RC SHIGELA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC MKOANI TANGA

September 15, 2017
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela leo Ijumaa Septemba 15,2017 amefungua mkutano Mkuu wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs- UTPC) mwaka 2017. 
Mkutano huo uliokutanisha viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa 27 nchini unafanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga. 
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo ambao utafanyika kwa muda wa siku mbili (Septemba 15 na 16,2017),Shigela alisema serikali inatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika maendeleo ya jamii. 
“Ukitaka maendeleo katika jamii lazima ushirikiane na vyombo vya habari,na hata tunapoelekea katika Tanzania ya viwanda ni vyema vyombo vya habari vihusike”,alieleza. 
Alitumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuzingatia maadili katika kazi yao ya uandishi wa habari huku akiwaasa kujiendeleza kielimu ili kufanya vizuri zaidi katika kazi yao. 
“Vyombo vya habari vinafundisha,vinaelimisha,vinahamasisha ,vinakosoa na kufichua maovu na ili kutimiza haya ni vyema mkazingatia maadili yenu,mfanye kazi kwa usawa bila upendeleo lakini pia ni vyema mkawa wazalendo”,aliongeza. 
Kwa Upande wake rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo alisema miongoni mwa changamoto zinazoikabili tasnia ya habari ni uwepo wa sera na sheria zinazobinya uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo sheria ya Habari ya habari ambayo baadhi ya vifungu vyake siyo rafiki kwa waandishi wa habari. 
“Tunaiomba serikali ifanye marekebisho katika baadhi ya vifungu kwenye sheria hii ambavyo siyo rafiki kwa vyombo vya habari”,aliongeza Nsokolo. 
Awali akizungumza katika mkutano huo,Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC,Abubakar Karsan alisema mkutano huo umekutanisha pamoja wadau mbalimbali wa habari nchini na viongozi wa klabu za waandishi wa habari kutoka mikoa 27 ya Tanzania bara na Zanzibar. 
Alisema katika mkutano huo wajumbe watashiriki watafanya majadiliano mbalimbali kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu waandishi wa habari. Habari na Kadama Malunde- Malunde1 blog,Picha zote na Oscar Assenga- Tanga Raha Blog
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela akifungua mkutano mkuu wa UTPC
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC,Abubakar Karsan akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza ukumbini
Rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo akitoa hotuba
Makamu wa Rais wa UTPC,Jane Mihanji akizungumza ukumbini

PROF. MAGHEMBE APOKEA CHETI CHA SHUKURANI KUTOKA SPORTPESA KWA KUTAMBUA MCHANGO WA WIZARA YAKE WA KUFANIKISHA UJIO WA TIMU YA EVERTON NCHINI TANZANIA

September 15, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkaribisha Meneja Mahusiano wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya ofisini kwake mjini Dodoma jana ambapo alifika kukabidhi Cheti cha Shukurani kutoka kwa kampuni hiyo kwa Wizara yake kufanikisha ujio wa timu ya Everton nchini Tanzania mwezi Julai mwaka huu, 2017. Ameipongeza SportPesa kwa kufanikisha kuileta timu hiyo nchini na kuwaomba kuzileta timu nyingine kutoka nchini Uingereza kwa kuanzia na timu ya Arsenal ili kuutangaza zaidi utalii wa Tanzania nje ya nchi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akipokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa Kampuni ya SportPesa Tanzania kwa wizara yake kufanikisha ujio wa timu ya Everton nchini Tanzania mwezi Julai mwaka huu, 2017, anaekabidhi cheti hicho ni Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo, Sabrina Msuya ofisini kwake mjini Dodoma jana. Ameipongeza SportPesa kwa kuileta timu hiyo nchini na kuiomba kuzileta timu nyingine kutoka nchini Uingereza kwa kuanzia na timu ya Arsenal ili kuutangaza zaidi utalii wa Tanzania nje ya nchi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Meneja Mahusiano wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya ofisini kwake mjini Dodoma jana mara baada ya kupokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa kampuni hiyo kwa Wizara yake kufanikisha ujio wa timu ya Everton nchini Tanzania mwezi Julai mwaka huu, 2017. Ameipongeza SportPesa kwa kuileta timu hiyo nchini na kuiomba kuzileta timu nyingine kutoka nchini Uingereza kwa kuanzia na timu ya Arsenal ili kuutangaza zaidi utalii wa Tanzania nje ya nchi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimsikiliza Meneja Mahusiano wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya ofisini kwake jana mjini Dodoma mara baada ya kupokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa kampuni hiyo kwa Wizara yake kufanikisha ujio wa timu ya Everton nchini Tanzania mwezi Julai mwaka huu, 2017. Ameipongeza SportPesa kwa kuileta timu hiyo nchini na kuiomba kuzileta timu nyingine kutoka nchini Uingereza kwa kuanzia na timu ya Arsenal ili kuutangaza zaidi utalii wa Tanzania nje ya nchi. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akimuaga Meneja Mahusiano wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya ofisini kwake jana mjini Dodoma baada ya kupokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa kampuni hiyo kwa Wizara yake kufanikisha ujio wa timu ya Everton nchini Tanzania mwezi Julai mwaka huu, 2017. Ameipongeza SportPesa kwa kufanikisha kuileta timu hiyo nchini na kuwaomba kuzileta timu nyingine kutoka nchini Uingereza kwa kuanzia na timu ya Arsenal ili kuutangaza zaidi utalii wa Tanzania nje ya nchi. Kulia aliyeshikilia cheti hicho ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki.
PICHA NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII