MAMA YAKE TEDDY MAPUNDA MAREHEMU BENADETTE IZENGO AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI DSM

MAMA YAKE TEDDY MAPUNDA MAREHEMU BENADETTE IZENGO AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI DSM

May 10, 2016

001
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanania Dk. Gharib Bilal wa tatu kutoka kushoto na Mama Salma Kikwete wa kwanza kushoto wakishiriki mazishi ya Merehemu Benadette Izengo mama wa Mkurugenzi wa kampuni ya Montage Limited Teddy Mapunda aliyekaa katikati yao pamoja na wanafamilia wengine wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanis kuu la Mtakatifu Joseph.
01
Mke wa Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete Mama Salma Kikwete akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
02 
Balozi Asha Rose Migiro akiweka mchanga kaburini wakati wa maishi ya marehemu mama Benadette Izengo.
1 
Fathre Matumaini akiongoza ibada ya mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Josepha jana.
2Wanafamilia wakiwa katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana jijini Dar es salaam na kufuatiwa na mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.
3 
Teddy Mapunda na Ndugu yake wakiwa pembeni mwa jeneza la mama yao mpendwa marehemu Benadette Izengo.
4 
Mkwe wa Marehemu mama Benadette Izengo akishiriki ibada ya mazishi pamoja na ndugu na jamaa wa familia kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana.
5 
Wajukuu wa marehemu wakishiriki ibada hiyo jana.
6 
Wana familia wakiwa na majonzi kwa kuondokewa na mpendwa mama yao Marehemu Mama Benadette Izengo.
7Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee Jon Momose Cheyi akishiriki sakramenti ya bwana kutoka kwa Father Kaombwe wakati wa ibada hiyo ya mazishi
8 
Teddy Mapunda na Mumewe Nestor Mapunda wakiwa na majozni huku wakiangalia jeneza la mama yao mpendwa marehemu mama Benadette Izengo.
9 
Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
10 
Kutoka kushoto ni Jeseph Kusaga Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Enertainment, Nandi Mwiyombela, Justin Pamba, Godfrey Kusaga na John Mbele nao walishiriki katika mazishi hayo ya mama Bebadette Izengo.
MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA 10 MEI, 2016.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA 10 MEI, 2016.

May 10, 2016

1 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (kulia) pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima wakiwa katika mazungumzo Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa vikao vya asubuhi vya bunge hilo 10 Mei, 2016.
3 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa vikao vya asubuhi vya bunge hilo 10 Mei, 2016.
2 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akisoma taarifa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa leo 10 Mei, 2016, Bungeni mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DODOMA.

MBUNGE ROSE TWEVE AKIKOMALIA SERIKALI FEDHA ZA KUWAENDELEZA VIJANA, WANAWAKE IRINGA

May 10, 2016

Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (CCM) akiuliza swali kwa Waziri wa Nnchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), bungeni Dodoma , kwamba ni fedha kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake mkoani Iringa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


 Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto), akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (katikati) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum, Kiteto Koshuma kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

 Taswira mbalimbali za Rose Tweve, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Iringa




MGODI WA DHAHABU WA BULHANHLU WAINGIA MAKUBALIANO NA TAASISI YA BENJAMINI WILLIAM MKAPA YA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA MKOANI SHINYANGA.

May 10, 2016
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akibadilishana hati za makubaliano na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa,Dkt Ellen Mkondya wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati hizo iliyofanyika wilayani Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew pamoja na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt Ellen Mkondya wakitia saini katika hati za makubaliano ya kuboresha mradi wa huduma ya afya ,Zoezi la utiaji saini ulishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa(kulia) ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,Patrick Karangwa (nyuma ya mkuu wa wilaya) pamoja na viongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Elias Kasitila na Mganga Mkuu wa wilaya ya Msalala Dkt Hamad Nyembea.
Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Graham Crew akizungumza mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya kuboresha huduma za Afya na Taasisi ya Benjamini William Mkapa wakati wa hafla iliyofanyika katika mji wa Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kwa michango ambao wameendelea kutoa kwa wilaya ya Kahama na Msalala.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyeko Shinyanga.

MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilayani Kahama umetiliana saini hatii ya makubaliano ya Dola 200,000 sawa na shilingi Milioni 440 za Tanzania na Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) kwa ajili ya mradi wa kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa mama na mtoto katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga

Mgodi  Bulyanhulu kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Acacia na Taasisi ya Benjamin W. Mkapa (BMF) wamesaini hati ya makubaliano ili kushirikiana katika kutekeleza mradi wa miaka miwili unaolenga kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto katika jamii .

