Makumbusho ya Tanga kusaidia kurithisha na kuelimisha vizazi asili, historia na umuhimu wa mji wa Tanga

Makumbusho ya Tanga kusaidia kurithisha na kuelimisha vizazi asili, historia na umuhimu wa mji wa Tanga

December 31, 2014

Na, Anna Makange
MJI wa Tanga unaweza kurudisha historia ya umaarufu na umuhimu wake kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kihistoria endapo wakazi wake wataunga mkono kwa dhati juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali kwa kushirikiana na wawekezaji na wadau wengine mbalimbali wa maendeleo.
Harakati mbalimbali zimekuwa zikifanywa na viongozi wa serikali kwa kuwashirikisha wananchi ili kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri kwa lengo la kurudisha hadhi ya Tanga na ustawi wake kwa ujumla.
Jengo la Cliff lililopo katika eneo la Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Jengo hilo ndilo hospitali ya kwanza ya serikali kujengwa nchini wakati wa utawala wa Wajerumani zaidi ya miaka 100 iliyopita. Kwa sasa halitumiki kutokana na kuwepo katika hali mbaya ya uharibifu.
Jengo la Cliff lililopo katika eneo la Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Jengo hilo ndilo hospitali ya kwanza ya serikali kujengwa nchini wakati wa utawala wa Wajerumani zaidi ya miaka 100 iliyopita. Kwa sasa halitumiki kutokana na kuwepo katika hali mbaya ya uharibifu.
Hadhi iliyokuwa imefifia kwa muda hasa baada ya kuanguka kwa shughuli za uzalishaji katika mashamba ya mkonge, viwanda na bandari kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1980.
Kupungua kwa shughuli za kiuchumi pamoja na kuchochewa na kuanguka kwa uzalishaji wa zao kuu la biashara la Mkonge lililokuwa likitegemewa sana kama uti wa mgongo wa uchumi mkoani hapa, pia kulisababisha idadi kubwa ya wakazi kukosa ajira katika mashamba ya Mkonge, viwandani, bandarini na hivyo kuwanyima uhakika wa kipato.
Pia athari hizo kwa upande mwingine zilisababisha kuzorota kwa mwendelezo wa shughuli za kijamii na utamaduni wa asili ya Tanga ikiwemo hali ya kurithishana mila, desturi na utamaduni uliokuwa umestawi miongoni mwa wakazi wake.
Aidha, katika kipindi hicho pia wakazi wa Tanga walishuhudia mabadiliko ya aina mbalimbali yakiwemo ya kufa kwa viwanda, kubadilishwa matumizi ya baadhi ya maeneo yaliyokuwa ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni na kuanza kutumika kwa kazi nyingine tofauti au kutelekezwa kabisa bila kuendelezwa.
Kwa mfano baadhi ya majengo yaliyojengwa zamani wakati wa ukoloni yalibomolewa na kujengwa nyumba mpya za Ghorofa, uvaaji wa mavazi kwa wanaume na wanawake ulibadilika kutoka yale ya asilia na kuingizwa mitindo mipya ambayo imeendelea kubeba majina ya mavazi hayo hayo likiwemo vazi la Buibui.
Mfano mwingine ni Uwanja maarufu wa Sabasaba ulioko eneo la Gofu Juu katika Kata ya Nguvumali ambao ulikuwa ukitumika kwa shughuli za maonesho ya shughuli za kilimo, ufugaji na uzalishaji wa viwanda wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Tanzani yaliyokuwa yakifanyika kuanzia Julai Mosi hadi Saba kila mwaka kabla ya kubadilishwa na kuitwa Nanenane ambayo hufanyika Agosti Mosi hadi Nane kila mwaka.
Birika maalum iliyokuwa ikitumika zamani kuhifadhia kinywaji aina ya kahawa ambacho ni maarufu sana jijini Tanga. Kwa sasa ni aghalabu kuona kifaa(chombo) cha aina hiyo kutokana na kutoweka na wauzaji wengi wa Kahawa kulazimika kutumia chupa za chai(Thermos)au Birika za kawaida za bati/alminiam. Birika hiyo imo ndani ya makumbusho ya Tanga
Birika maalum iliyokuwa ikitumika zamani kuhifadhia kinywaji aina ya kahawa ambacho ni maarufu sana jijini Tanga. Kwa sasa ni aghalabu kuona kifaa(chombo) cha aina hiyo kutokana na kutoweka na wauzaji wengi wa Kahawa kulazimika kutumia chupa za chai(Thermos)au Birika za kawaida za bati/alminiam. Birika hiyo imo ndani ya makumbusho ya Tanga
Eneo hilo la ‘Sabasaba’ Tanga kwa sasa limebaki kuwa jina tu la ki historia kutokana na kubadilika ki matumizi ambapo baadhi ya wafanyabiashara walipangishwa humo uwanjani wanatumia eneo hilo kwa shughuli za kilimo cha bustani za mboga, nyumba za ibada, vilabu vya pombe na biashara ya nyama ya Nguruwe (Kitimoto).
Kwa ujumla hali hiyo ya mabadiliko ya kijamii na kiutamaduni pamoja na kutajwa kwamba ni miongoni mwa hatua za maenedeleo kwa upande mwingine zilidhoofisha kasi ya wenyeji wa mji wa Tanga kutunza na kurithisha mila, desturi na tamaduni zao kutoka kizazi cha wakati huo hadi sasa.
Ni kwa kutambua umuhimu wa jamii kurithisha mila, destruti na tamaduni zake kutoka kizazi kimoja hadi kingine Taasisi isiyo ya kiserikali ya URITHI Tanga iliamua kubeba jukumu hilo ili kuhakikisha utamaduni wa asili unaendelea kudumishwa.
Imeazimia kuelimisha wanajamii na wageni wasio wenyeji wa mji wa Tanga kuhusu mambo muhimu ya kihistoria yaliyokuwepo Tanga kwa kuamua kuanza kukiimarisha kituo maalumu cha Makumbusho ya Tanga ili kuiweka pamoja historia na utamaduni wa mwenyeji wa hapo katika eneo moja linalofikika kwa urahisi.
Taasisi hiyo ya URITHI Tanga ilianzishwa mwaka 1998 kwa shabaha ya kufufua, kukusanya taarifa na kuhifadhi kumbukumbu za majengo, miundombinu, tamaduni, mila na desturi za mswahili wa Tanga na makabila mengine yaliyomo ndani ya makumbusho.
Lengo ni kuusaidia mkoa kuendelea kutangaza Utalii na urithi wa kiasili wa Tanga kitaifa na kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya vizazi vilivyopo na vijavyo vya wakazi wake na taifa kwa ujumla.
Wazo lililosababisha kuanzwa kwa mchakato wa uwepo wa makumbusho ya Tanga inaelezwa kwamba lililetwa na baadhi ya wazawa ambao waliona kwamba kuna umuhimu wa kufanya hivyo hasa baada ya kubaini kasi ya upoteaji wa urithi wa kiasili na vitu vya kihistoria vilivyoanzia Tanga kabla ya maeneo mengine nchini.
Alhaj Abdalah Majura ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo ya Urithi Tanga amezungumza na Mwandishi wa makala haya akisema ilipofika katikati ya miaka ya 1990 walibaini kwamba idadi kubwa ya vitu vilivyokuwa vikinakshi historia ya Tanga vilikuwa vikipotea kwa kasi ya ajabu.
“Vitu hivyo vinajumuisha majengo ya aina mbalimbali yaliyojengwa katika zama tofauti za ukoloni ambayo katika kipindi hicho yalikuwa yakiathiriwa na kasi ya ujenzi wa nyumba za kisasa na majengo mengine ya ghorofa…. hasa kwa kuyavunja majengo hayo ya zamani ili kutumia maeneo hayo kwa kujenga mapya” kisasa, anaeleza.
Anataja sababu nyingine kwamba ni kuibuka kwa biashara ya vifaa na samani mbalimbali zilizokuwemo katika majengo ya zamani yaliyojengwa na wakoloni.
Jengo la Cliff lililopo katika eneo la Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Jengo hilo ndilo hospitali ya kwanza ya serikali kujengwa nchini wakati wa utawala wa Wajerumani zaidi ya miaka 100 iliyopita. Kwa sasa halitumiki kutokana na kuwepo katika hali mbaya ya uharibifu.

