LAHM :NINAPANGA KUSTAAFU SOKA MWAKA 2018

February 01, 2015

Baada ya kustaafu kutoka soka la kimataifa aliposhinda Kombe la Dunia nchini Brazil, Philipp Lahm ametangaza kuwa anapanga kuzitundika njumu zake kabisa mwaka wa 2018, na kuiambia kwaheri klabu yake ya Bayern
Lahm, akizungumza na gazeti la michezo la Ufaransa, L'equipe, amesema wakati huo atakuwa na umri wa miaka 34, na anahisi huo ndio wakati mzuri wa kustaafu kabisa kutoka kandanda.
Septemba 2014, Lahm aliliambia gazeti la michezo la Ujerumani “Sport Bild” kuwa alikuwa na uhakika angeweza kucheza kwa miaka mingine minne katika kiwango cha juu, na katika Bayern Munich kwa sababu ni klabu yake.
Licha ya kuwepo na mtindo wa wachezaji wenye umri mkubwa kuhamia Qatar au Marekani, Lahm anasema anataka kustaafu akiwa kileleni kama tu alivyofanya katika rangi za timu ya taifa ya Ujerumani.
Huku akiwa amesalia na miaka mitatu kwenye mkataba wake, nahodha huyo wa timu ya Ujerumani iliyonyanua Kombe la Dunia 2014 angali na ndoto kubwa katika klabu ya Bayern, ambayo ni kunyakua Kombe jingine la Ligi ya Mabingwa Ulaya – UEFA Champions League baada ya lile walilotwaa mwaka wa 2013.
Japokuwa Laham hatakuwa uwanjani kucheza akiwa na umri wa miaka 34, beki huyo amesema ni “bayana” kuwa atasalia katika mchezo huo kwa sababu “kandanda ni kitu anachokipenda”.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu
BENKI YA CRDB NA KAMPUNI YA BIMA YA HERITAGE ZA NYAKUA TUZO ZA BBLA 2014

BENKI YA CRDB NA KAMPUNI YA BIMA YA HERITAGE ZA NYAKUA TUZO ZA BBLA 2014

February 01, 2015

2
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga, (Kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA) katika sekta ya kibenki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Bw. Martin Mmari (kulia). Benki ya CRDB iliibuka mshindi katika sekta ya kibenki wakati kampuni ya Heritage Insurance iliibuka kinara katika sekta ya bima katika tuzo hizo zilizofanyika  jijini Dar es Salaam.
4
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga, (Kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA) katika sekta ya bima, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya Heritage Insurance, Bw. Yogesh Manek (kulia). Heritage Insurance iliibuka mshindi katika sekta ya bima wakati Benki ya CRDB iliibuka kinara katika sekta ya kibenki katika tuzo hizo.
5
Mwenyekiti wa jopo la majaji waliosimamia Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA), Bw. Leonard Mususa akizungumza katika hafla ya kutangaza washindi wa tuzo hizo ambapo kampuni ya bima ya. Heritage iliibuka mshindi katika sekta ya bima wakati Benki ya CRDB iliibuka kinara katika sekta ya kibenki katika tuzo hizo.
6
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga akizungumza katika hafla ya kutangaza washindi wa Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA), ambapo kampuni ya bima ya. Heritage iliibuka mshindi katika sekta ya bima wakati Benki ya CRDB iliibuka kinara katika sekta ya kibenki katika tuzo hizo.
Picha mpiga picha wetu.
MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA LINDI KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA LINDI KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

