BENKI YA NMB YAFUNGUA TAWI JIPYA KATIKA MJI WA HEDARU WILAYANI SAME.

November 15, 2017
Barabara ya kuelekea tawi jipya la Benkiya NMB katika mji wa Hedaru wilayani Same.
Tawi jipya la Benki ya NMB lililopo katika mji wa Hedaru wilayani Same.
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Staki akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya NMB katika mji wa Hedaru wilayani Same.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini.
Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la NMB -Hedaru.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akifuatilia uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya NMB tawi la Hedaru.
Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB waliohudhuria ufunguz rasmi wa tawi la Benki hiyo katika mji wa Hedaru.
Afisa Mkuu wa Wateja wado na wa kati wa Benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Staki wakati wa uzinduzi wa tawi hilo.
Afisa Mkuu wa Wateja wado na wa kati wa Benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela akimuongoza mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Staki kwenda kuzindua rasmi tawi hilo.
Mkuu wa wilaya ya Same,Roemery Staki akizindua tawi la Benkiya NMB,katika mji wa Hedaru wilayani Same.
Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na wa kati wa Benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela na Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Staki wakipiga makofi mara baada ya tendo la uzinduzi wa tawi hilo kufanyika.
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Staki akitia sain kitabu ha wageni mara baada ya kuzindua rasmi tawi la Benki ya NMB,katika mji wa Hedaru.
Mgeni rasmi ,Rosemery Staki akizungumza na mmoja wa wafanyakaz wa benki hiy mara baada ya kuzinduliwa katka mji wa Hedaru.
Meneja wa NMB,Kanda ya Kaskazin Salie Mlay akitoa neno la shukrani mara baada ya kuhitimisha hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la NMBkatika mji wa Hedaru wilayani Same.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SERIKALI YALIPA FIDIA YA BIMA YA AMANA KWA WATEJA WA BENKI YA FBME SH. MILIONI 728

November 15, 2017
SERIKALI imetumia kiasi cha Sh. Mil 728 kuwalipa amana zao wateja zaidi ya 695 wa Benki ya FBME ambayo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeifutia leseni ya kufanya shughuli za kibenki hapa nchini.

Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Viti Maalum Mhe.  Rukia Kassim Ahmed (CUF), aliyetaka kufahamu, pamoja na mambo mengine, hatma ya wateja wa Benki hiyo baada ya kufutiwa leseni yake ya kujihusisha na masuala ya kibenki Mei 8, 2017.

Mhe. Ahmed alitaka kufahamu msimamo wa Serikali endapo fedha za kuwalipa wateja hao zinazotokana na kuuza mali, makusanyo ya madeni na fedha zilizowekezwa kwenye taasisi nyingine na Benki hiyo hazitatosha.

Aidha, alihoji kuhusu uamuzi wa Bodi ya Akiba ya Amana ambao unaeleza kuwa hata kama mteja aliweka amana yake kwa fedha za kigeni katika benki hiyo, watalipwa kwa fedha za kitanzania kwa kiwango kilichokuwepo wakati Benki hiyo inafilisiwa Mei 8, 2017.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa malipo ya wateja yanalipwa kutokana na sheria ya mabenki na Taasisi za fedha ya mwaka 2006 kifungu cha 39, na kwamba kinachofanyika hivi sasa ni utekelezaji wa sheria hiyo.

 “Serikali haina mpango wa kumuonea mteja yoyote, madeni yatakusanywa  na fedha zitalipwa kwa kila mteja kulingana na amana alizojiwekea, Serikali inalisimamia jambo hilo kwa  umakini wa kiwango cha juu.” alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali lake la msingi Mhe. Rukia Kassim Ahmed (CUF), alitaka kujua hatma ya wateja walioweka fedha zao katika Benki ya FBME, baada ya Benki Kuu ya Tanzania kuifutia leseni ya kufanya shughuli zake za kibenki na kuiweka chini ya ufilisi wa Bodi ya Bima ya Amana kuanzia Mei 8, 2017.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa hatua ya kwanza kwa mujibu wa sheria ni malipo ya fidia ya Bima ya Amana ya kiasi kisichozidi Sh. 1,500,000 kutegemea na kiasi cha salio la amana wakati beki inafungwa.

