Waziri Mwakyembe aishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa viungo bandia kwa walemavu

Waziri Mwakyembe aishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa viungo bandia kwa walemavu

April 03, 2016

1
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta wakati wa hafla ilyofanywa na kampuni hiyo ya  Kamal Steel Ltd kiwandani hapo  wakati wa utoaji wa msaada  wa viungo bandia,  kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya  sh. milioni 80, hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo imefanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akishukuru kampuni hiyo kwa msaada ilioutoa kwa watanzania hao wenye ulemavu wa miguu ambapo yeye ndiye aliyewakabidhi kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta.
3
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimvisha mguu wa bandia Bw. Siaga Raphael  Kiboko mara baada ya kukabidhiwa kutoka kampuni ya Kamal Steel ya jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Gagan Gupta.
4
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na  Bw. Siaga Raphael  Kiboko kabla ya kumkabidhi msaada wake wa viungo bandia vya mguu.
5
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Gagan Gupta ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya Kalam Steel tayari kwa ajili ya kukabidhi msaada huo.
6
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na  Bw. Siaga Raphael  Kiboko mara baada ya kumvisha mguu wake huku Mwenyekiti wa kampuni ya Kamal Steel Bw. Gagan Gupta pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo  wakishuhudia.
7
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Joshua Mwamunyange mara baada ya kumvisha mguu wakena kuanza kujaribu kutembea.
8
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimbidhi Bi Fatuma  mguu wake wa bandia ikiwa ni msaada kutoka kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel ya jijini Dar es salaam.
9
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa kampuni ya Kamal Steel na baadhi ya walemavu waliokabidhiwa msaada huo.
10
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mwenyekiti wa kampuni ya  Kamal Steel  Bw. Gagan Gupta.mara baada ya kukabidhi misaada hiyo katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta na wakuu wengine wa vitengo kutoka kampuni hiyo.
……………………………………………………………………………………………….
KAMPUNI ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel Ltd, imetoa msaada wa viungo bandia,  kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya  sh. milioni 80.
Akifunga kambi ya kutoa  viungo bandia hivyo  jijini Dar es Salaam sambamba na kukabidhi vifaa hivyo,   Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe,  alisema,  serikali  itaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu nchini ili waweze kukabiliana na changamoto zinazowazunguka ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa bandia.
Alisema, suala la ulemevu  linagusa  maisha ya kila mwanadamu na kwamba mtu yoyote anaweza kufikwa na tatizo hilo.
Alibainisha,   viungo bandia vinauzwa kwa ghalama kubwa ambayo watu wengi wenye ulemavu hawawezi kumudu kununua  hivyo serikali  kwa kushirikiana na wadau wake itaendelea kutoa msaada  wa vifaa hivyo.
“Jamii iamini kuwa wote ni walemavu watarajiwa. Kupoteza kiungo kimoja cha mwili ni changamoto kubwa.  Tunaishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa misaada hii muhimu  ambayo tunaamini kuwa inasaidia kupunguza madhira ya  ulemavu,”alisema  Dk. Mwakyembe ambaye kupitia msaada huo ameweza kuwasaidia watu wenye ulemavu wanne kutoka jimbo lake la Kyela mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta, alisema,kampuni yake haijatoa viungo bandia hivyo kama msaada, bali kama wajibu wake  kwajamii.
“Tunaamini kwamba, viungo hivi bandia vitawawezesha  kumudu kutembea, kufanya kazi mbalimbali zitakazo waletea kipato,”alisema Gupta.
Katika  hatua nyingine,  Gupta aliahidi kumuajiri  mmoja  wawatu hao wenye ulemavu  mwenye taaluma ya ufundi mitambo,  Siaga Raphael ambapo alisema ajira yake itaanza  leo.
“Huyu  atafundishwa ufundi wa kutengeneza vifaa mbalimbali hasa vya watu wenye ulemavu hapa, ili aweze kusaidia  kuwafundisha watu wenye ulemavu wengine.Mradi anataaluma hiyo ataanza kazi kesho asubuhi (leo asubuhi),”alisema  Gupta.
Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta, alisema, kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia viungo hivyo bandia kwa watu wenye ulemavu ambapo mpaka sasa imesaidia watu 200.
“Tutaendelea kuwasaidia  kila mara  ili tuweze kuisaidiana na serikali yetu kuwaondolea changamoto wenzetu hawa. Tunaamini wakipewa viungo hivi bandia wanaweza kushiriki  shughuli mbalimbali muhimu zitakazowaingizia kipato,”alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake walio pokea msaada huo, Siaga Raphael,   aliipongeza kampuni hiyo kwa masaada wa vifaa hivyo na kuitaka serikali  kuwa kumbuka watu wenye ulemavu kwa kuwasaidia pia kuwapa taaluma   ya ufundi itakazowawezesha kujimudu kimaisha.

