HIVI NDIVYO COASTAL UNION ILIVYOICHAPA NDANDA SC JANA KWENYE UWANJA WA CCM MKWAKWANI

October 05, 2014


Mchezaji wa Ndanda Gideon Benson akiangalia ampasie nani mpira wakati wa mechi yao na coastal union mpambano uliofanyika katika uwanja wa mkwakwani Tanga Coastal ilishinda 2.1

 Mchezaji wa timu ya Ndanda Nassoro Kapama akikimbilia mpira uliokufa kwa ajili ya kurusha nyuma ni Abdallah Mfuko wa timu ya Coastal union mchezo huo Ndanda walifungwa goli mbili kwa moja
Mchezaji wa Ndanda Gideon Benson  akitafuta mbinu ya kumtoka Mchezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga Rama Salim wakati wa mechi yao iliyofanyika jijini Tanga Coastal walishinda bao 2.1 Picha
Mashabiki wa Coastal wakiangalia mpira


Kocha wa timu ya Coastal Union ya TANGA AKIOJIWA
Mashabiki wa timu ya ndanda wakishindwa kuhamini macho yao ya kinachotokea baada ya kubugizwa bao 2.1 na coastal katika uwanja wa mkwakwani
Shabiki wa ndanda aliyejitambulisha kwa jina la Kadio Rashidi akiwa amejichola chola mgongoni
Raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mpambano wa Ndanda na Coastal uliokuwa ukipigwa katika uwanja wa mkwakwani Tanga Costal ilishinda 2.1

Raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mpambano wa Ndanda na Coastal uliokuwa ukipigwa katika uwanja wa mkwakwani Tanga Costal ilishinda 2.1

Kundi la”WAKALI SISI”latimka na Milioni 5 za shindano la Dance100% 2014

October 05, 2014

Hatimaye kundi la”Wakali sisi” lenye makazi yake Kiwalani jijini Dar es Salaam, ambalo lilikuwa miongongoni mwa makundi matano yaliyoingia fainali za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% linaloratibiwa na Kituo cha East Africa Television ltd na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, limeibuka mshindi katika shindano hilo lililokuwa la kukata kwa shoka kwa ushindani mkali katika Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam. 

