LUKUVI ATOA HATI 154 KWA WAKAZI WA BUNDA MKOANI MARA

December 22, 2016


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi Hati ya Kumiliki Ardhi Bibi Ester Lukondo mkazi wa Bunda Mkoani Mara, ambaye ni miongoni mwa wakazi 154 waliopelekewa Hati hizo na Waziri wa Ardhi Wilayani Bunda badala ya wakazi hao kuzifuata Mkoani Mwanza.
     Wananchi wa Musoma mjini wakikwasilisha Kero zao za migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ili aweze kuzipatia ufumbuzi.
   Wananchi wa Bunda wakikwasilisha Kero zao za migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ili aweze kuzipatia ufumbuzi.
  Waziri Lukuvi akikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya nyumba 50 zinazokaribia kukamilika.
    Waziri Lukuvi akikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya nyumba 50 zinazokaribia kukamilika.
 Jengo la Biashara la Musoma Mjini lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo Waziri Lukuvi alifika kuangalia maendeleo yake.
 Jengo la Biashara la Musoma Mjini lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo Waziri Lukuvi alifika kuangalia maendeleo yake.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa ndani ya jengo hilo.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa ndani ya jengo hilo.


Na. Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi Hati 154 za Kumiliki Ardhi kwa wakazi wa wilaya ya Bunda Mkoani Mara wakati alipofanya ziara ya siku mbili ya utatuzi wa Migogoro ya Ardhi mkoani humo. 

Lukuvi alitoa hati hizo kwa wananchi wa Wilaya ya Bunda ili kuwarahisishia wakazi hao utaratibu wa kupata hati zao pale walipo badala ya kuzifuata Mkoani Mwanza katika ofisi za Kamishana Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwawa.

Aidha, Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi ametatua migogoro ya Ardhi ya wananchi wa Musoma mjini na wananchi wa Bunda walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kupokea vielelezo vya kero za wananchi zaidi 300 walizoziwasilisha kwa Waziri ili azitolee maamuzi.

Waziri Lukuvi alikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya nyumba 50 zinazokaribia kukamilika, ambapo alimtaka Meneja wa Mradi wa NHC mkoa wa Mara Frank Mambo kukamilisha mradi huo ndani ya miezi mitatu.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.

Aidha, Mhe. Lukuvi baada ya ziara hiyo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo pia atatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo katika wilaya za Arumeru na Karatu.

Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desesmba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani Chato

Ubungo hali tete,yaelemewa na Abiria wa mikoa ya kaskazini

December 22, 2016



Mmoja wa abiraia aliyekosa usafiri katika kituo cha mabasi Ubungo akiwa amekaa chini na mtoto wak mara baada ya kuchoka na kadhia ya kukosa usafiri.
Sehemu ya kituo cha mabasi Ubungo ikionekana kwa juu majira ya saa mbili asubuhi huku abiria wakiwa wengi kuliko magari

Wananchi wakiwa wamemzunguka afisa wa SUMATRA akiwa amezungukwa na wasafiri mbalimbali ambao wamekosa usafiri
Abiria waliokosa usafiri wakiwa kando ya kituo cha Polisi. Usalama barabarani wakisubiri kupewa huduma
Sehemu ya kituo cha mabasi Ubungo ikionekana kwa juu majira ya saa mbili asubuhi huku abiria wakiwa wengi kuliko magari
Abiria wakiingia katika daladala,inayofanya safari zake Gongolamboto na Simu 2000 likiwa katika kituo kikuu cha mabasi ubungo likipakianabria wa kwenda mkoa wa Kilimanjaro.
 

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Hali ya usafiri imeendelea kuwa tete katika kituo kikuu cha mabasi  Ubungo kutokana kuwepo kwa uhaba wa usafiri kwa wasafiri wanaokwenda mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania na Nyanda za juu kusini.

Globu ya jamii ilifika katika kituo hicho cha mabasi na kujionea ni jinsi gani wasafiri wakipata taabu ya kupata mabasi,licha ya mammlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu (SUMATRA) kuomba wenye magari yenye vigezo kufika katika kituo hicho kwa ajili ya kupewa kibali cha kusafirisha abiria mikoani.