Samani na vifaa hivyo vya zamani vilijumuisha saa za ukutani, milango, madirisha na taa za karabai ambavyo watu wasiojulikana kwa makusudi walikuwa wakivamia majengo yaliyoko katika maeneo mbalimbali ya mji na kuviiba kasha kuvitorosha nje ya nchi kwa lengo la kuviuza.
Shughuli nyingine zilihusisha kazi ya uharibifu wa mazingira uliojumuisha vitendo vya ukataji wa miti ikiwemo ya aina ya ‘Mikanju’(Mikorosho) katika eneo la Mikanjuni na ‘Mitiki(iliyokuwa na majani mapana)’ katika eneo la MajaniMapana kwa ajili ya kupata maeneo ya ujenzi (viwanja) na mbao na kusababisha maeneo hayo kubaki na majina ya ki historia tu tofauti na umuhimu wa uoto wa asili uliokuwemo ambao umesadifi majina ya maeneo hayo.
Anasema kulikuwepo pia na utekelezaji wa shughuli za kilimo hasa uzalishaji wa Mkonge, uvaaji wa mavazi kama Buibui, Mapishi yaliyoambatana na ulaji wa Vyakula vya asili kwa kutumia vifaa(vyombo) vya asili pamoja na uvuvi.
“Tanga ulikuwa mji muhimu sana uliowahi kufanikiwa ki maendeleo kabla na baada ya kuja kwa wakoloni, ki ukweli histotia nyingi za Tanzania kwa ujumla zina mahusiano ya karibu sana na maeneo ya mkoa huu kutokana na kuunganishwa moja kwa moja na mji wa kihistoria na vijiji vya Tanga”.
“Kwa mfano katika enzi ya utawala wa Wajerumani walihusisha sana Tanga kwa mfumo wake wa kiuongozi uliotumia Maliwali, Maakida na Makadhi pamoja na kujenga majengo mengi makubwa katika mji wa Tanga”.
Alitaja baadhi ya majengo hayo ambayo yalijengwa jijini Tanga wakati wa utawala wa wakoloni wa Kijerumani ni Hospitali ya kwanza ya serikali “Cliff Block’ ambayo sasa inafahamika kama Hospitali ya Bombo.
Cliff Block ilijengwa katika kipindi cha zaidi ya mika 100 iliyopita wakati wa utawala wa Wajerumani kwa sasa jengo hilo halitumiki hasa baada ya serikali kujenga majengo mengine ya kisasa zikiwemo gorofa na nymba za kawaida ambayo hutumika kwa shughuli za Hospitali ya mkoa wa Tanga. Jengo hilo kwa sasa lipo kwenye hali mbaya ya uharibifu.
Majengo mengine yalihusisha sekta ya elimu ambapo wakoloni hao wa Kijerumani walijenga Sekondari ya kwanza ya serikali nchini ambayo ilifahamika kama ‘Tanga School’.
Shule hiyo ya ki historia ilijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na sasa inafahamika kama Old Tanga Secondary School na inamilikiwa na Halmashauri ya jiji.
Majura anataja vitu vingine vya ki historia vilivyoanzishwa Tanga na baadae kuenezwa katika maeneo mengine nchini ni kilimo cha Zao la Mkonge ambalo alisema kwa mara ya kwanza lilianza kupandwa katika kijiji cha Kikokwe kilichopo jijini humo.
“Kwa mara ya kwanza barani Afrika wakulima wa Kikoloni kutoka Mexico waliamua kubeba miche 1,000 ya mkonge ili kuja kufanya utafiti wa kuanzisha kilimo hicho huku Afrika Mashariki.
“Kutokana na safari ndefu na misukosuko ya njiani ni miche 62 tu kati ya miche yote ndiyo ilifika salama katika pwani ya bahari ya Hindi eneo la Tanga na kupandwa hapo Kikokwe kabla ya kuanzishwa mashamba makubwa baadae”.
Aidha, anasema pamoja na kutambua vitu hivyo vya kihistoria ambavyo ki msingi havikuwa katika eneo moja ndipo taasisi ya Urithi ikaona umuhimu mkubwa wa kuvihifadhi hasa kwa kuunganisha shughuli zote hizo katika eneo moja la Makumbusho ya Tanga.
Makumbusho ya Tanga inapatikana pembezoni mwa barabra ya Uhuru kwenye jengo lililokuwa la Ofisi ya mkuu wa wilaya kabla na baada ya uhuru na baadae likatumika kama ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Tanga miaka kadhaa baada ya uhuru wa Tanzania.
