Joint UN Women and UNESCO Message for International Women's Day - 08 March 2017

Joint UN Women and UNESCO Message for International Women's Day - 08 March 2017

March 07, 2017
Joint Message from UN Women Representative, Maria Karadenizli and UNESCO Head of Office and Representative for the United Republic of Tanzania, Ms Zulmira Rodrigues on International Women’s Day -Everybody has a stake in promoting equality between men and women, at all levels of society “The story of women's struggle for equality belongs to no single feminist nor to any one organization but to the collective efforts of all who care about human rights.” These words by activist Gloria Steinem testify to the universal nature of the fight for women’s rights and once a year, on 8 March, we restate our commitment to gender equality as a force driving dignity for all. Inequality between men and women penalizes societies at all levels of development. The violence, injustice and stereotypes suffered by too many women in their personal or professional lives undermine society as a whole, and deprive of it considerable potential for creativity, strength and confidence in the future. As the United Nations has adopted the ambitious 2030 Agenda for Sustainable Development, the full empowerment of girls and women is one of humanity’s most powerful levers for development. Rural women are directly responsible for the production of half the world’s food – and it is primarily women who manage and gather natural resources. Ninety per cent of rapes in the world take place precisely when women are on their way to collect water or firewood. Two thirds of illiterate adults in the world are women. One in three women is subject to physical violence in the private sphere, and the wage gap between men and women, for equal work and with equal skills, is a fact across the world. For UNESCO, the main engine for change rests on education, training, and the possibility given to all girls and women of pursuing careers in research, politics and culture. Equality also lies in ridding the media and collective imagination of prejudice by highlighting the women scientists, artists and politicians who are moving humanity forward in all fields. On the occasion of this 2017 International Women’s Day, UNWOMEN and UNESCO call on all to make a commitment to women’s’ rights, and thereby enhance rights and dignity for all. -- Zainul A. Mzige, Managing Director, Mzige Media Limited, www.thebeauty.co.tz +255714940992.

MKUTANO WA KUHITIMISHA MCHAKATO WA RASIMU YA SERA YA MILIKI BUNIFU WAFANYIKA JIJINI DAR

March 07, 2017
 Kikao cha siku tano cha wabobezi/wataalamu katika mambo ya miliki bunifu,kinaendelea kufanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano katika Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO),Msasani jijini Dar,ambapo kikao hicho kimejumuisha Wadau kutoka Serikalini sambamba na Sekta binafsi.

Mchakato wa kikao hicho unafuatia wakati shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) lilipoanza kufanya mchakato wa tatifi ya sera ya miliki bunifu  tangu miaka minne iliyopita kwa kufadhiliwa na  wahisani ‘Best Dialogue’ ,ambapo mwaka 2013 inaelezwa kuwa tafiti hiyo ndio ilipelekwa rasmi Wizarani  kwa ajili ya kuendelea na mchakato zaidi.

Rais wa Shirikisho la Filamu hapa nchini (TAFF),Simon Mwakifwamba,alisema kuwa Mkutano huo wa kuhitimisha rasimu ya sera ya miliki bunifu,ni sera ambayo ilipatikana kwa kufuata taratibu zote, kwa maana ya ushirikishwaji kwa upande wa serikali na Sekta binafsi,Mwakifwamba alisema kwa upande wao kama wasanii hiyo ndio sehemu yenyewe muhimu ambayo wasanii wamekuwa wakiiliia kwa muda mrefu.

"Kwa mchakato huu sisi kama wadau tunasema kwamba hapa tulipofika tuko pazuri, na nina imani na wataalamu hawa kwamba tukiwa  na juhudi za pamoja tutaweza  kuhitmisha hii rasimu hii ya miliki bunifu na mwisho  wake tutatoka na sera nzuri ,na kama tutakuwa na msingi mzuri wa kuwa na sera nzuri itatupelekea na kuwa na sheria nzuri,tukiwa na sheria nzuri tutakuwa na  kanuni nzuri,tukiwa na vitu hivyo vitatu tunaamini serikali itakuwa imetengeneza mazingira mazuri kwa wabunifu wote katika nyanja   mbalimbali, kwamba hii sera itakuwa  yenye tija na mafanikio makubwa kwa nchi na hata kwetu  wasanii kwa ujumla".alisema Mwakifwamba.

