Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof Elisante Ole Grabriel katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof Elisante Ole Grabriel katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

June 19, 2016

dat1 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kijiji cha Mtama  (hawapo pichani) wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa vituo vya Redio na Televisheni vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).dat2 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel( wa pili kulia) akizungumza na wawakilishi Kutoka Star Times wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kulia ni Mkurugenzi wa Shirika  hilo Dkt Ayoub Riyoba.
dat3 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja wawakilishi kutoka kampuni ya Star Times na wanakijijji wa kijiji cha Mtama wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Lindi Bw. Matei Makwinya.
 
PICHA NA WHUSM

MTUMISHI WA MUNGU MASANJA MKANDAMIZAJI ARINDIMA KATIKA MKUTANO WA OYES 2016 JIJINI MWANZA.

June 19, 2016
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016 wenye lengo la kuwafungua watu wote kiroho na hivyo kuondokana na vifungo mbalimbali vinavyowakabiri, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mkutano huo ulianza June 12,2016 na kufikia tamati jana June 19,2016 katika viwanja vya Kanisa hilo. Wahubiri na waimbaji mbalimbali walihudumu katika mkutano huo akiwemo Mchungaji wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone ambae amewahi kufariki na kufufuka siku ya nne, Mwimbaji na Mhubiri Joseph Rwiza pamoja na Mwimbaji Chamwenyewe Jembe ambapo watu wengi walifunguliwa kiroho na kuokoka katika mkutano huo.
Na George Binagi-GB Pazzo

MAALIM SEIF AKHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI MAREKANI

June 19, 2016
Na Mwandishi wetu Washington 
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), maalim Seif Sharif Hamad, jana alimaliza ziara yake nchini Marekani iliyochukua muda wa wiki moja.
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), maalim Seif Sharif Hamad (Picha na http://swahilivilla.blogspot.com/) Maalim Seif alikhitimisha ziara yake hiyo kwa mkutano wa hadhara ambapo alipata nafasi ya kuongea na Watanzania waishio nchini humu.
Katika Mkutano huo, mwanasiasa huyo gwiji nchini Tanzania alisema kuwa lengo la ziara yake ni kuuelezea ulimwengu kukhusu kile kilichotokea Zanzibar kufuatia uchaguzi wa Oktoba 25 na mwelekeo wa demokrasia nchini Tanzania kwa ujumla.
Aliielezea ziara yake hiyo nchini Marekani kuwa imezaa matrunda. “Sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa tumeeleweka na ziara yetu imezaa matunda” alisema Maalim Seif.
Sehemu ya hadhira wakimsikiliza kwa makini Maalim Seif
Kukhusiana na zoezi la uchaguzi wa mwaka jana Visiwani Zanzibar, Maalim Seif alisema kuwa, uchaguzi huo ulihudhuriwa na waangalizi wa Kimataifa na wa ndani kutoka pande zote za Muungano, Bara na Zanzibar, na wachunguzi wote hao walithibitisha kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. “Waangalizi wote, wote kabisa, walikiri kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki”, alisisitiza kiongozi huyo na kuongeza kuwa “Ulikuwa uchaguzi bora kabisa kuliko chaguzi zote zilizotangulia Zanzibar”
Aliuulezea mchakato wa uchaguzi kuwa ulikwenda vizuri mpaka kufikia tarehe 27 Oktoba ambapo jumla ya Majimbo 34 ya uchaguzi yalikuwa tayari yameshatangazwa, na mengine 9 yakiwa yameshahakikiwa ikiwa bado kutangwazwa tu. Na kwa upande wa udiwani na Uwakilishi, uchaguzi ulikuwa umeshakamilika na washindi kupewa shada zao za ushindi.
Wakulima wa zao la Shahiri wanaoshirikiana na TBL Group waadhimisha siku yao

Wakulima wa zao la Shahiri wanaoshirikiana na TBL Group waadhimisha siku yao

June 19, 2016

Wakulima wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania wanaoshirikiana na kampuni ya TBL Group wameadhimisha siku yao wilayani Karatu ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha wakiwemo wadau wao kutoka SABMiller,na makampuni mengine yanayouza  madawa na pembejeo za kilimo.
Wakulima waliweza kufanya maonyesho mbalimbali  ya kazi zao pia walielezea mafanikio walioweza kuyapata kutokana na kilimo cha zao la Shahiri
SHAI1 
Maofisa wa SABMiller na wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia TBL Group ilitunukiwa tuzo kwa kendeleza kilimo cha zao la Shahiri nchini
SHAI2 
Mkuu wa  Uendelezaji Kilimo cha Shahiri wa SABMiller kanda ya Afrika Thinus  Van Schoor akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Shahiri
SHAI3 SHAI4 
Wakulima wa Shahiri wakitembeza wageni mashambani
SHAI5 
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha (kulia) akimpongeza mkulima aliyejishindia zawadi ya kabati 2/4-Wakulima wa Shahiri wakitembeza wageni mashambani
SHAI6 
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha (kushoto) akimpongeza mkulima wa Shayiri kutoka Kijiji cha Lendikinya wilaya ya Monduli,Masiaya Oloshuda aliyeshinda kwenye bahati nasibu ya kupata vifaa vya usalama shambani
SHAI7 
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akihutubia wananchi
IGP Mangu -AKAGUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA KUPOKELEA SIMU ZA DHARURA (CALL CENTRE)