Jengo hilo lililopo jirani na makataba ya mkoa wa Tanga ni miongoni mwa maeneo ya historia ambayo yaliwahi kusahauliwa na kuanza kuhujumiwa na watu hao wasiojulikana hadi katikati ya miaka ya 2000 taasisi hiyo ilipofanikiwa kulichukua na kuanza kulikarabati.
mwonekano wa nje wa Makumbusho Tanga
mwonekano wa nje wa Makumbusho Tanga
Ukarabati wa jengo hilo ulifanywa kwa awamu kwa ufadhili wa shilingi Milioni 35 kutoka Ubalozi wa Ujerumani pamoja na majengo mengine ikiwemo mahakama ya mwanzo ya Usambara, mnara wa Saa ulioko jirani na benki ya CRDB.
Majura anasema madhumuni ya kuanzishwa kwa makaumbusho hayo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa kujaribu kuonesha maisha, makazi(majengo), historia ya Tanga, mila, ngoma za asili pamoja na habari muhimu za Tanga.
Pia kuelezea kwa ufasaha historia ya masuala mbalimbali ukiwemo uchumi wa Tanga ambao ulitegemea Mkonge, watu maarufu kama Shaaban Robert, Makata Mwintwana, Kihere, Kadhi Ali bin Hemed ambaye ndiye baba yake Mufti wa kwanza Tanzania ambaye alitokea Tanga.
Aidha, anasema Mkumbusho hiyo itahifadhi alama hizo ili kuendeleza historia halisi na maana ya Tanga kwa kutumia mbinu mbalimbali zikiwemo kuwajegea ufahamu mara kwa mara viongozi wa ngazi mbalimbali katika serikali za mitaa, serikali kuu, wanafunzi na vyombo vya habari ili kuongeza uhamasishaji.
Naye Joel Niganile ambaye ni mmoja wa watumishi katika makumbusho ya Tanga alisema kuanzishwa kwake kuwezesha kutoa fursa ya kuongeza ufahamu kwa wananchi hasa wakazi wa jiji la Tanga.
“Pia wageni kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wanatutembelea mara kwa mara kwa lengo la kuangalia na kupata taarifa mbalimbali muhimu zilizopo ndani ya makumbusho.
Hata hivyo Majura anasema licha ya kupata mafanikio hayo makumbusho hiyo bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo bajeti ya uhakika ya kuendesha utendaji wa kila siku hasa kwakuwa bado hawajakamilsha kazi ya kuingiza vitu vyote vya kihistoria kutoka katika maeneo yake ya asili.
“Kwa sasa bado tunalazimika kuendelea kutegemea sana wafadhili na mchango mdogo kutoka kwa wafanyabishara na kampuni binafsi za hapa jijini Tanga hivyo kushindwa kujitegemea na kujikimu ki mahitaji”,anaeleza.
Anasema changamoto nyingine ni uelewa mdogo miongoni mwa wananchi hasa kutambua kwamba majengo ya zamani yanathamani na wanawajibiika kuyatunza badala ya kuthamini ujenzi wa nyumba za kisasa naza gorofa ambazo zinabadilisha mwonekano wa asili wa mji.
“Pia tunakabiliwa na uhaba mkubwa wa watendakazi katika makumbusho haya ambako hivi sasa tupo watu wane tu ambao ki msingi tunafanya kazi kwa kujitolea”.
Majura anahimiza kwamba kuna haja kwa wakazi wa Tanga na vitongoji vyake kuanza kuuunga mkono harakati hizo ili kuwezesha makumbusho ya Tanga kufikia lengo lake ililokusudia.
Aidha, ni wakati muafaka umefika kwa serikali, wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanajitoa na kutumia fursa hiyo ya makumbusho kupeleka taarifa sahihi na vifaa muhimu vya kihistoria ili kuiwezesha makumbusho hiyo kusheheni vitu hivyo tofauti.
Ni vema baadhi ya wakazi ambao wamebahatika kuendelea kuhifadhi au kumiliki vitu vya asili ya Tanga na vya historia yake kwa ujumla kuviwasilisha hapo Makumbusho na kuachana na tamaa ya kutafuta wateja wa kuwauzia kama baadhi yao wanavyoendelea kufanya hivi sasa kwa siri.