 Mratibu wa shindano hilo Happy Shame alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, fainali za shindano hilo ambalo safari yake ilianza Julai 19, mwaka huu kuanzia hatua ya kusaka washiriki hadi mchujo lilishirikisha makundi matano.
 Shame alisema, shindano la mwaka huu lilikuwa gumu na lenye kuleta msisimko wa aina yake zaidi kuliko miaka miwili iliyopita baada ya mambo mbalimbali kuboreshwa na zaidi kiasi cha vijana kuwa wabunifu na kuona ni fursa kwao sio tu kupata fedha, pia kuendeleza vipaji vyao na kujinasua kiajira. 
 “Ushindani umekuwa mkubwa sana katika shindano la mwaka huu ikilinganishwa na miaka mingine kutokana na sababu mbalimbali. Shindano pia limeanza kupata mashabiki, tunashukuru sana sapoti ya wadhamini wetu Vodacom Tanzania,” alisema. 
 Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alieleza kwa niaba ya kampuni aliridhishwa kabisa na matokeo na aliwapa pongezi kundi la wakali sisi kwa kuipuka na ushindi huo. 
 Nkurlu alisema kuwa, kundi hilo lilistahili ushindi kwasababu lilikuwa makini na kufurahia kwa kile walichokuwa wanakifanya kwa moyo mkunjufu na kujitambua kana kwamba wapo kazini. 
 Alisema kampuni ya Vodacom inajivunia na kujisikia fahari kwa kudhamini shindano hilo kwa njia hiyo ya udhamini wakitambua umuhimu wa vijana kujiajiri kupitia vipaji vyao na kuongeza kuwa, kwa kipindi chote cha mchakato wa shindano hilo, amejifunza mengi kutoka kwa vijana hao walioshiriki katika shindano hilo kuwa ubunifu ni kitu muhimu sana. 
 “Vijana wameonyesha uwezo mkubwa kuanzia hatua ya mchujo hadi sasa kiasi cha kuwapa majaji wakati mgumu. Tunaamini hata baada ya fainali hizi, vijana hawa watajiendeleza zaidi kimuziki,” alisema Nkurlu. 
 Makundi matatu yaliyofanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali katika hatua ya fainali hiyo na vijana walikuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wakali sisi walioibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 huku kila mshiriki katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone ikiwa na muda wa maongezi wa sh. 100,000.
Mshindi wa pili ni kundi la The W.T. na kuondoka na kitita cha shilingi Milioni 1 na laki 5 na mshindi wa tatu ni kundi la Wazawa Crew na kujinyakulia shilingi laki 5. 
 Nkurlu aliyapongeza makundi yote hata ambayo hayakufanikiwa kushinda na kuyatakia kila la heri na yatipange upya kwa mwakani kwani asiye kubali kushindwa si mshindani aliongeza kuwa, kwa vile vijana hao wamejiweka katika mazingira ya kutumia vipaji vyao kujipatia ajira, Kampuni ya Vodacom-Tanzania inaona fahari kudhamini shindano hilo wakisaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo la ajira. 
 “Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka vijana zaidi ya 800,000 wanaingia katika soko la kusaka ajira ndio maana, Vodacom Tanzania kwa kulitambua hilo, tumekuwa mstari wa mbele kusaidiana na serikali na wadau wengine kuwajengea vijana msingi,” alisema Nkurlu.
Kikundi cha The WT cha jijini Dar es Salaam kilichoshinda nafasi ya pili katika fainali ya shindano la Dance 100% 2014 likionesha umahiri wao wa kudansi katika fainali hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.Ambapo kundi la”WAKALI SISI”toka kiwalani jijini liliibuka na ushindi huo na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Umma  wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akitaniana na kiongozi wa kundi la”Wakali sisi”la kiwalani jijini Dar es Salaam,Baraka Kambona(kushoto)alipokuwa akikabidhi hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 5 kwa kundi hilo kama wadhamini wakuu wa shindano la Dance 100% kundi hilo liliibuka washindi katika fainali  ya shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam
Washindi wa shindano la Dance 100% 2014 kundi la wakali sisi wakiwa kwenye picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo na Ofisa matukio  wa Basata Kurwijira Magesa (kushoto)pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili toka kulia) mara baada ya kutangazwa washindi wa shindano hilo na kujinyakulia kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la ”The Winners Crew” la jijini Dar es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa fainali wa shindano hilo lililoandaliwa na EATV lililofanyika  kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,ambapo kundi la”WAKALI SISI” liliibuka washindi na kunyakua kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Meneja mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Kinondoni, Edward Byampanju(kushoto)na Meneja uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(katikati)wakijadiliana jambo wakati wa fainali ya shindano la Dance 100% 2014.ambapo kundi la”Wakali sisi”liliibuka washindi na kukabidhiwa   kitita cha shilingi milioni 5 na wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania,watatu toka kushoto ni Afisa Matukio wa Basata, Kurwijira Maregesi.
Kundi la”Wakali sisi”ambao ni mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014,wakionesha umahiri wao wa kucheza wakati wa fainali ya shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuweza kujinyakulia kitita cha Tsh Milioni 5 toka kwa mdhamini mkuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofurika katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam kushuhudia mchuano mkali wa fainali ya Dance 100% ambapo kundi la Wakali sisi liliibuka na ushindi na kuweza kuondoka na kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa mdhamini mkuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.

MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA JD COMPLEX – KIBAHA, PWANI

October 05, 2014


Mgeni Rasmi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwantumu Mahiza (aliyesimama) akisisitiza jambo alipokua akifungua kikao cha Baraza hilo.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Tume ya Mipando kwa pamoja wakiimba wimbo wa Solidarity Forever kuonyesha mshikamano makazini.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakionyesha mshikamano kwa kuimba wimbo wa Solidarity forever mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kufungua rasmi kikao hicho.
Kabla ya kuanza majadiliano, wajumbe walimchagua Mwenyekiti Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi ambapo Bibi Magreth Simwela (aliyesimama) aliibuka mshindi kati ya wajumbe watatu waliokua wakigombea nafasi hiyo. Hapo Mwenyekiti Msaidizi alikua akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza (Walioketi wa pili kushoto). Walioketi pamoja nae kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Bibi Florence Mwanri, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mipango, Bw. Steven Katemba na Katibu wa Baraza Bw. Senya Robert.