IGP Mangu -AKAGUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA KUPOKELEA SIMU ZA DHARURA (CALL CENTRE)

June 19, 2016

G1 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo  ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
G2 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo  ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
G3 
Askari Polisi wakiwa katika mafunzo maalumu ya kupokea simu katika kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni  ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI CHA HOROHORO

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI CHA HOROHORO

June 19, 2016

1 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro,wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga.Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
2 
Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiweka saini katika kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga.Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti  njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
3 
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Horohoro, DCI Deogratius  Magoma, akimuelekeza jamboKatibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira mara baada ya ukaguzi wa ofisi za jengo la kituo hicho zinazotumika katika utoaji huduma za uingiaji na utokaji wa raia wa kigeni na raia wa Tanzania wanaopitia mpaka wa horohoro , wilayani Mkinga, jijini Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
4 
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga,DCI Andrew Kalengo, akimuelekeza jambo  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,mara baada ya kutembelea daraja la Mwakijembe, linalotumiwa na wakazi wa nchi za Tanzania na Kenya. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
5 
Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa kiraia), akifafanua jambo kwa viongozi wa Idara ya Uhamiaji Wilayani Nkinga, mara baada ya kutembelea jiwe linaloonyesha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kijiji cha Jasini kilichopo Kaunti ya Kwale. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua  na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
6 
Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akionyeshwa namba za jiwe la mpaka unaotenganisha nchi za Kenya na Tanzania mara baada ya kutembelea kituo cha Uhamiaji Horohoro. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua  na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Tumieni nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima kukabiliana na njaa - Waziri Mhagama

June 19, 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly kukagua shamba la mihogo la mkulima wa kijiji cha Nga’mbi wilayani humo Bahati Mtonyi (kushoto), aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa, Bahati Mtonyi, aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa (kulia kwake) Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje, (kushoto) Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly na Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Brig.Jen, Mbazi Msuya, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje kukagua mashamba ya muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mpwapwa, John Tembo, jinsi gereza hilo lilivyo panda mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo wilayani Mpwapwa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akifurahia mihogo iliyovunwa katika mashamba ya wakulima kijijini Mazae wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, mara baada ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akinawishwa mikono na Mkuu wa Gereza la Mpwapwa, John Tembo, mara baada ya kuonja chakula cha wafungwa wa gereza hilo, wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Katikati) Mkurugenzi idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akishiriki kuonja chakula cha wafungwa wa Gereza la Mpwapwa wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Kulia kwake), Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje na (kushoto) Mkurugenzi idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MUU).

WAZIRI wa ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge vijana ajira kazi na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama, amemwagiza mkuu wa wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha anatumia nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima ili kukabiliana na tatizo la njaa ambalo limekuwa likiukabili mkoa wa Dodoma.

Mhagama aliyasema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa zao la mhogo ambao walihamasishwa kulima zao hilo linalostahimili ukame ili kukabiliana na njaa.

Alisema kuwa katika kuhakikisha tatizo la njaa linakwisha mkuu wa wilaya huyo anatakiwa kuweka mikakati mipya ambayo itakuwa na tija katika kuhakisha njaa inakwisha wilayani hapo.

Aidha alisema kuwa uongozi wa wilaya hiyo unatakiwa kubuni mikakati mipya tofauti na ile ya zamani ili kutumia nguvu kazi iliyopo katika kushiriki kilimo na kusaidia kuondokana na tatizo la njaa.

“Kama mtaendelea na mikakati yenu ya kila siku tatizo la njaa halitakwisha mnatakiwa hivi sasa kutumia nguvu lazimisheni wananchi walime mazao yanayostahimilimi ukame kama mihogo na mtama”alisema Mhagama.

Alisema kuwa ofisi ya waziri mkuu kupitia kitengo cha maafa ilitoa sh. Milioni 35 kwajili ya kununua mbegu za mihogo na mtama kwajili ya wananchi ya wilaya hiyo waliokuwa wanakabiliwa na baa la njaa.

Aliongeza kuwa kwa namna alivyo jionea maendeleo ya baadhi ya wakulima waliolima mihogo wameweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na baa la njaa kwa kipindi kirefu.

“Kwa hali hii basi sisi kama ofisi wa waziri mkuu hatuna haja ya kuendelea kuleta chakula cha msaada tena huku kwakuwa zao la mihogo ambalo sisi tulileta mbegu imeweza kuwasaidia wakulima kuondokana na njaa lakini pia wengine wamejenga nyumba na kuezeka kwa bati”alisema Mhagama.

Aidha Mhagama alisema kuwa kutokana na wakulima hao kuonyesha mafanikio uongozi wa wilaya hiyo uongeze bidii katika kuhamasisha kilimo cha zao hilo.

