DC wa Wilaya ya Shinyanga akabidhi hati 92 za kimila

May 08, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Josephine Matiro akimkabidhi Anna Kadilana mkazi wa kijiji cha Nyida hati yake ya hakimiliki ya kimila. Anna alisema, "Nimeamua kukata hakimiliki kwa sababu ya kukwepa usumbufu hasa wa mipaka ambao ulikua unatokea mara kwa mara


Haji Kihwele kutoka shirika la Oxfam akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila zilizofanyika katika kijiji cha Nyida.


Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyida John Sahani Nungula akizungumza katika hafla hizo; Alitaja shughuli za wakazi wa kijiji chake kuwa wengi ni ukulima, ufugaji na biashara ndogondogo na kwamba mazao yanayolimwa zaidi ni mpunga, mahindi, karanga, kunde, njugu mawe na mihogo

kurugenzi wa SHIDEPHA+ Venance Muzuka akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila zilizofanyika katika kijiji cha Nyida.

Meneja wa program kutoka shirika la Oxfam Bonaventure Joseph akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila zilizofanyika katika kijiji cha Nyida. Kulia kwake ni Peppy Sparrow kutoka Oxfam Scotland ambao ndio wafadhili wa mradi huu kupitia serikali ya Scotland.

Wakazi wa kijiji cha Nyida wakihudhuria hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kiomoni Kibamba akizungumza katika hafla hiyo. Kibamba alisema “Kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo; Oxfam na SHIDEPHA+ tumefanikiwa kutekeleza mradi wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ndani ya vijiji vinne ambavyo ni Shabuluba, Nyida, Mwenge na Puni. Mradi ulioanza mwezi wa Februari 2016 na sasa upo katika hatua za mwisho za utekelezaji.”

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kiomoni Kibamba akizungumza katika hafla hiyo. Kibamba alisema “Kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo; Oxfam na SHIDEPHA+ tumefanikiwa kutekeleza mradi wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ndani ya vijiji vinne ambavyo ni Shabuluba, Nyida, Mwenge na Puni. Mradi ulioanza mwezi wa Februari 2016 na sasa upo katika hatua za mwisho za utekelezaji.”



Wakazi wa kijiji cha Nyida wakiangalia hati zao walizopokea. 



Anna Kadilana mkazi wa kijiji cha Nyida akionyesha hati yake ya hakimiliki ya kimila. Anna alisema, "Nimeamua kukata hakimiliki kwa sababu ya kukwepa usumbufu hasa wa mipaka ambao ulikua unatokea mara kwa mara"


Wakazi wa kijiji cha Nyida wakihudhuria hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila.
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amekabidhi jumla ya hati za hakimiliki za kimila 92 kwa wakazi wa kijiji cha Nyida mkoani Shinyanga.

Hatua hiyo ya ugawaji wa hati ilifanyika hivi karibuni katika Wilaya hiyo, baada ya viwanja vya wakazi hao kupimwa na kupatiwa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi.

Alisema Hati hizo zitawasaidia wananchi kupunguza au kuondoa kabisa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo kwa sababu watakuwa wanamiliki maeneo yao kisheria.

Matiro alisema migogoro mingi ya ardhi inatokea kutokana na watu kutokuwa na hati zinazoonyesha ukubwa wa maeneo yao na kusababisha mgogoro baina ya mtu na mtu.

Matiro aliwapongeza maafisa ardhi kwa kuweza kufanya kazi hiyo kwa kutumia shilingi milioni tatu kwa kila kijiji tofauti na milioni tisa iliyoelekezwa na serikali.

“Natoa shukrani zangu za dhati  kwa ushirikiano mkubwa na ufadhili kutoka kwa wadau wa maendeleo ikiwemo Shirika la Oxfam na SHIDEPHA+ kwa kusaidia kutoa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi ili wananchi wa wilaya yangu kufahamu umuhimu wa hati hizo,” alisema.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Kiomoni Kibamba alisema kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Oxfam na SHIDEPHA+ wamefanikiwa kutekeleza mradi wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ndani ya vijiji vinne ambavyo ni Shabuluba, Nyida, Mwenge na Puni.

Alisema mradi huo ulianza mwezi wa Februari 2016 na sasa upo katika hatua za mwisho za utekelezaji katika vijiji hivyo.

Alitaja changamoto mbalimbali  za kupata haki miliki za kimila kuwa ni pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha ndani ya jamii, baadhi ya wananchi kugubikwa na umaskini na kukosa fedha kwa ajili ya kuchangia gharama za upimaji.