SHIRIKA LA MAENDELEO LA UJERUMANI 'GIZ' NA SHUWASA WAENDESHA WARSHA KWA WADAU WA MAJI MANISPAA YA SHINYANGA

November 15, 2017
Mshauri wa masuala ya Maji na Mazingira kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’, Tina Eisele akielezea kuhusu mradi wa maji safi na mazingira katika maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini unaotekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) katika kata ya Ndala na Masekelo manispaa ya Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY DAR KUTOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE BAGAMOYO

November 15, 2017

Dar es Salaam, Novemba 15.2017

Klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam inatarajia kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani siku ya jumapili ya tarehe 19.2017.Kambi hiyo ya siku moja itatoa vipimo vya afya, ushauri, matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili, minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi na kwa mara ya kwanza itaendesha vipimo vya kansa ya shingo ya uzazi

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa kambi ya matibabu Bwana Frédéric Morel amesema amefurahishwa na maandalizi ya mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita. “Tumefurahishwa na ushirikiano tunaopata kutoka kwa makampuni na watu binafsi katika kuhakikisha kambi hii inafanyika kwa mara nyingine tena.pili, tunatarajia idadi ya watu kuwa mara mbili kulinganisha na mwaka uliopita”.Alisema, Morel. mbali na kambi ya Kerege, klabu yetu pia mwaka huu imetoa huduma ya matibabu ya bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msasani A. Hivyo tunaomba wakazi wa Kerege na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.” Frédéric Morel.

Kwa upande wake Rais wa klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam, Anne Saels, amesema kuwa kuwa kambi hii ni mfano wa huduma Za Rotary kwa jamii. “kutoa huduma za afya kwa watu takribani 2000 hufanywa pindi watu wanaojitolea kukutana pamoja na kushirikiana kufanya kazi ili kubadilisha maisha ya wengine kuwa bora. Mwisho, uhalali wetu kama Rotary hupimwa kwa na huduma tunayotoa na tunajivunia kuwa na uwezo wa kuandaa Matibabu ya Matibabu mwaka baada ya mwaka”.Alisema, Anne Saels.

Mbali na hilo, Mwakilishi kutoka benki ya Diamond Trust, Bwana Sylvester Bahati amesema ushirikiano na klub ya Rotary ya Oyster Bay katika miaka mitano iliyopita umekuwa ni ushrikiano mzuri wenye kubadili maisha ya watu.

“Mpaka sasa zaidi ya watu 1000 wamepatiwa huduma bora za kiafya katika kambi hii na kuhimiza watu kujitolewa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika jamii zao.Jeshi la wafanyakazi wa matibabu litakalo kusanyika siku ya tarehe 19.11.2017 haliwezi kupatikana popote kama kikundi wakati wowote ule, hii inafanya kambi ya matibabu ya Kerege kuwa ya kipekee na takribani watu 25 kutoka benki ya DTB hujitolea kila mwaka katika kambi.”Alisema ,Bwana Sylvester Bahati.

Kambi hii ya matibabu itafanyika kwa udhamini wa benki ya Diamond Trust, Whitedent, kampuni ya vinywaji ya Peps, Securex , ICAP kutoka chuo cha Colombia, pamoja na madakatri na wanafunzi kutoka Chuo cha kumbukumbu cha Herbert Kairuki, chuo kishirikishi cha afya cha MUHAS, na makundi mbalimbali kutoka asasi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali.

Klabu ya Rotary ya Oysterbay imeanzishwa mwaka 2009 na kwasasa ina wanachama 62. Ni klabu kubwa kati ya klabu 7 za rotary zinazopatikana Dar es Salaam. Klabu ya Rotary imekuwa ikiisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali baadhi yake kati ya hiyo miradi ni pamoja na Kambi ya matibabu kwa shule ya Msasani , Mradi wa vijana Poa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rotary Dar Marathon, “Rotary Mission Green” mradi wa kupanda miti, na kwasasa Rotary inajiandaa kuja na mkakati mpya utakaofanya kazi ya kuiisaidia jamii moja kwa katika maeneo mbalimbali tofauti na huduma za afya.

