Ravia aliibuka mshindi na kutetea nafasi yake, nafasi ya makamu wa rais Ugunja kienda kwa Mzee Zam Ali, na makamu wa Pemba ikichukuliwa na Ali Mohamed Ali.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSU MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSU MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI

April 15, 2016

kigamboni
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi.
Katika siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia.  Aidha, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli watavuka bure katika Daraja la Kigamboni.  Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa kutumia daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.
Magari yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za mwanzo ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia kufuatilia mwenendo wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu (Interchange) katika eneo la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba magari yanayotoka au kuingia katika daraja hayasababishi msongamano wa magari katika Barabara ya Nelson Mandela, Barabara ya Kilwa na maeneo mengine ya jiji.  Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.
Mambo muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia ni:-
  • Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu miundombinu ya daraja
  • Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
  • Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo hicho.
  • Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
  • Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la daraja.
Aidha, Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.
Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu  (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14 Aprili, 2016

RAIS WA SUDANI KUSINI, MHE. JENERALI SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI NCHINI

April 15, 2016

Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye kofia nyeusi) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (wa tatu kulia) akisalimiana na Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akipita katikati ya gwaride la Jeshi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

DC MKINGA AHIMIZA VIJANA KUJIKITA KWENYE KILIMO

April 15, 2016


VIJANA wilayani Mkinga Mkoani Tanga wametakiwa kujikita kwenye kilimo ili waweze kupata mafanikio makubwa badala ya kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufikiria kufanya vitendo viovu badala yake wahakikisha wanashiriki katika shughuli za uzalishaji ili waweze kuchangia ukuaji wa maendeleo yao.

 Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza aliyasema hayo juzi wakati ziara yake iliyolenga kuhamasisha shughuli za kilimo ambapo alisema endapo vijana hao watatumia muda wao kwenye kilimo itawasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi.

Alisema kuwa vijana hao wanapaswa kubadilika na kuona umuhimu wa kuwajibika hasa wakati huu ambao wananchi wilayani humo wanaweka msukumo kwenye kilimo kwa kushiriki shughuli hizo kwa umakini mkubwa.

  “Unajua vijana ndio nguvu kazi kubwa kwa Taifa letu hivyo niwaase badala ya kukaa vijiweni na kucheza pool table wakati wa kazi watumie nafasi hiyo kwenye kilimo ambacho ndio ute wa mgongo kwa maendeleo ya nchi “Alisema

Aidha ili kuhakikisha jambo hilo linapata mafanikio makubwa aliwaagiza maafisa ugani kuacha kukaa maofisini badala yake wawafuate wakulima kwa ajili ya kuwapa utaalamu wa kilimo ili waweze kulima kisasa.

Sambamba na hayo mkuu huyo wa wilaya aliwataka maafisa ugani kuona umuhimu wa kwenda vijijini na kuacha kukaa maofisini ili waweze kutoa mbinu kwa wakulima waweze kulima kilimo chenye tija kwao.

Hata hivyo pia aliwataka wananchi kubadilika na kulima kilimo cha kisasa ikiwemo kuandaa mashamba yao sambamba na kupanda kisasa ili kupata mavuno mengi hali itakayowasaidia kukuza vipato vyao.

MLATA: SERIKALI NJOENI NA MKAKATI WA UZAZI WA MPANGO

April 15, 2016

Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability'' Quick Reply