RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA ITIGI-MANYONI- CHAYA AKITOKEA MKONI TABORA AKIELEKEA DODODMA

July 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wananchi Kijiji Cha Tula Uyui Mkoani Tabora waliojitokeza Barabarani Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo akiwa njiani katika moja ya mikutano ya barabarani kwa  waliojitokeza  Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi wakati mheshimiwa Rais alipowasili Mkoani Singida eneo la Itigi ili kufungua Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5aliyojengwa na Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Itigi na Manyoni wakati wa Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma  Julai 25,2017.

 Wananchi wa Itigi na Manyoni wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatubia kwenye Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma  Julai 25,2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wapili kushoto na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida,wakiondoa kitambaa kuashiria Kufunguliwa Rasmi kwa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma  Julai 25,2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida na Tabora Wakikata Utepe kama ishara ya kufunguliwa Rasmi kwa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma  Julai 25,2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiteta jambo na Mwakilishi wa Kampuni ya PowerChina International Group Limited nchini Bw. Wang Chao wakati wa Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma  Julai 25,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwasalimia kwa kupunga mikono kwa wananchi wa Itigi na Manyoni walioshiriki na Kushuhudia Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma  Julai 25,2017

UTALII WAZIDI KUONGEZA PATO LA TAIFA

July 25, 2017


Na Thobias Robert-Maelezo
Sekta ya utalii nchini imeendelea kukuza na kuongeza mapato ya serikali kwa kuchangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa, huku ikitazamiwa kuongezeka katika mwaka huu wa fedha. 
Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) Bwana Allan Kijazi wakati akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA” kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1).
“Utalii unatoa mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi hii, kwa sasa hivi unakisiwa kwamba unachangia kama asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha ya kigeni,” alisema Bw. Kijazi. huku akisisitiza kuwa TANAPA watazidi kulinda na kuendeleza hifadhi zilizopo nchini ili zizidi kuongeza pato la taifa kwa maendeleo ya watanzania wote.
Mkurugenzi huyo wa TANAPA alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 TANAPA ilichangia kiasi cha billion 27 kwenda Mfuko wa Taifa wa serikali na matarajio yao katika kuchangia mfuko wa fedha wa Taifa kwa mwaka huu  wa fedha 2017/2018 ni bilioni 33.4 hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa Watalii kutoka nje ya nchi.
Aliongeza kuwa Tanzania ina vivutio vingi kama vile Mito, Mabonde, Milima, lakini hifadhi za Taifa kama Vile Ngorongoro, Serengeti, Gombe, Ruaha ndizo zinazoongoza kwa kuchangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 80 ikilinganishwa na vivutio vingine.
Bwana Kijazi aliongeza kwa kusema kuwa, utalii nchini umekuwa ukikuunaongezeka kila mwaka ambapo kwa takimwu walizo nazo zinaonesha kuwa, ongezeko la watalii kwa miaka mitano iliyopita limekuwa lilkiongezeka kwa asilimia 4 hadi 7 kila mwaka.
Kuongeza kwa watalii hasa katika hifadhi za Taifa kunatokana na TANAPA kujitangaza zaidi katika nchi mbalimbali duniani kupitia Mitandao ya kijamii, Makampuni binafsi ndani na nje ya nchi, Balozi za Tanzania katika mataifa ya Nje, Vilabu mbalimbali vya Ulaya na Amerika pamoja Vyombo vya Habari vya kimataifa kama vile CNN na BBC.
Mkurugenzi Kijazi alisema kuwa, Mataifa yanayoongoza kutembelea hifadhi za taifa ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Uingereza, Italia, Ufaransa, pamoja na Hispania huku akitaja kuwa vivutio vya utalii vilivyopo Nchini  hasa hifadhi ni vya kipekee, mazingira mazuri, hali ya hewa pamoja na amani na utulivu uliopo nchini  ndiyo sababu zinazowavutia  watalii kuongezeka kila mwaka.
Pamoja na kukua na kuongezeka kwa utalii nchini kunakopelekea kuongeza la Taifa, Mkurugenzi Kijazi alisema kuwa, utalii wa ndani bado ni changamoto kwani watalii wengi wanatoka nje ya Nchi huku wazawa wakishindwa kuzuru maeneo mbalimbali ya utalii ili kujionea fahari ya nchi yao hivyo ametoa wito kwa Watanzania kutembelea vivutio hivyo ili kukuza na kuongeza pato la Taifa.

