Tanzania kufaidika na Mfuko wa Programu ya Maendeleo ya Kimataifa ya LFI

September 16, 2014


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa (kulia) alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl (kushoto) na wandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl (kushoto) akiongea na wajumbe kutoka TAMISEMI na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa Fedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI). Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa.
Mtaalamu wa Ushauri wa UNCDF Peter Malika (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini dara es salaam kuhusu LFI na chini ambapo amesema kuwa lengo lake ni kutoa ushauri wa kitaalamu, fedha na namna ya kuchagua miradi yenye tija katika jamii ili wananchi waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa na kushoto ni Afisa Habari TAMISEMI Rebecca Kwandu. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Na Eleuteri Mangi – MAELEZO

Serikali ya Tanzania itafaidika kwa kupata fedha za maendeleo zaidi ya Sh. 46400 za kitanzania ambazo ni sawa na dola milioni 29 za kimarekani ili kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Kati ya fedha hizo, zaidi ya sh. milioni 41600 za kitanzania ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 26 ni mkopo na sh. 4800 za Kitanzania ambazo ni sawa na  Dola milioni tatu ni msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na  Mfuko wa Maendeleo (UNCDF) nchini ambazo zinatarajiwa kunufaisha miradi mitano kwa miezi sita hadi tisa inayokuja.

Ili kufanikisha azma hiyo, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na  Mfuko wa Maendeleo ( Capital Development Fund) wamezindua Mpango wa Kifedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI) ambao utatekelezwa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2014 hadi 2017.
Mradi wa LFI nchini unasaidia miradi 25 katika sekta za umeme, miundombinu vijijini, mawasiliano, viwanda na masuala ya usindikaji katika mikoa 10 ambapo mikoa ya Pwani na Kilimanjaro kupitia halmashauri za Kibaha na Same ni miongoni mwa halmashauri zinazonufaika na mradi huo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl leo jijini Dar es salaam.

Dkt. Mtasiwa amesema kuwa Serikali inajukumu la kutoa huduma za jamii kulingana na mazingira ya ndani ambapo jukumu hili linasimamiwa katika ngazi ya halmashauri wakati Serikali Kuu jukumu lake ni kupanga na kutoa sera zinazosimamiwa na kutekelezwa katika ngazi ya Serikali za Mitaa.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania kupitia TAMISEMI umekuwa ni kiini cha kutekeleza mipango mbalimbali inayosimamiwa na UN.

Aidha, Judith amesema kuwa mpango wa LFI unalenga kuongeza uboreshaji wa rasilimali fedha kwa maendeleo ya kiuchumi kupitia mitaji na masoko ili kuweza kukuza na kufikia malengo ya maendeleo ya ndani ya nchi.


Naye Mtaalamu wa Ushauri  wa  UNCDF Peter Malika amesema lengo la LFI l ni kutoa ushauri wa kitaalamu, kifedha na namna ya kuchagua miradi yenye tija katika jamii ili kuwawezesha wananchi waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa lao.

MKUTANO WA 29 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (MEAC) KUFANYIKA SEPTEMBA 20-2014 JIJINI ARUSHA

September 16, 2014


 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji  na Biashara wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (MEAC), Dk. Abdallah Makame (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano huo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji  na Biashara wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (MEAC), Dk. Abdallah Makame (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuia ambao utafanyika Septemba 20, 2014 jijini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Wizara hiyo, Anthony Ishengoma.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji  na Biashara wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (MEAC), Dk. Abdallah Makame (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano huo.
. Kulia ni Ofisa Habari Idara Habari Maelezo, Frank Mvungi na  Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Anthony Ishengoma.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Maofisa wa Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Teodos Komba na Mtaalamu wa Mawasiliano, Faraja Mgwabati.
Mkutano ukiendelea

