Baadhi
ya Wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha Kleruu wakifuatilia maada
inayowasilishwa kuhusiana na Mradi wa SPANEST jinsi inavyoshirikisha
wananchi katika masuala ya uhifadhi mara baada ya kufunguliwa kwa
kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara
ya pili mjini Iringa.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili
kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili
kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha
ya pamoja na viongozi mara baada ya kufungua kongamano la maonesho ya
utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa.
(Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili
kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili
kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa kwenye picha
ya pamoja na Sekretarieti ya Waandaji wa kongamano mara baada ya
kufungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika
kwa mara ya pili mjini Iringa (Picha na Lusungu Helela- MNRT).
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, amefungua kongamano la
maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili
mjini Iringa.
Kongamano hilo limefanyika kwa muda wa siku moja
katika Ukumbi wa Chuo cha Walimu wa Kleruu likiwakutanisha wasomi na
wahadhiri kutoka vyuo vikuu nchini, wanafunzi pamoja na wadau wa utalii
wanaofanya shughuli za kiutalii likiwa na lengo la kutathmini na
kuangalia namna mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inavyoweza kunufaika
kutokana na utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo.
Sambamba na
kongamano hilo, maonesho hayo yanaendelea kufanyika hadi Oktoba 2 katika
viwanja katika viwanja vya Kichangani yakiwa yamewakutanisha
Wajasiriamali wadogo 350 kutoka kona zote za mikoa hiyo.Akizindua
Kongamano hilo Naibu Waziri Makani amewataka wananchi kuanza kuutupia
macho utalii wa nje ya hifadhi kwa kuwa watalii wengi kwa sasa hawaji
kuangalii wanyamapori pekee.