Hivi karibuni Mtandao wa SafariBookings.com unaojihusisha na masuala ya ukuzaji wa safari za kitalii barani Afrika uliitaja   Tanzania kama kivutio kizuri cha safari za watalii barani humu.

MAOFISA UGANI WASIPEWE KAZI ZA WATENDAJI

July 25, 2017
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri, akizungumza na maofisa ugani wa wilaya hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB), wilayani humo mkoani Tabora leo. Kutoka kushoto ni Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTECH, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Hashim Kazoka na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Pascal Ngunda.

KAIMU MENEJA MKUU WA BANDARI YA KIGOMA AKANUSHA MADAI JUU YA KUTOKULIPWA WANANCHI 1228 WA ENEO KATOSHO

July 25, 2017
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika  kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao kushoto ni Meneja wa Mawasiliano TPA Janeth Ruzangi
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika  kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao kushoto ni Maneja wa Mawasilino TPA Janeth Ruzangi
 PRO wa TPA Tanga Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo
 Waanmdishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia matukio
 Waandishi wa habari wakiwa kazini kuchukua stori
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza kushoto akimpa ufafanuzi mwandishi wa gazeti la Dail News Mkoani Tanga,Amina Kingazi
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza amekanusha madai yanayoenezwa juu ya kutokulipwa wananchi 1228 wa eneo la Katosho katika Manispaa hiyo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bandari kavu ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 12 zimetengwa kwa ajili ya gharama za fidia.
 
Hayo ameyazungumza jana Jijini Tanga alipokuwepo kwenye kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao.

Aidha alisema jumla ya hekari 158 ndizo zilizochukuliwa na mamlaka ya bandari(TPA) kwa ajili ya mradi huo huku wananchi 1196 kati 1228 tayari wamekwisha lipwa fedha zao kama semehemu ya fidia za ardhi,mazao na makazi jambo ambalo limefanyika kwa mujibu wa kisheria na ushirikishwaji wa pande zote.
 
Mchindiuza alizidi kufafanua kuwa kutokana na hatua hiyo wananchi 32 kati yao walishindwa kulipwa fidia zao kutokana na kushindwa kuwakilisha akaunti zao katika Halmashauri ya manispaa ya Mji wa Ujiji jambo ambalo linapotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari.
 
“Yapo malalamiko mengi ya utaratibu wa ulipwaji wa fidia hizo kwa wananchi walioko katika maeneo ya ya maradi lakini labda niseme kitu tayari tumekwisha walipa wananchi 1196 kati 1228 na waliobakia ni 32 tu na fedha zao zipo wapeleke akauti zao tuweze kuwalipa”Alisema.

Alisema Mamlaka hiyo baada ya kukua kutokana na kuongezeka kwa shehena mamlaka ilitafuta eneo kwa ajili ya kujenga mradi wa bandari kavu ambalo litatumika kuhudumia nchi jirani za maziwa makuu kama DRC,Burundi na Rwanda.

Taratibu za kupatikana kwa eneo hilo ambalo lilikuwa mali ya wananchi katika eneo hilo la Katosho Mkoani humo zilifanyika kisheria na kuishirikisha Halmashauri ya Mji huo ambao wao ndio wanaozijua kaya zinazoishi katika maeneo hayo.
 