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM, RAJAB LUHWAVI AZUNGUMZA NA MAKATIBU WA MATAWI NA KATA WILAYA YA DODOMA MJINI LEO

April 03, 2016

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akiwasalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma, leo Aprili 3, 2016, kuzungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Paulo Luhamo na Katikati ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Salum Kalli.
 Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Salum Kalli akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya kuanza kikao hicho
 Makatibu wa matawi na Kata za wilaya ya Dodoma mjini, wakiwa tayari ukumbini kuzungumzana Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi katika Ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi (wapili kulia) akiwasili katika ukumbi wa Sekretarieti katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma, leo Aprili 3, 2016, kuzungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini. Kulia ni Katibu wa CCM wa mkoa wa Dodoma, Jamila Yusuph.
 Katibu wa CCM wilaya ya Dodoma mjini akihamasisha, baada ya Luhwavi (katikati) kuwasili ukumbini. kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph
 Wajumbe wakiwa ukumbini Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Paulo Luhamo akimkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma ili kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu kuzungumza katika kikao hicho
 Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) kuzungumza katika kikao hicho
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akizungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Aprili 3, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Dodoma mjini, Paulo Luhamo
 Maofisa waandamizi wa Chama wakifuatilia kwa karibu kikao hicho
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akizungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Aprili 3, 2016. 
Baadhi ya wajumbe wakitoa yao ya moyoni kuhusu kero au changamoto wanazoziona katika utumishi wa Chama. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

SERIKALI YA UJERUMANI YATOA MSAADA WA NDEGE MAALUM AINA YA HUSKY A-1C KUSAIDIA DORIA YA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UJANGILI KATIKA HIFADHI YA AKIBA YA SELOUS

April 03, 2016

Waziri wa Maliasili
Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa
Kiuchumi na Maendeleo kutoka Serikali ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Gerd
Muller alipowasili katika uwanja mdogo wa ndege wa Matambwe uliopo ndani ya
Hifadhi ya akiba ya Selous Mkoani Morogoro kwa ajili ya hafla ya makabidhiano
ya ndege maalum aina ya Husky A-1C kutoka Serikali ya Ujerumani itakayosaidia kufanya
doria za kupambana na ujangili katika hifadhi hiyo.
Waziri wa Maliasili
Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza na Waziri wa Ushirikiano wa
Kiuchumi na Maendeleo kutoka Serikali ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Gerd
Muller (kushoto) katika hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa ndege
maalum aina ya Husky A-1C kutoka Serikali ya Ujerumani itakayosaidia kufanya doria
za kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Akiba ya Selous. Wengine ni Meneja
wa Hifadhi ya Selous Bw. Mabula Misungwi (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania Bw. Martin Laibooki (wa pili kulia) na
Bw. David Kanyatta Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Wanyamapori.
Waziri wa Maliasili
Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa ndege
maalum kutoka Serikali ya Ujerumani aina ya Husky A-1C kwa ajili ya kufanya
doria za kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Akiba ya Selous. Kutoka
kushoto ni Balozi wa Ujerumani hapa nchini Mhe. Egon Konchanke, Waziri wa
Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo kutoka Serikali ya Shirikisho la Ujerumani
Dkt. Gerd Muller, Dkt. Christof Schenck Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Maendeleo la Uhifadhi la Kimataifa la FZS na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania Bw. Martin Laibooki.
Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo kutoka Serikali ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Gerd Muller akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa
Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani
Dkt. Gerd Muller (wa pili kushoto) akimkabidhi Waziri wa Maliasili Prof.
Jumanne Maghembe msaada wa ndege maalum aina ya Husky A-1C kwa ajili ya kufanya
doria za kupambana ujangili katika Hifadhi ya Akiba ya Selous. Wanaoshuhudia
Kulia ni Rubani wa Ndege hiyo Capt. Bernard Shayo, Dkt. Christof Schenck
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Uhifadhi la Kimataifa la FZS (wa
pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA)
Bw. Martin Laibooki.
Waziri wa Maliasili
Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akifanya majaribio ya kupanda ndege maalum
aina ya Husky A-1C iliyotolewa na Serikali ya Ujerumani kwa ajili ya kufanya
doria za kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Akiba ya Selous. Wanaoshuhudia
ni Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya
Shirikisho la Ujerumani Dkt. Gerd Muller (wa pili kushoto), Capt. Bernard Shayo
(kulia), Bw. David Kanyatta Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Wanyamapori
(kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania Bw.
Martin Laibooki (wa tatu kushoto).
 
Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo kutoka Serikali ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Gerd Muller akiwa na baadhi ya askari wa Wanyamapori katika Hifadhi ya Akiba ya Selous.
Waziri wa Maliasili
Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiwasalimia askari wa Wanyamapori katika
Hifadhi ya Akiba ya Selous. Kulia anayeshuhudia ni Waziri wa Ushirikiano
wa Kiuchumi na Maendeleo kutoka Serikali ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Gerd
Muller ambaye amemkabidhi Prof. Maghembe msaada wa ndege maalum aina ya Husky
A-1C ya kufanya doria za kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Akiba ya
Selous.
 Sehemu ya kundi la Swala katika hifadhi ya akiba ya Selous.
Moja ya Twiga akiwa anakimbia katika hifadhi ya akiba ya Selous.
Sehemu ya wajumbe wa msafara wa Waziri Maghembe na Waziri wa Muller wakibadilishana mawazo katika hifadhi ya akiba ya Selous.
……………………………………………………..
 
Serikali ya Ujerumani
imetoa msaada wa ndege maalum aina ya “Husky A-1C Aircraft” kwa Serikali ya
Tanzania kupitia Wizara ya Malisili na Utalii kwa ajili ya kusaidia katika doria
za kupambana na Ujangili katika Hifadhi ya Akiba ya Selous.
 
Msaada huo wenye thamani
ya Euro 200,000 sawa na Tsh. 498,292,000, umekabidhiwa kwa Mhe. Waziri wa
Maliasili Prof. Jumanne Maghembe na Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na
Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Gerd Muller katika hafla
fupi iliyofanyika Matambwe ndani ya pori la Akiba la Selous.
 
Hafla hiyo
ilihudhuriwa na Maafisa wa Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini wakiongozwa na
Balozi Mhe. Egon Konchanke, viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na
Utalii,          Mamlaka ya Wanyamapori
Tanzania (TAWA), Mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa ya FZS, WWF, GIZ na KFW.
 
Akizungumza katika
hafla hiyo Waziri Maghembe amesema ndege hiyo itasaidia jitihada za Serikali za
kupambana na Ujangili kwa kufanya doria katika anga ya hifadhi ya Akiba ya Selous
na kusaidia kutoa taarifa za kiuhalifu pale itakapobainika na kuchukuliwa hatua
stahiki za kukabiliana na uhalifu huo.
 
“Ndege hii
tunayoshuhudia mapokezi yake leo ni ukombozi kwa Wanyamapori katika Pori hili
la Akiba la Selous kwani itasaidia na kuimarisha doria za kupambana na ujangili
ndani na kuzunguka eneo zima la hifadhi”. Alisema Prof. Maghembe.
 
Waziri Maghembe
ameishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia kwa Waziri Muller kwa msaada huo na
mingine ambayo wamekuwa wakiitoa kusaidia uhifadhi wa Wanamapori hapa nchini, Amebainisha
kuwa misaada hiyo imekuwa na tija kubwa katika kuendeleza uhifadhi wa
Wanyamapori ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kabla ya kuwepo kwa misaada
hiyo.
 
Waziri Maghembe
alieleza kuwa sera ya Wanyamapori Tanzania inatambua ushirikiano wa wahisani na
watu binafsi katika kuisaidia Serikali Kifedha na Kitaaluma kwenye eneo la
uhifadhi, hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuipa ushirikiano Serikali
katika jitihada zake za kuendeleza Uhifadhi wa Wanyamapori nchini.
 
Kwa upande wake
Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani Dkt. Gerd Muller alimueleza
Prof. Maghembe kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika
kuendeleza uhifadhi hapa nchini. Waziri huyo pia aliwapongeza Askari wa Wanyamapori
kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulinda Wanyamapori katika mazingira magumu ya
porini.
 
