*KAMAZI ZA BUNGE MAALUM ZAWASILISHA MAONI YA SURA YA KWANZA NA SITA YA RASIMU YA KATIBA MPYA

April 11, 2014


 Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba kumi (10) Salmin Awadh Salmin, akiwasilisha uchambuzi wa Kamati yake wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya jana mjini Dodoma.
 Msemaji wa walio wachache wa Kamati namba kumi (10) Profesa Ibrahim Lipumba, akiwasilisha maoni ya wachache kuhusu sura ya kwanza na sita ya Katiba mpya jana mjini Dodoma.

*BALOZI IDDI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI YA KUU YA TAIFA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA 2012 MJINI DODOMA

April 11, 2014

 Mwenyekiti mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiendesha Kikao cha Kamati hiyo kilichokutana katika Ukumbi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa { TAMISEMI } Mjini Dodoma.
 Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao ni Wajumbe wa KamatiI Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania wakiendelea na Kikao chao Mjini Dodoma. Kutoka Kulia ni Waziri wa Habari M,h. Said Ali Mbarouk, Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mh. Zainab Mohd, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omar KLheir pamoja na Waziri wa Nchi Ofiisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Mwinyihaji Makame.

*LIONS CLUB YAMTUNUKU RAIS KIKWETE MEDALI YA UONGOZI BORA

April 11, 2014


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Balozi wa Canada nchini Mh.Alexandre Leveque na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Gavana wa Shirika la Lions Club nchini Bwana Wilson Ndesanjo akimvika Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete medali maalum ya Uongozi Bora na mahusiano mema wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Bwana Ndesanjo alisema klabu hiyo imeamua kumtunuku Rais Kikwete medali hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini katika Nyanja mbalimbali kutokana na uongozi wake mahiri.

WANANCHI WASISITIZWA KUWEKEZA KATIKA MIRADI YA GESI NCHINI.

April 11, 2014


 Mwandishi wa kitabu kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji ya hapa Tanzania yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia, Bi. Neema Lugangilra Apson,  akielezea maudhui ya Kitabu chake kwa wageni waalikwa  (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiteta Jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue jana wakati wa uzindizi wa kitabu cha “Local Content in Supplier Development” kilichoandikwa na Neema Lugangilra Apson.

MAADHIMISHO YA SOKOINE NI KESHO: MBUNGE WA MONDULI MHE. EDWARD LOWASSA AKAGUA MAANDALIZI YA SOKOINE DAY, MONDULI JUU, ARUSHA

April 11, 2014
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa watoto wa Marehemu Edward Sokoine aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Namelok Sokoine (MB) na Joseph Sokoine ambaye ni Afisa katika Ubalozi wa Tanzania nchini Canada, kuhusiana na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli,Marehemu Edward Moringe Sokoine, yatakayoadhimishwa kesho April 12. Rais Jakaya Kikwete ataongoza maadhimisho hayo pamoja na marais na mawaziri wakuu wastaafu.

KINANA AMALIZA KWA KISHINDO ZIARA YAKE WILAYANI BUHIGWE LEO, AKAGUA MIPAKA YA TANZANIA NA BURUNDI KWENYE WILAYA HIYO NA KUAGIZA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAENEO YA MIPAKANI NCHINI KUBORESHA MAISHA YA WATU

April 11, 2014


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma leo Alhamisi, Aprili 10, 2014. Kinana yupo katika ziara ya siku tano mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani humo. Moja ya kero kwenye mpaka huo unaokutanisha vijiji vya Kibande (Tanzania) na Murambi (Burundi) ni Watanzania kulazimika kukumbana na adha ya kuvuka mto huo kwenda kufanya biashara na kununua mahitaji kwenye soko lililopo upande wa Burundi. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Kinana akitazama mpaka huo na namna wananchi walivyokuwa wakivuka na wengine kushwa kwenye mto wa Malagarasi wakitoka Burundi kuingia Tanzania
AUNT ATIMULIWA KWA WEMA NA MARTIN KADINDA, SOMA MCHONGO MZIMA HAPA.

AUNT ATIMULIWA KWA WEMA NA MARTIN KADINDA, SOMA MCHONGO MZIMA HAPA.