Akizungumza na globu ya Jamii,Mwananchi mmoja wa wasafiri anayekwenda Rombo mkoani Moshi, Elikunda Towo, amesema kuwa walikuwa wakihitaji usafiri tangu jana lakini wamekosa .

"Magari yaliyopo hapa yanagoma kupakia abiria yakisema kuwa ni mabovu na hawana uhakika wa safari ,hivyo hawawezi kupakia lakini ghafla unaona basi limejaa na linaondoka, sasa tunajiuliza hizo basi abiria wanapakilia kwa staili ipi,huku Sumatra wakiwa wamejazana hapa katika kituo cha mabasi" anasema huku akihoji abiria huyo .

Ameongeza kuwa ni vyema serikali ikandeleza umakini katika kusimamia magari hayo,ili abiria waweze kusafiri kwa uhakika kuliko ilivyo hivi sasa.ambapo  kundi kubwa la abiria likiwa linakaa hapo Kituoni Ubungo bila mafanikio yoyote ya kupata usafiri.

Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jamila Mwampulule amesema kuwa walifanikiwa kukata tiketi katika basi la Rungwe, lakini ilivyofika asubuhi wakajikuta wanarudishiwa nauli kwa kuambiwa basi loa ni bovu huku kukiwa hakuna usafiri mwingine mbadala wa kwenda Mbeya.

LIGI KUU (VPL) KUENDELEA TENA KESHO

December 22, 2016


 LIGI kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kesho  Ijumaa kwa mchezo  Na. 129 utakaozikutanisha timu za African Lyon na Young Africans kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam  utakaochezeshwa na Mwamuzi, Ludovic Charles kutoka mkoani Tabora akisaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya (Mshika Kibendera Na. 1) na Alnord Bugado wa Singida (Mshika Kibendera Na. 2), Mwamuzi wa Akiba – Mezani anatarajiwa kuwa Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam.

Jumamosi Desemba 24, 2016 kutakuwa na mechi sita ya Mbeya City na Toto African kwenye Uwanja wa Sokoine jijiji Mbeya katika mchezo Na. 130 utakaosimamiwa na Kamishna George Komba wa Dodoma wakati Mwamzi wa kati atakuwa Shakaile ole Shangalai wa Pwani huku wasaidizi wake wakiwa ni Khalfan Sika pia wa Pwani na Vecent Milabu wa Morogoro. Mwamuzi wa akiba atakuwa Cherles Mwamlima.

Mchezo Na. 131 utazikutanisha timu za Kagera Sugar na Stand United katika Uwanja wa Kaitaba, uliko Kagera ambako utasimamiwa na Kamishna Nassoroi Hamduni wa Kigoma huku Mwamuzi akiwa ni Jacob Adongo wa Mara akisaidiwa na Joseph Masija na Robert Luhemeja kutoka Mwanza na Mezani atakuwa Jonesia Rukyaa wa Kagera.

Ndanda itaendelea kubaki nyumbani kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na baada ya kucheza na Simba juma lililopita na kupoteza mchezo huo, safari hii inaikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo Na. 132 utakaosimamiwa na Kamishna Jimmy Lengwe wa Morogoro wakati Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba wa Pwani akisaidiwa na Haji Mwalukuta wa Tanga na Jeremiah Simon wa Dar es Salaam. Mezani atakuwa Abubakar Mtulo.

 Mchezo Na. 133 utafanyika Uwanja wa Uhuru, kati ya
 Simba na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam 
utasimamiwa na Tito Haule wa Morogoro na kuchezeshwa na Mwamuzi Hans Mabena wa Tanga akisaidiwa na Omari Kambangwa wa Dar es Salaam na Khalfan Sika wa Pwani wakati Mbaraka Rashid wa Dar es Salaam atakuwa Mwamuzi wa Akiba – mezani.







 Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Azam FC ya Dar es Salaam  k
atika mchezo huo ambao Mwamuzi atakuwa Ngole Mwangole wa Mbeya akisaidiwa na Mirambo Tshikungu na Mashaka Mwandembwa – pia wote wa Mbeya huku kamishna akiwa ni David Lugenge wa Iringa.



Mwadui atakuwa mwenyeji wa  Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga kwenye mchezo huo Na. 135, utakaosimamiwa na Kamishna Staricko Nyikwa wa Singida na mw


aamuzi atakuwa ni Emmanuel Mwandembwa akisaidiwa na Abdallah Uhako na Agnes Pantaleo wote wa Arusha na mezani anatarajiwa kuwa Ezekiel Mboi wa Shinyanga.


 Desemba 26,  Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo Na 136 na 




Manyama Bwire wa Dar es Salaam atakuwa Kamishna wa mchezo huo wakati Mwamuzi ni Forentina Zabron wa Dodoma akisaidiwa na Hassan Zani wa Arusha na Silvester Mwanga wa Kilimanjaro. Mwamuzi wa akiba - Mezani atakuwa Andrew Shamba wa Pwani.

Desemba 28, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili ambako Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na. 137 ambako Juma Chiponda wa Tanga atakuwa kamishna wa mchezo huo. 



Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakuwa Eric Onoca wa Arusha akisaidiwa na Michael Mkongwa wa Njombe na Janeth Balama wa Iringa. Mwamuzi wa akiba atakayekaa mezani atakuwa Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam.

Kadhalika siku hiyo, Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Mvomero katika mchezo Na. 138 utakaosimamiwa na Kamishna Pius Mashera wa Dodoma, utachezeshwa na Mathew Akrama kutoka Mwanza akisaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Gasper Ketto wa Arusha. Mwamuzi wa akiba atakuwa Selemani Kinugani.

Kadhalika Desemba 29, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili. Ruvu Shooting ya Pwani inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam katika mchezo ambao mwamuzi atakuwa Alex Mahagi wa Mwanza.

Katika mchezo huo Na. 139, Mahagi atasaidiwa na Ferdinand Chacha pia wa Mwanza na Rashid Zongo wa Iringa huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hellen Mduma wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Peter Temu wa Arusha.

Azam itavaana na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo Na. 140 utakaosimamiwa na Elizabeth Kalinga wa Mbeya huku Mwamuzi akiwa ni Jimmy Fanuel wa Shinyanga huku wasaidizi wake wakiwa ni Makame Mdog pia wa Shinyanga na Abdallah Mkomwa wa Pwani huku Kassim Mpinga akiwa ni mwamuzi wa akiba.

Kamishna anatarajiwa kuwa Nassib Mabrouk wa Mwanza na Mwamuzi ni Isihaka Mwalile na wasaidizi wake ni Hellen Mduma na Omary Kambangwa – wote kutoka Dar es Salaam. Julius Kasitu wa Shinyanga anatarajiwa kuwa Mwamuzi wa Akiba.

Kadhalika siku ya funga mwaka, Mbeya City inatarajiwa kucheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika Mchezo Na. 143 ambao msimamizi wa mchezo atakuwa Joseph Mapunda wa Ruvuma.

Mwamuzi katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Hussein Athuman wa Katavi wakati wasaidizi wake watakuwa ni Lulu Mushi wa Dar es Salaam na Nicholaus Makaranga wa Morogoro. Mwamuzi wa Akiba Mezani atakuwa Mashaka Mwandembwa wa Mbeya.

Januari mosi kutakuwa na michezo miwili tu ya kukaribisha Mwaka Mpya ambako Toto African ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo Na. 144 utakaosimamiwa na Jovin Bagenda wa Kagera. Mwamuzi atakuwa Israel Nkongo sambamba na wasaidizi wake Soud Lila na Frank Komba, wote wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba mezani atakuwa Mathew Akrama wa Mwanza.

Pia African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu katika mchezo Na. 142 utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kamishna atakuwa Hamisi Kitila wa Singida wakati Mwamuzi anatarajiwa kuwa Selemani Kinugani wa Morogoro wakati wasaidizi wake ni Omary Juma wa Dodoma na Agnes Pantaleo wa Arusha wakati mezani atakuwa Shafii Mohammed wa Dar es Salaam




Mara baada ya michezo hiyo, Ligi Kuu ya Vodacom itasimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari mosi, mwaka huu.