TMA YATOA TAARIFA JUU YA MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA JANUARI, FEBRUARI, 2015 NCHINI

December 31, 2014


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Agnes Kijazi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, kuhusu mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha Januari na Februari, 2015 nchini. Kushoto ni Mkurugenzi, Huduma za Utabiri, Dk.Hamza Kabelwa.
Wana habari wakiwa kwenye mkutano huo leo
………………………………………………………………..
Habari kwa hisani ya  mtandao wa www.habari za jamii.com
SIKU moja baada ya mvua kubwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha madhara Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa za vipindi.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Agness Kijazi Dar es Salaam jana wakati akiwasilisha tathmini ya mvua za vuli kuanzia Ocktoba hadi Disemba mwaka huu na mwelekeo wa mfumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi cha Januari na Febduari 2015.
Alisema kutokana na mifumo iliyopo ya hali ya hewa inatarajiwa kusababisha vipindi vya ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo ya Magharib kwenye mikoa ya, Nyanda za juu Kusini-Magharibi na mikoa ya Kusini mwa nchi kuanzia Januari na Febduari 2015.
Hata hivyo alisema kuwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka hususan Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki, Pwani ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa Viktoria na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma mvua zinatarajia kuisha mwishoni mwa Disemba mwaka huu.
Alisema matukio ya mvua katika maeneo ya mvua za nje ya msimu yanatarajiwa katika kipindi cha miezi ya Januari 2015.Hali hiyo inatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Kusini mwa Mkoa wa Pwani na baadhi ya meneo ya Mikoa Arusha , Manyara, Kagera, Geita, Shinyanga na Mwanza.
Dk. Kijazi alisema katika maeneo mengine yaliyosalia yanatarajia kuwa makavu huku maeneo ya Magharibi mwa nchi, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini-Magharibi, Kusini mwa nchi na Pwani ya Kusini ambayo yanayopata msimu mmoja wa mvua yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.
“Izingatiwe kuwa pamoja na kuwepo kwa uwezekano wa matukio mengi ya mvua kubwa katika maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani, hali hiyo pia itajitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani,” alisema.
Aliongeza kuwa matukio ya vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa bahari hindi yanatarajiwa kuchangia katika mwenendo wa mvua nchini.
“Maeneo ambayo hali ya mvua inaweza kuathiriwa zaidi na vimbunga ni pamoja na kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, magharibi mwa nchi na maeneo ya ukanda wa Pwani,” alisema.
HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

December 31, 2014


AZAM, MTIBWA, SIMBA, YANGA KUCHEZA MAPINDUZI
Timu za Azam, Mtibwa Sugar, Simba na Yanga zitashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika kisiwani Zanzibar kuanzia Januari 1 hadi 13 mwakani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ruhusa kwa timu hizo kucheza mashindano hayo baada ya kuhakikishiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kuwa kesi iliyofunguliwa dhidi ya viongozi wake imeondolewa mahakamani.
Kutokana na timu hizo kushiriki Kombe la Mapinduzi, mechi zao za raundi ya tisa na kumi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitachezwa katikati ya wiki baada ya kumaliza mechi zao za michuano hiyo.