April 11, 2014

Stori: iMELDA MTEMA
TIMBWILI la aina yake limetokea nyumbani kwa ‘Beautiful Onyinye’ wa Bongo, Wema Sepetu, kati ya Martin Kadinda na nyota wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel, ‘Kubwa’ lina kisa klizima.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, gogoro zima lilishika nafasi asubuhi ya Aprili 6, 2014 nyumbani kwa Wema, Makumbusho jijini Dar es Salaam, kufuatia Kadinda ambaye ni meneja wa Wema kumvurumishia shutuma Aunt akidai ni mnafiki mkubwa, tena ndiye chanzo cha Kajala Masanja na Wema kutibuana huku akimtaka aondoke.
TWENDE POLEPOLE

TAZAMA PICHA 3: RAY C ALIVYO MTEMBELEA IBRA DA HUSTLER WA NAKO2NAKO KATIKA KITUO CHA WALIOATHIRIWA NA MADAWA YA KULEVYA KIGAMBONI JIJINI DAR

TAZAMA PICHA 3: RAY C ALIVYO MTEMBELEA IBRA DA HUSTLER WA NAKO2NAKO KATIKA KITUO CHA WALIOATHIRIWA NA MADAWA YA KULEVYA KIGAMBONI JIJINI DAR

April 11, 2014


Rehema Chalamila ‘Ray C’ baada ya mchakato wakutafuta logo kwa ajili ya foundation yake ya kupambana na kusaidia vijana wasiingie kwenye matumizi ya dawa za kulevya hatimaye ameanza kazi.
Ray C ametembelea kituo cha vijana walioamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na tabia hatarishi huko Kigamboni ambapo kwenye kituo hicho Ray C alikutana na msanii aliyekua wa Nako II Nako Ibra Da

MAKALLA AHIMIZA WATANZANA KUWA WAMOJA .

April 11, 2014

Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla ( suti yeusi ), na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, akimkabidhi Katekista, Isaka Manyoni , wa Kanisa Katoliki la Mchungaji Mwema katika Kigango Wami Sokoine fedha tasilmu sh milioni mbili ambazo zimetolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, juzi ikiwa ni kutimiza ahadi yake ya mwaka mmoja uliopita kwa Kwaya ya Muungano wa Kanisa hilo lililojengwa kuenzi mchango wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Sokoine , eneo la Wami Sokoine.

Na Mtanda Blog, Morogoro.

KANISA Katoliki na madhehebu mengine nchini yameombwa kuombea Bunge la Katiba ili liweze kujadili rasimu ya katiba iliyopo mbele yao kwa amani ,upendo na uvumilivu ili kuwezesha upatikanaji wa Katiba bora itakayowanufaisha watanzania wote.Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla , kwenye hotuba yake wakati wa ibada ya Jumapili Aprili 7, mwaka huu iliyofanyika katika Kanisa la Mchungaji Mwema , Wami Sokoine , wilayani Mvomero. 

Naibu waziri huyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mvomero pia alimwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kukabidhi sh: milioni mbili alizokuwa ameahidi mwaka juzi kwa kwaya ya Kanisa hilo, wakati mwenyewe akichangia haramberee sh: 100,000 kwa ajili ya watoto wa kanisal hilo. 
Awai Kabla ya kukabidhi fedha hizo, alitumia fursa hiyo kuliomba kanisa na madhehebu mengine kutochoka katika kuliombea bunge la katiba kufiatua hali inayoendelea kujitokeza Bungeni hapo. 
“ Kama ilivyo Bungeni kujadili Katiba inahitaji maombezi makubwa ...ili kila mmoja wetu awezakuwa na upendo na uvumilivu ili Tanzania ipate Katiba iliyobora “ alisema Naibu Waziri huyo. 
Mbali na hayo aliwaomba Watanzania kuliombea Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete anaye maliza muda wake ili aiache nchi ikiwa na Katiba Bora kwa manufaa ya watanzania wote. 
Pia Naibu Waziri Makalla alihimiza watanzania waendelee kudumu katika umoja , ushirikianao wakidugu na pia wananchi kupinga kila njama itakayowatumbukiza kwenye masuala la ubaguzi wa dini, rangi na jinsia. 
Hivyo alisema , kwa kudumisha misingi hiyo iliyoazisiwa na waasisi wetu wa Taifa hili, ni wajibu wa kila watanzania kuendeleza umoja huo kwa kizazi cha sasa na kijacho. 
Katika hatua nyingine, Makalla aliwa hakikishia waumini wa Kanisa hilo na maeneo mengine ya karibu watapatiwa umeme muda mfupi ujao mara baada ya Tanesco kukamilisha kuweka nguzo na kusambaza nyaya chini ya mradi wa nishati vijijini ili Kanisa liweza kutumia vifaa vya kisasa kwenye ibada .