Akizungumza kwa lugha
ya Kijerumani huku ikitafsiriwa kwa Kiingereza na Mkalimani wake Dkt. Muller alisema
ipo haja kubwa ya kuendelea kuwalinda Wanyamapori kwa nguvu zote kwa kuwa hawana
hatia na kwamba walikuwepo katika mazingira yao ya asili kabla hata ya binadamu
kuwepo hapo.
 
“Hawa viumbe hai
wanaowindwa walikuwepo katika mazingira haya kabla ya sisi binadamu kuja hapa,
Sote tunahitaji kuwalinda na kuishi kwa amani na viumbe hawa ndio kutakuwa na
amani duniani kote” Alieleza Dkt. Muller.
 
Mapema akizungumza
kabla ya tukio la kukabidhiwa ndege, Meneja wa Pori hilo la Akiba la Selous Bw.
Mabula Misungwi alieleza baadhi ya changamoto kuu zinazoikabili hifadhi hiyo
kuwa ni ujangili, miundombinu mibovu ya barabara kwa ajili ya doria na vifaa
ikiwemo magari ya doria.
 
Msafara wa Waziri
Maghembe na ugeni wake kutoka Serikali ya Shirikisho la Ujerumani walipata
fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi ya Selous ikiwemo Matambwe na
Behobeho ambayo inajulikana kama Serengeti ndogo na kujionea Wanyamapori
mbalimbali wakiwemo Tembo, Twiga, Pundamilia, Swala, Nyani, Ngiri, Nyumbu na
mandhari mazuri ya mto behobeho.
 
Hifadhi ya Akiba ya Selous
ni moja ya hifadhi kubwa duniani ikiwa na ukubwa wa zaidi ya Kilomita za mraba
50,000. Hifadhi hii ipo ndani ya Mikoa mitano ya Tanzania ambayo ni Pwani,
Morogoro, Lindi, Mtwara na Songea. Hifadhi hii imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na
ujangili kwani katika Sensa ya mwaka 2013 ilionesha idadi ya tembo katika
hifadhi hiyo kuwa 13,000 idadi ambayo ni ndogo sana ikilinganishwa na ile ya
mwaka 2003 ambayo ilikuwa 70,000.
(Picha na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utali #WWW.WIZARAyaMALIASILInaUTALII.BLOGSPOT.COM)
Former Heads of African State and Government Meet in Addis Ababa Ethiopia.

Former Heads of African State and Government Meet in Addis Ababa Ethiopia.