 
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Biashara ya nje,Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Wilson Malosha akizungumza mbele ya wanahabari na Wadau  mbalimbali katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,Kulia ni Rais Shirikisho la Filamu hapa nchini,Simon Mwakifwamba.
 Wadau mbalimbali wakifutilia yaliyokuwa yakizungumzwa kutoka meza kuu,katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadh ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,
 Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,
MASAUNI ATEMBELEA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA ABEID AMANI KARUME, AAGIZA VYOMBO VYA ULINZI KUDHIBITI UINGIAJI DAWA ZA KULEVYA

MASAUNI ATEMBELEA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA ABEID AMANI KARUME, AAGIZA VYOMBO VYA ULINZI KUDHIBITI UINGIAJI DAWA ZA KULEVYA

March 07, 2017

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, wakati wa ziara ya kukagua udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani humo, huku akiagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana kudhibiti madawa hayo ambayo yanaharibu nguvu kazi ya Taifa.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, akitoa taarifa za utekelezaji wa zoezi la kudhibiti Dawa za Kulevya Visiwani humo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa ziara ya naibu waziri kufuatilia utekelezaji wa zoezi la kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya Visiwani humo.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kushoto), juu ya hatua zinazochukuliwa na Idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kukabiliana na udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya kiwanjani hapo.Wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisikiliza jinsi mifumo ya kudhibiti uingiaji haramu inavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha.Ziara ya Naibu Waziri huyo ilikua na lengo la kukagua mifumo inayotumika kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akitoa maelezo kwa watumishi wa Idara ya uhamiaji waliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiteta jambo na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Sheikh Abeid Amani Karume.


Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MeTL Group yajidhatiti kutoa ajira kwa usawa baina ya wanawake na wanaume

MeTL Group yajidhatiti kutoa ajira kwa usawa baina ya wanawake na wanaume

March 07, 2017
 Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imesema itaendeleza sera yake ya kutoa ajira bila kufanya ubaguzi wa kijinsia baina ya wanawake na wanaume. Hayo yamesemwa na mwakilishi wa MeTL Group, Catherine Decker wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya wanawake lililoandaliwa na Shirikisho la Wafanyakazi nchini Tanzania (TUCTA). Catherine amesema kampuni ya MeTL imeamua kuweka utaratibu huo wa kuweka usawa kwa wafanyakazi kati ya wanaume na wanawake ili kuwapa nafasi wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo lakini pia kuepusha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kazini.
Mwakilishi wa MeTL Group, Catherine Decker akizungumza katika kongamano la kuadhimisha siku ya wanawake.
“Kama kampuni ya MeTL imeweka sera katika kuwasaidia wanawake, sera hiyo ni kuangalia uwiano kati ya mwanamke na wanaume kila mwaka. Sababu ya kufanya hili ni kuhamasisha usawa ndani ya kampuni yetu,” amesema Catherine na kuongeza. “Kama kampuni tunatambua umuhimu wa usawa katika kuepusha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, sera hii inatusaidia katika kuwafatilia wafanyakazi wetu lakini pia inatutengenezea mazingira mazuri ya kupambana na matatizo kama ya utovu wa nidhamu na vitendo vya unyanyasaji ya kijinsia.”
Baadhi ya watu waliohudhuria kongamano hilo.
Aidha Catherine amesema MeTL imekuwa ikiandaa mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwahusisha wanawake na wanaume ili kuwakutanisha wafanyakazi wa kampuni kutoka sehemu mbalimbali kwa lengo la kufahamiana na kufurahi kwa pamoja. “Itambulike kuwa MeTL sio tu mwajiri wa wafanyakazi hawa au kampuni bali ni familia moja ambayo inalenga kuboresha maisha ya watu kwa viwango mbalimbali na huwa tunaanda matukio ya michezo ambapo wanaume na wanawake hukutana na kushiriki vyema,” amesema Catherine.
Mbunge wa Urambo, Magreth Sitta kongamano la kuadhimisha siku ya wanawake.
Kwa upande wa mgeni rasmi katika kongamano hilo, Mbunge wa Urambo, Magreth Sitta amewataka kutumia vyema nafasi za kazi wanazopata katika mashirika mbalimbali na kuwashauri kuwa ni vyema wakaweka utaratibu wa kuwashirikisha wanaume katika mipango yao. “Wanawake ni vyema mkashirikiana na wanaume, kama kuna jambo mnawambia ili kulifanya kwa pamoja, hata mimi siri ya kufika hapa nilipo ni sababu ya kuwashirikisha, mkifanya hivyo mtakuwa mmefanya jambo jema sana,” alisema Magreth.