Na Dotto Mwaibale

MKUTANO wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa kuanza Septemba 20, 2014 katika jiji la Arusha.
Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji na Biashara wa wizara hiyo Dk. Abdullah Makame alisema katika mkutano huo baraza linatarajia kujadili agenda mbalimbali na kutolea maamuzi masuala kadhaa.
Alisema katika mkutano huo watazungumzia na kuadhimisha aina mpya ya hati ya kusafiria ya kielectroniki zikiwemo sampuli za hati ya kusafiriaza kibalozi za maofisa na wananchi wa kawaida.
‘Hati  hizo za kusafiria zitasaidia  kukuza biashara na soko la kimataifa na kusafiria nchi mbalimbali  kwani za awali zilikuwa  haziruhusiwi” alisema Dk. Makame.
Aliongeza kuwa katika baraza hilo pia kuatajadiliwa mapendekezo na hadidu za rejea za uanzishwaji wa dira ya maendeleo ya Afrika Mashariki 2050.
” Moja ya ajenda itakuwa ni kuandaa mapendekezo ya mpango mwelekeo wa shughuli mbalimbali kama vile  kuaandaa katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki na sarafu moja ya nchi zilizopo katika jumuia hiyo,’ alisema.
Akizungumzia ni vipi Tanzania imekuwa ya kwanza kukubali kuwa na sarafu kuliko nchi nyingine alisema ”Tanzania imekubali kwa haraka kwa sababu ilikuwa kinara katika kujadili umoja wa forodha na umoja wa fedha,”.
Alisema Baraza la Mawaziri huwa linaundwa na Mawaziri wa Ushirikiano wa Afrika Masahariki pamoja na mawaziri wengine kutoka nchi wanachama na baraza hilo huwa linakutana mara mbili kwa mwaka.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN ZIARANI COMORO

September 16, 2014


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mawaziri mbali mbali wakati alipowasili katika   Ikulu ya Comoro kwa mazungumzo na Rais wa Nchi hiyo Dr. Ikililou Dhoinine jana akiwa katika ziara ya kiserikali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine Ikulu Mjini Comoro jana,Dk.Shein yupo Comoro kwa ziara ya kiserikali akiwa na ujumbe aliofuatana nao.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine (katikati) wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na ujumbe wa Rais na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Comoro   Ikulu Mjini Comoro jana katika  ziara ya kiserikali akiwa na ujumbe aliofuatana nao. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akifuatana na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine baada ya  mazungumzo Ikulu Mjini Comoro jana,akiwa katika  ziara ya kiserikali  na ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na  mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine Ikulu Mjini Comoro jana, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ujumbe Serikali ya Mapinduzi ukiwa katika ziara Nchini Comoro. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
KAGERA SUGAR WAIFUATA MGAMBO JKT MJINI TANGA

KAGERA SUGAR WAIFUATA MGAMBO JKT MJINI TANGA

September 16, 2014

Na Faustine Ruta, Bukoba
Kikosi cha Timu ya Wakata Miwa Kagera Sugar wameanza leo hii safari  kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu soka Tanzania bara katika uwanja wa CCM Mkwakwani dhidi ya wenyeji Mgambo JKT, septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange amesema klabu hiyo ina jumla ya wachezaji 25 na hii leo tayari wapo safari na  viongozi watano kwenda kusaka pointi tatu muhimu.
Kabange aliongeza kuwa wameamua kuanza safari mapema kwasababu kutoka Kagera kwenda Tanga ni mbali sana.Viongozi wa Kagera Sugar
Ubutu wa safu ya ushambuliaji lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar lakini kwa sasa limepata marekebisho kwani wamesajili Vijana wa nguvu msimu huu.
WAKATA miwa wa Kaitaba, `Wanankulukumbi` Kagera Sugar wakijifua kwenye Uwanja wa Kagera Sugar hivi karibuni tayari kwa Ligi kuu Vodacom sep 20 mwaka huu. Kagera Sugar wataanza ufunguzi wa Ligi kuu Vodacom Ugenini na timu ya Mgambo JKT mkwakwani Mjini Tanga wikiendi hii.
Kocha huyo alisema: “Tuna imani na vijana wetu kuwa wanaweza kutufikisha tunapotaka, japokuwa ligi ya msimu huu inaonekana itakuwa ngumu, lakini tutajitahidi kupigana ili kuweza kushika nafasi za juu”.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakifaya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Kaitaba Hivi karibuni.



Baadhi ya Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa Uwanjani Kaitaba wakishuhudia mazoezi ya Vijana wao. Wakijifua kujiandaa na Ligi Kuu Vodacom msimu mpya 2014/15 inayotarajia kuanza hivi Karibuni sep.20 mwaka huu.
Kikosi cha Kagera Sugar
Murage Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar (kulia) tayari amebainisha kuwa mapungufu waliyokuwa nayo katika kikosi chao kuwa wameishayafanyia marekebisho na wako tayari kupambana na Mgambo JKT ya Mjini Tanga.
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar (kulia) Bw. Jackson Mayanja akiangalia vijana wake wakati w mazoezi yao kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Kaitaba hivi karibuni.