April 03, 2016

1Former Mozambican President Joaquim Alberto Chissano in discussion with former Tanzanian Presidents H.E. Ali Hassan Mwinyi and H.E. Benjamin William Mkapa during the 4th  Forum For Former African Heads of State and Government(Africa Forum) held at the United Nations Economic Commission for Africa(UNECA) Conference centre in Addis Ababa Ethiopia. The Two Days forum(2-3 April 2016) has been sponsored by UNECA.2
Former Tanzanian President H.E.Benjamin William Mkapa in conversation with former Malawian President H.E.Bakili Muluzi in Addis Ababa
 (photo courtesy of Tanzania Embassy in Addis Ababa Ethiopia).
…………………………………………………………………………………………….
Sound economic policies geared at propelling African countries into industrialization coupled with properly trained young workforce could make the continent more prosperous lifting millions of Africans out of poverty.
The United Nations Under Secretary-General and Executive Secretary of the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) Dr. Carlos Lopes said this during the opening session of the 4th General Assembly of the forum for Former African Heads of State and Government (Africa Forum) held at UNECA Conference Centre in Addis Ababa today.
The two days General Assembly of the Forum for Former Heads of State and Governmen(2-3April 2016) has been sponsored by The United Nations Economic Commission for Africa UNECA.
African countries need to undertake economic structural transformation geared towards industrialization,” adding that recent growth of economies in most African countries was a result of increase export of raw commodities to industrialized countries.
Dr. Lopes said that manufacturing in most African countries has been going down significantly in the past decade despite doubling of GDP in the same countries as a result of increase of export of raw commodities and that there has been an increase in internal consumption of imports.
The UNECA Executive Secretary outlined some challenges the continent is facing towards industrialization including patenting and protection by the industrialized countries of their intellectual property rights in commodity production, complex trade regimes in global market, inadequate technology and stiff competition.
Dr.Lopes, however, said the there is a great hope for Africa to industrialize by embarking upon the production and proper utilization of renewable energies to process raw commodities(Agro processing) in various countries creating job opportunities to most young people in Africa.  
He further said that countries should formulate sound economic policies aimed at encouraging the population to consume what is produced locally to boost local industries and that commodity based industrialization is capable of creating between five to seven million jobs annually in Africa reducing tremendously youth unemployment in the continent.
Dr. Lopes said that proper and appropriate technology should be adopted in various African countries to curb low productivity and boost storage capacity to prevent post harvest loses which is a common feature in most African countries that subsequently trigger food insecurity in the advent of bad weather.
In her remarks during the same occasion, The Chairperson of the African Union Commission Dr.Nkosazana Dlamini Zuma emphasized the need for African countries to take a seriously a move to review their academic curricula so as to equip the young generation with relevant skills to fit into modern production processes adding that emphasis should be placed on science subjects and vocational training.
Dr.Zuma reiterated the need for African countries to speed up the process of integration through the promotion of intra-African trade and tourism and simplify procedure on cross border movements so that young people could travel freely in the continent in search for jobs other economic ventures.
The AUC Chairperson further emphasized the need for African countries to mobilize domestic resources to fund various local development projects and reduce donor dependence and that the focus should be placed on building infrastructures including roads and railways to connect African countries and boost intra African trade and labor movements.  
The 4th General Assembly of Former Heads of State and Governments will among other things exchange views on the Economic partnership Agreement, and the issue of illicitly financial flows and their development impact, as well as Africa’s development Agenda 2063.
Former Heads of State attending the Africa Forum include Tanzania’s former Presidents Ali Hassan Mwinyi and Benjamin William Mkapa, Malawi’s former President Bakili Muluzi, Namibia’s former President Hifikepunye Lucas Pohamba, Nigeria’s former President General Jackob Gowon, South Africa’s Thabo Mbeki and Mozambique’s former president Joaquim Alberto Chissano who is  also the chair of the forum.
The Africa Forum Constitutes an informal network of former African Heads of State and Government and other African Leaders designed to support the implementation of the broad objectives of the African Union(AU) and its initiative, the New Partnership for Africa’s Development(NEPAD), at the national, Sub regional  and Regional levels. With the specific functions of advocacy and think tanking, the Arica Forum will help to harness the experience, moral authority and good offices of  former African Heads of State and Government and African Leaders  with the view to assisting the advancement of Africa’s Social and Economic Development.
From Tanzania Embassy information Department Addis Ababa Ethiopia
Waziri wa Habari Nape Nnauye akutana na Viongozi wa TAJATI

Waziri wa Habari Nape Nnauye akutana na Viongozi wa TAJATI

April 03, 2016

4 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na viongozi wa TAJATI (hawapo pichani) alipowatembelea ofisini kwao kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya.5 
Baadhi ya viongozi wa TAJATI wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) alipofika katika ofisi zao kuona shughuli wanazozifanya na kuwapa motisha wa kuandika habari za kiutafiti leo Jijini Mbeya.3Mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea ofisi za TAJATI kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya. 1 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea zawadi ya kikombe kutoka kwa mtunza fedha wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) Bi. Brandy Nelson alipowasili katika ofisi zao kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini .2 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisoma kipeperushi alichopewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) ili kuweza kujua kazi wanazozifanya leo Jijini Mbeya alipowatembelea na kuwataka kuendela kuandika habari za kiutafiti ili kuboresha fani ya uandishi wa habari. Kushoto ni mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili na kulia ni makamu mwenyekiti TAJATI Bw. Christopher Nyenyembe.6 
Makamu mwenyekiti TAJATI Bw. Christopher Nyenyembe (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye moja ya ofisi wanayoiandaa kwa ajili ya matumizi ya studio ya kurushia matangazo alipotembelea ofisi zao kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya.8 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akizungumza na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) alipowasili katika ofisi zao kuona kazi wanazozifanya leo Jijini Mbeya.7 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) baada ya kuzungumza nao leo Jijini Mbeya.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI YARIDHISHWA NA MATUMIZI YA FEDHA MTAMBO WA RUVU CHINI