February 01, 2015


111112 
Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Rai hiyo imetolewa jana na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jerry Silaa wakati akiongea kwenye kilele cha sherehe za kutimiza miaka 38 ya chama hicho mkoani Lindi zilizofanyika katika tawi la Mnazi Mmoja lililopo kata ya Mingoyo wilaya ya Lindi mjini. Silaa mbaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala alisema iwapo mtu atajiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura atashiriki katika uchaguzi mkuu ujao hivyo basi wakati ukifika ni jukumu la mabalozi kuwahimiza wananchi kujiandikisha ili wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga kura. Aidha Meya Silaa aliwapongeza wana CCM kwa ushindi wa asilimia 77 walioupata wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana na kuwataka kuwa makini katika kuteua viongozi wanaokubalika na wananchi na kuachana na makundi yanayokibomoa chama hicho kwa kufanya hivyo itawawezesha kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao. Kwa upande wa vijana aliwahimiza kujishughulisha katika shughuli za kimaendeleo ili waweze kujipatia maendeleo kwani mkoa wa Lindi uko katika dira ya maendeleo kwa kuwa na ardhi yenye rutuba, barabara nzuri na gesi. Silaa alisisitiza, “Nawashauri vijana wenzangu mjiunge na CCM chama kinachowasaidia vijana kuwaletea maendeleo ukilinganisha na vyama vingine vinavyowapotezea muda na kurudisha nyuma maendeleo yenu”. Alikipatia kikundi cha Zamira ambchi kinajishughulisha na kilimo na ujasiriamali shilingi laki tano ili ziweze kuwasaidia kuinua mtaji. Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete alisema sherehe hizo zina umuhimu wa kipekee kwa wana CCM kwani zimeangukia mwaka wenye matukio muhimu na makubwa kwa nchi ambayo ni kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais. Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema mwaka 2015 ni mwaka wa kuhitimisha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 ambapo Chama hicho kiliwaomba wananchi wakichague ili kiwafanyie kazi watanzania ambao walikiamini na kukichagua. “Matokeo yake watanzania wameyaona , miundombinu ya barabara, shule na vyuo vimejengwa na watoto wengi hivi sasa wapo mashuleni. Huduma za afya zimeboreka kwa kujengwa Hospitali, vituo vya afya na Zahanati”. Lakini hata kwa yale ambayo hayakuwepo kwenye Ilani na yalikuwa ni matakwa ya wananchi chama chetu sikivu hakikusita kuyakubali kwani yalikuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa na vizazi vyetu”, alisema Mama Kikwete. Kuhusu Katiba inayopendekezwa MNEC huyo alisema itapigiwa kura ya maoni mwaka huu mwezi wa nne hivyo basi aliwataka wanaCCM na watanzania wote kwa ujumla kuipigia kura ya ndiyo katiba pendekezwa kwani inakidhi matakwa ya watanzania kwa kuwa imegusa katika maeneo yote. Akiwasalimia wananchi waliohudhuria sherehe hizo Mkuu wa wilaya ya Lindi Dkt. Nassoro Hamidi aliwahimiza wazazi kuhakikisha watoto walioandikishwa darasa la kwanza na wale waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaenda shule kuanza masomo ili waweze kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao. Katika kilele cha sherehe hizo zilizoenda sambamba na wiki ya Chama na Jumuia zake kauli mbiu yake ni Umoja ni ushindi, Katiba yetu, Taifa letu jumla ya wanachama wapya 448 walijiunga na chama hicho ambapo saba walitoka vyama vya upinzani, Chama cha Wananchi (CUF) watano na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wawili
WABUNGE WAPEWA SEMINA YA USAMBAZAJI WA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012

WABUNGE WAPEWA SEMINA YA USAMBAZAJI WA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012

February 01, 2015

1
Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta ambaye amemuwakilisha Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akifungua Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika mjini Dodoma.
2
Waziri wa Fedha Saada Mkuya akitoa ufafanuzi juu ya maswali ya wabunge.
3
Kamishna wa Sensa Tanzania, Hajjat Amina Mrisho akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo.
4
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiwasilisha mada.
5
Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta ambaye amemuwakilisha Mgeni Rasmi wa Semina hiyo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya.
6
Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye akichangia mada yake.
7
Mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Mohamed Habibu Mnyaa akisisitaza jambo.
8
Waziri wa Sheria na Katiba Selina Kombani akichangia kwenye semina hiyo.
9
Baadhi ya wabunge waliohudhutia semina hiyo.
……………………………..
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma

HII NDIO ILIKUWA KAULI YA WAFANYABIASHARA MKOA WA TANGA BAADA YA JOHNSON MINJA KUSHIKILIWA NA POLISI DAR

February 01, 2015



WAFANYABIASHARA mkoa wa Tanga wiki iliyoipita walilazimika kufunga maduka yao kuanzia asubuhi wakishinikiza kuachiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Johnson Minja anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kuachiwa la sivyo wataendelea na mgomo huo.