“Lengo letu la kuishirikisha Halmashauri ya manispaa hiyo ni
kuhakikisha wanafanya tathmini ya kina dhidi ya wananchi hao na tunatambua kuwa wanazitambua kaya zote zinazostahili kulipwa na hivi ndivyo tulivyo fanya”Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi hao kama wanamadai kuhusiana na kiwango kidogo cha fidia wanaweza kufika katika mamlaka za sheria za ardhi na kufuata mkondo wa sheria ili waweze kupata msaada wa kisheria zaidi.
 
“Wananchi wasipotoshwe na wajanja wajanja idadi ya wafidiwa
inatambuliwa na na kama kuna kitu hakijafuatwa wafuate sheria ili mkondo huo uchukue maamuzi ya kisheria bila ya kuonea mtu na sisi kama viongozi wa mamlaka tupo salama na kwa wale ambao hawajalipwa wafike na vielelezo katika ofisi husika wachukue fedha zao.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hao waache kupotoshwa na watu wachache ambao hawataweza kuwasaidia kitu chochote jambo la msingi kujenga ushirikiano katika miradi hiyo ya maendeleo ya Taifa.

Wakulima wa mahindi Handeni wanogewa na mbegu za mradi wa WEMA

July 25, 2017

Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) pamoja na wakulima na wageni mbalimbali walipotembelea shamba hilo. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).

Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) pamoja na wakulima na wageni mbalimbali walipotembelea shamba hilo. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).

Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) juu ya ubora wa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA), katika moja ya shamba darasa la mkulima.

Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa.

Shamba darasa la mkulima, Kidika Swai lililotembelewa na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).

Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali akimenya moja ya hindi katika shamba darasa.

Ofisa Mawasiliano wa jopo la watafiti wa Mradi wa WEMA Tanzania, Dk. Janet Kaya (kushoto mwenye kofia) akifafanua jambo kwa mgeni rasmi na viongozi wengine walipotembelea moja ya shamba mfano lililopandwa kwa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).

Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe (wa pili kulia) wakiangalia moja ya hindi kwenye shamba mfano lililohudumiwa na mbegu za mradi wa WEMA.

Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa darasa kwa wakulima wenzake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani.

Na Joachim Mushi, Handeni
WAKULIMA wa Mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA), wilayani Handeni wameiomba Serikali irekebishe sheria ya uzalishaji wa mbegu ili kutanua wigo wa uzalishaji mbegu kupitia taasisi za Serikali kama vile Jeshi la Kujenga Uchumi (JKT), Jeshi la Magereza pamoja na zinginezo zilizopo.
Wakulima hao wametoa ombi hilo jana kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani, kilichopo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kufuatia uwepo wa changamoto ya kutopatikana kwa uzalishaji wa mbegu ya kutosha kulingana na mahitaji kama ile ya WE 2109 ambazo zimeonekana kufanya vizuri zaidi maeneo ya Wilaya ya Handeni.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mwakilishi wa Wakulima hao, Costansia Msola alibainisha kuwa bei kubwa ya mbegu zinazozalishwa na makampuni ya mbegu ulikuwa changamoto licha ya uwepo wa wadudu waharibifu waliojitokeza kwenye mashamba ya wakulima na kukwamisha matarajio ya uzalishaji.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali aliwapongeza kikundi cha wakulima 22 waliokubali kushirikiana na watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuendesha mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA) ambao umeonesha mafanikio makubwa.
Aidha aliwataka wakulima Wilayani Handeni kukubali mabadiliko na kuanza kutumia mbegu hizo za kisasa zaidi ya aina 11 zilizoonesha mafanikio makubwa katika utafiti. "...Huko nyuma tulikuwa tukitumia mbegu za asili ambazo zilikuwa hazifanyi vizuri, naombeni sasa tutumie mbegu hizi bora zilizofanyiwa utafiti na WEMA kwa kilimo bora," alisisitiza, Bw. John Mahali akizungumza na wakulima.
Aliyaomba makampuni ya uzalishaji mbegu kujitokeza na kufanya uzalishaji wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame ili kuwasaidia wakulima upatikanaji wake kwa wakulima.