ZIARA YA MAAFISA WA AAKIA KIWANJA CHA NDEGE CHA JNIA

November 15, 2017

Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Lugano Mwansasu (kulia), akitoa maelezo kwa Maafisa wa Idara mbalimbali kutoka kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA) waliofanya ziara ya mafunzo. Kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa kitengo cha Ulinzi na usalama JNIA, Bw. Hamis Mashaka.
Maafisa wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), Bw. Shaaban Kombo (kuanzia wa pili kulia), Bi. Zakhia Mohamed, Bw. Salehe Said na Bi. Fatma Yussuf wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Lugano Mwansasu (kulia) akiwaelekeza jambo wakati wa ziara yao ya mafunzo iliyofanyika jana.
Msaidizi wa Mkuu wa kitengo cha Ulinzi na usalama wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Hamis Mashaka (kushoto), akitoa maelezo mbalimbali yanayohusiana na ulinzi na usalama kwa maafisa kutoka idara mbalimbali za Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) cha Zanzibar jana walipofanya ziara ya mafunzo.

Meneja Uendeshaji  cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian (kulia) akiwapa maelezo mbalimbali Maafisa kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) walipofanya ziara ya mafunzo jana.

Afisa Habari katika jengo la Watu Mashuhuri la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (VIP-JNIA), Bw. Kenny Kwenga (kushoto) akitoa maelezo ya namna watu mashuhuri wanavyohudumiwa kwa maafisa kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA), walipofanya ziara jana. Kulia ni Msimamizi wa VIP, Bi. Josephine Mwaisukule.
Na Mwandishi Wetu

MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.

Maafisa hao kutoka Idara mbalimbali walitoa kauli hiyo jana katika ziara ya siku moja ya mafunzo JNIA, ambapo walitembelea maeneo mbalimbali na kupata maelezo ya kina kutoka kwa maafisa husika.

Mkuu wa msafara wa maafisa hao, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha AAKIA, Bw. Shaaban Kombo alisema JNIA inaulinzi madhubuti kwa abiria na mizigo hukaguliwa kwa kutumia mitambo maalum kabla ya kupanda ndege au kuingia ndani ya jengo kwa kazi mbalimbali, ambapo wameahidi kufuata nyayo hizo ili kuzuia uhalifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.

Bw. Kombo alisema pamoja na kupata mambo mengi ya msingi ya uendeshaji wa viwanja vya ndege, JNIA imekuwa darasa tosha, ambapo pia katika upande wa utoaji wa vitambulisho wamejifunza namna utoaji wa vitambulisho unavyofanyika, ukiwa ni tofauti na AAKIA ambao hutoa vitambulisho vya kudumu mara baada ya taratibu kukakamilika, wakati JNIA hutoa vitambulisho vya muda kwa muombaji ili aweze kuendelea na kazi, wakati akisubiri cha kudumu kikamilike kutengenezwa.

“Tumefaidika na mambo mengi ukiangalia sisi kwetu hii ya vitambulisho ni tofauti kabisa, ila kwetu kwa kipindi chote mteja anasubiri kitambulisho cha kudumu anakuwa hawezi kuendelea na kazi zake eneo la kiwanja hadi atakapopata cha kudumu, lakini hapa anakuwa na cha muda kinachomfanya aendelee na shughuli zake huku cha kudumu kikiwa katika matengenezo,” alisema Bw. Kombo.

Naye Mkuu wa kitengpo cha Ulinzi na Usalama cha JNIA, Bw. Lugano Mwansasu alisema ziara ya maafisa wa AAKIA imewafariji na kuanza ukurasa wa mahusiano katika ushirikiano, ambapo nao wamejifunza kulingana na maelezo ya uendeshaji wa AAKIA.

Bw. Lugano alitoa wito kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuiga mfano huu wa kupeleka maafisa wake kwenye viwanja mbalimbali vya nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza utendaji kwa lengo la kuboresha huduma za viwanja kwa ujumla. TAA inasimamia viwanja 58 vilivyopo chini ya serikali.

“Kila siku mambo ya uendeshaji yanabadilika, basi tunaiomba mamlaka yetu itusaidie na sisi kwenda kutembelea viwanja vya wenzetu tujifunze huko, zipo changamoto labda sisi hatujui zinatatuliwaje lakini kwa ziara za mafunzo tunaweza kupata mbinu kutoka kwa wenzetu,” alisema Bw. Lugano.

Katika hatua nyingine, Meneja Uendeshaji wa JNIA, Bw. Vedastus Fabian alisema faida ya ziara ya mafunzo ni kujijengea uwezo na mahusiano mazuri baina ya kiwanja kimoja na kingine.

Bw.Fabian alisema ziara hizo zinasaidia katika kutatua matatizo yanayovikumba viwanja vya ndege, ambapo kwa sasa kumekuwa na masuala ya ugaidi, uvushaji wa dawa za kulevia na nyara za serikali.