April 03, 2016

Meneja wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini Mhandisi Emmanuel Makusa (katikati) akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kutembelea Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini,wilayani Bagamoyo kujionea maendeleo yaliyofikiwa kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa bomba lenye urefu wa Kilometa 56 linalotoka katika mtambo huo kwenda jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiangalia sehemu ya kukusanyia maji kutoka mto Ruvu kwenye Mtambo wa Ruvu Chini.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiangalia mitambo ya kuchujia maji kutoka mto Ruvu kwenye Mtambo wa maji wa Ruvu Chini.
Meneja wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini Mhandisi Emmanuel Makusa akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji namna chumba cha kuongozea mitambo ya Ruvu chini kinavyofanya walipotembelea Mtambo wa Ruvu Chini,wilayani Bagamoyo kujionea maendeleo yaliyofikiwa kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa bomba lenye urefu wa Kilometa 56 linalotoka katika mtambo huo kwenda jijini Dar es salaam.
Meneja wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini Mhandisi Emmanuel Makusa akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Mary Nagu wakati kamati hiyo ilipotembelea Mtambo wa Ruvu Chini,wilayani Bagamoyo .
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ( katikati) na baadhi ya wajumbe wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini Mhandisi Emmanuel Makusa mara baada ya kutembelea sehemu ya kuchujia maji na kuchanganyia dawa.

Sehemu ya kuchujia maji katika mtambo wa Ruvu Chini.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiangalia eneo lenye pampu za kusukumia maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini kwenda matangi ya maji yaliyoko Chuo Kikuu Ardhi jijini Dar es salaam.
Eneo la kukusanyia maji kutoka mto Ruvu kwenda kwenye mtambo wa kusafishia Maji.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeridhishwa na matumizi ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 141 zilizotolewa na Serikali kugharamia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini,wilayani Bagamoyo kwenda jijini Dar es salaam kufuatia ujenzi wake kukamilika.

Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kutembelea maeneo mbalimbali ya mradi huo ikiwemo mtambo wa Maji wa Ruvu Chini ulioko Bagamoyo mkoani Pwani, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanan'g Mhe. Mary Nagu amesema kuwa kamati kamati yake imeridhishwa na ubora wa kazi iliyofanyika chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salam ( DAWASA).

Amesema mradi huo wenye urefu wa kilometa 56 umekamilika na kueleza kuwa itakua historia kwa wananchi wa Dar es salaam waliounganishwa na mtandao wa mabomba ya DAWASCO kukosa maji.

Amesema kama kamati wamejiridhisha kuwa kiasi cha maji kinachozalishwa kwa siku lita milioni 270 kutoka mtambo wa Ruvu Chini ni kingi na kueleza kuwa kiwango hicho kitaongezwa kwenye uzalishaji wa awali.

"Sisi kama Kamati ya Bunge tumeridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika, tumeshuhudia wenyewe maji yanayozalishwa ni mengi tunaipongeza Serikali kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wakazi wa jiji la Dar es salaam" Amesema Mhe.Nagu.

Amesema kazi iliyopo sasa kwa Serikali na mamlaka zinazohusika ni kuhakikisha kuwa inakabiliana na na changamoto ya usambazaji wa maji hayo ili wakazi wengi zaidi wa jiji hilo wanaunganishwe na mtandao wa mabomba ya DAWASCO.

Amewataka DAWASCO kuifanya kazi hiyo kwa kasi pia kuangalia upya gharama za usambazaji wa maji pia kuwaangalia upya mawakala waliowekwa kusimamia usambazaji wa maji ili kuwadhibiti wale wasiowaaminifu ili wananchi waweze kupata maji kwa bei nafuu na kuepuka kutumia maji yasiyo salama ambayo yamekuwa chanzo cha milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu.

Aidha,ametoa wito kwa wananchi kulinda na kutunza vyanzo vya maji ili upatikanaji wa maji hayo uwe endelevu huku akitoa wito kwa Wizara kulifanyika kazi suala la kuwapatia maji wananchi wote wanaoishi kuzunguka miundombinu mikubwa ya maji kote nchini ili kuimarisha ulinzi na usalama.

Kwa upande wake Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ziara ya wabunge hao kwenye mtambo wa Maji wa Ruvu Chini amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutalifanya jiji la Dar es salaam kupata maji.

Amesema katika kuchukua hatua za kukabiliana na uhaba wa maji Serikali iliamua kufanya maboresho makubwa mifumo ya maji kwa kujenga mipya na kurekebisha ile ya zamani ili kuendana na kasi ongezeko la uhitaji wa maji.

Amesema kazi kubwa ambayo inaendelea sasa ni kuhakikisha usambazaji katika maeneo yenye mitandao ya mabomba na ile ambayo haikuwa na mitandao ya mabomba ili kuwapatia maji ya uhakika.