Benki ya NMB yafungua matawi mapya mikoa mitatu

July 25, 2017
Mkuu wa Wilaya Itilima –Benson Kilangi (kati kati ) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NMB Itilima katika Mkoa wa Simiyu. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa NMB kanda ya Magharibi –Peter Madaha na Mbunge wa Itilima- Njalu Silanga wakishuhudia uzinduzi wa tawi hilo. Tawi hili ni miongoni mwa matawi mengine mawili yaliozinduliwa kwa pamoja katika kanda ya magharibi mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Wilaya Igunga –John Mwaipopo (kati kati ) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NMB Nkinga katika wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora wengine pichani ni Meneja wa NMB kanda ya Magharibi Leon Ngowi (wa kwanza kushoto) na Meneja wa NMB tawi la Nkinga Jasmina Tengia (kulia). Tawi hili ni miongoni mwa matawi mengine mawili yaliozinduliwa kwa pamoja katika kanda ya magharibi mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imezidi kung’ara nchini huku ikifanikiwa kutanua mtandao wake kwa kufungua matawi mapya matatu katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Simiyu. Uzinduzi wa matawi hayo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kufunguliwa kwake kutaleta neema kwa wakazi wa maeneo hayo.
Mkoani Kigoma benki hiyo ilizindua tawi jipya Wilaya ya Uvinza, Tabora (Igunga) katika mji wa mashuhuri wa Nkinga na Simiyu Wilaya mpya ya Itilima.
Awali akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko, aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya benki hiyo ikiwemo kuhifadhi fedha zao na huduma za kifedha ikiwemo mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo.
Alisema hatua ya kuzinduliwa kwa tawi hilo la Benki la NMB sasa ni wazi wilaya hiyo itajikwamua kiuchumi ikiwemo wananchi wake kujenga urafiki na benki hiyo kwa kupata huduma bora za kifedha.
“Kuzinduliwa kwa tawi hili jipya katika Wilaya yetu ya Uvinza sasa ni kielelezo kwamba wananchi wataweza kujikwamua kiuchumi kwa kuwa na urafiki wa karibu na benki ikiwemo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa,” alisema Mrindoko.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, John Mwaipopo, akizinduwa tawi jipya katika mji wa Nkinga alisema ni kielelezo tosha cha wilaya hiyo kupiga hatua kimaendeleo. Aidha akifafanua zaidi kwa wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo, Mwaipopo alisema hatua hiyo ni ishara nzuri na wananchi wataweza kutumia fursa kidekede zinazotolewa na benki hiyo.
“Asanteni NMB kwa kufika hapa Nkinga, awali wananchi walikuwa wakitembea umbali mrefu hadi Igunga mjini kutafuta benki lakini sasa huduma za kifedha zitapatikana hapa kupitia benki hii nzuri na bora kutokana na huduma zake,” alisema Mwaipopo.
Naye Meneja wa TRA Wilaya ya Nzega, Adolf Mtumbuka, akizungumza katika uzinduzi huo, alisema tawi hilo litasaidia kukusanya mapato ya Serikali ambapo awali wananchi wa Nkinga walilazimika kwenda makao makuu ya wilaya.
“Ninapenda sana kuishukuru Benki ya NMB sasa imekuja kufungua milango ya kiuchumi katika eneo hili la Nkinga ambalo lipo Wilaya ya Igunga lakini pia lipo jirani sana na Wilaya ya Nzega. Hivyo kuzinduliwa kwake kutasaidia kukusanya mapato ya Serikali kupitia benki hii ambao pia hukusanya mapato ya Serikali kwa niaba ya TRA,” alisema Mtumbuka.
Kutokana na kuimarisha huko kwa mtandao wa benki hiyo Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Benson Kilangi, alisema kuzinduliwa kwa tawi hilo kutachochea wananchi kuzalisha vizuri na fedha watakazopata watahifadhi benki.
“Tunahitaji kuweza ndani ya Wilaya ya Itilima ili wananchi wapate muda wa kutosha katika shughuli za uzalishaji ili kuondokana na umaskini. Hivyo nawaomba wananchi wa Itilima mtumie fursa hii ya Benki ya NMB kwa kisingizio hamna mitaji au hajui mfanyaje.