Hivyo mechi za VPL ambazo hazitachezwa wikiendi hii ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar, Mbeya City na Yanga, na ile kati ya Mgambo Shooting na Simba. Mechi za wikiendi ijayo zinazopisha michuano hiyo ni kati ya Kagera Sugar na Azam, Coastal Union na Yanga, Mbeya City na Simba, na Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons.
18 WAPATA BEJI ZA UAMUZI FIFA
Waamuzi 18 wa Tanzania wamepata beji za uamuzi za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2015.
Idadi hiyo ambayo ni rekodi kwa Tanzania inahusisha waamuzi saba wa kike. Waamuzi wa kati wa kike waliopata beji hizo ni pamoja na Jonesia Rukyaa Kabakama aliyechezesha mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga. Wengine ni Florentina Zablon Chief na Sophia Ismail Mtongori.
Waamuzi wasaidizi wa kike waliopata beji hizo ni Dalila Jafari Mtwana, Grace Wamala, Hellen Joseph Mduma na Kudura Omary Maurice.
Kwa waamuzi wa kati wa kiume ni Israel Mujuni Nkongo, Martin Eliphas Sanya, Mfaume Ali Nassoro na Waziri Sheha Waziri. Waamuzi wasaidizi ni Alli Kinduli, Ferdinand Chacha, Frank John Komba, John Longino Kanyenye, Josephat Deu Bulali, Samuel Hudsin Mpenzu na Soud Iddi Lila.

Matukio ya kutishia amani ya nchi na usalama wa raia yatapungua kama mabalozi wa nyumba kumi watafanya kazi zao kwa uaminifu - Vuai Ally Vuai

December 31, 2014

Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi

Matukio ya kutishia amani ya nchi na usalama wa raia yatapungua kama mabalozi wa nyumba kumi watafanya kazi zao kwa uaminifu kwani wao ni viongozi wa kwanza walio karibu na wananchi hivyo basi wanatakiwa kuwafahamu wakazi wa maeneo yao.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Vuai Ally Vuai wakati akifungua semina ya siku moja ya  uwezeshaji wa chama hicho kwa  mabalozi (viongozi wa mashina) wa wilaya ya Lindi mjini.

Vuai alisema Balozi ni kiongozi wa kwanza anayetakiwa kujua idadi ya wakazi wake, kazi wanazozifanya na majina yao kitendo ambacho kitasaidia kuimarisha usalama wa eneo husika lakini miaka ya hivi karibuni wameacha kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na kuviachia vyombo vya dola pekee.

“Jukumu la kulinda amani ya nchi na usalama wa taifa letu ni la kila mtu, lakini hivi sasa kazi hiyo vimeachiwa vyombo vya dola pekee, mabalozi fanyeni kazi ya kuwatambua wakazi wa maeneo mnayoishi hii itasaidia kumtambua mualifu pale atakapofika katika eneo lenu”, alisema Vuai.

Alisema kikao cha kwanza cha CCM ni kikao cha shina hivyo basi mabalozi ni viongozi wa muhimu ndani ya shina wanatakiwa kutetea ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 na kutowaachia viongozi wakuu wa chama pekee kufanya kazi hiyo.

Vuai alisisitiza, “Muwe na uthubutu wa kujibu hoja potofu za wapinzani na kutokubali wawapotoshe wananchi juu ya mafanikio yaliyofanywa na Serikali. Kipindi cha uchaguzi kikifika endeleeni kuwahimiza na kuwasimamia wananchi wakapige kura ili wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga kura”.

Aliwataka mabalozi hao kuhakikisha wakati wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo mwakani wawahimize  wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi kujiandikisha majina yao.

unnamed1
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai (wa kwanza kushoto) wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa semina ya uimarishaji Chama kwa mabalozi wa Lindi Mjini tarehe 29.12.2014.
unnamed2
unnamed3
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akifungua rasmi semina ya siku moja ya kuimarisha Chama kwa mabalozi wa Lindi Mjini tarehe 29.12.2014.
unnamed4
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akifungua rasmi semina ya siku moja ya kuimarisha Chama kwa mabalozi wa Lindi Mjini tarehe 29.12.2014.

unnamed5
Baadhi ya washiriki wa semina ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi kwa mabalozi wa Lindi Mjini wakifurahia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai wakati akifungua semina hiyo huko Lindi tarehe 29.12.2014.
unnamed7
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM Mama Salma Kikwete akiaagana na Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi rasmi wa semina ya siku moja ya mabalozi wa Lindi Mjini tarehe 29.12.2014.
unnamed8
Baadhi ya watoa mada (waliokaa mstari wa mbele) kwenye semina ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya mabalozi wa Lindi Mjini tarehe 29.12.2014.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete alisema mabalozi ni msingi na nguzo ya chama bila ya mabalozi chama hakiwezi kwenda vizuri ni kama vile binadamu anaweza kuwa na kila kitu lakini kama hana miguu hawezi kutembea.