Kibamba alisema changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa vigezo elekezi vya Wizara na kanuni ya sheria ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 kuhusu kupatiwa hati miliki ndani ya serikali za vijiji ambavyo ni pamoja na kukosa ofisi zenye hadhi za Halmashari za vijiji pamoja na ukosefu wa masijala za ardhi na daftari za ardhi za vijiji kwa ajili ya usajili wa Hakimiliki za kimila.

“Faida zilizotokana na mradi wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika halmashauri ni pamoja na uhamasishaji na utoaji wa elimu juu ya hati za haki miliki za kimila uliotolewa kwa vijiji vinne pamoja na kupunguza na kutokomeza kabisa migogoro ya ardhi ndani ya jamii katika vijiji husika,” alisema Kibamba.

Alitaja faida nyingine kuwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira kwa kupanga matumizi sahihi ya ardhi ndani ya mipaka ya kijiji, umiliki wa ardhi kisheria ndani ya jamii kwa wananchi kupatiwa hati za hakimiliki za kimila pamoja na jamii kupata uwezesho wa kifedha kutoka taasisi za kifedha baada ya kupatiwa hati miliki.

Nae miongoni mwa wakazi waliopokea hati hizo ambae ni  Mkazi wa Kijiji cha Nyida, Flora Nkingwa alishukuru kukabidhiwa hati hizo kwani sasa anamiliki eneo lake kisheria.

Nkingwa alisema eneo alilopatiwa hati lina ukubwa wa nusu ekari ambalo analitumia kwa kilimo cha Mahindi na Karanga.

Hati hizo za bila kikomo zilitolewa kwa mchanganuo wa hati 75 za familia, hati 7 za wanawake, hati 5 za wanaume, hati 2 za Taasisi na hati 3 za ukoo.
photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Website;www.koncept.co.tz IMAGINE INSPIRE INFLUENCE

WANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI WAJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

May 08, 2016
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Joyce Hagu (wa pili kushoto), akimkabidhi Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel, kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),  katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo kwa waimbaji wa nyimbo za injili uliofanyika Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima na Rais wa chama hicho, Ado Novemba.
 Hapa mwimbaji nguli wa nyimbo za injili Mzee Kitenzogu Makassy akikabidhiwa kadi yake baada ya kujiunga na NHIF.
 Burudani kutoka Kwaya ya Victorous Station ya Mwananyamala ikiendelea.
 Wanakwaya wakibadilishana mawazo katika uzinduzi huo.
 Burudani zikiendelea.
 Waimbaji wa kwaya ya Kanisa la Nabii Flora la Salasala wakitoa burudani.
 Wanakwaya ya Ukombozi ya Kanisa la Anglikana Tegeta wakionesha umahiri wa kumtukuza mungu kwa kuimba.
 Muonekano wa meza kuu katika uzinduzi huo.
 Ushuhuda ukitolewa kuhusu mungu anavyowatendea watu wake miujuzi.
 Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima (kushoto), akiwa ameketi na mgeni rasmi mama Joyce Hagu.
 Maofisa wa NHIF kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa tayari kuwandikisha wanachama wapa katika uzinduzi huo. Kutoka kulia ni Derick Ndyetabula, Margaret Malangalila na Dk.Fortunatus Salala.
 Mchungaji David Nyanda ambaye ni muimbaji (wa pili kulia), akionesha manjonjo wakati akitoa burudani kwa kuimba katika uzinduzi huo.
 Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Waimbaji na maofisa wa NHIF kutoka Kinondoni wakifuatilia uzinduzi huo.
 Rais wa Chamuita, Ado Novemba akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Furaha na shangwe zikiendelea katika uzinduzi huo watu wote mikono juuu.
 Meneja wa NHIF Wilaya ya Kinondoni, Constantine Makala akitoa darasa kuhusu faida za kujiunga na NHIF na jinsi ya kujiunga.
 Dk.Fortunatus Salala wa NHIF akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Mmoja wa waimbaji wa nyimbo za injili akielezea jinsi alivyonufaika na mfuko huo baada ya kujiunga miezi miwili iliyopita pamoja na mke wake.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Joyce Hagu (kushoto), akionesha kadi za wanachama hao baada ya kuzizindua. Kulia ni Maadam Ruti Mwamfupe.


Na Dotto Mwaibale

WANACHAMA wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), wamejiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ili waweze kupata matibabi ya uhakika pindi watakapo umwa.