“Inabidi muwe na hata sheria ambazo zitawalazimisha wananchi kila mmoja wao kulima heka mbili za muhogo na mbili zingine za mtama na katika hili msimbembeleze mtu tumieni nguvu ili kuweza kuondokana na na tatizo la njaa mkoani hapa”alisema.

Hatahivyo alimwagiza ofisa kilimo wa wilaya Yustina Munishi , kuhakisha idadi ya wakulima inaongezeka tofauti na iliyopo hivi sasa.

“Hadi mwakani tarehe kama ya leo nataka kuja kukaguma mashamba zaidi ya 300 na kama sitayakuta kwa idadi hiyo utakuwa huna kazi afisa kilimo”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly alisema kuwa watakipanga kuhamasisha kilimo cha zao hilo la muhogo ambalo limeonekana kuwa mkombozi wa njaa.

“Katika kipindi kijacho cha kilimo kupitia mikakati yetu tutahakikisha kila kaya inalima heka mbili za mhogo na heka mbili za mtama ili kuondokana na baa la njaa ambalo limekuwa likiikabili wilaya hiyo kila mwaka”alisema Utaly.

Naye mmoja wakulima hao Bahati Mtonyi,alisema kuwa kupitia zao hilo la muhogo ameweza kujenga nyumba na kujilipia ada kila mwaka kiasi cha sh. 600.000.

KUPANDA MABASI YA MWENDO WA HARAKA JIJINI DAR ES SALAAM SASA NI KWA KADI HUDUMA HIYO KUANZA RASMI KESHO

June 19, 2016
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart),  David Mgwasa (kushoto),akionesha kipeperushi chenye maelezo ya matumizi ya kadi zitakazotumika katika mabasi hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Habari UDART, Deus Bugaywa.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabar ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MRADI wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART,  David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.

"Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu" alisema Rajabu

Aliongeza kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya kuzoeleka.

Alisema licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaenelea kama kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na hu duma hiyo unatakiwa kupiga *152*22#

MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU MAKATIBU WAKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI

MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU MAKATIBU WAKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI

June 19, 2016

KIT01 
Wakufunzi wa mafunzo ya Uongozi kutoka Chuo cha Uongozi Institute Dkt. Jochen Lohmeier (kushoto) na Nathaniel Mjema wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza mafunzo ya siku tatu kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Serikali ya Zanzibar yaliyofanyika katika Ofisi Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Maisara Mjini Zanzibar.
KIT1 
Mkufunzi Nathaniel Mjema akiwasilisha mada ya  kujitathmini kwa viongozi wanaoshiriki mafunzo ya uongozi yaliyowashirikisha Makatibu wakuu na wasaidizi wao.
KIT2 
Waratibu wa Mafunzo hayo wakifuatilia kwa kina uwashilishwaji wa mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo.
KIT4 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum akitoa mchango katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya  Maendeleo endelevu yaliyowashirikisha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Serikali ya Zanzibar.
KIT6 
Dkt. Jochen Lohmeier kutoka Uongozi Institute akitoa mada kuhusu kuitathmini Jamii katika mafunzo ya Makatibu wakuu na Wasaidizi wao yanayofanyika Ofisi ya CAG Maisara, Mjini Zanzibar.
KIT7 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Ali Khalil Mirza (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Juma Ali Juma wakinakili mafunzo hayo.
KIT8 
Washiriki wa mafunzo hayo wakibadilishana mawazo na kujadiliana kutokana na kazi waliyopewa na wakufunzi wao.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR JANA

KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR JANA

June 19, 2016

KAMA01Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye Ofisi Ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Juni 18, 26. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu))
KAMA1 
Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi  wakifuatilia kikao cha Kamati  Kuu ya CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwenye Ofisi ndogo ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Juni 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KAMA2 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wakati alipofungua kikao chao kwenye Ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Juni 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KAMA3Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson mara baada ya kumaliza kikao maalum kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es salaam ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
KAMA4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson mara baada ya kumaliza kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM  kilichofanyika , Makao makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
SENDE

UTALII WA NDANI WAZIDI KUPATA MASHIKO ,WASOMI CHUO KIKUU SMMUCo WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO

June 19, 2016

Simba dume  akiwa anaunguruma 
Simba jike akiwa amepumzika kwenye nyasi 
Na Dickson Mulashani

Suala la utalii wa ndani limeonekana kupata mashiko baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) kuhamsika na kuamua kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngoro ngoro ili kujionea vivutio vya kipekee vinavyopatikana humo.
Wanafunzi hao wakiwa katika geti la kuingia hifadhi ya Ngoro ngoro

Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi hao Emmanuel Kalenzi amesema waliguswa kupanga ziara hiyo kuunga mkono wadau mbali mbali wanaohamasisha utalii wa ndani ili kuweza kuwa mabalozi kwa wengine. “Sisi kama wasomi ndio tunapaswa kuwa mabalozi kwa jamii inayotuzunguka na ili uwe balozi mzuri basi uwe umashajionea kwa macho”  alisema.

Nyati dume mwenye umri mkubwa ambaye tayari ametengwa na kundi lake 
Ndege aina ya Cranes nao wanapatikana katika eneo la crater

Nyumbu akiwa amepumzika mara baada ya kula nyasi