Mwenyekiti huyo aliyekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es
Salaam wakati akitokea kwenye kikao cha kuwatetea wafanyabiashara hao kupinga mamlaka ya mapato nchin (TRA) kuwapandishia kodi asilimia 100 wakati wafanyabiashara hao walikubaliana asilimia 2.

Mgomo huo uliweza kuwaathiri wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga ambao wanatoka wilayani kufungasha bidhaa na kujikuta wakishindwa kupata mahitaji ambayo yalikuwa wakitegemea kukutokana na hali hiyo.

Mwandishi wa gazeti hili aliweza kutembea kwenye maduka mbalimbali barabara ya kumi na tatu na kumi na mbili kujione namna wafanyabishara hao walivyokuwa nje ya maduka yao yakiwa wamefungwa wakiendelea kupiga soga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mmoja kati ya wakazi hao,Athumani Jumanne kutoka wilaya ya Pangani alisema kuwa wamepata hasara kubwa kutokana na wao kuingia gharama za kutoka maeneo walipo mpaka kufikia mjini huku wakijua wataweza kufanikisha mipango yao lakini mambo yalikuwa ni tofauti.

Athumani alisema kuwa yeye tegemeo lake kubwa lilikuwa ni kuja kufanya biashara mjini Tanga na kurejea wilayani humo akitegemea malipo atakayoyapata ili aweze kujikimu kwenye usafiri na malazi ili siku inayofuata arejee alipotoka hivyo kufungwa kwa maduka hayo kumemuadhiri sana na hajua nini la kufanya.

Hali kadhalika mfanyabiashara,Alphonce Mboya alisema kuwa kushikiliwa kwa mwenyekiti huyo ni uonevu wanaofanyiwa hivyo kuitaka serikali kuangalia namna ya kumuachia ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku kwa sababu bila ya hivyo wataendelea na mgomo huo.

   “Sisi kama wafanyabiashara tunataka mwenyekiti wetu Taifa aachiliwe popote alipo ili aweze kurejea kwenye utendaji wake wa kila siku…kubwa zaidi tunaiomba serikali kuingilia kati suala hili kwa sababu wafanyabiashara tunanyanyasika “Alisema Alphonce Mboya ambaye ni mfanyabiashara barabara ya tatu jijini Tanga.

Kwa mfanyabiashara, Marry Shio aliiomba serikali kuangalia namna ambavyo wanaweza kuwasikiliza wafanyabiashara kuweza kunufaika na kazi wanazozifanya kuliko kitendo cha kushinikiwa kulipa kodi ambazo hazina maslahi kwao zaidi ya kuwadidimiza.

Shio alisema kuwa kitendo cha Mwenyekiti wao Taifa kushikiliwa na kutokujua mahali sahihi alipo kina wapa uchungu mkubwa kwa sababu serikali haiwezi kumkamata mtu kwa sababu anapiga mfumo wa mashine za mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)EFD.

Akizungumzia mfumo wa mashine za EFD alisema kuwa mashine hizo hazina faida kwao na wala hawatambui mfumo huo kwa sababu unawapa hasara kubwa hivyo wanaiomba serikali kuangalia upya mashine hizo.

    “Wamemkamata mwenyekiti wetu kwa sababu anatetea wanyonge na sisi hatutakubali tutahakikisha tunakuwa naye bega kwa bega mpaka hatua ya mwisho wao ndio walihisi yeye ndio anapinga agizo la kodi hiyo kumbe sivyo “Alisema Marry Shio.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo na wafanyabiashara, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga(JWT) Peter Amosi alisema kuwa kitendo hicho ni uonevu zidi ya kiongozi huyo ambaye ameonekana kuwa mstari wa mbele kuwatetea wafanyabiashara ambao wanajitafutia ridhiki zao kwa njia ya halali.

