RAIS DKT. SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

September 14, 2023

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Stephen Patrick Mbundi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (atayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Balozi Profesa Kennedy Godfrey Gastorn kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Septemba 14, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Balozi Said Shaib Mussa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Septemba 14, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Abdul-Hakim Ameir Issa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2023.

- Advertisement -
Ad image

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Lameck Michael Mlacha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimuapisha Paul Joel Ngwembe kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Septemba 14, 2023. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Septemba 14, 2023.

SILAA AHIMIZA WAKUU WA MIKOA KUTEKELEZA MAAMUZI YA BARAZA LA MAWAZIRI VIJIJI 975

SILAA AHIMIZA WAKUU WA MIKOA KUTEKELEZA MAAMUZI YA BARAZA LA MAWAZIRI VIJIJI 975

September 14, 2023

 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara alipokwenda kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 

 

 Sehemu ya viongozi na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (hayupo pichani) alipokwenda kufuatilia utekelezaji Maagizo ya Baraza la Mawaziri kuhusina na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 13 Septemba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Na Munir Shemweta, WANMM NANYUMBU

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amehimiza wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha wanatekeleza maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975

‘’Niwaombe wakuu wa mikoa wote nchini kuendelea kusimamia utekelezaji maagizo ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na migogoro ya vijiji 975’’. Alisema

Waziri Silaa alisema hayo tarehe 13 Septemba 2023 wakati akizungumza na uongozi wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara akiwa kwenye ziara ya siku moja kufuatilia utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya  matumzi  ya adhi katika vijiji 975.

Alisema, ameridhishwa sana na tekelezaji wa maamuzi hayo kwa mkoa wa Mtwara kupitia wilaya ya Nanyumbu ambapo kwa mujibu wa Waziri huyo wa Ardhi wilaya hiyo imeweze kutekeleza maagizo hayo kwa asiliamia mia moja.

Kwa mujibu wa Silaa, atahakikisha serikali inapotoa kauli lazima itekelezeke kwa kuwa ndiyo kazi aliyotumwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuweka bayana kuwa, kazi aliyotumwa ataifanya mapema na kupeleka majibu ya mpango wa serikali kwa wananchi wa Nanyumbu ili kupunguza taharuki.

‘’Mimi naamini utekelezaji maamuzi ya Baraza la Mawaziri utakamilika kwa haraka kwa sababu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi ni maelekezo mahsusi ya Rais Samia kuwa, wizara ihakikishe jambo hili linafika mwisho’’ alisema Waziri Silaa

Aidha, alibainisha kuwa, migogoro ya ardhi inahusisha watu na pale utatuzi wake unapocheleweshwa unaleta mgogoro mwingine mkubwa kuliko wa awali jambo alilolieleza utatuzi wake unaweza kuwa mgumu kwa sababu utatuzi wa pili unaondoa imani ya wananchi kwa jambo lililoamuliwa na serikali kuwa linaweza kutekelezeka kwa haraka.

‘’Kwa kuwa kamati ilishaenda maeneo yote kasoro Peramiho, wajibu wangu ni kupita maeneo yote kwenda kuangalia utekelezaji maagizo ya Baraza la Mawaziri na nikiri tu utekelezaji wa maamuzi hayo kwa baadhi ya maeneo unasuasua’’ alisema.

Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 yanafuatia timu iliyoundwa kuchunguza changamoto za uvamizi wa maeneo ya hifadhi ambapo timu hiyo iliwasilisha taarifa ya migogoro katika vijiji 366 na ndipo ikaundwa Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta mwaka 2019 iliyokuja na mapendekezo ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye vijiji 975 huku vijiji 55 utatuzi wake ukisalia.

Wizara za kisekta zinazohusika katika utatuzi huo ni Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kama mwenyekiti, Maliasili na Utalii, Mifugo na Uvuvi, Kilimo, Maji, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), TAMISEMI na Wizara ya Ulinzi.

SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUWAKUMBUKA WAZEE UJENZI WA MAKAZI BORA

SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUWAKUMBUKA WAZEE UJENZI WA MAKAZI BORA

September 14, 2023

 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia baiskeli za watoto wenye Ulemavu zinazotumika katika Kituo cha ATFGM Masanga kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati wa ziara yake mkoani Mara.

Na WMJJWM,  Tarime-MARA

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeihimiza jamii kote nchini kukumbuka ujenzi wa makazi ya wazee wasiojiweza wakati huu wa mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis wakati akishiriki katika shughuli za maendeleo

Wilayani Tarime mkoani Mara.

Akiwa kwenye  ujenzi wa nyumba ya daktari wa zahanati ya Kijiji cha Soroneta amesema Jamii inatakiwa kushiriki katika shughuli za maendeleo ili wawe na umiliki wa miradi hiyo hususan  suala la utunzaji ili idumu.

Mwanaidi amesema, Kampeni ya Amsha Ari ni moja ya juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum juu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii ya Mwaka 1996 inayohimiza Wananchi kujitolea wakati wa shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

“Mimi nimekuja hapa kuamsha ari ya wananchi kuweza kujenga makazi bora na pia kusaidia watu wengi kuwa na makazi bora hasa wazee wasio na uwezo” amesisitiza Naibu Waziri Mwanaidi.

Naye Diwani wa Kata ya Nyarelo   Japheth Marwa, amesema wananchi wa kata hiyo wamekuwa na moyo na ari ya kujitolea katika shughuli za maendeleo na wataendelea kujitoa ili kufanikisha miradi mbalimbali ya huduma za jamii iweze kuwasaidia kuondokana na changamoto zinazowakabili

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya  Kijiji cha  Soroneta Kata ya Nyarelo Dkt. Richard Kitende ameishukuru Serikali  kwa kuunga mkono juhudi za wananchi kutekeleza miradi ya Maendeleo kwani inasaidia kuwapa moyo wa kujitoa na kusaidia upatikanaji wa huduma muhimu karibu na maeneo yao.