Tigo yashirikiana na Milvik kutoa huduma za bima ya afya wanazomudu wateja

March 07, 2017

Meneja mkazi wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin(kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa huduma iliyoboreshwa ya bima kwa simu za mkononi kwa kutumia Tigopesa ijulikanayo kama Bima Mkononi, Pembeni yake ni Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanepoel.



Mteja aliyenufaika Melikizedeki Nyalufujo mkazi wa kimara , akitoa ushuhuda

Mteja aliyenufaika na huduma ya Bima Mkononi kwa kutumia Tigo pesa , Hawa Ramadhani mkazi wa Kibaha Maili Moja akiongea na waandishi wa jijini Dar Es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa huduma iliyoboreshwa ya bima kwa simu za mkononi. Wengine kutoka kushoto Meneja mkazi wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin, Mteja aliyenufaika Melikizedeki Nyalufujo mkazi wa kimara na Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanepoel.

Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanepoel(kulia) , akiongea na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa huduma iliyoboreshwa ya bima kwa simu za mkononi kwa kutumia Tigopesa ijulikanayo kama Bima Mkononi, Pembeni yake ni Meneja Mkazi wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin.

 Dar es Salaam, Machi 2017- Moja ya makampuni yanayoongoza kwa bima ndogo Tanzania  ambayo inatumia teknolojia ya simu za mkononi katika kutoa huduma za bima ya afya inaleta mapinduzi katika sekta ya ndani ya  bima  kupitia TigoPesa.  
Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na kampuni Milvik ziliingia katika makubaliano ya kutoa Huduma hii tangu mwaka jana kwa kutoa Huduma ya bima kwa simu za mkononi ijulikanayo kama Bima Mkononi ambayo inatoa bidhaa za kipekee na za hali ya juu kama vile,bima ya maisha, ugonjwa na ajali kwa wateja wanaotumia Huduma ya TigoPesa.
Ikiwa na wateja hai zaidi ya 200,000, BimaMkononi ni mfumo mpya wa bima kwa Watanzania wa kawaida ambayo inawawezesha kuwakinga dhidi ya matukio yasiyotarajiwa yanayoweza kuwa na athari kubwa kwa hali ya kifedha kama wasingekuwa wamejiunga na huduma au mpango huu wa bima.  
Tayari BimaMkononi ishalipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 27 katika miezi sita iliyopita.
Hawa Ramadhani  ambaye ni mama wa watoto watatu  kutoka wilaya ya Kibaha, mkoa wa Pwani  ni mmoja wa wanufaika wa BimaMkononi. Akieleza jinsi BimaMkononi  ilivyobadilisha maisha yake alisema; “Nilikuwa nimelazwa katika Hospitali ya tumbi kwa siku 21 na baada ya kuruhusiwa kutoka, niliwasilisha  taarifa za hospitali katika duka la Tigo la huduma kwa wateja na nilifurahi waliponiita baada ya siku tatu  na kupokea  kitita cha 840,000/-! Alisema kuwa aliambiwa  bima  imemfidia kwa kipindi  alichokuwa amelazwa hospitalini.
“Kwa pesa hizo niliweza  kulipia ada ya shule ya watoto iliyokuwa imebaki, pamoja na kukuza  biashara yangu ndogo,” alisema na kuwashauri wale ambao hawajajiunga na mpango huu  kufanya hivyo ili wavune faida.
Mwingine ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Uhandisi na Teknolojia cha St. John,  Dar es Salaam Melikizedeki Nyalufujo ambaye ni mnufaika mwenye furaha wa BimaMkononi baada ya kupokea 86,000/- kufuatia kulazwa kwake hospitalini kwa siku mbili kutokana na jeraha alilolipata.