Alisema kuwa wao kama wafanyabiashara wanacholalamikia ni tozo kubwa ya kodi kupanda mara mia jambo ambalo linawaumiza watu wengi na kushindwa kupiga hatua za maendeleo na kurudi nyuma kila siku.

Aidha alisema kuwa suala jengine ni malipo ya huduma za faya
extengisha ambapo kila mfanyabiashara ambay ana mlango anatakiwa kulipa elfu arobaini kila mwezi wakati ingeweze kukaa nyumba moja ikaweza kuhudumia maduka yote yanayozunguka nyuma hiyo.

WAZIRI WA UJENZI AFUNGUA BARABARA YA IGAWA-RUJEWA KM 9.8

February 01, 2015

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa barabara ya Igawa-Rujewa KM 9.8 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Mbarali.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara hiyo. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro pamoja na viongozi wengine.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza na wakazi wa Ubaruku wilayani Mbarali waliokuwa wanaomba wajengewe barabara ya Rujewa-Ubaruku kwa kiwango cha lami.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katikati akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kuhusu ujenzi wa barabara ya Rujewa-Ubaruku inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo inatarajiwa kuwarahisishia wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao ni wakulima wa mpunga na mahindi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wakazi wa Rujewa na Ubaruku wilayani Mbarali kuhusu ujenzi wa barabara ya Igawa-Ubaruku km 18.
Wakazi wa Rujewa na Ubaruku wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi wakati akiwahutubia.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akifurahia ngoma pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha Rujewa mara baada ya kuwahutubia wakazi wa Rujewa na Ubaruku wilayani Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwahutubia wakazi wa Ubaruku na Rujewa Wilayani Mbarali.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma taarifa ya mradi wa barabara ya Igawa-Ubaruku inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wakazi wa Rujewa na Ubaruku mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 38 YA KUZALIWA CCM MJINI SONGEA LEO

February 01, 2015

Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa viongozi mbali mbali wa CCM wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na UVCCM katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais,Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa CCM wakipokea gwaride la heshima lililoandaliwa na UVCCM katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Gwaride la lililoandaliwa na UVCCM likitoa heshima kwa viongozi katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo wakati wa kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Msanii Diamond akipongezwa na chipukizi wa UVCCM baada ya kutumbuiza katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo,katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM. PICHA NA IKULU.

Yanga yashindwa kufutukuta mbele ya Ndanda,zatoka suluhu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar leo

February 01, 2015

 Mshambuliaji Machachari wa timu ya Ndanda,Masoud Ally akitoa pasi maridadi kabisa mbele ya beki wa timu ya Yanga,Juma Abdul wakati wa mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Mrisho Ngassa wa Yanga akiondoka na mpira huku akifuatwa na Beki wa Ndanda,Paul Ngalema wakati wakati wa mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
 Nyanda wa timu ya Yanga,Ally Mustafa akiwa makini kulilinda lango lake.
 Mshambuliaji wa timu ya Ndanda,Omega Seme akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Yanga,Oscar Joshua mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
 Beki Hasifiwi: Beki wa timu ya Yanga,Rajab Zahir akiruka juu kuondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwao katika mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
 Beki wa timu ya Yanga,Rajab Zahir akiwania mpira na Jacob Massawe wa Ndanda.
 Nadir Haroub wa Yanga akijaribu kuondosha hatari ilikuwa langoni kwake.
 Dan Mrwanda wa Yanga akitafuta namna ya kumtoka beki wa Ndanda,Paul Ngalema.
 Hapiti mtu hapa: ni kama anaonekana kusema  beki wa timu ya Ndanda,Paul Ngalema wakati akimdhibiti Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva.
 ajali kazini.
 Hatariiiii paleee....... daaahh.... wanakosa goli Yanga hapaaa....
 Kocha wa Timu ya Yanga,Hans Van Der Pluijm akifanyiwa mahojiano na Mtangazaji wa Michezo wa Radio Clouds,Issa Maeda.
 Chombo kiko tayari kwa kazi.
 Wadau uwanjani.
 Washabiki wa timu ya Ndanda wakiishangilia timu yao.