Aliwapongeza kwa ushindi walioupata wakati wa uchaguzi wa Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za mitaa na kusema kuwa upendo na mshikamano ni msingi wa ushindi na usiri na uadilifu ni nyenzo muhimu katika utendaji wao wa kazi.

“Katika semina hii mtafundishwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kazi na wajibu wenu kwa Chama na Jamii inayowazunguka hivyo basi muwe wasikivu na kuyashika yale mtakayofundishwa na watoa mada”, alisisitiza Mama Kikwete.

Akiongea kwa niaba ya wajumbe walioshiriki semina hiyo Rashid Thabit kutoka kata ya Rahaleo alishukuru kwa mafunzo waliyoyapata na kusema kuwa yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi.

“Tunakushukuru MNEC kwa ajili ya kuandaa mafunzo haya ambayo yametupa uelewa na wajibu na kazi zetu kama mabalozi. Uwepo wako wakati wa uchaguzi uliopita ulitufanya tukashinda kwani tulishiriki pamoja nawe katika kampeni za kuwanadi wagombea wetu”.

Nawaomba wajumbe wenzangu tusibweteke na ushindi huu bali tuongeze kasi na bidii na kuweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo mwakani ili tuweze kulikomboa jimbo la Lindi mjini kutoka mikononi mwa Chama Cha Wananchi (CUF)”, alisema Thabit.

Semina hiyo ya siku moja iliyohudhuriwa na wajumbe 993 kutoka kata zote 18 za wilaya hiyo iliandaliwa na Mama Kikwete ambaye aliwaahidi mabalozi kuwapa mafunzo hayo ili wajue majukumu yao ya kazi. Mada zilizojadiliwa ni kazi na wajibu wa mabalozi na katiba mpya iliyopendekezwa.
MAHABUSU APIGWA RISASI AKIJARIBU KUTOROKA MAHAKAMA YA KISUTU

MAHABUSU APIGWA RISASI AKIJARIBU KUTOROKA MAHAKAMA YA KISUTU

December 31, 2014


unnamed 
Mahabusu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa amenasa kwenye ukuta wa chuma baada ya kupigwa risasi na maaskari wakati alipokuwa akijaribu kutoroka kwa kuruka ukuta huo katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam, inadaiwa  mahabusu huyo ambaye si raia wa Tanzania alikuwa anakabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya.
unnamed2
Baadhi ya askari na watu mbalimbali wakiangalia tukio hilo lililotokea leo asubuhi katika mahakama ya kisutu
unnamed1
Maaskari wakimtoa kwenye ukuta huo wa chuma
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA AHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2014 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2014, MAKAO MAKUU YA MAGEREZA, D’SALAAM

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA AHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2014 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2014, MAKAO MAKUU YA MAGEREZA, D’SALAAM