--
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.

Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470


          http://joemushi.blogspot.com

DC ASIA ABDALLAH :IRINGA ACHENI MAJUNGU FANYENI KAZI KUKUZA KIPATO CHENU

July 25, 2017
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanachama na wadau wa timu ya lipuli kwenye mkutano wa uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa timu ya lipuli uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Mwembetogwa.
Baadhi ya wadau na wanachama wa timu ya lipuli wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo bi Asia Abdallah

Na fredy Mgunda, Iringa.

Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah aliwataka wananchi wa Mkoa wa Iringa kuishi bila kuwa na majungu kwa sababu majungu yanarudisha nyuma maendeleo.

Hayo yamesemwa wakati wa hotuba ya uchaguzi wa kuwapa viongozi wapya wa timu ya Lipuli katika ukumbi wa shule ya sekondari ya mwembetogwa  ulipo Manispaa ya Iringa.

Abdallah alisema kuwa Iringa kumekuwa na majungu ambayo yamekuwa yakileta uchonganishi baina ya watu na watu pia viongozi na viongozi hivyo inatakuwa kubadilika na tusiishi kwa mazoea.

"Ukiiinga huku majungu kule majungu hasa mtu hana pesa ya kula lakini anashinda kwenye mitandao ya kijamii kuleta majungu,fanyeni kazi kwa nguvu zenu zote maana mnaendekeza tu majungu ambayo hayana manufaa kwako binafsi hata taifa kwa ujumla"alisema Abdallah

Aidha Abdallah alisema kuwa viongozi wa timu ya lipuli watakaoingia madarakani kuhakikisha wanavunga makundi yote ya majungu na kuhakikisha timu inakuwa na umoja na ushirikiano kila nyanja ili kupata mafanikio makubwa ambaya yataleta faraja kwa wakazi wa Iringa na wapenda Soka.

"Haiwezikani kila kona ni majungu tu hivi nyie hamna kazi za kufanya tena afadhali wanawake wangekuwa na majungu lakini majungu hayo yanaongozwa na wanaume kwenye magroup ya what's up,achaneni na magroup ambayo hayana faida kwako wala hanaya afya kwa taifa la Tanzania" alisema Abdallah

Mohammed aliongeza kwa kusema kuwa Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli anahimiza wananchi kufanya kazi na sio kutengeneza majungu ambayo yamekuwa yakikwamisha maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha Soka Mkoani Iringa Dr Ally Ngalla alimshukuru Mkuu wa wilaya huyo kwa hotuba nzuri na kumuahidi kuwa Iringa itabadilika na kufuta majungu kutokana na tayari wamepata viongozi wapya wa timu ya lipuli.

"Nikiwa kama kiongozi nitahakikisha makundi yote ya majungu yanavunjwa na kuwa kitu kimoja ambapo tutafanya kazi kama siafu ili kuinua Mpira wa miguu Mkoani Iringa "alisema Ngalla

Ngalla aliwata wadau wa mpira miguu Mkoani Iringa kusahau yaliyopita na kuangalia nini cha kufanya ili kuisadia timu ya lipuli ifanye vizuri kwenye ligi kuu Tanzania bara na kulejesha furaha ya wananchi wa Iringa.

Naye Mwenyekiti Mpya wa timu ya lipuli Ramadhani Mahano aliwaomba wadau wa Mpira na wapenzi wa timu ya lipuli kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja kuvunja makundi yote yaliyokuwa yanasababisha migogoro ya lipuli na Mpira wa miguu kwa ujumla.

Nawaombeni sana kuyaka kichwani vizuri maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Kilolo bi Asia Abdallah kwa kuacha majungu au kusababisha migogoro ambayo haina maana bali naomba tushauriane kwa kila jambo kwa manufaa ya lipuli na wadau wa mpira.