“Mara ya kwanza nilipoelezwa kuhusu BimaMkononi nilikuwa na wasiwasi lakini nilijiunga. Hata hivyo nilishawishika kujiunga baada ya kupokea fedha hizo ndipo  nilithibitisha kwamba ilikuwa ni kweli. Ankara za hospitali  ilikuwa ni 16,000/-; hivyo kwa fedha  hii ya ziada  niliweza kulipia  gharama nyingine  kama vile kujikimu  chuoni, kununia vifaa  vya masomo na kulipia baadhi ya madeni madogo ambayo nilikuwa nimekopa  hapo awali. Naishukuru mno BimaMkononi,” alisema Nyalufujo kwa furaha.
Kwa mujibu wa Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin huduma ya BimaMkononi imetengenezwa makusudi  kutoa bidhaa za Bima kwa Watanzania wote ambao wanaihitaji  ambao vinginevyo wasingeweza  kumudu huduma hiyo.
“Mteja anaweza kwenda  kujisajili hospitali yoyote  kwa vile hatuweki kizuizi  cha hospitali gani mteja anaweza kutumia- tutayafanyia kazi madai wanapotutumia taarifa sahihi (taarifa ya kuruhusiwa kutoka, taarifa ya madai ya hospitali, fomu ya madai ya bima iliyosainiwa). Kitambulisho cha mteja ni  ni namba yake ya simu na anaweza kujisajili kwa  kutumia namba *148*15#,  huduma  hii inafikia wateja kupitia simu za mkononi kusaidia  kufikiwa kwa urahisi  kadri inavyowezekana  kwa wakazi wa  mjini na vijijini. Bima Mkononi  hadi sasa imekuwa na matokeo makubwa  katika kusukuma mbele  kujumuishwa kifedha ndani ya  sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania  kuzifikia  huduma  za bima wanazozimudu  kutoka ndani ya simu zao.”
Tom Chaplain  alieleza kuwa  huduma hiyo imetengenezwa  mahsusi kwa  kuwapatia watu wote bima za maisha, afya na huduma binafsi ya ajali  ambazo zinaweza kuzisaidia  familia zao  kusimamia madhara ya kifedha ambayo yanaweza kusababishwa na matukio yasiyotarajiwa.
Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanapoel  alisema kwamba ushirikiano huu wa Tigo na Milvik katika kutoa huduma  hii ni moja ya mkakati wa Tigo katika kuendeleza mageuzi ya kidijitali  na kuendelea kuongoza katika kutoa huduma za kibunifu na zenye ubora wa hali ya juu kuwezesha BimaMkononi kupatikana kwa kutumia TigoPesa.
“Huduma hii imekuwa ni fursa kubwa kwa wateja wa Tigo kuifikia bima kwa urahisi kwa sababu BimaMkononi  inalenga kuwapatia Watanzania  njia mbadala wanayoimudu katika bima ya afya na maisha,” alisema Swanepoel.
Kujisajili kwa ujumla wanachokihitaji wateja kufanya ni  kupiga *148*15# na kufuata maelekezo.  Kudai piga namba: 0659071001 na tutakusaidia namna unavyoweza kufungua madai. 
 Mwisho

MANISPAA YA UBUNGO YABAINISHA MPANGO WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI ILI KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU

March 07, 2017
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake. (Picha zote na Nassir Bakari)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kuelezea Makadirio ya Mapato na Matumizi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akielezea jinsi Bajeti ya Manispaa hiyo ilivyopitishwa kwa kuungwa mkono kwa 100% kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kilichofanyika 4/03/2017.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imebainisha namna ya  kuboresha maisha ya wakazi wake kwa kuweka mpango mzuri wa muda wa kati wa mwaka 2017/2018 – 2019/2020 ambao  unalenga kukuza uchumi, na kupunguza umaskini ili kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa wananchi wake.