December 31, 2014

 Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba yake fupi katika Baraza la kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Magereza, Mmeta Manyala. unnamed1 
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza. unnamed2 
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa neno la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(katikati) mara baada ya kutoa hotuba fupi katika Baraza la kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2015. unnamed3 
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu Watumishi wenzao ambao wametangulia mbele ya haki kwa mwaka huu 2014.
………………………………………………………………………………..
Na Inspekta Lucas Mboje, Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza nchini kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika utendaji wao wa kazi za kila siku ili kuleta ufanisi kazini.
Kamishna Jenerali John Minja ameyasema hayo leo wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka 2015 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Magereza Mkoa wa D’Salaam.
Aidha, amewataka Maofisa, Askari na Watumishi wote kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea bali wawe wabunifu kwa kutumia raslimali zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo.
” Kila mmoja wenu atimize wajibu wake katika eneo lake la kazi kwa bidii, ari na moyo wa kujituma ili kuliwezesha Jeshi kupata ufanisi unaotarajiwa”. Alisisitiza Jenerali Minja.
Wakati huo huo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja pia ametumia fursa hiyo kuelezea baadhi ya mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa Mwaka uliopita 2014 ambapo Jeshi la Magereza limepata jumla ya leseni 102 za uchimbaji wa madini ya ujenzi kama vile chokaa, mawe, kokoto, mchanga na Murram katika maeneo mbalimbali ya magereza ambayo ni Gereza Wazo Hill – D’Salaam, Gereza Msalato – Dodoma, Kambi Bahi – Dodoma, Gereza Maweni – Tanga, Gereza Lilungu – Mtwara, Gereza Butimba – Mwanza na Gereza Kalilankulukulu – Katavi. Leseni hizo zitatumika kuingia ubia na wawekezaji wenye nia ya kushirikiana na Jeshi katika uchimbaji wa madini.
Pili, Shirika la Magereza limeeingia Mkataba wa ubia na Kiwanda cha Saruji Wazo (Twiga Cement) katika uchimbaji wa madini ya ujenzi Gereza Wazo Hill. Aidha, Kiwanda hicho katika kutekeleza wajibu kwa jamii wametoa msaada wa mifuko ya saruji 1200 na Tzs.100, 000, 000.00 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Gereza Wazo Hill. Pia Shirika la Magereza limeingia makubaliano na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF kwa ajili ya ujenzi na uendeshaji wa vituo vya biashara (business malls) kwenye maeneo ya Gereza Kihonda, Morogoro na Gereza Karanga, Moshi. Tatu, Rasimu ya kwanza ya Sera ya Taifa ya magereza imekamilika na tayari imewasilishwa kwenye mamlaka za juu kwa hatua zaidi. Kukamilika kwa sera hiyo kutawezesha Jeshi kutekeleza Mpango Mkakati wa Sera na Maboresho ya Jeshi kwa ujumla.
Pamoja na Mafanikio hayo, Kamishna Jenerali Minja ameelezea maeneo yatakayopewa kipaumbele kwa Mwaka huu wa 2015 ikiwemo Jeshi litaendeleza jitihada za kuimarisha na kuongeza uzalishaji kwenye miradi mbalimbali ya Jeshi la Magereza. Jitihada hizi ni pamoja kutangaza fursa zilizopo ili kuwavutia wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi waje kuingia ubia katika miradi hiyo kwa kuleta mitaji na teknolojia, pia Kuendeleza mikakati ya kupunguza msongamano magerezani
Baraza la kufunga Mwaka na kuukaribisha Mwaka unaofuata ni utamaduni wa siku nyingi ambao unaenziwa na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Magereza. Baraza la aina hii hufanyika kila Mwaka ambapo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini hupata fursa ya kuongea na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini kupitia Baraza hilo lengo ikiwa ni kufanya tathmini ya yale yaliyojiri katika Jeshi kwa kipindi cha Mwaka unaisha kwa kuzungumzia mafanikio na changamoto zilizojitokeza na kutazama matarajio ya Mwaka mpya.

Miss Tanzania 2014 asaidia kituo cha New Life Orphans Home,Boko jijini Dar

December 31, 2014

Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akimkabidhi zawadi ya mwaka mpya Msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko, Mwanaisha Magambo kwa ajili ya watoto 102 waliopo kituoni hapo, tukio hilo lilifanyika juzi.
Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na Miss Kinondoni Maria Shila wakiwa wamembeba mtoto aliekuwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life cha Boko, mtoto huyo alifikishwa hapo akiwa na siku nne tu tangia kuzaliwa kwake.
Sehemu ya Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko,wakimsikiliza Miss Tanzania Lilian Kamazima.
Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na watoto katika kituo cha New Life cha Boko.

Redds Miss Tanzania 2014 Lilian Deus Kamazima jumapili iliyopita alitoa misaada ya vyakula vya aina mbalimbali kwa kituo cha New Life Orphans Home kilichopo eneo la Boko nje kidogo ya jiji la D’salaam. 

Kituo hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2005 awali kilikuwa maeneo ya magomeni makuti kilianza na watoto yatima 17 na baadae kuongezeka hadi kufikia 70. Na kulazimika kuhama eneo hilo na kuhamia kigogo ambapo waliishi eneo hilo hadi hivi karibuni walipopata mfadhili mmoja kutoka nchini Qatar ambaye amewajengea jumba moja kubwa na la kisasa eneo la Boko Dawasa, alisema bi Mwanaidi Magambo ambaye ni Mlezi wa Kituo hicho. 

Kituo hicho kina watoto wapatao 105 ambapo  60 kati yao ni wasichana na 45 wavulana. Kituo hicho kinalea watoto wadogo kabisa wa umri wa mwezi mmoja hadi miaka 18. Hivi karibuni tulimpokea mtoto mwenye umri wa siku 5 kutoka hospitali ya wilaya ya Temeke ambaye mama yake alifariki mara tu baada ya kujifungua, alisema bi. Magambo. 

Kituo hicho kwa sasa kina matatizo ya vyakula, vitanda, magodoro, madaftari pamoja na sare za shule kwa ajili ya watoto hao yatima. Bi Magambo alimshukuru sana Mfadhili huyo kutoka nchi ya Qatar kwa kuwajengea jengo hilo, lakini alisema kwa sasa watahitaji mfadhili wa kuwalipia bili za umeme na maji pamoja na mahitaji mengine kituoni hapo. 