Akizungumzia hatua hiyo, Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara amesema ni jambo jema viongozi kuonesha mfano kwenye masuala ya maendeleo na jamii kwani itasaidia kuwa na moyo na mwamko kwa wananchi kuchangua katika shughuli za maendeleo.

Awali, Afisa Maendeleo ya Jamii Janeth Michael alisema mradi huo umeshirikisha wananchi kwa shughuli za kuchimba msingi, kusomba mawe na kujenga boma ambapo gharama zote za nguvu ya wananchi ni shillingi Millioni 8.1 huku wakiungwa mkono na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime iliyotoa shillingi Millioni 20 kuunga mkono juhudi za Wananchi.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia baiskeli za watoto wenye Ulemavu zinazotumika katika Kituo cha ATFGM Masanga kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati wa ziara yake mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akisoma mabango ya ujumbe mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Kituo cha ATFGM Masanga kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati wa ziara yake mkoani Mara

  

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akishiriki ujenzi wa Nyumba ya Daktari katika Kijiji cha Seroneta Halmashauri ya Wilaya ya Tarime akihamasisha wananchi kujitolea katika shughuli za Maendeleo na ujenzi wa Makazi Bora wakati wa ziara yake mkoani Mara

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na wananchi mara baada ya kushiriki ujenzi wa Nyumba ya Daktari katika Kijiji cha Seroneta Halmashauri ya Wilaya ya Tarime akihamasisha wananchi kujitolea katika shughuli za Maendeleo na ujenzi wa Makazi Bora wakati wa ziara yake mkoani Mara 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikabidhi meza za vyereheni vilivyotolewa na Shirika la  Care Foundation kwa Kikundi cha  wakati wa ziara yake mkoani Mara Septemba 13, 2023.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM

WAZIRI BITEKO - WATANZANIA WANATAKA UMEME SIO MANENO

September 14, 2023

 


 Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanesco kuhakikisha watanzania wote wanafikiwa na huduma ya Umeme kuanzia Mijini hadi vijijini ili kusaidia shughuli za kiuchumi kuendelea.


Agizo hilo amelitoa Jijini Dar es salaam katika kikao cha Wafanyakazi wa Tanesco kutoka kila Mkoa ya Dar es Salaam  ambapo amesema jitihada za makusudi lazima zifanyike ili kila mahali umeme ufike kwani watanzani wao hawana maneno mengi isipokuwa kero yao kubwa ni suala la kukatika katika umeme inasababisha shughuli zao za kiuchumi kudhorota


"Watanzania wanataka umeme hawataki maneno umeme ukiwepo wa uhakika na haukatiki katiki huwezi ukasikia Shirika la Umeme likilaumiwa kama nyinyi hamjashirikiana kuacha kulinda vyeo vyenu mkaka na kushungulikia suala Moja tu upatikanaji wa umeme wa uhakika mtafanikiwa kwa kiasi kikubwa tuache kushughulika na matatizo ya wafanyakazi ” amesema Biteko 


Aidha, amewataka wakurungenzi kuunganisha wafanyakazi ambao ndiyo raslimali watu na viongozi wasiwavunje moyo kwa kuwagawanya makundi makundi wawaone wote ni sawa mbele ya macho yao ili hata wanapotoka majumbani mwao watamani kuja kazini na lengo lililokusudiwa likamilike upatikanaji umeme wa uhakika kwa watanzania wote.


"Kupendana kushikamana pasipokujali vyeo, kuthaminiana ni nguzo pekee kazini kwani kila mmoja ana mchango katika kufikia lengo lililokusudiwa acheni maneno maneno yanayopelekea kuleta makwazo shughulilieni suala Moja acheni kushughulika na watu tambueni majukumu. yenu kila. mmoja afanye kazi kwa bidii" amesisitiza

Hata hivyo,amesema ni  vyema kuungana kwa taasisi zote zilizopo chini ya wizara ya nishati ,ikiwemo REA TPDC kwani zote hizi hutegemeana na Waziri wake ni mmoja ili tuweze kuwafikia watanzania kwa haraka, na kazi hii ni ya kwetu.


Sambamba na hayo amewaonya viongozi mahali pa kazi patakuwa pagumu kama mtakuwa mmekusanya genge la soga na wapiga majungu kazini, na mwisho watanzania hawatapata umeme, wafanyeni watu hao kuwa ni daraja linalofanana na kama tutashughulika na masuala binafsi ya watu badala ya masuala ya kazi hamtafikia malengo.


" Kuna watu wanahofu ya mabadiliko, na hali hiyo tunaitengeneza sisi viongozi, kwa sababu ukiingia mahali badala ya kushughulika na jambo unaanza kushughulika na watu, na wafanyakazi wote hawa maisha yao yote ya utumishi wao masaa mengi wanatumia wakiwa kazini, hawa ni binaadamu, kuna wakati watakuwa wamekwazwa, wamevunjika moyo msikimbilie kuwasimamisha kazi kaeni nao chini ujue tatizo lake na ujue siyo kutoa maamuzi magumu wengine ni wagonjwa"amesema Biteko.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amemuhakikishia Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko kuwa Wizara yake kupitia shirika la TANESCO imekuwa ikifanya mikakati na kila jitihada za kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na za uhakika za Nishati ya Umeme.