Katika hatua nyingine Mlezi wa chama hicho Askofu Rejoyce Ndalima amewataka waimbaji wa nyimbo za injili kujianzishia miradi mbalimbali itakayowaingizia kipato badala ya kutegemea uimbaji pekee na amewasihi wanamuziki hao kuachana na utamaduni wa kudurufu (kukopi) kazi za wenzao badala yake wawe wabunifu katika kutunga nyimbo zao.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Afya kwa wanachama wa chama hicho Dar es Salaam jana kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ndalima alisema kuokoka sio kuwa mjinga hivyo ni vyema kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo.

“Kuokoka sio kuwa mjinga kwani kuna fursa za biashara ambapo mnatakiwa kuonesha uwezo wenu wa kuzifanyia kazi ili muweze kujikwamua kiuchumi badala ya kung'ang'ania kazi moja tu ya uimbaji,” alisema Ndalima.

Askofu Ndalima aliwataka waimbaji hao wajiunge na bima ya afya kwani hakuna mtu atakayechangiwa tena pindi atakapoumwa na kama ni msaada mtu husika atasaidia katika masuala mengine.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Joyce Hagu kutoka, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo, alisema Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha mfuko wa wasanii kutokana na kutambua mchango wao katika jamii.

Hagu aliipongeza NHIF kwa kufikisha huduma hiyo kwa waimbaji hao kwani itawasaidia katika maisha yao hasa pale watakapohitaji kutibiwa katika Hospitali mbalimbali.

Meneja NHIF  Wilaya ya Kinondoni,  Constantine Makala alisema kuwa huduma hiyo watalipia 76800 kwa mwaka mzima.


Alisema watu wote waliojiunga na huduma hiyo wanaweza kupa matibabu katika Hospitali zilizoainishwa pamoja na kupata dawa katika maduka 200 yaliyosajiliwa na NHIF.


BENKI YA AZANIA YATOA MSAADA WA MILIONI 5 KWA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

May 08, 2016
Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kulia), kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, akimkabidhi kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Francis Yango (kushoto), dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.milioni 5 vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Dar es Salaam leo asubuhi. Wapili kulia ni Muuguzi wa zamu,Getrude Massawe na  Antusa Lasway.
Wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa mbele ya vifaa na dawa walivyotoa msaada kwa Hospitali hiyo.
Hapa ni furaha tupu kabla ya kukabidhi msaada huo.
Makabidhiano zaidi ya msaada huo ukitolewa
mwonekano wa maboksi yenye msaada huo baada ya kupokelewa.
Vifaa hivyo vikipelekwa kwa walengwa.
Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kushoto), akimkabidhi dawa za meno na sabuni, Judith Kimei katika wodi ya wazazi. Kulia ni Muuguzi wa zamu Antusa Lasway.
Ofisa wa benki hiyo, Neema Tumsifu akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.
Ofisa wa benki hiyo, Valentina Chesama akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.
Wafanyakazi hao wa Bebki ya Azania wakiondoka Hospitalini hapo baada ya kukabidhi msaada huo.

Na Dotto Mwaibale

BENKI ya Azania imetoa msaada wa dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 5 wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Amani Ilala jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo wakati wa kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara, Mwanahiba Mzee alisema kila mara benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii kulingana na ratiba yao ambapo mwaka huu waliona ni vema msaada huo waupeleke Hospitali hiyo.

Alisema mwaka katika kusherehekea sikukuu ya wanawake waliona ni vema kutoa msaada hasa katika wodi ya wajawazito ukizingia kuwa sikukuu hiyo inawahusu.

"Tumetoa msaada wa dawa mbalimbali kama dettol, spiritis, mabomba ya sindano, micoprostol, vitamini k na nyingine nyingi pamoja na vifaa vya usafi kama vile mifagio, sabuni na dawa za mswaki" alisema Mzee.

Kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali hiyo, Francis Yango akizungumza wakati wa kupokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mkuu, Shadrack Shimwela aliishukuru benki hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia.

"Tunawashukuru sana Azania Bank Ltd kwa msaada wenu lakini tunawaomba muende mbele zaidi kama mtaweza mtujengee walau wodi ambayo itaingiza walau vitanda 30 na wodi hiyo muandike jina la benki yenu kwani changamoto kubwa tulionayo kwa sasa licha ya kuwa na vitanda vya kutosha tuna uhaba wa wodi" alisema Yango.

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA KUPAA KWA BWANA KATIKA PAROKIA YA TOLEO LA BWANA JIMBO LA ARUSHA

May 08, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia na wanakwaya  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Padri Kiongozi  PETER PINTO baada ya kushiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016. Kulia ni Pdr. PETER PINTO na kushoto kwake ni Padri  wasaidizi Prosper Tesha na Furchong James Luis
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na vijana wa altari katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Rozari  kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishukuru baada ya kupokea zawadi ya Rozari kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Biblia Takatifu kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.