Mpango huo umeandaliwa kwa kuzingatia sera na miongozo ya Kitaifa, kwa mujibu wa sheria ya bajeti  Na. 11 ya mwaka 2015,   Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango mkakati ni  kutekelezwa kwa matokeo makubwa sasa (BRN), Sera ya Taifa ya UKIMWI, Sera za kisekta, Mipango Shirikishi Jamii ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) ya Kata na Mitaa.

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kuelezea juu ya  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya kawaida na ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018, Makadirio yalijadiliwa na Waheshimiwa Madiwani katika Kamati za Kudumu,na kuidhinishwa na baraza maalumu la madiwani jumamosi ya tarehe 04/03/2017 kwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.   

Mstahiki Meya alisema kuwa ili kutekeleza dhana nzima ya ung’atuaji wa madaraka, mpango huu umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi ambao huanzia ngazi ya Mtaa ambapo Hali hiyo imezingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi katika maeneo yao.

Alisema kuwa Mpango huo umejielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo ya haraka (quick wins) ambayo yatasaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka katika kipindi kifupi na kutoa huduma bora kwa wananchi wa Ubungo.

MAADHIMISHO YA GIRL GUIDES TEMEKE YA KUMUENZI MWASISI WA TGGA DUNIANI

March 07, 2017
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya Chama Cha Girl Guides Tanzania (TGGA) ya kumuenzi mwanzilishi wa chama hicho Duniami, Roden Barden Powell yaliyofanyika Manispaa ya Temeke Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TGGA Tanzania, Profesa Martha Qorro na Kamishna Mkuu wa TGGA Tanzania, Symphorosa Hangi . PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  Kamishna Mkuu wa TGGA Tanzania, Symphorosa Hangi  akiwasalimia wanafunzi ambao ni wanachama a TGGA Temeke
 Wanafunzi wanachama wa TGGA Temeke wakiandamana wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Shule ya Tandika wilayani Temeke, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 Viongozi wa TGGA wakipiga makofi wakati wa kuyapokea matembezi ya wanachama wa TGGA
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA
 Kaimu Ofisa Tarafa Chang'ombe, Hezron Mweladzi (kushoto) aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza jambo wakati wa Madhimisho ya Chama Cha Girl Guides Tanzania ya kumuenzi mwanzilishi wa chama hicho. Roden Barden Powell... Kulia ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi na Mwenyekiti wa Chama hicho,Martha Qorro
 Wanafunzi hao wakiimba nyimbo wakati wa maadhimisho hayo
 Wanafunzi wakiwa katika igizo la mchezo wa kuelimisha na kukataa kurubuniwa na wanaume. wa katikati ni Eunice Joseph, kushoto ni Hajra Mhamedy na kulia ni Seiph  Kingwande ,
 Wanafunzi wakiwa katika igizo, kushoto ni Eunice Joseph kama mwanafunzi, kulia aliyekaachini ni  ni kama Daktari aliyekuwa akimpima mwanafunzi aliyekuwa na ujauzito Husna Mussa na wakatikati ni Farider Mohammed kama mzazi wa mwanafunzi  
 Kamishna wa TGGA Temeke, Komba akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo
 Profesa Qorro akihutubia wakati wa maadhimisho hayo
 Profesa Qorro akiwaelekeza jambo wanafunzi
Profesa Qorro akiagana na wanafunzi baada ya maadhimisho hayo kumalizika