Kituo hicho kina bahati ya kutembelea na warembo wa Miss Tanzania ambapo mwaka 2007,  Miss Tanzania 2000 Jacqueline Ntuyabariwe alitembelea kituo hicho wakati bado wapo eneo la Magomeni Makuti na kuwapatia misaada mbalimbali. 

Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima alikabidhi vyakula vya aina mbalimbali ikiwemo mchele, unga wa ngano, sembe, sukari, maharage, mafuta ya kupikia, sabuni, soda, juisi, maji ya kunywa, na biskut vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mbili. 

Miss Tanzania 2014 Lilian aliishukuru kampuni ya Swissport Tanzania ambao ndio waliofadhili ziara yake hiyo, na kuwaomba watanzania wengine kujitokeza kwa wingi kusaidia watoto yatima na wengine wanaoishi katika mazingira magumu. 

Ziara hiyo ya mrembo wa Taifa Lilian ilikuwa ni zawadi ya sikukuu za mwisho wa mwaka ambao ililenga kuwafariji watoto waliopoteza wazazi wao kwa namna moja au nyingine, na pia kutimiza Kauli mbiu ya mashindano ya urembo ya Miss Tanzania isemayo [Beauty with Purpose] Urembo na Malengo.

Bayport yamjaza manoti mwanafunzi wa MUCE

December 31, 2014

Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akizungumza jambo katika makabidhiano ya hundi kwa bwana  Kennedy Kaupenda kushoto kwake, Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii. Picha zote na Mpigapicha Wetu.

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM 
TAASISI ya kifedha ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania, imempatia Sh Milioni tatu mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.

Huduma hiyo mpya ya Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania ilianza mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya mzazi aliyejiunga na huduma hiyo kufariki Dunia.

Mwanafunzi wa MUCE, Kennedy Kaupenda kushoto, akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi yake ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye Bima ya Elimu inayoendeshwa na Bayport. Kulia kwake ni Mratibu wa Bima hiyo, Ruth Bura.   

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima ya Elimu inayotolewa na Bayport Tanzania, Ruth Bura, alisema Kaupenda alitajwa kama mnufaika kwa mzazi wake aliyefariki Dunia, hivyo waliamua kumtafuta kwa ajili ya kumpatia mafao yake kwa ajili ya kuendelea kupata elimu bila vipingamizi vyovyote.

Alisema huduma hiyo ina vipengele vine ambavyo ni Bronze, Gold, Silver na Exucutive, huku akisema kuwa makato ya kila mwezi ya Bronze ni Sh 2,500, ambapo fao lake ni Sh Milioni 3, wakati makato ya Gold ni Sh 6,250, huku fao lake likiwa ni Sh 7,500,000.
Ruth Bura, Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania kulia akimkabidhi hundi bwana Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu baada ya kufariki mzazi wake.

Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura, kulia akizungumza jambo baada ya kumkabidhi Kaupenda hundi ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye huduma hiyo mpya iliyoanzishwa kwa ajili ya kukamilisha ndoto za elimu kwa uwapendao.

“Pia tunacho kipengele cha Silver ambapo makato yake kwa mwezi ni Sh 3,800, huku mteja akilipwa fao la Sh Milioni 4,500,000 na kipengele cha Executive kikihusisha makato ya Sh 9,000 na kumpatia mteja fao la Sh 10,800,000, huku tukiamini kuwa huduma hii ni sehemu ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanawawekea ulinzi wa elimu watoto wao na yoyote wanayemchagua wao,” alisema Ruth.

Akizungumzia fao hilo, Kaupenda alisema hakuwa na imani kuwa angesoma vizuri baada ya baba yake kufariki, ila baada ya kutafutwa na Bayport na kutaarifiwa juu ya mafao hayo, amepata nguvu mpya.

Kennedy Kaupenda akitafakari baada ya kuiona hundi iliyoandaliwa kwa ajili yake kutoka Bayport Tanzania juu ya fao la Bima ya Elimu.
 
“Nasikitika sana baba kwa kunificha juu ya kujiunga na huduma hii sambamba na kuwa mkopaji wa Bayport, hata hivyo namshukuru kwasababu fedha hizi zimekuja kunipa mwanga mpya wa kuhakikisha kuwa nasoma kwa bidii, nikiamini kiasi cha Sh Milioni tatu kitaniweka katika wakati mzuri mno,” alisema Kaupenda, huku akiwasisitiza wazazi kujiunga kwenye huduma hiyo kwa manufaa ya familia zao.

Mbali na huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao, pia Bayport inajihusisha na mikopo kwa watumishi wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, ambapo mwishoni mwa mwaka 2014 walizindua huduma ya Mikopo ya Bidhaa, ambapo bidhaa za bodaboda aina ya Lifan, Toyo na Boxer zinakopeshwa kwa wateja wa Bayport Tanzania.