Mgodi wa Bulyanhulu kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Acacia utatoa kiasi cha dola za Kimarekani 200,000 kusaidia awamu ya pili ya mradi wa BMF utakaosaidia kuboresha huduma ya vituo viwili vya afya wilayani humo, Kituo cha Afya cha Bugarama na Zahanati ya Kakola kupitia mradi huo.

Mradi huo katika vituo tajwa unatarajiwa kunufaisha wananchi 321,852 katika Halmashauri ya Msalala ambapo makubaliano hayo ya miaka miwili yanaanzia, 01 April 2016 hadi 30 Machi 2018.

“Mgodi wetu unaendesha shughuli zake katika halmashauri ya Msalala hapa mkoani Shinyanga na sehemu ya uwajibikaji wetu kwenye jamii, kupitia mkakati wa mipango endelevu kwenye jamii na kusaidia mikakati ya uboreshaji wa sekta ya afya kwa ajili ya jamii inayozunguka mgodi.”alisema Graham Crew.

“Ushirikiano huu na Taasisi ya BMF umekuja wakati muafaka ambapo BGML imewekeza katika miundombinu ya kuipandisha hadhi zahanati ya Bugarama kuwa kituo cha afya na pia kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Kakola.” Aliongeza meneja huyo mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew.

Awamu ya pili ya Mradi wa BMF inalenga kutekeleza mradi utakaoboresha huduma za HIV/AIDS, huduma za mama na mtoto kwa kuongeza upatikanaji wa wataalamu wa afya na kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya.

Afisa Mtendaji Mkuu wa BMF Dk Ellen Mkondya Senkoro amesema; “Takwimu zinaonyesha kwamba mkoa wa Shinyanga una maambukizi kwa asilimia 7.4% ambapo kiwango kikubwa kipo katika halmashauri ya Msalala kutokana na shughuli za uchimbaji madini hasa uchimbaji mdogo mdogo.”

“Kiwango hiki kimeendelea kuwa hivyo tangu mwaka 2007/2008 hadi 2011/2012 ingawa kiwango cha maambukizi nchini kimepungua kutoka asilimia 5.7% hadi 5.1% hivyo sehemu hii inahitaji hatua maalumu. “alisema Dkt Mkondya.

Alishukuru Kampuni ya  ACACIA kwa msaada huo na kwamba utasaidia kwenye utekelezaji wa uboreshaji wa mifumo ya kukabiliana na tatizo la Virusi vya Ukimwi, huduma za uzazi na watoto kwa kuongeza rasilimali watu ya watalaamu wa afya, uendelezaji wa miundombinu na kujengea uwezo maeneo yanayohitaji ufanisi zaidi.

 Tangu mwaka 2013 Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) imekuwa ikishirikiana na Acacia kupitia Mfuko wake wa Acacia Maendeleo Fund katika kutekeleza sehemu ya miradi ya awamu ya pili ya mfuko wa taasisi ya BMF katika wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera na Halmashauri iliyokuwa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa Acacia:
Mfuko wa Maendeleo wa Acacia maarufu kama Acacia Maendeleo Fund ulianzishwa mwaka 2011 kama sehemu ya dhamira katika kuboresha maendeleo endelevu katika jamii kwenye maeneo tunayofanya kazi. Hadi sasa tumefanikiwa kuwekeza dola za kimarekani milioni 35.0 katika miradi 150 kwenye maeneo mbalimbali.

Misaada kutoka kwenye mfuko huu hutoa kipaumbele kwa vitega uchumi vinavyosaidia maendeleo ya jamii, ujengaji wa uwezo, sekta ya afya, elimu, maji, mazingira katika maeneo tunakoendesha shughuli zetu.

Taasisi ya Benjamin W. Mkapa 
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa ilianzishwa April 2006 na Rais Mtaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Benjamin W. Mkapa, taasisi hii isiyo ya kiserikali ina dhamira ya kuboresha afya na hali za watanzania hasa katika maeneo yaliyoko vijijini kwa kutekeleza miradi yenye kutoa matokeo.

Mwisho.

KILIMO HIFADHI CHA NYANYA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

May 10, 2016




Dk. Sophia Mlote, mkazi wa Kinyerezi Zimbili jijini Dar es Salaam akiweka sawa vifaa mbalimbali kwenye banda lake la kilimo ambamo amepanda nyanya. Dk. Mlote anatekeleza kilimo hai kupitia mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya Foundation for Women of Africa ambayo inaongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega. (Makala na Picha zimeandaliwa na www.brotherdanny.com).