" Naishukuru kamati kwa kuja kutembelea mradi wetu wametupa changamoto ya kuhakikisha maji yanafika kwa wananchi, sisi kama serikali tuna mpango wa kuhakikisha tunaondoa mifumo yote chakavu katika jiji la Dar es salaam kwa kuweka mipya na hii tunaendelea nayo kwa kasi" Amesisitiza.

Amesema kazi ya kuweka miundombinu ya usambazaji maji katika jiji la Dar es salaam imeshaanza akifafanua kuwa Serikali imeingia mikataba na wakandarasi kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika kwa viwango.

Aidha, amesema kuwa baadhi ya maeneo ya jiji ikiwemo eneo la Kimara kazi inaendelea huku maeneo ya katikati ya jiji miundombinu yake ni chakavu inaendelea kubadilishwa ili iweze kuhimili wingi na nguvu ya maji inayosukumwa

Ametoa wito kwa wananchi na wenye viwanda kutumia maji hayo ili kulinda afya za walaji kwa kuwa maji hayo ni salama na yamepita kwenye vipimo vya ubora ili kuepuka kutumia maji yasiyo salama ambayo yamekuwa chanzo cha magonjwa.

" Tumeshatoa maelekezo viwanda vyote vya Dar es salaam vihakikishe kuwa vinatumia maji haya, sasa tuna maji ya kutosha, waje tuwaunganishe na maji haya japo baadhi yao wamekuwa wakijiunganishia maji kiholela na kutumia visima wanavyochimba ambavyo si salama".

Kuhusu Serikali kuhakikisha ulinzi wa mtandao wa bomba hilo lenye urefu wa Kilometa 56 amesema kuwa kazi hiyo inafanywa na DAWASCO ikiwahusisha viongozi na wananchi ambao mradi unapita katika maeneo yao.

" Ni kweli ulinzi wa bomba hili ni muhimu,DAWASA wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo linakopita bomba, pia tumeshaweka matoleo kwa ajili ya kuhakikisha tunawafikishia huduma ya maji wananchi wanaoishi kuzunguka bomba hili ili nao wawe sehemu ya walinzi wa mradi wao" Amesema.

Mhe. Lwenge ameongeza kuwa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) litaweka mfumo wa ulinzi wa kieletroniki ili kulinda bomba hilo, mfumo huo utakua unapima kiwango cha msukumo wa maji yanayotoka Ruvu Chini kisha kutoa taarifa kwenye vituo vitakavyoanzishwa endapo itatokea hitilafu ya miundombinu hiyo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ambao ni Wabunge wakizungumzia kukamilika kwa mradi huo wamesema kuwa wameridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na serikali na kwamba itaondoa kero ya maji katika jiji la Dar es-slaam.

Mbunge wa jimbo la Itirima, Mhe. Njalu Silanga ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo ameeleza kuwa ameridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa na Serikali kwa kuwa mradi huo umejengwa katika viwango vya hali ya juu na kuongeza kwamba wakazi wa Dar es salaam sasa watarajie kupata maji Safi na Salama.

"Naipongeza sana Serikali kwa kufanikisha mradi huu,kweli wamefanya kazi kubwa sana, mimi na wabunge wenzangu tumeona na tumeridhishwa na utendaji wa Serikali katika kuhakikisha jiji la Dar es salaam linapata maji safi na salama"

Ameiomba Serikali kuweka msisitizo katika uimarishaji wa miundombinu ili kuwezesha maji kufika kwa urahisi katika makazi ya watu.

Naye Mhe. Dkt.Sware Semesi, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Dodoma akiuzungumzia mradi huo amesema kuwa ameridhishwa na miundombinu imara iliyojengwa na kuiomba serikali kusimamia usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

" Mimi pamoja na wabunge wenzagu tumeshuhudia mradi huu ni mkubwa,kilichobaki kwa mamlaka zinazohusika ni kujipanga na kuhakikisha kunakuwa na mgawanyo mzuri wa maji haya,kufanyika kwa Uhakiki na ukusanyanji wa ankara za wateja unaoendana na matumizi halisi ya maji hayo ili huduma hii iwe endelevu" Amesema.

Aidha, ametoa wito kwa DAWASCO kusimamia kikamilifu usambazaji wa lita milioni 270 zinazozalishwa kwa siku na mtambo wa Ruvu chini kwenda matangi ya maji yaliyoko Chuo Kikuu Ardhi