PSPF YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUSOMEA KWA WANAFUNZI WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MIKOA YA MWANZA NA GEITA

May 10, 2016

Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta Mnyamani akiwaelimisha wanafunzi wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyoko mkoani Geita kuhusiana na Mfuko wa Penseheni wa PSPF na lengo la kusaidia jamii katika hususan katika masuala ya elimu. Mabegi yenye vifaa vya kusomea yalitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kama msaada kwa wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyopo Mkoani Geita.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakifurahia msaada uliotolewa na PSPF kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu shuleni hapo.
 Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta Mnyamani ,akiongea na kamati ya shule ya Msingi Igaka (ambao hawapo pichani) pamoja na wanafunzi kuhusiana na lengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kusaidia jamii hasa kwenye nyanja ya elimu nchini.
Wanafunzi waishio katika mazingira magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Wanafunzi waishio katika mazingira magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Afisa Uendashaji wa PSPF Mkoa wa Geita, Bw. Noel Tuga, akiwapa maelezo wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya msingi Nyansalwa namna ya kutumia vifaa vilivyopo kwenye mabegi PSPF iliyotoa msaada. Mabegi yenye vifaa vya kusomea yalitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kama msaada kwa wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyopo Mkoani Geita.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka, Bw. Jumanne Masumbuko, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa masaada wa mabegi ya shule yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Mwanza, Bw. Salim Salum, akitoa rai kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kusoma kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu na kuja kulitumikia Taifa katika siku za baadaye.
NMB yawashirikisha wananchi kuwekeza mtaji, Yawauzia 'bond'.

NMB yawashirikisha wananchi kuwekeza mtaji, Yawauzia 'bond'.

May 10, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia). Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia).Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jambo na Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas (kushoto), katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jambo na Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas (kushoto), katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati benki hiyo ilipozinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akiwa na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia). Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati benki hiyo ilipozinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akiwa na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia).Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kushoto) mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas akishuhudia.  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kushoto) mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas akishuhudia.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kulia ni Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa akifuatilia tukio hilo. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kulia ni Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa akifuatilia tukio hilo.Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia) akizungumza na wanahabari kufafanua hali ya hisa nchini na kuipongeza NMB kwa hatua ya kuwashirikisha wananchi kwenye uwekezaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker.  Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia) akizungumza na wanahabari kufafanua hali ya hisa nchini na kuipongeza NMB kwa hatua ya kuwashirikisha wananchi kwenye uwekezaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker.[/caption]   BENKI ya NMB imetoa ofa ya hati fungani kwa wananchi wanaotaka kuwekeza kwa muda wa miaka mitatu katika mtaji wa benki hiyo, huku wakijipatia faida ya asilimia 13 ya fedha waliyowekeza kwa kila miezi sita. Ofa hiyo imefunguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker. Alisema NMB itauza hati fungani ya thamani ya shilingi bilioni 20 ikiwa ni njia ya kuwashirikisha wananchi kuwekeza fedha zao na kujipatia faida. Akifafanua zaidi, Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas alisema ofa ya chini kwa kila anayetaka nunua hati fungani hizo ni kuanzia shilingi 500,000 na kuendelea kulingana na uwezo wa mtu kwa kiasi atakachoitaji kukiweka katika mtaji wa NMB..Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.[/caption]   Alisema wawekezaji hao wataanza kupata gawio lao la asilimia 13 kwa kiasi ulichowekeza baada ya miezi sita na litaendelea kutolewa kila baada ya miezi sita kwa kipindi cha miaka mitatu. Aliongeza kuwa baada ya kutimia miaka mitatu mwekezaji atalipwa fedha yake pamoja na asilimia 13 ya kiasi alichowekeza. Hati fungani hizo zitaanza kuuzwa kwa wananchi kuanzia Mai 10 hadi Juni 8, 2016 ambapo ofa itafungwa na utaratibu wa kupangwa kwa hati hizo kuanza. Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwekeza fedha zao hasa wale wanaohifadhi fedha bila kuzizalisha kwani wataziongezea thamani.Mmiliki wa Blogu ya Father Kidevu, Mroki Mroki (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) mara baada ya hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mmiliki wa Blogu ya Father Kidevu, Mroki Mroki (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) mara baada ya hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.